WACHUMBA : ( WATARAJIWA WA NDOWA)

      
Chukuwa tahazari zote,na kama umeshaingia  ndani ya ndowa  tulia kabisa na Omba mungu akupitishe ili uvuke hatuwa hiyo nawe upate faraja tena:

Ni vema kuchukuwa tahathari mapema kabla ya ajali!!!,

kosea kuchanguwa kitu chochote hapa Duniani kuliko kukosea kuoa au kuolewa,

Uwe mvulana au msichana, Kama umekaribia au umeshaoa,au – karibia kuoa au kuolewa, na hujawahi kujiuliza maswali ya namna hii, basi Mungu anakuweka mahali pazuri kwa kukupa nafasi ya kusoma Safu hii. Labda nikuambie kitu cha namna hii kitakusaidia,

 kabla sijakupa mistari mingine kwenye biblia, ni hivi: Hakuna sababu ya kuolewa na kijana ambaye atakufa baada mwezi mmoja. Au hakuna sababu ya kuoa msichana atakayekufa muda si mrefu baada ya arusi yenu.
Kwa nini uolewe leo uwe mjane baada ya miezi miwili? Na ukiishaolewa umekwisha badilisha kabisa hali yako na ya mume wako; akiisha kufa wewe sio msichana tena, utaitwa mjane, hata kama umri wako ni mdogo. Tulienda mahali ulani tukasema tunaomba wajane tuwaombee, tulishangaa kuona ya kuwa robo tatu yao walikuwa ni wasichana. Ungeambiwa wameolewa ungekataa, lakini wamefiwa bado wana umri mdogo.
Sasa mimi ninataka nikuulize swali, kwa nini unataka uolewe, halafu mume wako afe baada ya miezi miwili au unataka uoe mke wako afe baada ya mwezi mmoja, au baada ya mwaka? Hakuna kitu kinachosumbua kama hiki. Ngoja nikueleze hili tena ya kuwa ndoa ya pili sio ndoa ya kwanza. Ndoa ya kwanza ina utofauti wake, na ndoa ya pili ina utofauti wake.
Ikiwa unataka kuishi muda mrefu na mwenzi wako wa ndoa unahitaji


 Kuwa mwangalifu kutii ile mistari ilioko kwenye biblia inayozungumzia juu ya muda wa mtu kuishi. Kwa mfano: Waefeso 6:1-3 inasema; “Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, upate heri, ukae siku nyingi katika dunia”.
Kwa hiyo angalia uhusiano wako na wazazi wako kama bado wako hai. Lakini pia chunguza uhusiano wa huyo anayetaka kukuoa au anayetaka umuoe, na wazazi wake, kama bado wako hai.

Omba Mungu akupe maisha marefu na huyo mwenzako hata kabla hamjaamua kuoana. Ili kama kuna mmoja wenu hataishi muda mrefu – basi Mungu awaarifu na kuwaongoza cha kufanya.
Mwingine anataka aingie kwenye ndoa kwa kubahatisha au kwa majaribio. Maana yake ndani ya nafsi yake anajiweka tayari kuachana na mwenzi wake kama anaona mambo ya ndoa yake hayaendi alivyotarajia. Mtu wa namna hii hataweza kuwa mvumilivu na mwepesi wa kutafuta suluhisho kukitokea tatizo katika ndoa yake.
Uamuzi wa kuoa au kuolewa unamtaka mtu aingie katika ndoa asilimia mia moja. Ikiwa hautakuwa tayari kuingia kwenye ndoa kwa asilimia mia moja – tafadhali usiamue kuoa au kuolewa. Utampotezea tu mwenzako – maana hakuna ndoa isio na matatizo. Lakini pia hakuna tatizo ambalo Mungu hawezi kulitatua. Lakini, je, uko tayari kushirikiana na Mungu katika ndoa kwa kiwango cha asilimia ngapi?.

CHANZO CHA HAYA NI NINI?,

    

Ndugu yangu umewahi kujiuliza hata siku moja sababu za watoto wa mitaani kuongezeka kila siku? je hao watoto wa mitaani tunaowaona kila siku je?hawakuwahi kuwa na wazazi wao, je wazazi wao hawakuwa na elimu kama yako? au hawakuwaikuishi katika hii dunia kama wewe,je hili unafikiri kwako haliwezi kutokea?

