Ndugu Mtazamaji/ MSOMAJI; Bila shaka unampenda Mungu Sana tunaamini hivyo Kwa vile ulivyoweza kufika mahali hapa tulipo kupitia Mtandao huu, lipo kusudi la Mungu kutaka kukusaidia jambo Fulani ikiwa uko tayari katika yote jiepushe na mafundisho yasiyokuwa ya ki-Mungu Mathayo 16:6-12) piga simu kwa masaada zaidi huduma hii ni bure 0757328311
FORM KWAAJILI YA WAGENI
Njoo tushiriki pamoja ibada inayoongozwa na Nguvu za Roho Mtakatifu fuatilia Ratiba za Ibada hapa
Juma tano Ibada ya mafundisho ya Bibilia
Saa 10:00-12:00 Jioni kwa kanisa nzima
Ijumaa Ibada ya maombezi kwa kanisa zima
Saa 10:00-12-00 Jioni
Jumamosi Asubuhi usafi wa kanisa nzima Saa 8:00-6:00
Kwanzia Mchana Saa 7:00 hadi 12:00 ni Huduma ya waimbaji wote, wa kanisa,(Mazoezi)
Jumapili Asubuhi kwanzia Saa 1:00 Hadi Saa 3;00 Maombi kwa kanisa zima, Saa 3:00 Hadi 4:30 Mafundisho
Baada ya mafundisho Ibada kuu 4:30 Hadi Saa 7;30
Ibada ya jioni Inaanza Saa 9:30 Hadi 12:00 Karibu Sana,
…………………………………………………………………
Jina langu naitwa ……………………………………….Mk/M/m Mtaa………………...NO……………………………Maombi Yangu 2ni ………………………………………..
Je Maandiko yanaongelea nini Kuhusu pombe?
UTANGULIZI:Maandiko yanaongelea nini kuhusu Pombe?
Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;
mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;
na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;
hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo. Efeso 5:19
“Wala wevi,wachoyo, walevi, wasengenyaji, wanyang’anyi, hao wote hawatakishiriki Utawala wa Mungu 1 Kor 6:10 –
“ Basi jiangalieni ……. Na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha Luke 21:34 –
1. Msijidanganye! Mtu yeyote miongoni mwenu akijidhania mwenye hekima mtindo wa kidunia, heri awe mjinga kusudi apate kuwa na hekima ya kweli. Ikorintho3:18
2. Hoja za watu wengi kuhusiaana na andiko hili:
Paulo akamwambia Timotheo kunywa mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lako
(1 Timothy 5:23 Ndugu yangu swali langu kwani wote wanaojazana huko bar matumbo yanawauma ? Basi leo kuna frajili na dawa nyinginezo. Zamani hazikuwepo, Hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya dawa. Ni kama vile nusu kaputi ukiitumia kama dawa Mungu hana tatizo; lakini ukijidunga kwa kujifurahisha? Ni kama mtu anayebadilisha matumizi ya dawa za usingizi anajiwekea kama anasa inakuwa kama Dhambi y dawa za kulevya
Umejaa aibu badala ya utukufu; unywe nawe, uwe kama mtu asiyetahiriwa; kikombe cha mkono wa kuume wa Bwana kitageuzwa ukipokee, na aibu kuu itakuwa juu ya utukufu wako. Habakuki 2:16
Watu wanatetea kukuwa kuna nguvu inayowashukilia na kuwalazimisha kutenda wasilopenda wala kutaka,
Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.
Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.
Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema. Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu warumi 7:14
Jibu analo yeye mwenyewe anayekunywa,
Kukaa kimya haisaidii kutokutambulika,
Kama una tatizo na ulimi ujue unatatizo kubwa moyoni kuliko unavyofikiria.
· Mtu mwenye maneno makali ana moyo wenye hasira.
· Mtu mwenye maneno hasi ana moyo wa woga na hofu.
· Mtu mwenye ulimi /maneno ya kulipuka ana moyo ambao haujatulia.
Mtu mwenye maneno ya kujivuna na kujisifia ana moyo usiojiaamini,hana usalama wa moyoni.
· Mtu mwenye maneno ya kutukana ana moyo usio safi
· Mtu ambaye wakati wote ni mkosoaji na wa kulaumu ana moyo wa uchungu
lakini upande wa pili,mtu mwenye kutia moyo siku zote ana moyo wa furaha.mtu anazungumza kwa upole ana moyo wa upendo,anayezungumza ukweli ana moyo wa uaminifu.
B. JINSI YA KUKUFANYA ILI NIWEZE KUUTAWALA NA KUUCHUNGA ULIMI WANGU:
1. PATA MOYO MPYA Ezekeli 18:31, zaburi 51
2. OMBA MSAADA WA MUNGU KILA SIKU Zaburi 141:3 huwezi kwa nguvu zako unahitaji msaada wa Mungu
Usalama wa ulimi ni kujifunza kusikiliza na si kuongea,
Ufikiri kabla ya kusema-jifunze nidhamu ya kusikiliza Yakobo1:19 ,Kusikiliza kutakufanya kuwa na maneno machache.Ukiwa mwepesi kusikiliza hautakuwa mwepesi kusema, kusukiliza ni sanaa,ni jambo la kujifunza ni kazi sana, mfano katika maongezi ya simu,kuiingilia kati mwingine anapozungumza,kumkata kauri mtu mwingine,kutaka kutawala mazungumzo pekee yako,n.k.
Kusikiliza listening ni tofauti na kusikia hearing,unaweza kuwa unasikia lakini husikilizi,
kusikiliza ni ngazi ya juu ya mawasiliano inayo husisha, macho, masikio,mwitikio wamwili,lugha ya mwili,hisia za mwili-ni katika kusikiliza unaweza kumjua mtu zaidi,na kuusoma moyo wake,ana uchungu kiasi gani,ameumia kiasi gani,n.k.
Tunauweza wa kusikiliza maneno 600 kwa dakika,wakati tunauwezo wa kusema maneno 150 tu kwa dakika,tofauti ya maneno 500,tunafikiria haraka kabla ya mtu hajamaliza kusema tayari tunamaliza naye sentence,Inahitaji Nidhamu.
“Maneno yetu yana nafasi kidogo sana katika mawasiliano na kufikisha ujumbe,mawasiliano ni zaidi yakuzungumza maneno.utafit wa Kodak uligundua hili –Nusu ya mawasiliano yetu ni ujumbe usio wa maneno yeyote,kutazama ,lugha ya mwili kunachukua 58% ya kuwakilisha ujumbe,sauti yetu na namna tunavyo sema 35%,maneno yenyewe hasa ni7% ya ujumbe wote.hii ni kusema maneno au kuzungumza hakuna nafasi kubwa katika mawaasiliano tofauti na tunavyofikiria na kuamini.”
Asante kwa kushiriki na sisi
kwa nini ulimi ni hatari,
je Unajuwa ulimi wako unakokupeleka?
Kielelezo cha usukani na lijamu.Ukitaka kujua utakuwa wapi au vipi miaka mitano ijayo akangalia nini unazungumza zaidi leo juu yako mwenyewe,maneno yetu yana tupa uelekeo wa kule tuendako.unaongea juu ya nini zaidi?.
“ulimi unatawala mwelekeo wa maisha yako.ulimi ni usukani wa maisha yako,ni mfumo wako wa uongozi wa maisha yako Ukitaka kumbadilisha mtu anvyoamini,mbadilishe vile anavyo zungumza,vile unavyozungumza mwisho wa siku nindivyo vile unavyoamini.”
yale unayo yazungumza sana,mara kwa mara mwisho wa siku ndivyo utakayo yaamini. wazo Huiingia katika ufahamu,kasha katika MOYO,MANENO hutoka moyoni na kasha MATENDO huzaliwa.(MITHALI 18:20)
Nukuu: Martin LUTHER-“huwezi kuzui ndege wasiruke juu ya kichwa chako,lakini unaweza kuzuia wasijenge kiota na kuhamia hapo”
2. ULIMI WANGU UNAWEZA KULETA UHARIBIFU NA MADHARA KWANGU NA KWA WENGINE
Kielelezo cha moto na mnyama mkali asiyefugika.Mithali 21:23 18:21 Madhara makubwa sana yameletwa na ulimi,ndoa zimevunjika, urafiki,mahusiano,makanisa ,ndugu,wamekosana n.k ulimi unasabisha magovi,chuki n.k ULIMI unadhuru unaitwa mishale…una dhuru hata mbali.Neno moja liweza kusababisha “chain reaction”unaweza kuzungumza kitu ambacho hudhamiria kilete madhara lakini matokeo yake makubwa yasiyozuilika.
3. ULIMI WANGU UNA NIDHIHIRISHA VILE MIMI NILIVYO
Kielelezo cha chemchemi namti wa matundaYAKOBO 3:9-12Watu wengi wanafikiri labda kukaa kimya pekee yake kunasaidi,cha muhimu zaidi ni ndani yako kukukojeMfano wa kisima/chemichemi na mfano wa mti na matunda-Kile kilichopo katika kisima ndicho kitakacho toka na kuwepo katika maji,kadharika kilichopo katika mti kitajidhihirisha kwa njia ya matunda.
ubarikiwe sana asante kwakushiriki na sisi hapa
Vikwazo vya Aliyetumwa
Kila aliyetumwa, Lazima akumbane na vikwazo,
Kutuma-
ni hali ya kupewa ujumbe kwa ajili ya kupeleka palipo kusudiwa. Unaweza ukawa ujumbe wa familia au nchi. Mungu naye Ana kawaida ya kuwafumba watu duniani na Jumbe mbalimbali…
Maandiko yanayotaja uweza wa Mungu wa kutumia watu.
Kama hutaki matatizo mwachie aliyetumwa, kwa desturi Mungu huwa anatuma watu duniani na hii ni desturi ya Mungu.
Yeremia 49:14 . 14 Nimepata habari kwa Bwana, Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, Akisema, Jikusanyeni, mkaujie, Mkainuke kwenda vitani.
Na hawa watu hutumwa kwa makusudi mbalimbali
Kutoka 23:20 Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali.
Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande.
malaki 3: 1,Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi.
Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo;
mathayo 11:10 , Huyo ndiye aliyeandikiwa haya, Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako mbele yako.
watu wa dunia hii kwa kumuonea mtu anakupa pamoja nao, au anaishi katikati Yao huisikia kuwa hajatumwa, lakini hata kwenye biblia watu waliotumwa walikuwa wanaishi na kula kama watu wengine.
mifano ya watu waliotumwa kwenye biblia.
Marko 1:2 Kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako.
huyu ni Yohana mbatizaji, alitumwa kuandaa njia kwa ajili ya Yesu .
Hata Yesu mwenyewe alikuwa ametumwa Kutoka mbinguni lakini alitungwa mimba, akazaliwa, na Akaishi Kama watu wengine, Hesabu 20:16 tena tulipomlilia Bwana, akatusikiza sauti yetu, akamtuma malaika, na kututoa tutoke Misri; nasi tupo hapa Kadeshi, mji wa mpakani mwako mwa mwisho;
Mungu anatabia ya kutumia. 2Samweli 12:1 zaburi 105:26. Mathayo 21:37 waamuzi 6:28 Mungu anatabia ya kutuma watu.
Mfano wa wanasayansi.
Wanasayansi wengi wa zamani amabao walikuwa wakristo na ni wavumbuzi wa zamani wa sayansi, mfano 1. isaack newton, 2. Boyle, na watu Kama wakina 3. kelvin waliogundua umeme hawa watu walikuwa wameokoka na hawa waligundua vitu mbalimbali. 4. Michael faraday Kama tulivyoona wagunduzi wa zamani wengi wanakubali kuwa Mungu yupo. 5. John Rey, 6. Creg Maxwell 7. Caros Linus, 8. Kepler. waliokuwa wameokoka.
