SIKUJA DUNIANI KULETA AMANI:
Maneno aliyoyatamka Yesu kristo: Sikuja duniani kuleta amani bali kuwafarakanisha Mtu na mtu,
24. "Mwanafunzi si mkuu kuliko mwalimu wake, wala mtumishi si mkuu kuliko bwana wake.
Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumwa hampiti bwana wake. 25. Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mkubwa wa jamaa Beelzebuli, je hawatawaitawatu wengine wa jamaa hiyo majina mabaya zaidi?
Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake?
26. "Basi, msiwaogope watu hao. Kila kilichofunikwa kitafunuliwa, na kila kilichofichwa kitafichuliwa.
Basi, msiwaogope, kwa maana hakuna neno lililositirika, ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa, ambalo halitajulikana.
27. Ninalowaambieni ninyi katika giza, lisemeni katika mwanga; na jambo mlilosikia likinong`onezwa, litangazeni hadharani. Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru; na msikialo kwa siri, lihubirini juu ya nyumba.
28. Msiwaogope wale wauao mwili, lakini hawawezi kuiua roho. Afadhali zaidi kumwogopa yule awezaye kuuangamiza mwili pamoja na roho katikamoto wa Jehanamu.
Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.
29. Shomoro wawili huuzwa kwa senti tano. Lakini hata mmoja wao haanguki chini bila kibali cha Baba yenu.
Je! Mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua Baba yenu;
30. Lakini kwa upande wenu, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote.
lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote.
31. Kwa hiyo msiogope; ninyi mu wa thamani kuliko shomoro wengi. ic
Msiogope basi; bora ninyi kuliko mashomoro wengi.
32. "Kila mtu anayekiri hadharani kwamba yeye ni wangu, mimi pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
33. Lakini yeyote atakayenikana hadharani, nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.
Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
34. "Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga.
Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.
35. Maana nimekuja kuleta mafarakano kati ya mtu na baba yake, kati ya binti na mama yake, kati ya mkwe na mkwe wake.
Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;
36. Na maadui wa mtu ni watu wa nyumbani mwake.
na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.
37. "Ampendaye baba au mama yake kuliko anipendavyo mimi, hanistahili. Ampendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
38. Mtu asiyechukua msalaba wake na kunifuata, hanistahili.
Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.
39. Anayeyashikilia maisha yake, atayapoteza; lakini anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata.
Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.
40. "Anayewakaribisha ninyi, ananikaribisha mimi; na anayenikaribisha mimi, anamkaribisha yule aliyenituma.
Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma.
41. Anayemkaribisha nabii kwa sababu ni nabii, atapokea tuzo la nabii. Anayemkaribisha mtu mwema kwa sababu ni mtu mwema, atapokea tuzo lamtu mwema.
Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki.
42. Kweli nawaambieni, yeyote atakayempa mmojawapo wa wadogo hawa kikombe cha maji baridi kwa sababu ni mfuasi wangu, hatakosa kamwekupata tuzo lake."
Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake. kwa maana hiyo yeyote anayemkiri bwana Yesu kuwa kama bwana na muokozi wa maisha yake si kitu rahisi akaweza kufungamana na waovu, kwa kuwa hawa wawili hawafanani kuishi wala kuenda kwao
kwa maana giza na Nuru haviwezi kukaa pamoja lazima kimoja kita athiri kingine, na kama wewe unamuamini mungu na njia zako zikawa za haki huwezi ukaishi kama mtu asiye mjuwa Mungu maisha ya mtu wa Mungu anaiga kutoka kwa kristo kwanza mtiifu myeyekevu,mwepesi wa kusamehe na kuachilia moyoni mwenye mzigo mkubwa kwa ajili ya wale wanaopotea na si kuwaumiza kwa maneno makali ya kuhukumu makosa yao, neno linasema hukumu zenu ziwe za haki unacho mtamkia mtu uwenauhakika nacho kabisa
lakini pia utakapo shutumiwa kwa mambo ya uwongo furahia maana umekwisha wekewa thawabu yako kule mbinuni inaendelea Mathayo 10:24
Ndugu Mtazamaji/ MSOMAJI; Bila shaka unampenda Mungu Sana tunaamini hivyo Kwa vile ulivyoweza kufika mahali hapa tulipo kupitia Mtandao huu, lipo kusudi la Mungu kutaka kukusaidia jambo Fulani ikiwa uko tayari katika yote jiepushe na mafundisho yasiyokuwa ya ki-Mungu Mathayo 16:6-12) piga simu kwa masaada zaidi huduma hii ni bure 0757328311