sasa ufanye nini,nchi inanunuwa mabomu badala ya kununuwa matreckta ya kulimia, sababu ni nini? bila shaka inajihami kwa vita je wewe umejipanga vipi kupambana na hali kama hii isijekukutokea wewe ukashindwa kuokowa familia yako,

mimi ni na kukumbusha tu umekubali au hujakubali siyo kazi yangu, maana na mimi ninamzigo nilioubeba kwaajili ya kuwasaidia wahitaji kama wewe uliyejisahau,tazama kwa makini

sana watoto kama hawa hapa hawajajizaa wenyewe wamezaliwa na mzazi kama wewe kwa namna moja au nyingine fumba na kufumbuwa wanajiona katika hali hii na hawajuii hatima ya maisha yao ni nini, ukweli ni kwamba watoto wa mitaani wanahitaji misaada sana kutoka kwetu,

wapo watu wanaopuuzia na kusema hao wamekimbia tu nyumbani ili kuja kuomba omba swali mbona wa kwako hawakimbii nyumbani na kwenda kuomba omba mtaani hapo lipo tatizo kubwa ila niseme kitu kimoja kabla hatuja fuatilia tatizo lililo sababisha watoto wakimbie nyumbani tuwasaidie kwanza ndipo tuweze kutatuwa tatizo haisaidii kutatuwa tatizo ikiwa hawa wamesha toweshwa na njaa au magonjwa ni mambo yanayoumiza sana kwa kila mzazi aliyezaa mtoto, uzuiliwi kusema chochote kuhusu watoto wa mitaani, ila

Neno la mungu linatuamuru kuwa saidia na kuwajali yatima na wajane,haijalishi mtoto huyu wazazi wake wako wapi inawezekana kwa sababu ya hali ngumu ya maisha wazazi waka mkataa au alitupwa au wazazi walitengana haya yakatokea nyumba ikiyumba ni mathara mengi na makubwa yanatokea haswa kwa watoto, watoto kupoteza masomo kubwakwa,kutumikishwa kazi wasizostahili kufanya uzalilishaji ndugu yangu unapo yaona haya unajisikia kufanya nini juu ya hata mtoto mmoja?

nirudi kwa wazazi wanaokataa  watoto wao  je?  watoto wakiwa omba omba kama hivi ndivyo unafurahia wengine wanazaa bila mpangilio wa kufaahamu watoto wanaoweza kuwalea siku ya siku wanazalisha watoto wa mitaani,  tena hili tatizo linachangiwa sana kwakiasi kikubwa na wanaume,

unamkuta mtu ameoa bado hataki kutosheka na aliye naye bado anazaa nje ya ndowa kwa siri,anaogopa kumtambulisha nyumbani mtoto huyo wa nje ya ndowa ikitokea amezaa wengi huko nje ya ndowa,kisha uchumi wake ukayumba au kufariki dunia watoto wanakosa pakwenda mwisho wana malizikia mtaani wanasomea elimu yao ya kuomba mpaka anahitimu basi anakuwa ni wa mtaani, mtu anazaa na binti yake na mama yake yuko hai jamani tumekuwa wanyama?

au mwingine anazaa na binti yake wa kazi za nyumbani,sasa utazaa na wangapi au umeoa wanawake wangapi ili ijulikane,maana kila binti anayekuja kwako lazima ufanye naye mapezi, na ndiyomaana unapata ugonjwa wa zinaa bila hatakujuwa kwasababu una tabia kama hiyo unamkuta na mwingine mwenye tabia kama yako unajikuta umeukaribisha ukimwi ndani ya familia je? huja zalisha watoto wa mitaani wakati mwingine ukiombwa msaada na watoto wa mitaani una wakimbiza lakini inawezekana wengine umewazalisha wewe au ndugu yako au rafiki yako,

kwa sababu ya tabia mbaya, wale waliyopotelewa na wazazi kwaajili ya sababu inayoeleweka wengine wanaunafuu kidogo maana hawawajui kabisa wazazi wala kuwawona sasa wewe ukipita walishatambulishwa baba yako ni fulani na anakuona mtoto ana pata sana uchungu,

usahuru wangu kama umeitawanya familia yako irudishe tu,au kama umezaa nje ya ndowa fanya uwamuzi mapema ya kujadiliana na unayeishi naye sasa hivi kwaajili ya kuandaa kizazi chema  mateso wanayoishi nayo baathi ya watu hata leo yamesababisha na wazazi, Mungu atusaidie tufahamu jinsi ya kuyashika maagizo yake,

Hey! listen my friend.. Find one street child and make friendship with him or her!... something that you don't know is that...believe me he will change your life for real by hearing from him difficulties they faces everyday in their life.You will find yourself that you are so luck to be one you are and where you are right now.that and believe me you will be blessed.


You know what?..Because no one knows  about   tomorrow:

Followers