Lakini ukiangalia maisha yao binafsi, utagundua maisha yao yakipita mambo magumu,
Mfano: isaack newton mama yake akiwa mjamzito, baba yake akafariki … Hivyo mama yake akaenda kuolewa na mume mwingine, Na hapo newto akaenda kuishi kwa mjomba yake na katika maisha magumu na kutokana na maisha magumu yale , yakamfanya newton akazane kusoma kumbe mtu aliyetumwa kuibadili dunia na hapa lazima dunia imshikilie na kumzuia, lakini mwisho wa siku alikwenda na kumaliza wito wake.
Mfano mwingine ni Robert Boyle naye alizaliwa kwenye shida pia, Faraday pia Alipitia wakati mgumu kwenye maisha yake.
Maisha halisi ya sasa.
Tunapozungumzia kutumwa ni neno pana sana na hapa inaweza ikawa mtu katumwa kubadili nchi, familia, nyumba na Hali ya jamii nzima. Lakini dunia hii tuliopo ina system mbalimbali mfano. Dini, serikari, jeshi ambavyo vinazuia ujumbe wa aliyetumwa. Marko 1:2 , “palitokea mtu ametumwa…..” unajikuta unakiu ya jambo fulani kufanikiwa, una kiu ya kufanikisha kitu fulani kinaweza kuwa cha familia au cha taifa na hapo hali ya maisha na umaskini ina kuzuia, na hii ni kawaida ya dunia kujaribu kuwashikilia watu waliotumwa..
Kumbe inawezekana kuwa Mungu amekutuma duniani, na hujijui na kwa vile dunia ilivyokushikilia inakufanya hata usahau kuwa umetumwa. Mfano: inawezekana umetumwa kuwa waziri wa mambo ya nje na hapo inakubidi upate elimu angalau, lakini dunia inakuzuia kwa kukuletea umaskini ili ukose elimu na mwisho wa siku ushindwe kufikia kwenye kule ulipotumwa.
Msaada kutoka kwa Mungu kwa Yule aliyemtuma.
Kama tulivyoona Mungu anadesturi ya kutuma malaika, binadamu ili kuitengeneza dunia kuishape dunia kuileta mahala pake… Na Mungu ili kuwasaidia aliowatuma huitikisa dunia kwa jambo fulani ili kufanya wale aliowatuma waingie kwenye system, na hapa ndio maana unaona hata nchi Kama Tanzania inapitia kwenye mtikisiko ikionyesha kuwa kuna watu waliotumwa na wanakusudiwa kuingia kwenye nafasi zao.
Mfano mwingine ni wa Ibrahim , ambaye ni baba wa Imani, na huyu aliahidiwa kuwa baba wa mataifa na ili kuwa baba wa mataifa lazima azae awe na watoto, lakini dunia( shetani) akaanza kupinga hiyo, kwa kumwekea utasa, na hapa tunajifunza kuwa kwa kila mtu aliyetumwa lazima atakutana na upinzani.
Mfano mwingine ni Musa , na Musa alipozaliwa tu , shetani akajua na alitumwa na Mungu kuunda taifa imara, la Israel na ndio maana alipozaliwa tu, Farao akaamuru watoto wote waangamizwe, na hapa tunajifunza kumbe ukiwa na kitu kikubwa cha Mungu , lazima utapingwa na kuzuiwa. Lakini Musa kimuujiza alienda kula mezani mwa Farao. Bila Farao kujua hadi wakati wake hutimie.
Kumbe aliyetumwa hawezi kuangamizwa hadi atimize hatma yake.
Kwahiyo Mungu anakwaida ya kuwasaidia wale aliowtuma, tunaona katika habari ya Musa alipokuwa mdogo, na hata yale mapigo aliowaandalia wamisri,
Mfano mwingine wa taifa la Israel, kipindi Sauli alipofanya machukizo… Mungu akamtuma nabii Samuel kwenda kumpaka Mafuta mfalme Daud . Mungu anakawaida ya kutuma watu. kwa hiyo samweli akamchagua na kumtia Mafuta daudi.
Vitu ambavyo vilimshikilia Daud Kama mpakwa mafuta.
1. Kudharuliwa na ndugu zake.
2. Yuko machungoni polini.
3. Alidharauliwa na watu wa taifa lake.
Lakini pamoja na yote daudi aliishia kuwa mfalme sawasawa na alivyoitwa.
Jambo la kufanya:
Ni muhimu kupambana vita vya kiroho ili kuondoa vizuizi vya dunia, ambavyo vinazuia watu waliotumwa… Kwa hiyo ni muhimu kusambaratisha nguvu ya shetani ili kutuachia watu tuliotumwa.
Mungu akubariki sana, kwakushiriki nasi,
Kafara maana yake nini?
vitano.. yaani kuhani wa madhabahu , Mungu wa madhabahu , Nguvu ya madhabahu ( moto wa madhabahu) , kafara ya madhabahu na madhabahu yenyewe .. na kwa leo tujikite zaidi kwenye neno hili kafara ya madhabahu
KAFARA YA MADHABAHU
Nini maana ya kafara?
Kwa akili zawatu zilivyo wakisikia neon kafala wanakimbilia kwenye waganga wa kienyeji.. lakini neno hili kafara kwenye biblia ndio linaitwa dhabihu kwenye biblia.. kuna maadiko kadhaa yanayo taja kafara kwenye biblia kama ifuatavyo :- mambo ya walawi 2 :2, 9, 16; mambo ya walawi 10 : 13, 14.. maandiko haya yanataja neon kafara kwenye biblia .. na limeonekana mara nyingi.. hii ni kukuonyesha kuwa neno kafala lipo kwenye biblia na lina maana sahihi.. kwahiyo Kafara ni sadaka inayotolewa kwa ajili ya kupokea jambo fulani kutoka ulimwengu wa roho aidha kwa Mungu au kwa shetani..
Ni Muhimu kujua matatizo mengi ya watu yanasababishwa na kafara zinazotolewa.. .. na shetani amewafunga watu wasijue vyanzo vya matatizo yao na kufungwa huku ndio biblia anaita “mafumbo ya kishetani” Ufunuo 2: 24-25 na kwa namna hii shetani amewapofusha watu wasijue siri hii ndio maana hata baadhi ya wakristo wamefungwa wasijue siri hii..
Kwa desturi watu hupanda ngazi kwenye maisha kulingana na sifa zao na haki, lakini watu wengine kwa kutumia njia ya mkato wanatoa kafara ili kuwa funika wengine na kuchukua nafasi zao.. Yeremia 32 :35 1wafalme 16 : 34 tunaona hapa kwenye hili andiko, maana Joshua alipoubomoa ukuta wa Yeriko akaweka kanuni nya kuwa yeyote atakaye taka kujenga atafiwa na mwanaye pale atakapo anza na atakapo fika katikati atafiwa na motto mwingine … lakini tunaona Hieli mbethel akaamua kumtoa kafara mwanaye kwa kuweka misingi na tena akamtoa kafara mwanaye mwingine..
Tunaona hapa kuwa kafara na kutoa kafara hayakuanza leo bali yalianza tangu kipindi cha cha zamani kwenye biblia.. 2 wafalme 3:24-27 hapa tunaona wayahudi wakavamia Moabu na wakakaribia kuteka mji wa Moabu na hapa ndio maandiko yaasema ndipo alipomtoa mwanaye ambaye angekuwa ni mtawala badala yake kwenye ukuta ili wayahudi wasiweze kuwavamia..
Ndio maana ni rahisi kumkuta mtu anasikitika kuhusu matatizo yake., lakini ni Muhimu kujua watu wa duniani hutoa kafala ili apate ushindi katika maisha na kwa njia hii hufunika wengine.. ndio maana kuna aina ya mashetani yanaitwa mizimu hawa sio roho za watu waliokufa bali ni mashetani waliokaa muda wa kutosha nafamilia hadi wakajua tabia zenu na pale mtu anapoenda kutoa kafara anakuwa anayaalika yale mapepo nyumbani au kwenye ukoo husika.. na ndio maana ni rahisi kukuta ukoo mmoja kuwa na matatizo yanayo fanana..
Kimsingi waganga wa kienyeji hutumia kafala kuwafunga watu, na ndio maana ukienda kwa mganga atakutaka ulete kafara aidha ya kuku au ya mbuzi kwa maana kwa mganga wa kienyeji ni madhabahuni pa shetani… na wachawi pale ile damu inapomwagika mashetani anamiminika pale na kufanya vile kafara inavyowataka wafanye.
Ndugu zangu kuna watu hata hawapendi kukuona unakula vizuri, au unapika vizuri au unasomesha.. na akiona huo wivu anaamua kwenda kukufanyizia kwa mganga wa kienyeji..ambapo ataambiwa atoe kafara kwa ajili ya kukuangamiza wewe..
1wakorintho 10:2020
Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa
Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.
21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.
22 Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?
.. zaburi 126:38 kumbe kuna uwezekano wa watu kutoa kafara kwa mashetani. Na biblia inalikubali hili kupitia maandiko hayo tuliyoyaona hapo.. unaweza kuwekewa pepo la udhaifu kupitia kafara.. Luka 13:10 Pepo wa udhaifu.. mtu anaweza kukutolea kafara ili ufe kifo cha Ghafla..
Kwetu tuliookoka..
Unapomkubali Yesu unakuwa umejiunganisha na mauti ya Yesu hivyo hakuna haja ya kutoa kafara tena.. maana Yesu alifanyika kafara kwa ajili yetu na damu ya Yesu ilimwagika ili kutufungua wote na Yesu alipigwa na kufa ili sisi kutookoa kama kafara kwaajili yetu.. watu wa dunia wanaweza kwenda kwa waganga na kutoa kafara lakini sisi tuna Damu ya Yesu ambayo ni nguvu ya madhabahu yetu..
Hivyo sasa kwa kutumia damu ya Yesu unaweza sasa kuharibu kafara na madhabahu zao zote,, ukishughulikia madhabahu na kafara unakuwa umeiangamiza nguvu ya madhabahu nza kishetani na tatizo ulilonalo litakwisha .. kwahiyo ni muhimu kuharibu makuhani wa madhabahu yaani wachawi na waganga, madhabahu yenyewe yaani wanapokusanyikia, inatubidi kubomoa kafara yao, nguvu yao na pia Mungu wa madhabahu zao ambazo ni shatani.. na hapo utapata ushindi mkamilifu..
Mathayo 17:14 utajiuliza inakuaje, Yesu anaamua kumtoa pepo wakati tatizo lake lilitajwa ni kifafa, hapo utagundua kuwa matatizo ya watu wengi yanatoka na mapepo au majini yanayo tumwa na kumfanya awe vile alivyo.. lakini unatakiwa ushughulikie madhabahu na mambo yanayofuatana nayo…
Balozi wa serekali ya mbinguni
Maana ya kuzimu na mauti
Kila jambo lina nguzo linazozitegemea, na kila utawala una nguzo unaotegemea.. vilevile utawala washetani umejengwa juu ya nguzo ziitwazo MAUTI na KUZIMU.. Ayubu 38:18 na nguzo hizi mbili ndizo ambazo zinashikilia utawala wa shetani na ndio maana maeneo mengi ambayo kuzimu inatajwa basin a mauti ipo pia.. mfano katika kitabu cha zaburi 116 :3 .. HAPA UTAONA kila mahali ambapo mauti imetajwa basi kuna mahusiano na kuzimu ..
MAANA YA MAUTI NA KUZIMU :
MAUTI ni roho ambayo kazi yake ni kuuondoa uhai ulio ndani ya mtu. Na KUZIMU ni roho ambayo kazi yake ni kuwahifazi wale waliokufa.. ufunuo 6: 9, Isaya 28 :15 ..
