MAOMBI YA MWENYE THAMBI:"

Ombi la mwenye dhambi ni gani?"
 
Ombi la mwenye dhambi ni Ombi ambalo mtu huomba kwa Mungu wakati anapotambua ya kwamba yeye ni mwenye dhambi au ametenda thambi na anahitaji  kusamehewa na Mwokozi.

 Kusema Ombi hili la mwenye dhambi haikamilishi tayari kila kitu. Ombi la mwenye dhambi hufanya kazi tu sawasawa linapokuwa limesimamia kile mtu anacho fahamu, anacho elewa, na kukubali kuhusu dhambi zake na hitaji la Wokovu.
Hatua ya kwanza ya Ombi la mwenye dhambi ni kufahamu ya kwamba sisi sote ni wenye dhambi. Warumi 3:10 , “Kama ilivyoandikwa,ya kwamba,Hakuna mwenye haki hata mmoja.” Bibilia inaonyesha wazi ya kwamba sisi sote tumefanya dhambi. Sisi sote ni wenye dhambi na tunahitaji rehema na msamaha toka kwa Mungu
 (Tito 3:5-7). Kwa ajili ya dhambi zetu,tunastahili adhabu ya milele (Mathayo 25:46). Ombi hili la mwenye dhambi ni kwa kutafuta neema badala ya hukumu. Ni ombi la kuulizia rehema badala ya hasira kuu.rehema ni kuhesabiwa haki usiyoistahili,
Hatua ya pili ya Ombi la mwenye dhambi ni kufahamu vile ambavyo Mungu amefanya kwa ajili ya kutibu hali ya upotevu wetu dhambini.Mungu alichukua mwili nakufanyika kuwa mwanadamu katika utu wa Yesu Kristo (Yohana 1:1,14). Yesu alitufundisha ukweli kuhusu Mungu na akaishi maisha makamilifu yenye haki na yasiyo kuwa na dhambi (Yohana 8:46; 2 Wakorintho 5:21). Yesu alikufa msalabani kwa ajili yetu, kwa kuchukua adhabu tuliyostahili (Warumi 5:8). Yesu alifufuka kutoka kwa wafu kudhihirisha ushindi wake juu ya dhambi,mauti,na jehanamu (Wakolosai 2:15; 2Wakorintho 15). Kwa ajili ya haya yote, tunaweza kusamehewa dhambi zetu na kuahidiwa uzima wa milele Mbinguni-tutakapo weka imani yetu ndani ya Yesu Kristo. Kile tunacho hitajika kufanya ni kuamini ya kwamba alikufa kwa ajili yetu na akafufuka kutoka kwa wafu (Warumi 10:9-10). Tunaweza kuokolewa kwa neema tu, kupitia imani peke yake, kwake Yesu pekee. Waefeso 2:8  “Kwa maana mmeokolewa kwa neema,kwa njia ya imani;ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu,ni kipawa cha Mungu.’’

Kusema Ombi hili la mwenye dhambi ni njia ya rahisi ya kumwelezea Mungu yakuwa unamtegemea Yesu Kristo kama mwokozi wako. Hakuna maneno ya kiuganga yenye kuleta wokovu. Ni kwa imani tu ndani ya kifo cha Yesu na kufufuka kwake vinavyo weza kutuokoa. Kama unafahamu yakwamba wewe ni mwenye dhambi na unahitaji wokovu kupitia kwa Yesu Kristo, hapa kunalo Ombi la mwenye dhambi unaloweza kuomba kwa Mungu:
Sala hii ni ya muhimu sana kama kweli umetambuwa uovu wako ulioutenda:

Mungu, najua yakwamba mimi ni mwenye dhambi. Ninajua ya kwamba ninastahili adhabu ya dhambi zangu. Hata hivyo,ninamwamini Yesu Kristo kama mwokozi wangu. Ninaamini ya kwamba kifo chake na kufufuka kwake ilikuwa ni kwa ajili ya msamaha wangu. Ninamwamini Yesu na Yesu peke yake kama Bwana na Mwokozi wangu. Ahsante Bwana,kwa kuniokoa na kwa kunisamehe! Amina!’’