Mauti ni roho yenye akili na yenye kupanga.. ndio maana wanafunzi wa Yesu , walipomuona Yesu yuko juu ya maji, biblia inasema wanafunzi wa Yesu wakadhani wameona roho.. kumbe roho ina personality ina akili kili, inaweza kupanga na kutekeleza na pia yaweza kumpagaa mtu. Kwahiyo mauti ni roho yenye personslity hapo tunaweza sema mauti ni mtu.. Tunaweza sema mauti ni mtu ina “personality” ufunuo 20 : 13.. mauti inaweza kumeza watu..
ufunuo 20 : 14 kila mahali inapotajwa mauti kuzimu inafuata pale, hii inaonyesha kuwa mauti inaanza alafu kuzimu inafuata.. katika hiki kitabu cha ufunuo 20 : 14 tunaona kuwa “ mauti na kuzimu vikatupwa kwenye jehanamu” kumbe mauti unaweza uka ikamata kabisa na kuitupa mahali.. kama mauti na kuzimu vingekuwa ni matukio basi visingeweza kushikwa na kutupwa kwenye moto. Ndio maana Yesu alipokufa alishinda mauti na kuzimu. ( yohana 20 :3)
tuangalie hili andiko mwanzo 37:25 katika agano la kale kuzimu lilikuwa linatumika kama mahali wafu walipokuwa wanakwenda, na palikuwa panaitwa “sheol” kwa lugha ya kingereza na huko wako wafu wote waliotenda haki na walitenda maovu walikuwa wanakwenda kule.. lakini palikuwa wamepagawa mahali pa watenda haki na mahali pa watenda maovu.. na mahali walipokuwa wanaenda watenda palikuwa panaitwa Kifuani pa Ibrahimu, ( yaani wale walioamua kuungana na imani ya Ibrahim) na sasa kunaitwa paradiso..
TOFAUTI YA JEHANAMU NA KUZIMU:
Jehanamu ni shimo la rohoni la moto watakapo angamizwa watu watendao dhambi, kwasasa jehanamu hakuna mtu ndani maana hukumu bado haijatolewa lakini watu wanaokufa kwa sasa wanaenda kuzimu (bottomless pit) hii ni roho iliyojifunua kama shimo. Isaya 14:11,15 . tunaona shetani alipoasi akatupwa kwenye hilo shimo ndio maana ya maneno yaliyo katika kitabu cha ufunuo 12:7-9 kumbe kuzimu ipo hapa katika nchi, hapaonekani kwa kuwa lipo katika ulimwengu wa roho. Ufunuo 9:15 , KUZIMU ndio kwenye makao makuu ya shetani , wanakofanyia kazi zao.. (operation centre) ufunuo 17:8 .. kwa hiyo ni muhimu kujua kuzimo ipo angani, baharini na hata kwenye nchi.. ndio maana biblia inataja mara nyingu neon hili wakuu wa anga’
KAZI ZA KUZIMU NA MAUTI.
Kuzimu ndio inayo achilia uovu duniani, inaachilia magonjwa, tabu, dhambi, mateso, balaa,mikosi, ukimwi, kuchanganyikiwa, kuchukiwa na watu, inadhoofisha, inatesa na inaleta uhalibifu.. kwahiyo kuzimu inaleta roho ya uzinzi na uasherati, uovu na dhambi na hizi zote zinamfanya mtu kudhoofika na kuishiwa nguvu. Hapo sasa mauti ndo inakuja pale mtu anapokuwa kwenye comma. KWAHIYO kuzimu kazi yake ni kudhoofisha kwanza.. na ndio maana unaweza muona mtu anaumwa hadi kudhoofika sana lakini huyo mtu hafi.. hii ni kwasababu mashetani ya mauti hayajaanza kufanya kazi..
Hapo mgonjwa anapokuwa dhaifu ndipo sasa mauti inakuja na kufanya kazi yake, ya kumuua . na mauti ikifanikiwa kuutoa uhai basi sasa mauti inatuma mapepo wa kuja kumchukua Yule mtu kama alikuwa mtenda dhambi.. na ndio maana utaona kuwa mtu anapotaka kufa waliowengi utawasikia wanasema maneno kama ‘naona giza’ au msinichukue’ basi ujue wakati huo.
Kuzimu inaleta duniani hata mitindo ya kuvaa.. ili kuingiza tamaa za uzinzi na uasherati.. na unapoona tamaa ya dhambi inaongezeka basi jua unakaribia kufa.. kama ulipangiwa kuishi miaka 80 utajikuta unaishi miaka 40.. kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.
Marko 16 :19-22.. Mtu anapokata roho anachukuliwa na malaika kwenda mbinguni au anachukuliwa na malaika kwenda kuzimu..
NGUZO MBILI ZA KIPINDI CHA SAMSON
SAMSON alikuwa mnadhiri alikuwa na jukumu la kuangamiza wafilisti, lakini wafilisti walimnasa baada ya kudanganywa na mkewe, ILI kutoa siri ya nguvu zake, baada ya kujua wafilisti wakmnyoa nywele , wakamtoboa macho na kumweka asage ngano, mfano huu wa Samson unaonyesha hali ya kanisa ya sasa baada ya kanisa kukosa nguvu, na kudharauriwa Mungu ameanza kulipa nguvu kanisa kama nywele za samason zilipoanza kuota.. Samson alipopata nguvu akajitegemeza kwenye nguzo mbili ambazo jingo linazitegemea. Na akazitikisa hadi jingo lote likaanguka kabisa. Ndivyo kanisa linavyotakiwa kuwaangamiza nguzo za mauti na kuzimu.. ili liweze kurudi kwenye uweza wake na ndio maana ushindi wa Yesu msalabani kimsingi ni ushindi dhidi ya mauti…
Na balozi wa serekali ya Mbinguni
Fahamu mambo machache, yanayokuchosha tofauti na huduma
1. Kazi nyingi kupita kiasi
2. Kuwa mtu wa kukubaliana kila kitu na mkuu wako au bosi wako.
3. Kuhisi umekwama katika ujuzi wako/taaluma yako.
4. Kuwa mlevi wa kazi5. Kulazimishwa katika mazingira yanayokukandamiza. Kuona una majukumu kupita kiasi
6. Kufanya kazi na wateja ambao hawana mwitikio na ushirikiano. Matatizo ya kifamila kama fedha.
7. Mafanikio ya uponyaji.
TIBA YA UCHOVU
1. Jifunze kuweka mipaka.
● Jifunze kuwa na hisia za uchechi-uwe rahisi na unaye weza kukalibiwa kirahisi. Tengeneza mtandao usiwe mpweke, gawa majukumu kwa wegine. Unapokuwa peke yako kimbia kwa kasi lakini kwa muda mfupi.mnapokuwa wengi kimbia taratibu lakini kwa muda mrefu..
2. Uwe na shughuli nyingine mbali na shughuli za kanisa,kama vile michezo,matembezi.
3. Wakati wote tunza akilini mwako lengo yako.
4. Jifunze kuthamini kudhihirisha hisia hasi zako.
5. Hudhuria semina mahali kwingine,katika makanisa mengine na maeneo mengine.
6. Tengeneza tabia ya kupumzika –chukua siku moja kupumzika katika wiki na chukua likizo ndefu.
7. Chukua tabia ya afya njema:kula vizuri,fanya mazoezi,lala vizuri.
JINSI YA KUZIMA HALI YA KUCHOKA
1. Shughulikia mfadhaiko wako kwa kufanya mazoezi ya viungo
● Tumia mazoezi rahisi.
● Andiko maneno rahisi hewani kama vile Jina lako n.k. kwa kutumia mwili waka au mwenendo wa kichwa.
● Chukua siku moja ya kupumzika.
2. Tawala muda wako.-usihairishe mambo,uwe na orodha ya mambo ya kufanya.
3. Gawa majukumu,epuka kujitegemea mwenyewe.
4. Pata uwajibikaji-mthibitishe mtu unayemwamini.
5. Fanyaia kazi nidhamu za kiroho kama vile Maombi,Kusoma Biblia,kufunga,n.k..
tiba ya uchovu ya Huduma
2. Badilisha shughuli-pumzika
3. Badilisha Muda
4. Badilisha Vipaumbele vyako
· Wewe na Mungu-maisha yako binafsi ya Kiroho
· Wewe na Mke wako-maisha yako ya ndoa,hakuna ndoa ,hakuna huduma yako.
· Wewe na watoto wako-familia –Kanisa huanza nyumbani
· Wewe na Huduma.
· Wewe na watu wengine
Dumu katika neno La Mungu
Sababu za Mtumishi kuvunjika moyo katika huduma
Kuna aina mbili za dalili za kuchoka –dalili za ndani na dalili za nje
. DALILI ZA NJE NI PAMOJA NA MAMBO YA FUATAYO
· Kuongezeka kwa shughuli lakini uzalishaji/ufanisi unabaki uleule, ambao unaitwa uwendawazimu insanity-kufanya jambo lilelile kwa muda mrefu na kupata matokeo yale yale. Kuwa na shughuli nyingi si Kiroho.Kimsingi unapaswa kutumia nguvu kidogo tu na kuwa na matokeo makubwa-maarifa ni ya muhimu zaidi ya nguvu na bidii nyingi.
Kuchoka kimwili,kuishiwa nguvu-kuchoka mfululizo ni dalili ya Burn-out,kujiona hupendi kufanya jambo lolote lile.Kupenda kulala tu,kuona kero kuamka hasa alfajiri.
Kutokuwa tayari kujihatarisha au kuthubutu-kukwepa changamoto katika huduma,kukwepa watu na marafiki,kupoteza imani juu yako mwenyewe na kupoteza uwezo wa kukamilisha mambo.
· Kukwazika kirahisi/kukasirishwa na mambo na watu ,hata Mungu mwenyewe kirahisi- Musa na Yeremia ni mfano mzuri –Hesabu 11:11 Yeremiah 20:7,
Kukosa usingizi ,kupoteza hamu ya kula,Kuwa na mawazo mengi,kupenda kuwa pekee yako , “kujificha katika upweke”
Kupooza /stroke,shinikizo la moyo,kipanda uso,kichwa kuuma mara kwa mara
Matatizo ya kuyeyusha chakula,matatizo katika utumbo mkubwa (coronary problem),vidonda ya tumbo/ulcers.
. DALILI ZA NDANI NI PAMOJA NA MAMBO YAFUATAYO:
Kupoteza ujasiri
Kupoteza kujiamini na uthamani wako binafsi
· Kuwa na mtazamo hasi
Kupoteza makusudi- kumwona Mungu ni chanzo cha kushindwa kwako,kujikasirikia mwenyewe kwa kushindwa kufikia malengo
Kuchoka kihisia,depression,mkandamizo
Hatia ya kujiona hufanyi vya kutosha,huna matokeo ya kutosha, na kufikiri pengine ukiongeza bidii nyingi ndipo utaona matokeo,kwa wengine hupelekea kufunga sana mfululizo kuomba sana,kukesha sana,wakifikiri kwa kufanya hivyo kutakuwa na matokeo kinyume chake,hupelekea uchovu zaidi na hakuna matokeo.
Martha complex-kuwa na shughuli nyingi sana na kukosa muda binafsi wa Mungu kukuhudumia
. Kuanza kuwadharau watu ulioitwa kuwapenda na kuwahudumia
. Unaanza kurushu mawazo yako kuchukuliwa na mambo mengine ambayo ungeweza kuyafanya zaidi yakufanya huduma .
. Unajihisi ni kama “mashine ya huduma” hivyo unafanya yale ufanyayo ukiwa na hatia ya kwamba ni Lazima uyafanye badala ya kutenda kwako kutokane na kutembea kwako karibu na Mungu(Mahusiano),kazi ya Bwana Vs Bwana wa Kazi.Juhudi vs Ufanisi.