Kama umemaanisha hii sala ni msaada mkubwa sana kwako hata mimi niliamuwa kama wewe mchana kweupe bila uwoga wala aibu,fahamu tu kuwa kuokoka siyo Dini bali ni kuchaguwa usalama wa maisha yako sasa naya Baadaye hongera na Mungu akubariki na kukusaidia kwa haya maisha mapya uliyoyaamuwa wewe mwenyewe,

ukiamuwa kutushuhudia  kile  Mungu alichokufanyia ili tumshukuru Mungu pamoja usisite kutuandikia au kutupigia simu no 0756809209/0784713604/076608801,au Samsonoxpel@gmail.com karibu sana

NENO LA MUNGU LINA NENA NINI JUU YA USHOGA?

Je, Neno la Mungu lina nena  nini juu ya ushoga? Je, ni( dhambi?)

 
Biblia inasisitiza kila mara kwamba ushoga ni dhambi (mwanzo 19:1-13; mambo ya walawi 18: 22; warumi 1:26-27; wakorintho wa kwanza 6:9). Warumi 1:26-27 inatufundisha ya kwamba ushoga ni njia mojawapo ya kumkana na kutomtii Mungu. Mtu anapodumu katika dhambi na kutokuamini biblia inatuambia ya kwamba “Mungu huwaachilia” kutenda maovu zaidi ili wapate kujua ubatili wa maisha bila Uwepo wa Mungu. Wakorintho wa kwanza 6:9 inasema kuwa mashoga hawataurithi ufalme wa Mungu.

Mungu haumbi mwanadamu mwenye tamaa ya ushoga. Biblia inatuambia mtu huwa shoga kwa sababu ya dhambi. (warumi 1:24-27), na pia kwa sababu ya uamuzi wake mwenyewe. Mtu anaweza kuzaliwa na msukumo juu ya ushoga

kama vile watu pia huzaliwa na msukumo juu ya fujo na dhambi nyinginezo. Hili halihalalishi dhambi yoyote inayofanywa na wanadamu. Je, mtu akizaliwa na msukumo wa hasira mbaya, ni halali aendeleze hasira zake mbaya? La, hasha. Hata kwa ushoga pia si halali.

Hata hivyo Biblia haiitaji dhambi ya ushoga kuwa ndiyo kubwa zaidi. Kila dhambi ni chukizo kwa Mungu. Ushoga ni mojawapo ya mambo yaliyoorodheshwa katika wakorintho wa kwanza 6:9-10 yatakayozuia mtu asiingie katika ufalme wa Mungu. Kulingana na Biblia msamaha wa Mungu juu ya shoga upo sawa na wa mzinzi, muabudu sanamu, muuaji, mwizi na kadhalika. Mungu tena aahidi uwezo juu ya kushinda dhambi, pamoja na ushoga, kwa wale wote watakao mwaminiYesu kristo kwa wokovu wao (wakorintho wa kwanza 6:11; wakorintho wa pili 5:17).

Sina maana ya kufuatilia maisha ya mtu lah! Bali ni mimi ninatumika tu kufikisha ujumbe kwa jamii yetu na nina amini hata mashoga matatembelea hii Safu bila shaka itanamsaidia mwenye tabia hii ya ushoga kuiacha mara moja

,japo wapo wengine ambao sijazungumzia sana  hapa ila watakuwa wameelezewa ukurasa mwingine wale wanao lawiti, watoto,wadogo,wake zao au wake za watu wengine  kwa yeyote anayefanya tendo hili ni vema kama ulikuwa haufahamu  fahamu sasa kuwa unafanya  chukizo mbele ya uso wa Mungu, acha mara moja na utubu kabisa,

MSAMAHA WA KWELI NI UPI?

Nina wezaje kupokea msamaha wa dhambi toka kwa Mungu?

 
Matendo 13:38 yasema, “Basi naijulikane kwenu, ndugu zangu ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi.”Kuhubiri msamaha ikiwa wewe husamehi ni kazi bure una fanya,

Msamaha ni nini?

Neno “samehe” linamaanisha kusafisha nia au jambo na kulifanya kutokuwa na mawaa yoyote, ku achilia kutoka moyoni mwako , kufutilia mbali ulichokuwa umekishikilia. Tunapo kosea mtu, huuliza msamaha wao ili kurudisha uhusiano. Msamaha haupewi mtu kwa sababu mtu anastahili kusamehewa.