. Unaanza kufanya maaumzi kulingana na nini ni rahisi kuliko vile unavyojua ndivyo Mungu anakutaka ufanye.
. Unazidi kuwa mkosoaji na kupita kiasi juu ya makanisa,watu,na huduma za watu wengine ambazo unafikiri Mungu anazibariki kuliko huduma yako na wewe
. Hukumbuki lini mara ya mwisho ulifungua Biblia kwaajili kwaajili ya ushirika wako binafsi na Mungu,bali ni kwaajili ya kutafuta Mahubiri na Masomo ya kufundisha Biblia
. Unaanza kuwaona watendakazi wanaotumika pamoja na wewe kama watumishi wako badala yakuwaona kama ni watumishi wa Mungu.
Unatumia kugawa majukumu kama udhuru ya kuwa mvivu,una kwepa majukumu kwa kuwagawia wengine wafanye.
. Hukumbuki mara ya mwisho ni lini ulikuwa na mazungumzo na mke wako ambayo haya husiani na mambo ya kanisa
Hukumbuki mara ya mwisho ni lini ulitumia muda na watoto wako na mkafurahia pamoja.
. Unaanza kutilia mashaka nguvu za Mungu ndani yako na ndani ya maisha ya watu wengine.
Nguvu ya Kusikia
Nguvu ya kusikia
Utangulizi:
CHANZO CHA IMANI
warumi 10:17, “Imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la kristo.” Mambo ya kujifunza ni kuwa imani chanzo chake ni kusikia, tukiishia hapo tunajifunza kitu hapa, tukiangalia kwenye biblia utagundua baada ya neno kusikia kuna alama ya mkato ikimaanisha imani chanzo chake ni kusikia. Kumbe imani yoyote ya kushindwa au ya kushindwa yanatokana na kile unachosikia.
Kama tulivyoona kwenye andiko hapo juu, kuwa imani inaandia kwenye kusikia. “masikio yetu yanaweza kutupelekea katika kuanguka au kuinuka” ni muhimu kujua kila unachosikia kinaleta IMANI ndani ya mtu, ambayo yaweza kuwa nzuri au mbaya kutegemea kile ulichosikia. Na ndio maana , shetani hutumia sana masikio kuwafanya watu wamtumikie yeye.
.1 Uzuri wa kusikia.
Unaponahabari za Mungu, na neno la kristo basi imani na nguvu ya Mungu itaingia kwenye maisha yako. Kwa maana hata wale wakoma walisikia neno kutoka kwa kristo. Na hapo wakapata imani ya kuchukua hatua na baada ya kuchukua hatua ya kuamua kwenda kujionyesha hapo wakapokea utakaso wao.. lakini la kujifunza hapa ni kwamba imani yao imepatikana baada ya kusikia NENO kutoka kwa kristo.
Hatari ya mambo tunayoyasikia.
Ni muhimu kujua kile unachosikia kina leta kesho yako, “maisha unayoishi leo ni matokeo yayale uliyowahi kusikia” na ndio maana shetani anatumia hiyo kukamata na anataka usikie mambo mabaya ili utende mabaya. Na ndio maana ukifuatilia kwenye maisha yako huwezi kukumbuka kama kuna mtu aliyewahi kukufundisha dhambi, lakini unajikuta unatenda kwa kuwa habari za dhambi zimeenea zaidi kuliko taarifa za nuru.
3. MAPENZI YA MUNGU
2 Timotheo 4:7 “nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, imani nimeilinda”. Yohana 10:10 “mwivi haji ili aharibubu,kuua na kuchinya lakini mimi nilikuja ili muwe na uzima tele” kumbe kazi ya Yesu duniani ni bayana nay a shetani ni bayana.. Paulo alisema amemaliza kazi ya kristo. Na ndiomaana neno imani linaingia pale, kwasababu huwezi kutenda kazi ya kristo bila kuwa na imani ya YESU ndani yako. Na imani chanzo chake ni kusikia kumbe unaposikia habari za kristo unajikuta unatenda kazi ya kristo. Na unaposikia habari za upande wa shetani utajikuta unatenda kazi za shetani.
Unalolisikia laweza kukuingiza kwenye laana nau Baraka. Jifunze kusikia neno la Mungu. Nandio maana biblia inasema kwenye kitabu cha 2 wakorintho 10:3-5 “tukiteka nyara kila fikra” kumbe fikri zetu na mawazo yetu ni muhimu yawe katika kumtii Mungu , lakini ili fikra iweze kumtii Mungu ni lazima isikie neno la Mungu. (warumi 10:17)
Hatuwa ya muhimu kwa muongofu
1. Zungumza na Mungu kwa maombi kila siku
(Yohana 15:7)
Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu.
Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.
Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.
Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.
Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.
Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.
Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.
2. Soma Neno la Mungu (Biblia) kila siku
(Matendo ya Mitume 17:11)
Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.
Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini, na wanawake wa Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache.
Lakini Wayahudi wa Thesalonike walipopata habari ya kwamba neno la Mungu linahubiriwa na Paulo hata katika Beroya, wakaenda huko nako wakawachafua na kuwafadhaisha makutano.
Mara hiyo wale ndugu wakampeleka Paulo aende zake mpaka pwani; bali Sila na Timotheo wakasalia huko.
3.Mruhusu Roho Mtakatifu akutawale
(Wagalatia 5:16-25;
Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana.
Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.
Warumi 8:14-17)
Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.
Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;
na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.
Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako
(1Petro 5:7;
huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.
Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.
Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu.
Zekaria 4:6)
Nami nikajibu, nikamwambia yule malaika aliyesema nami, nikasema, Ee Bwana wangu, vitu hivi ni nini?
Ndipo malaika aliyesema nami akajibu, akaniambia, Hujui vitu hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu.
Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi.
Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie.
5. Usiache kukusanyika na kushirikiana na wengine waliompokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wao kama wewe ili uimarike zaid
(Waebrania 10:25)
wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.
Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;
bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.
Mungu akubariki sana msomaji
Balozi wa serekali ya mbinguni
samson na mkewe wanalo neno la kinabii juu yako
kwa msaada zaidi piga 0756 809 209,
Je Unajuwa Kuwa Wewe ni Balozi wa serekali ya Mbinguni
Kwa maana Mungu tumwabuduye kwa roho na kweli katika Injili ya Mwana wake Yesu kristo, naye ni shahidi wetu kwa yale tu yanenayo au tunayoyatenda Amestahili yeye kutukuzwa kupitia maswali
Bwana wetu na Mungu wetu kwa wale wanaomwamini, kuwa yeye ndiye aliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yake vilikuwako, navyo viliumbwa. ujumbe huu unajibiwa katika Jina lile lipitalo majina yote, Jina la Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai, Bwana na Mwokozi wetu. Kwa kuwa majibu ni mengi ninaomba niyafupishe ila ikihitajika kwa urefu zaidi ya hapa nalo linawezekana, pia nitafanya hivyo
UTANGULIZI
• Siri ya Mungu ipo kwa wao wamchao tu, zaburi 25:14
• Kilichozwaliwa kwa mwili ni mwali na kilicho zaliwa kwa Roho ni Roho
• Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu Mithali 22:1
Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyenzi ……………….Kwa siku NYINGI nitamshibisha, nami nitamwonyesha wokovu wangu” (Zaburi 91:16)“Ili wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo’ (Wakolosai 2:2).
Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo” (2Wakorintho 5:20)
Kuwa mjumbe kwa ajili ya Kristo maana yake nini? Tunatakiwa tuwe wajumbe kwa ajili ya Kristo juu ya nini? Na kwa namna gani? Na kwa nani? Na kwa wakati gani? Neno la Kiingereza lililotafsiriwa kuwa mjumbe ni ‘Ambassador” Na neno zuri linalotoa picha nzuri ya maana ya ‘Ambassador’ ni neno Balozi. Balozi ni mjumbe na mjumbe ni balozi
Neno balozi na neno mjumbe lina maana sawa lakini kwa jinsi tunavyoyatumia maneno haya, utafikiria neno balozi lina uzito zaidi kuliko neno mjumbe.
Kwa hiyo tunaweza kusema: “ Basi tu mabalozi (wajumbe) kwa ajili ya Kristo” Katika nchi ya Tanzania tuna mabalozi wa nyumba kumikumi, ambao pia wanajulikana kuwa ni wajumbe wa nyumba kumikumi. Pia tuna mabalozi walioko nchi za nje waliotumwa kuiwakilisha nchi hii katika maswala na majukumu mbalimbali.
Sasa na tuliangalie katika ngazi ya kitaifa. Balozi ni mjumbe au mwakilishi wa nchi moja katika nchi nyingine. Kwa mfano: Balozi wa Tanzania nchini Kenya; kwanza ni raia wa Tanzania anayefahamu vizuri msimamo wa nchi hii katika maswala mbalimbali. Yuko Kenya kwa ajili ya Serikali ya Tanzania na raia wa Tanzania.
Yeye ndiye msemaji mkuu wa Serikali ya Tanzania nchini Kenya. Serikali ya Tanzania inapopeleka ujumbe kwa serikali ya Kenya, inapitia kwa balozi wake aliyeko Kenya.
Balozi huyo ni picha kamili ya Watanzania kwa watu wa Kenya, katika maneno yake na mwenendo wake. Yeye ni mlinzi wa hadhi ya Tanzania nchini Kenya. Na makazi yake ni nchini Kenya.
Balozi ni mjumbe aliyetumwa na mtu mwingine. Balozi wa Tanzania katika umoja wa Mataifa, ametumwa na nchi yetu, awe msemaji na mtetezi wa mawazo ya Tanzania katika maswala mbalimbali ya kimataifa. Balozi hasemi mawazo yake mwenyewe. Balozi anasema tu kile alichotumwa kusema na anafanya kile tu ambacho ametumwa kufanya.
Tunasisitiza hivi, BALOZI HASEMI MAWAZO YAKE MWENYEWE: BALOZI ANASEMA TU KILE ALICHOTUMWA KUSEMA, NA ANAFANYA KILE TU AMBACHO AMETUMWA KUFANYA.Na kitu cha kwanza anachofanya anapofika katika nchi aliyotumwa ni kutoa vitambulisho vilivyo na muhuri na sahihi ya kiongozi wa nchi anayotoka.
Biblia inatuambia kuwa sisi ni mabalozi kwa ajili ya Kristo hapa duniani; sisi ni wajumbe tuliotumwa kwa ajili ya Kristo hapa duniani. Ndiyo maana Paulo alisema kuishi kwake ni Kristo. Wewe ni mjumbe wa Kristo na kwa ajili ya Kristo hapa duniani. Ikiwa wewe ni Mjumbe, basi wewe ni balozi wa Kristo na kwa ajili ya Kristo.
Kumbuka kuwa balozi hasemi mawazo yake mwenyewe. Wewe ni balozi wa Kristo hapa duniani kwa hiyo kutokana na wadhifa huo uliopewa unatakiwa usiseme mawazo yako, wala kufanya mambo yako hapa duniani; bali USEME MAWAZO YA KRISTO NA MANENO YAKE; NA UFANYE YAKE TU ALIYOKUTUMA KUFANYA.
Lakini ni wazi kwamba huwezi kusema mawazo na maneno ya Kristo wakati huyafahamu. Na ikiwa hapa duniani wewe ni balozi basi, inamaanisha hapa duniani si kwako. Na ikiwa hapa duniani si kwako, na wala wewe si mwenyeji wa hapa duniani; basi unatokea wapi na uenyeji (uraia) wako ni wa wapi?