Hakuna anaye stahili kusamehewa. Msamaha bali hii ni kama  ishara ya upendo, huruma na neema. Msamaha ni uamuzi anaotakiwa kufanya mtu aliye kwazwa  kutoshikilia jambo ndani yake kinyume cha mtu mwengine, haijalishi amekukosea kiasi gani.

Bibilia inatuambia ya kwamba sote tunahitaji msamaha toka kwa Mungu. Sote tumefanya dhambi. Mhubiri 7:20  “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.” 1Yohana 1:8  “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.” Dhambi zote ni kitendo cha uasi kinyume chake Mungu  (Zaburi 51:4). Basi kwa hivyo, tunahitaji kwa vyovyote msamaha wake Mungu. Kama dhambi zetu hazitasamehewa, tutakuwa katika adhabu ya milele tukiteseka kwa ajili ya madhara ya dhambi zetu (Mathayo 25:46;Yohana 3:36).

 ni upate vipi msamaha?

Kwa shukurani, Mungu ni mwenye upendo na huruma-mwenye hali  ya kutusamehe dhambi zetu au makosa yetu, 2Petro 3:9  “Yeye hutuvumilia maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.” Mungu anatamani kutusamehe, kwa hivyo alimtowa yesu kristo kwa ajili ya msamaha wetu.

Adhabu ya haki pekee inayostahili kwa ajili ya dhambi zetu ni mauti. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti…..” Mauti ya milele ndiyo  tuliyopokea kama mshahara wa dhambi zetu. Mungu, kwa mpango wake mahususi, alifanyika kuwa mwanadamu - Yesu Kristo

 (Yohana 1:1, 14). Yesu alikufa juu ya msalaba kwa kuchukua adhabu tuliyo stahili-mauti. 2Wakorintho 5:21 inatufundisha, “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye. “Yesu alikufa msalabani, akichukua adhabu tuliyo stahili!Kama Mungu, kifo chake Yesu kilitoa msamaha wa dhambi kwa ulimwengu mzima. 1Yohana 2:2 asema, “Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. “Yesu alifufuka katika wafu, akishuhudia ushindi juu ya dhambi na mauti
 (1Wakorintho 15:1-28). Mungu apewe sifa kwa kupitia kifo na kufufuka kwake Yesu Kristo, Sehemu yote ya pili ya kitabu cha Warumi 6:23 ni kweli, “…bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”kwahiyo maovu tunayoyatenda kwasababu ni kinyume cha makusudio ya Mungu athabu yake ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa mlele,

Je, ungetaka dhambi zako zisamehewe?
 Je, uko na hisia za kuudhi za kila mara zinazo kuhukumu na kuonekana kuwa ngumu kuepukika? Msamaha wa dhambi zako upo ikiwa utamwamini Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yako.

 Waefeso1:7  katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.” Yesu alitulipia deni ili tukapate kusamehewa. Unacho stahili ni kumuuliza Mungu akusamehe kupitia kwake Yesu, ukiamini yakwamba Yesu alikufa ili upate msamaha-naye atakusamehe!

 Yohana 3:16-17 ina habari hii ya ajabu, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.”
Je, ni jambo lililo rahisi kusamehe au kusamehewa?

Ndio, ni rahisi! Huwezi kupata msamaha toka kwa Mungu. Huwezi kulipia msamaha wako toka kwa Mungu. Unaweza ku upokea tu, kwa imani, kupitia neema na huruma za Mungu. Kama unataka kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi wako na kupokea msamaha toka kwa Mungu, hapa kuna ombi unalo weza kuomba. Kwa kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haiwezi kukuokoa. Ni kwa kumwamini Yesu Kristo pekee ndiko kutaleta msamaha wa dhambi.
Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kwa kumshukuru kwa kukupea msamaha. “Mungu, najua ya kwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu na nina weka   imani yangu kwake ili niokolewe ashukuriwe yesu aliyetulipia madeni yote na katufundisha na sisi kusamehe wengine kama tulivyo samehewa,

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? Kama ndiyo, tafadhali tafuta link ya sala ya toba na uifanye kwa kumaanisha toka moyoni mwako,

Followers