Wewe ni mwenyeji wa wapi? Hili swali ni muhimu sana ambalo ni budi ufahamu jibu lake katika roho yako. Bila kufahamu ulikotoka utaifanye kazi ya ubalozi au ya kuwa mjumbe wa Kristo. Balozi (Mjumbe) yeyote anajua alikotoka; anafahamu uraia wake ni wa wapi. Je wewe unafahamu kuwa wewe ni balozi wa nchi gani ukiwa hapa duniani?
ninakazia swali hili kwa sababu ujumbe utakokuwa unatoa; au mahubiri unayofanya mbele za watu; na matendo yako yanategemea sasa mahali gani umetoka kiroho na kimazingira.
Kuna wengine ni mabalozi wa miili yao wenywe. Wanahubiri kwa sababu ya mwili ili wapate mishahara yao na kuvaa. Wao wanaona kuwa kuhubiri ni kama kazi nyingine ya kuajiriwa.
Lakini la kushangaza ni kwamba wote wanasema ni mabalozi wa Kristo, wajumbe wa neno la Injili. Na hii si kweli. Muda umefika ambapo Roho wa Mungu amekududia kuliweka wazi hili. Mabalozi wa Kristo wawe wazi; mabalozi wa madhehebu wawe wazi, na mabalozi wa miili yao wawe wazi.
Muda umefika wa kufichuliwa watu wote wanaojiita mabalozi wa Kristo, wameokoka, na ni wakristo?, watumishi wa Kanisa kumbe ni mbwa mwitu wakali wanaowaendea watu wakiwa wamevaa mavazi ya Kondoo (Mathayo 7:15).
Muda umefika ambao watu wote wanokaa karibu na wewe, vitu vyote vinavyokuzunguka, mahali unapopita, watu wote hao wanaokuzunguka wajue, kwamba wanajua KUWA WEWE NI BALOZI WA KRISTO MJUMBE KWA AJILI YA KRISTO!Kweli
UTASEMA MAWAZO NA MANENO YA KRISTO. NA UTAFANYA MATENDO YA KRISTO KWA AJILI YA KRISTO MAHALI POPOTE ULIPO NA UTAKAPOKUWA DUNIANI:
Kuishi kwako hapa duniani ni Kristo na kufa kwako ni faida! Mtume Paulo alipoandika kuwa “Basi tu wajumbe (Mabalozi) kwa ajili ya Kristo,” alikuwa anamhusisha kila mtu ambaye amefanyika kuwa kiumbe kipya ndani ya Kristo. Ikiwa wewe ni kiumbe kipya ndani ya Kristo, basi wewe ni mjumbe(balozi) kwa ajili ya Kristo.
Ikiwa basi wote waliozaliwa mara ya pili, walio viumbe vipya ndani ya Kristo (waliookoka) wanatakiwa kuwa mabalozi wa Kristo; mbona basi ubalozi wao hauonekani ukifanya kazi? Ubalozi hauonekani katika maisha yako, kwa sababu hujafuatilia katika Biblia kujua neno linasemaje juu ya hili.
Ni Duwa yangu na maombi kila atakayepata ujumbe huu akubali kwanzia leo yeye awe Balozi wa serekali ya mbinguni Baada ya kujitabuwa lati tingefahamu uzito wa wadhifa huu wa kuwa mjumbe wa Kristo hapa duniani, hali ya mambo isingekuwa kama ilivyo hivi sasa ya kukata tamaa – iliyojaa katika mioyo ya yetu.na kujiweka mbali na Mungu kiasi hicho
Laiti basi wewe ungejua uzito wa wadhifa huu wa kuwa mjumbe wa Kristo mahali ulipo ikiwa in nyumbani, kazini, safarini, kanisani, sokoni, hali ya mambo isingekuwa kama unavyoiona sasa. Nchi yetu inaharibika kwakuwa watu wameyaacha majukumu yao wakatamani ya wengine wasiyoyaweza je tunakwenda wapi,Hoko?
Ubalozi uzalendo uraia wa mbinguni
Mtu yeyote Yule aliyemwamini kristo kama Bwana na muokozi wa maisha yake yeye ni raia wa mbinguni. Na mzalendo wa Mbinguni kwa mjibu wa maandiko matakatifu,
“Basi tangu sasa ninyi si wageni wala Wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu” (Waefeso 2:19).
Yesu Kristo alipokuwa akituombea alisema:
“Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa WAO SI WA ULIMWENGU, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule muovu. Wao SI WA ULIMWENGU KAMA MIMI NISIVYO WA ULIMWENGU. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo NILIWATUMA HAO ULIMWENGUNI (Yohana 17:4-18)
Weka jambo ili katika moyo wako. Watu wa Kristo si wa ulimwengu huu, bali ni wenyeji wa mbinguni. Watu wa Kristo wako hapa ulimwenguni kwa sababu Kristo amewatuma kufanya kazi muhimu. Kumbuka upo hapa duniani kwa kuwa kuna KAZI ambayo KRISTO amekupa uifanye kabla ya kurudi nyumbani kwetu MBINGINU.kama huitambui leo Roho mtakatifu kupitia Balozi wa Serekali ya Mbinguni ameamua utambuwe sasa, ila kwa msaada zaidi piga simu yangu ya mkono au ya meza Ext;1961/ 0756 809 209, kwa maswali zaidi na msaada,niko tayari usiku na mchana 24 kwa siku 7 za juma hakuna aliyechelewa kuaza kazi ya ubalozi anza sasa kama jana hukufanya
Balozi wa serekali ya mbinguni
(Samson)
Mke wa kuwoa- Sifa zake
Na Balozi samson mboya
Unapoongelea mke fahamu yakuwa huongelei habari ya mwanamke kwakuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya mke na mwanamke,
Tofauti hiyo
1:Mwanamke anaweza kuwa yeyote yule aliye na jinsia ya kike
: Mke ni yule aliyeandaliwa Na Mungu maalumu kwaajili ya mtu fulani kuishi naye maisha yake yote ya hapa Duniani Kitabu cha mithali 31 kuanzia msitari wa 10 hadi 31 kimeelezea sifa mbalimbali za mke mwema, tuangalie kwa uchache sifa hizo kwa kuzichambua katika maeneo tofauti.
1. Imani
Mithali 31:26, 29, 30
Mke mwema anayashika na kuyafanyia kazi maneno ya Mungu na ni mtu ambaye anamtumikia Mungu kwa moyo wake wote na akili yake yote. Anatafuta makusudi ya Mungu katika maisha yake na kuyafuata. Zaburi 119;15
2. Ndoa
Mithali 31:11-12, 23, 28
Mke mwema humuheshimu mume wake na anahakikisha anamtendea mambo mema siku zote za maisha yake. Ni wa kuaminika na msaidizi kwa mume wake. Efeso 5:22-24, 1Petro 3
3. Malezi
Mithali 31: 26, 28
Mke mwema anawafundisha watoto wake njia za Mungu na pia anawatunza kwa upendo. Huwafundisha kwa hekima na kuwaelekeza njia iwapasayo kuiendea. Mithali 22:6
4. Huduma
Mithali 31:12-15, 17, 20
Mke mwema anamhudumia mume wake na familia yake yote kwa ukarimu na upendo. Anahakikisha wanapata chakula kilicho bora na chenye afya. Ni mtu mwenye huruma na ukarimu.
5. Mali
Mithali 31:14, 16, 18
Mke mwema anatafuta kwanza ushauri wa mumewe kabla ya kutumia fedha na pia anafanya manunuzi kwa hekima. Ni muangalifu kununua bidhaa zenye ubora kulingana na mahitaji ya familia yake.Efeso 5:23
6. Nyumba
Mithali 31:15, 20-22, 27
Mke mwema ni mtu anayeifanya nyumba iwe mahali pa kuishi. Anatengeneza mazingira ya kuvutia kwa familia yake na wageni wote na anawahudumia watu wake wote kwa ukarimu. 1pet 4:9, Ebrania 13:2
7. Muda
Mithali 31:13, 19, 27
Hutumia muda wake vizuri na kuhakikisha anakamilisha kazi zake za kila siku. Kamwe hapotezi muda katika kufanya mambo ambayo hayampendezi Mungu na yasiyo na faida.
8. Uzuri / Urembo
Mithali 31:10, 21-22, 24
Ni mrembo na mwenye thamani, ana uzuri wa ndani unatoka kwa Yesu Kristo. Anatumia ubunifu wake na utanashati wake kuleta uzuri katika maisha yake na ya watu wake.
Mungu atusaidie ili maisha yetu yaonyeshe kweli tunamjua na kumwamini yeye.
Kwa mafundisho zaidi endelea kufuatilia
(baloziwamungu) au piga simu no kwa msaada
0756 809 209/0786608801
Kwa nini maombi yako hayajibiwi?
ni vema ukafahamu leo kwanini maombe yako hayajibiwi kila mmoja wetu anatamani akifanya maombi majibu ayapate siku hiyo hiyo au kesho yake, kwanza faaha kuwa Mungu hafikirii kama wewe unavyo fikiri yeye anakuwazia mambo makubwa sana,na mazuri, ila katika hayo unayoyaomba Mungu akijibu au asijibu, Bado ni Mungu na usimtafute mtu wa kumlaumu,
Sasa kuna hatua chache hapa ambazo napenda tushirikiane na wewe,
(1) hakikisha unajitakasa tafakari kwanza kabla hujaaza kuomba ili utambuwe ni wapi umeishi kinyume na mapenzi ya Mungu kisha omba toba ya kumaanisha toka moyoni naye Mungu atakusamehe, Isaya 59:1
1 Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
3 Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong'ona ubaya.
4 Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.
moja ya vizuizi vya maombi ya muombaji ni Dhambi,
(2) Baada ya toba mkaribish Warumi 8:26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
Roho mtakatifu akusaidie kuomba,
(3) Mathayo 6:12 jambo la tatu jitahidi kusamehe wale wote waliokukosea bila kuchukulia kosa ulilofanyiwa,
12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
Nenda sasa kafanya maombi nawe utayaona majibu,
kwa ushahuri na maombezi kutoka kwa balozi piga simu,
UMEFANYA MAAMUZI MAZURI SANA
MWOKOZI WAKO.
Mpendwa, nataka ujue kwamba, Mungu amefanya mambo mengi makubwa katika maisha yako, tangu sasa/saa/siku ile ulipompokea Yesu, kuwa Bwana na Mwokozi na Mwokozi wako. Ni muhimu uelewe kwamba, wewe si yule wa zamani tena. Sahau yaliyopita, kwasababu umefanyika kiumbe kipya. (2 kor 5:17)
Yafuatayo ni baadhi ya mambo yaliyotokea kwako tangu ulipofanya uamuzi huu mzuri na wa busara, wa kumpokea Yesu Kristo, kuwa Bwana wako na Mwokozi wa maisha yako.
KWANZA: UMEFANYIKA MWANA WA MUNGU
Umefanyika mwana wa Mungu, kwasababu umempokea Yesu Kristo na kuliamini Jina lake; Kwasababu Biblia inaema “Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake (Yoh 1:12) … Roho (Mtakatifu) mwenyewe, hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu…” (Rum 8:16)
Tangu sasa, wewe ni mmoja wa wana-familia ya Mungu. Nasi tunakukaribisaha kwa upendo wa Kristo. Karibu sana, Baba (Mungu) na sisi tumefurahi kukuona umerudi nyumbani. This is where you belong. We missed you so much. Karibu!
Ni rahisi kabisa Kuokoka kama uko Tayari,
HATUA YA KWANZA; Tambua kuwa wewe ni mwenyedhambi na Utubu,Makosa yako hatakuto kumwamini Mungu yaani kutokumkiri ni Dhambi ya kwanza, anza na hiyo tumbu kabisa
DHAMBI ZAKO, KWA KUMAANISHA KUZIACHA.KABISA
“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele” (Rum 3:23). “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” (Mdo 2:38)
HATUA YA PILI; MWANINI NA KUMPOKEA YESU MOYONI MWAKO. TOA
MAISHA YAKO KWAKE, AWE BWANA NA MWOKOZI WAKO.
Yule mlinzi wa gereza akamwambia Paulo na Sila “Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako” (Mdo 16:30-31).
“Kwasababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri, hata KUPATA WOKOVU. (Rum 10:9-10)
HATUA YA TATU: ISHI MAISHA YA WOKOVU, MAISHA SAFI YA KUMPENDEZA MUNGU NA KUZISHIKA AMRI ZAKE (NENO LAKE)
“nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi… Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye (Mungu) ikiwa tunashika amri zake. Lakini Yeye asema neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli, katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake….” (1Yoh 2:1-6). Kwahiyo sasa, kwakuwa awali hukufahamu na kutambuwa kilichokupasa kufanya anza sasa maisha mapya ndani ya Yesu. Ukifanya hivyo maisha yako hayatabaki kama yalivyo hivi sasa,
“…mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya”. (2Kor 5:17) Jitenge na uovu wote na Usiishi katika maisha ya dhambi tena.
Josh 1:8 Na Rum 6:1-23.
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.
Unafahamu kuwa kuna mauti ya pili, unajua namna ya kuiepuka Okoka leo,
kuingia uzimani”. Ina maana AMEOKOKA kutoka mautini (jehanum). Jehanum ndio mauti ya pili. (Ufu 20:14-15)
Watu wengi wnadhani kutokunywa pombe, kutovuta sigara, kutofanya zinaa, kutoiba, n.k ndio kuokoka na hukumu ya Mungu. Wengi wanadhani, kwenda kanisani, kuimba kwaya, kuhubiri, kuwa mzee wa kanisa au kiongozi wa kikundi, n.k ndio kuokoka na hukumu ya Mungu. Kuna wokovu halisi na matendo au maisha ya wokovu. Watu wengi wanaishi maisha ya wokovu, lakini kwa uhalisi, hawajaokoka bado, hawajampa Yesu mioyo yao na maisha yao yote
Kushika sheria za dini na kuishi maisha ya wokovu, siko kunakompendeza Mungu, kama huyo mtu hajampokea Yesu na kumwamini kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Yesu alisema hivi kwa Mungu Baba,
“ Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yoh 17:3). Hatuokoki na hukumu ya Mungu kwa kushika sheria, bali kwa kuipokea neema ya wokovu kwa kumwamini Yesu Kristo. “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haitokani na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu (zawadi). Wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu (Efe 2;8-9)
Kushika sheria za dini na kuishi maisha ya wokovu, siko kunakompendeza Mungu, kama huyo mtu hajampokea Yesu kristo au kumwamini kama Bwana na mwokozi wa maisha yake.
“hali tukijua ya kuwa, mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; Sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria.
Maana kwa matendo ya sheria, hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki” (Gal 2:16; Gal 3:7-14) Kuna wokovu halisi na matendo au maisha ya wokovu. Watu wengi wanaishi maisha ya wokovu, lakini kwa uhalisi, hawajaokoka bado, hawajampa Yesu mioyo yao na maisha yao yote,
Kuna habari ya mtu aliyeishi maisha kama hayo hapa duniani Biblia inasema aliye shika sheria, aliyedumu katika sala, aliyefunga na kuomba, aliyetoa sadaka nyingi kwa watu maskini, n.k lakini alikuwa hajafanya hatua muhimu kuliko zote ya kumwamini na kumpokea Yesu Kristo,yaani (kuokoka) ilia pate uzima wa milele na kuokolewa. Mtu huyo jina lake Aliitwa Kornelio. Matendo ya Mitume 10:1-8, 23-48.
Mungu akamhurumia kuwa, japo amekuwa mwaminifu kushika sheria na kuishi maisha ya kumcha Mungu, lakini kwasababu hajamjua Yesu bado, asingeokoka na hukumu ya milele, kwa maana hana uzima wa milele. Mungu akamtuma malaika kumwambia Kornelio, amfuate Petro, naye atamweleza cha kufanya. Ndipo Petro akaja na akamweleza habari za Yesu, Kornelio na familia yake, wote wakamwamini na kumpokea Yesu. Wakapata wokovu halisi (uzima wa milele). Baada ya hapo, maisha ya wokovu ndipo yanakuwa na maana.
Kushika sheria za dini na kuishi maisha ya wokovu, siko kunakompendeza Mungu, kama huyo mtu hajampokea Yesu na kumwamini kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Inawezekana nawe umekuwa mcha Mungu kama Kornelio, lakini hujampokea Yesu moyoni na kumkiri. Mpokee sasa!
Je unastahili kuwa Tajiri Ndiyo hunasababu ya kuteswa na umasikini,na kuaibika kiasi hicho,
Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake. Na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka. Na kila kitu ulichonacho kitakapoongezeka; Basi hapo moyo wako usiinuke ukamsahau Bwana Mungu wako,
aliyekutoa katika nchi ya Misri,(utumwa) katika nyumba ya utumwa … hapo usiseme moyoni mwako, nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu, ndio ulionipatia utajiri huo; Bali utamkumbuka Bwana Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri, ili alifanye imara agano lake … (Kumb 8:12-18)
Lakini hawatakuwepo masikini kwenu, kwakuwa Bwana atakubariki kweli, katika nchi akupayo Bwana Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako. (Kumb 15:4)ukisha kombolewa ninaamini Maisha yako yanaanza kubadilika ile siku ya kwanza ulipokubali kumkiri kristo Yesu,
Naye Abrahamu alikuwa tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha na kwa dhahabu (Mwa 13:2) naomba ufahamu utajiri unaoongelewa hatadondoka kama maemba juu ya mti, bali bidii ya kumtumikia Mungu na ya kujishuguliza na kazi halali za mikono yako, ili baraka zipitie mikononi mwako, ukweli swala hili limewasumbuwa watu wengu sana, na si washirika pekeyao, bali hata kwa baadhi ya watumishi, wachungaji,wainjilisti,mitume na manabii, kisingizio kwamba wanakulia madhabauni, wengi Tunatafsiri tunavyo taka kwa maslahi yetu sisi wenyewe bali si kwaajili ya vile bwana anavyo taka, Mungu ni wautaratibu, nitaifafanuwa vizuri sana kitabu kijacho maana hayo nayo nimafundisho yake, niendelee kwanza na hili la shule ya awali, Linaloanza na Uwokovu nini na fida zake,
Maana mmejua Neema ya Bwana wetu, Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa masikini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajri. Ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake. (2Kor 8:9) … mkitajirishwa katika vitu vyote, mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. (2Kor 9:11) …
Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. (Fil 4:19) … Maana yeye yule ni Bwana wa yote, mwenye utajiri kwa wote wamuitao; kwa kuwa, kila atakayeliitia jina la Bwana ataokoka. (Rum 10:12)
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi, mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi. (Malaki 3:10 – 12)
Thawabu ya unyenyekevu, ambao ni kumcha Bwana, ni utajiri na heshima, nayo ni uzima.
(Mith 22:4)
Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya dunia; na baraka hizo zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani, utabarikiwa na uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo. Maongeo ya Ngombe wako, na wadogo wa kondoo zako: utabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.
Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako watakutokea kwa njia moja; lakini watakimbia mbele kwa njia saba. Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubariki katika nchi akupayo Bwana wako Mungu wako.
Bwana atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakapoishika maagizo ya Bwana Mungu wako na kutembea katika njia zako na mataifa yote ya dunia watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako. Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako, na uzao wa nchi yako, kama Bwana alivyowaapia baba zako kwamba atakupa.
Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri, nayo ni Mbingu , kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubariki kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi wala hutokopa wewe. Bwana atakufanya uwe kichwa wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini;
utakapo yasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo,kuyaangalia na kuyafanya; msipokengeuka katika maneno niwaamuruo leo kwa lolote, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia. (Kumb 28:1-14)
Damu ya msalaba iliyoondoa dhambi, ndiyo iliyoondoa umasikini pia, Yatupasa kuuona umasikini kama tunavyoiona dhambi. Umaskini ni matokeo ya anguko la mwanadamu katika dhambi. Tukiisha okolewa katika dhambi, yatupasa kuokolewa katika umasikini pia.
Utajiri ni matunda ya msalaba kama ilivyo wokovu. Yatupasa kuchukia umasikini kama tunavyochukia dhambi. Kifo cha Yesu, kitakuwa hakina maana kamili, kama tutaokolewa katika dhambi, halafu tubaki maskini katika mwili pia, wakati Yesu aliyefia dhambi, ndiye aliyefia umasikini pia. Msalaba ulifanya vyote, yaaani uliondoa dhambi na umasikini pia.
Biblia inasema; “Maana mmejua Neema ya Bwana wetu, Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa masikini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri. Ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake. (2Kor 8:9) … mkitajirishwa katika vitu vyote, mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. (2Kor 9:11)
Kwanini magonjwa ya kuonee kiasi hicho? ikiwa kunatiba
Nanyi mtamtumikia Bwana Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako na maji yako. Nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. (Kut 23:25) … Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote, wala hatatia juu yako maradhi yeyote, mabaya uyajuayo …” (Kumb 7:15)
Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo, akawatoa pepo kwa jina lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi (wagonjwa). Ili litimie lile neno lililonenwa na Nabii Isaya akisema; “Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu na kuyachukuwa magonjwa yetu.” (Math 8:16-17) “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote, na udhaifu wa kila aina”. (Math 9:35) “ … Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu; wawatoe na kupoza, magonjwa yote na udhaifu wa kila aina (Math 10:1)
Yeye mwenyewe alizichukuwa dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; Na kwa kupigwa kwake mliponywa (1Pet 2:24) “Hakika ameyachukuwa masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu …. Bali alijeruliwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu. Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake; Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. (Isa 53:4 -5)
sipingi kwa mtu aliyeokoka kuuguwa, ilakama mwana wa Mungu Fahamu kuwa hustahili kukaa na magonjwa kwakuwa tayari msalaba ulichukuwa madhaifuna magonywa yote,, na ukiona kuwa imani yako nindogo au hujamwamini kristo kuwa bwana na mwokozi wa maisha yako
Ushahuri wangu kata shahuri sasa, ndipo udai uponyaji wa msalabani, vinginevyo kama hutaki kupa yesu krsto maisha ukiuguwa nenda hospitali bibilia haimzuwii mtu kwenda hosipitali, bali inadhihirisha uponyaji wa bure unaotokana na Msalaba,
Damu ya Msalaba iliyoondoa dhambi, ndiyo iliyoondoa magonywa pia. Yatupasa kuyaona magonjwa kama tunavyoiona dhambi. Hatupaswi kuyaona kuwa ni sehemu ya maisha yetu.
Magonjwa ni matokeo ya anguko la mwanadamu katika dhambi. Tukiisha okolewa toka dhambini, yatupasa kuokolewa kutoka katika magonjwa pia. Afya njema ni matunda ya msalaba kama ilivyo wokovu.
Tunatakiwa kuchukia magonjwa kama tunavyochukia dhambi, kwasababu yote haya, ni kazi za shetani. Yatupasa kuzikataa na kuzivunja katika maisha yetu. Kifo cha Yesu, kitakuwa hakina maana kamili, kama tutaokolewa katika dhambi, halafu tubaki katika magonjwa pia,
wakati Yesu aliifia dhambi, ndiye aliyefia magonjwa pia. Msalaba ulifanya vyote, uliondoa dhambi na magonjwa pia. “Mwenyewe aliutwa udhaifu wetu na kuyachukuwa magonjwa yetu.” (Math 8:16-17)
Kupona kwako na Jehanamu ni Kuokoka,
“Kwahiyo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji ikaangamia, lakini mbingu za sasa na nchi, zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na kuangamia kwao wanadamu wasio mcha Mungu.
Lakini wapenzi, msilisahau neno hili … Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba. Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwizi; katika siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea..
Basi kwakuwa vitu hivi vyota vitafumuliwa, hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani? Katika mwenendo mtakatifu na utauwa! Mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo, mbingu zitafumuliwa na zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka. Lakini kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake”. 2 Pet 3:6-13
“Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, nayeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake;
Na mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadri ya matendo yake mauti za kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Naiwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima alitupwa katika lile ziwa la moto.”
Ufu 20:11-15 “Amini, amini nawaambia, yeye asikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna na uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mauti kuingia uzimani”. (Yoh 5:24) Pia Lu 10:20; Fil 4:3; 1Yoh 3:14; Rum 5:6-9;
KWA NINI UOKOKE?
“Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba, na Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu, iliyopo sasa. Gal 1:3-4
“Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. Nilipokuwapo pamoja nao,
mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmoja wapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie. Na sasa naja kwako; ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao. Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umechukia; kwa kuwa wao si waulimwengu, kama mimi nisivyo na ulimwengu. Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; basi uwalinde na yule muovu. Wao sio wa ulimwengu, kama mimi nisivyo waulimwengu. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndio kweli kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami hivyohivyo naliwatuma hao ulimwenguni. Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli”. Yoh 17:11-19 (14-16)
Yoh 8:21-24 (23); 1Kor 5:9-11; Rum 12:1-2
Torati inasema nini juu ya Kuokoka?(Uwokovu)
“Fahamuni basi, yakuwa wale walio na imani, hao ndio wana wa Ibrahim. Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahim habari njema zamani, kusema, katika wewe mataifa watabarikiwa. Basi hao walio na imani hubarikiwa pamoja na Ibrahim aliyekuwa mwenye imani. Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana maana imeandikwa amelaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati, ayafanye.
Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu mwenye haki ataishi kwa imani. Na torati haikuja kwa imani, bali ,ayatendaye hayo, ataishi katika hayo. Kristo alitukomboa katika laana ya Torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu;
maana imeandikwa , amelaaniwa kila mtu aangikwae juu ya msalaba; ili kwamba baraka ya Ibrahim iwafikirie mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya roho kwa njia ya imani”. (Gal 3:7-14, 23-29).
“Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki. (Rum 10:4) Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka”. (Ebr 8:13)
Basi twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria tena,…
Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au Sabato; ( Rum 3:28; Kol 2:16)
Pia Mdo 15:1-10-29; Gal 2:16; Rum 8:3; Rum 7:12,14-16; Rum 8:1-4; Yer 31:31-34 mimi ninaandika muongozo, mengi
maandiko Matakatifu yanathibitisha, Yote ila kama una swali na ungependa kuuliza ninakushahuri ujiulize au uliza kwakutaka kumwelewa kristo zaidi na kazi zake,
na siyo kupinga au kubishana na wengine, angalizo kitabu hiki hakitowi nafasi kwaajili ya malumbano au mabishano,ya Dini au mafundisho ya chuo chochote bali ni kwaajili ya kuwasaidia wale wote wenye nia ya kutaka kuwa wanafunzi wazuri wa Yesu kristo au walimu wazuri, kama unapenda au unataka kubishania Maneno matakatifu, basi kitabu hiki hakiwezi kukusaidia, kabisa
Nini maana ya kuokoka?(wokovu)
MAANA YA WOKOVU: kila mmoja amekuwa na jibu lake kuhusiana na swali hili, kile kilichotupelekea kujibu tumewahi kukutana na swali hili mara nyingi sana katika masha yetu, ni tukafahamu swali hili limewavuruga wengi, sasa hebu tusome majibu yanayojibiwa na neno la Mungu, yaani Bibilia, na ndugu msomaji fahamu ya kwamba ukishamaliza kumkiri kristo kuwa kama bwana na muokozi wa Maisha yako basi, utaoko,
“Kwasababu ukimkiri Yesu Kristo kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa mtu hukiri hata KUPATA WOKOVU”. (Rum 10:9-10.)
Baada ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako, ni muhimu sana kupata mafundisho ya awali, yatakayokusaidia kujua kwa hakika, maana ya KUOKOKA au WOKOVU; “ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.” (Efe 4:14)
Ndio maana Yesu alisema, tukishawahubiri na kuwasaidia kuokoka, tuwafundishe yote! “Yesu akaja kwao akasema nao, akawaambia, nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na mkiwafundisha kuyashika yale yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote hadi ukamilifu wa dahari”. (Math 28:18-20).
“Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara katika imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani”. (Kol 2:6-7)
“Wakawa wakidumu katika fundisho la Mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali” (Mdo 2:42)
“Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu, lakini kwa upole na kwa hofu” (1Pet 3:15)
Watu wengi wamechanganya sana maana halisi ya neno “kuokoka”. Unaweza kupewa tafsiri nyingi na watu, juu ya neno “kuokoka”. Wengine hudhani kuokoka ni dini au dhehebu Fulani la “walokole”. Wengi hudhani wokovu ni maisha Fulani ya kujinyima raha na kujitenga na jamii.
Wengi hudhani wokovu ni maisha duni na ya umasikini au kutokuwa na mali za kifahari. Ndani ya fikra za watu, kuna tafsiri nyingi sana tofauti juu ya “kuokoka” na hizo tafsiri nyingi ni mitazamo tu ya mwanadamu kumtafuta Mungu na hajampata. Unaweza ukaangalia tafsiri nyingine iliyorahisishwa kabisa, kukupa wewe msomaji kuelewa maana halisi ya maana ya Kuokoka
NINI MAANA YA KUOKOKA?
KUOKOKA ni lugha ya kawaida kabisa, yenye maana ya;
Kunusurika, kusalimika, kupona, kukombolewa, kufunguliwa au kutoka katika janga au hatari fulani. Ambavyo jamii yetu maneno haya tunayatumia sana,
Mfano:- kwa kila neno nililoliorodhasha hapo,
- Kunusurika; Paulo aliposafiri mashuani pamoja na watu wengine mia mbili na sabini na sita, alisema;“safari hii itakuwa na madhara na hasara nyingi, si ya shehena na merikebu tu, ila na ya maisha yetu pia … baada ya muda mchache, ukavuma upepo wa nguvu wa namna ya tufani … na kwa maana tulikuwa tukipigwa sana na ile tufani, siku ya pili yake, wakaanza kuitupa shehena baharini. Siku ya tatu wakatupa vyombo vya merikebu kwa mikono yao wenyewe. Jua wala nyota havikuonekana kwa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika,
basi tukakata tamaa ya kuokoka … na baharia walipotaka kukimbia na kuiacha merikebu … Paulo akawaambia akida na askari, hawa wasipokaa ndani ya merikebu, hamtaweza kuokoka … Shauri la askari lilikuwa kuwauwa wafungwa, mtu asiogelee na kukimbia. Bali akida akitaka kumponya Paulo, akawazuia wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea, wajitupe kwanza baharini, wafike nchi kavu … na hivyo watu wote wakapata kuifikilia nchi kavu salama. Tulipokwisha kuokoka, ndipo tulipojua ya kuwa kisiwa kile chaitwa Melita”. (Mdo 27: 1-44. 28:1)
Hivyo tunaona “KUOKOKA” katika mistari hii, imetumika kama “KUNUSURIKA”.
- Kupona; Wayahudi walimdhihaki Yesu , “Jiponye nafsi yako, ushuke msalabani. ( Mk 15:30)
Sisi je, tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kasha ukadhibitishwa kwetu na wale waliosikia. (Ebr 2:3)
“KUOKOKA” katika mistari hii imetumika kama “KUPONA”.
“Na niseme nini tena? Maana wakati usingetosha kuleta habari za Gideoni, na Baraka, na Samsoni, na Yefta, na Daudi, na Samweli, na za Manabii; Ambao kwa imani, walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga.
- KUOKOKA katika mistari hii, imetumika kama KUPONA, KUSALIMIKA AU KUNUSURIKA!
- Kusalimika; Wakati Mungu anaangamiza dunia kwa maji ya gharika, Biblia inasema;
“Wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu mjumbe wa haki na watu
wengine saba, hapo alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa wasio mcha Mungu. Tena
akaihikumu miji ya sodoma na Ghomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya
akaifanya iwe ishara, kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya hayo.
Akamwokoa Lutu, yule mwenye haki, aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa ufisadi wa hao wahalifu. (2Pet 2:5-7)
“Hapa KUOKOKA” imetumika kama “KUSALIMIKA” kutoka katika janga la gharika na moto.
- Kufunguliwa au Kukombolewa;
Herode alipomtia Petro gerezani ili amuuwe, Biblia inasema;
“Panapo majira yale yale, herode mfalme akanyoosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa. Akamuuwa Yakobo ndugu yake Yohana kwa upanga. Na akiona yakuwa imewapendeza Wayahudi, akaendelea, akamshika na Petro … akamweka gerezani, akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde,
Akitaka baada ya Pasaka, kumtoa na kumweka mbele ya watu. Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa lilikuwa likimwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake. Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule, Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, alikuwa amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza. Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi! Minyororo yake ikamwanguka mikononi. Malaika akamwambia, jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo.
Kisha akamwambia, jivike nguo yako, ukanifuate. Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua yakuwa ni kweli, yaliyofanywa na malaika. Bali alidhani kwamba anaona maono. Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hata mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia wenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha. Hata Petro alipopata fahamu akasema,
“sasa nimejua yakini yakuwa, Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi”. Na alipokuwa akifikiri hayo, akafika nyumbani kwa Mariamu, mamaye Yohana Marko … na watu wengi walikuwa wamekutana humo wakiomba. Naye alipobisha, kijakazi jina laki Rhoda akaja kusikiliza. Alipoitambua sauti ya Petro, hakufungua mlango, kwa ajili ya furaha, bali alipiga mbio, akaingia ndani, akawaambia kwamba, Petro anasimama mbele ya lango. (Mdo 12:1-14-19)
“KUOKOKA” katika mistari hii, imetumika kama “KUFUNGULIWA” au “KUKOMBOLEWA” katika kifungo.
UHAKIKA WA WA NENO WOKOVU
Kwahiyo KUOKOKA ni KUNUSURIKA, KUSALIMIKA, KUKOMBOLEWA, KUFUNGULIWA au KUPONA kutoka katika JANGA au HATARI fulani.
Yesu alikuja kuleta wokovu (kuokoa) na Biblia inataja mistari mingi sana juu ya koukoka au wokovu.
Kwa mfano:-
• Yoh 3:16-18; Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanae wa pekee ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyehamini amekwisha kuhukumiwa;
• kwa sababu hakuliamini jina la mwanawe wa pekee.
• Luk 9:59; Kwa maana mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa,
• Yoh 12:47; Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi si mhukumu, maana sikuja niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu.
• 1Tim 1:15; Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa ya kwamba, Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.
• 1Tim 2:14; Mungu … hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yalio kweli.
• Efe 2:5,8; Hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo, yaani, mmeokolewa kwa Neema, Kwa maana mmeokolewa kwa Neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
• 1Kor 1:18; Kwa sababu neno la Msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi, bali kwetu tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
• Mdo 4:10-12; Jueni nyote na watu wote wa Israel ya kuwa, kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulubisha, na Mungu akamfufua katika wafu … kwa jina hilo mtu huyu anasimama Hali mzima mbele yenu. Yeye ndiye jiwe lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limekuwa jiwe kuu la pembeni.
• Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina lingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Mdo 2:22-24, 36-40, 43-44, 47; Enyi waume wa Israel, sikilizeni maneno haya: Yesu wanazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua; Mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulubisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua; ambaye Mungu alimfufua, akifunga uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao…
Basi nyumba yote ya Israel nawajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulubisha kuwa Bwana na Kristo. Walipoyasikia hayo wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akamwambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu,
nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa watu wote watakao itwa na Bwana Mungu wetu wamjie. Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi …
Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume. Na wote walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika … Wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
(Mdo 2:22-24, 36-40, 43-44, 47)
Rum 10:9-10; Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, nakuamini mioyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
Mdo 16:30-31; Kisha akawaleta nje akasema. Bwana zangu, Yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.
2Kor 6:2; Kwa maana asema, wakati uliokubalika nalikusukia, siku ya wokovu nalikusaidia; Tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; Tazama, siku ya wokovu ndio sasa.
Ebr 2:1-3; Kwa hiyo, imetupasa kuangalia zaidi hayo yaliyosikiwa, tusije tukayakosa, kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika, lilikuwa imara, na kila kosa na uasi, ulipata ujira wa haki. Sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukadhibitika kwetu na wale wanaosikia.
AWALI TULIKUWA WAPI NA TUNAFANYA NINI
1. Tumeokolewa kutoka katika Nguvu ya Dhambi yaani uasi,
Maana sijui nifanyalo; kwasababu lile nilipendalo silitemdi; Bali lile nilichukialo ndilo nilitendalo … naikiri kuwa ile sheria ni njema. Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo,
Bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Kwa maana najua kuwa, ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema, kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati … lakini katika viungo vyangu, naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. Ole wangu, masikini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukru Mungu kwa Yesu kristo Bwana wetu R7:15-
“Nanyi mlikuwa wafu kwasababu ya makosa na dhambi zenu. Ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuaata Mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tama za miili yetu, tulipo yatimiza matendo ya mwili na nia, kukawa kwa tabia yetu watoto wahasira kama na hao wengine. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwasababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, mmeokolewa kwa neema akatufufua pamoja naye akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu.”(Efe 2:1-1-2-6)
“Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti”. (Rum 8:1-2) … “tukijua neno hili, ya kuwa, utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike. Tusitumikie dhambi tena …
Basi dhambi isitawale ndani ya miili yenu … kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi. Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mli-itii kwa mioyo yenu, ile namna ya elimu (Injili ya wokovu), ambayo mliwekwa chini yake. Na mlipokwisha kuwa huru mbali na dhambi,
Mkawa watumwa wa haki … kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki. Ni faida gani mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayo yatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti. Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima. … Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa. (Ezek 28:20-23) … kwa maana mshahara wa dhambi nimauti wa milele, bali karama (zawadi) ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. (Rum 6:23)
Pia soma; Tito 2:11-12; Tito3:3-4; 2Kor 4:3-4; Efe 4:18-19; 1Tim 1:13-15
2. TUMEOLOKEWA KUTOKA KATIKA NGUVU ZA GIZA.
“Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake”. (Kol 1:13)
“Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, mliwafanya hai pamoja naye, akisha kutusamehe makosa yote;
akisha kuifuata ile hati iliyoandikwa kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi za mamlaka, na kuzifanya kwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo”. (Kol 2:13-15)
Tazama, nimwewapa amri ya kukanyaga nge na nyoka na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. (Luk 10:19)
Math 27:45,50-54; Ebr 2:14-15; Luk 11:21-22; Yoh 19:28-30
ANDAA MUDA WA MAOMBI, NA MTU WAKUSHIRIKIANA NAYE,
CHAGUA MUDA MZURI. *Mhu 3:1,7
Ili uweze kuomba kwa umakini mzuri, chagua muda mzuri ambao akili yako ma mwili
wako viko fresh. Usilazimishe kuomba hata kama akili yako au mwili wako umechoka sana. Kila jambo lina wakati wake. Kama umechoka sana, huo si muda wa kuomba, bali wa kupumzika. Usilazimishe ratiba. ni bora upumzike ili baadaye uweze kuomba vizuri baadaye. Usije ukajikuta unamkemea Yesu badala shetani. Penda kuomba wakati una nguvu ya akili na mwili, ili uwe makini kuongea na Mungu kwa akili timamu. Ndio maana Yesu alipenda kuamka alfajiri sana kwenda kuomba mlimani. (Mk 1:35, Luka 4:42)
OMBA KATIKA ROHO (NENA KWA LUGHA). *Efe 6:18, Rum 8:26-27
Mbinu nyingine nzuri ya kuomba kwa muda mrefu na kwa ufanisi, ni kuomba kwa Roho; yaani kuomba kwa kunena kwa lugha. Tunapoomba kwa akili za kibinadamu, Mungu anasikia pia, lakini maombi yako yanakuwa na mipaka / limited kwasababu akili ya mtu haijui kila kitu. Bali Roho wa Mungu anajua kila kitu. Naye hutupa kipawa cha kuomba kwa lugha ya mbinguni iliyo bora zaidi. (Yuda 1:20, Mk 16:17, 1Kor 14:1-4, 15-16,7)
OMBA KWA KUFUNGA WAKATI MWINGINE. *Math 6:16-18
Kufunga kula kunasaidia kudhoofisha mwili, ili roho iwe makini zaidi kuongea na Mungu kwa kina zaidi. Mwili huu siku zote haupendi kufanya mambo ya Mungu. Na mwili ukiwa umeshiba, unakuwa na uchovu na uzito wa kufanya mambo ya kiroho. Mbinu mojawapo ya kuudhibiti, ni kuunyima/kuupunguzia posho yake ya chakula. Mwili ukidhoofika kiasi, roho yako inapata nguvu na upenyo mzuri zaidi (Zab 35:13). Mashujaa wote wa imani walifunga na kuomba. Ndio maana Yesu anasema ‘mfungapo’ akimaanisha ratiba ya kufunga, ipo. Inasaidia.
OMBA NA RAFIKI (PRAYER PARTNER). *Mhu 4:9-10
Neno la Mungu linasema, ni heri wawili kuliko mmoja. Kuna faida ya kuomba pamoja na rafiki yako. Kwanza, mnapokuwa wawili au watatu, inaleta hamasa na ari ya kuomba zaidi. Si rahisi kujisikia mvivu unapokuwa na waombaji wenzako. Pili; nguvu ya kiroho inaongezeka. Neno linasema, mwombaji mmoja anafukuza adui elfu moja, bali wakiwa wawili, wanafukuza (sio elfu mbili) bali elfu kumi! Shangaa! (Kumb 32:20) Hiyo ni kanuni ya mbinguni/kanuni ya Ki-Mungu. Kadri mnavyoongezeka, nguvu ya Mungu huongezeka.
Kwahiyo, wakati mwingine, omba na rafiki yako, unayemwamini, unayeweza kumshirikisha mambo yako ya binafsi. Mashujaa wengi wa imani, walikuwa na marafiki wa kiroho. (Prayer Partners). Kwa Mfano:- Math 17:1-9
- Musa - alikuwa na Joshua, Haruni na Huri
- Eliya - alikuwa na Elisha
- Daniel - alikuwa na Shadrack, Meshack na Abednego.
- Yesu - alikuwa na Petro, Yakobo na Yohana.
- Paul - alikuwa na Barnaba, Timotheo na Tito.
- Wewe Je? Uko na nani katika urafiki wa kiroho haswa katika maombi unayofanya?
Kama huna rafiki wa karibu wa kuomba naye, usikurupuke kujichaglia. Tulia umwombe Mungu akupe mtu atakayekuwa wa msaada kwako. Mtu mtakayefungamanishwa naye katika roho, hata kama mmetengana kijiografia, lakini katika roho, mko na umoja mzuri wa imani. (Math 18:18-19)
OMBA KATIKA MKAO UNAOKUPA UHURU NA NGUVU ZAIDI.
Katika kuomba kwa muda mrefu, mkao uliouzoea utakusaidia kwenda mwendo mrefu. Yakupasa kujua nguvu yako na udhaifu wako (strong point and weak point). Wakati wa kuomba, epuka mikao inayokuchosha haraka na tumia mikao inayokua nguvu zaidi. Kwa Mfano:- Ukiwa umechoka, usipende kuomba kwa kupiga magoti au kwa kuegemea kitandani. Ni bora uombe ukiwa umesimama au unatembea tembea, ili kuepuka usingizi na uchovu. Waombaji hodari wanaujua mikao inayowasaidia kuomba maombi marefu. Wengine hawana mikao maalum, bali wakiwa katika maombi, huwa wanabadilisha-badilisha mikao ili wasichoke. Hiyo ni mbinu nzuri pia.
Mifano ya Mashujaa wa imani;
Ibrahim – aliomba kwa kusimama (Mwa 18:22)
Daniel - aliomba kwa kupiga magoti (Dan 6:10)
Paul - aliomba kwa kupiga magoti (Efe 3:14)
Yesu - aliomba kwa kulala chini (Math 26:38-39)
Eliya - aliomba kwa kukaa chini na
kuweka kichwa kati ya miguu (1Fal 18:42)
Mimi - huwa napenda kuomba kwa kutembea tembea
Naweza kumaliza kilomita nyingi chumbani kwangu
Nikitembea huku nikiomba.
Wewe Je? Unaujua mkao wa nguvu? Kama hujui, Tafuta kujua.
OMBA NA MUZIKI LAINI KWA KUMWABUDU MUNGU.
Muziki wa kiroho, na wataratibu, unaweza kukutengenezea mazingira mazuri sana ya kuomba kwa muda mrefu. Muziki wa kuabudu, unavuta uwepo wa Mungu kwa namna ya pekee. Neno linasema, waimbaji na wanamuziki walipoimba na muziki ukapigwa, nao wakawa kama mtu mmoja, utukufu wa Mungu ukashuka na kulijaza lile hekalu hata makuhani hawakuweza tena kuhudumu (2Nyak 5:12-14). Kule mbinguni, kila malaika wa sifa, ana kinubi (zeze/gitaa). Elisha hakutoa unabii, mpaka mpiga kinubi alipopiga kwa ustadi, ndipo mkono wa Bwana (Roho wa Mungu) alipokija juu yake, naye akatabiri.
Najaribu kukuonyesha, kuna muunganiko mkubwa sana kati ya muziki wa kiroho na utukufu wa Mungu. Kwahiyo, ukiweza kuomba huku umeweka kanda au CD ya nyimbo za kiroho za taratibu, utapata (experience) hamasa ya kiroho (motivation) na utasikia una nguvu ya kuomba kwa muda mrefu. Kama unaweza, tengeneza kanda au CD maalum yenye nyimbo nzuri unazozipenda wewe, ili uwe unaipiga wakati wa maombi. Utajikuta unaweza kuomba kwa muda mrefu na kwa bubujiko zuri zaidi, ila hatua zote nilizoelezea hapo juu zitimizwe,
Hii ni njia rahisi ya kukuwezesha wewe kuomba kwa bidiii na kwa muda mrefu, endelea kufuatilia masomo mengine kuushu kuomba itakusaidia sana siyo tu kuomba bali hata katika kulifahamu Neno la Mungu, kama unatatizwa zaidi usiache kutupigia simu na sisi tutakusaidia zaidi,
Blog Archive
-
▼
2012
(30)
-
►
May
(13)
-
►
May 04
(11)
- Nini maana ya kuokoka?(wokovu)
- Torati inasema nini juu ya Kuokoka?(Uwokovu)
- KWA NINI UOKOKE?
- Kupona kwako na Jehanamu ni Kuokoka,
- Kwanini magonjwa ya kuonee kiasi hicho? ikiwa kuna...
- Je unastahili kuwa Tajiri Ndiyo hunasababu ya kut...
- Unafahamu kuwa kuna mauti ya pili, unajua namna ya...
- Ni rahisi kabisa Kuokoka kama uko Tayari,
- UMEFANYA MAAMUZI MAZURI SANA
- kwa ushahuri na maombezi kutoka kwa balozi piga simu,
- UNGANA NA MAMIA YA WATU WALIYOKUTANA NA MAJIBU Y...
-
►
May 04
(11)
-
►
May
(13)