Je Unajuwa Kuwa Wewe ni Balozi wa serekali ya Mbinguni

Kwa Watakatifu, watu wa Mungu aliye Baba yetu, na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. namshukuru Mungu wetu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu niyi wote mtakao soma majibu ya swali la Ndugu yetu kebhayo,


Kwa maana Mungu tumwabuduye kwa roho na kweli katika Injili ya Mwana wake Yesu kristo, naye ni shahidi wetu kwa yale tu yanenayo au tunayoyatenda Amestahili yeye kutukuzwa kupitia maswali

Bwana wetu na Mungu wetu kwa wale wanaomwamini, kuwa yeye ndiye aliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yake vilikuwako, navyo viliumbwa. ujumbe huu unajibiwa katika Jina lile lipitalo majina yote, Jina la Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai, Bwana na Mwokozi wetu. Kwa kuwa majibu ni mengi ninaomba niyafupishe ila ikihitajika kwa urefu zaidi ya hapa nalo linawezekana, pia nitafanya hivyo

UTANGULIZI

• Siri ya Mungu ipo kwa wao wamchao tu, zaburi 25:14

• Kilichozwaliwa kwa mwili ni mwali na kilicho zaliwa kwa Roho ni Roho

• Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu Mithali 22:1

Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyenzi ……………….Kwa siku NYINGI nitamshibisha, nami nitamwonyesha wokovu wangu” (Zaburi 91:16)“Ili wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo’ (Wakolosai 2:2).


Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo” (2Wakorintho 5:20)

Kuwa mjumbe kwa ajili ya Kristo maana yake nini? Tunatakiwa tuwe wajumbe kwa ajili ya Kristo juu ya nini? Na kwa namna gani? Na kwa nani? Na kwa wakati gani? Neno la Kiingereza lililotafsiriwa kuwa mjumbe ni ‘Ambassador” Na neno zuri linalotoa picha nzuri ya maana ya ‘Ambassador’ ni neno Balozi. Balozi ni mjumbe na mjumbe ni balozi

Neno balozi na neno mjumbe lina maana sawa lakini kwa jinsi tunavyoyatumia maneno haya, utafikiria neno balozi lina uzito zaidi kuliko neno mjumbe.

Kwa hiyo tunaweza kusema: “ Basi tu mabalozi (wajumbe) kwa ajili ya Kristo” Katika nchi ya Tanzania tuna mabalozi wa nyumba kumikumi, ambao pia wanajulikana kuwa ni wajumbe wa nyumba kumikumi. Pia tuna mabalozi walioko nchi za nje waliotumwa kuiwakilisha nchi hii katika maswala na majukumu mbalimbali.

Sasa na tuliangalie katika ngazi ya kitaifa. Balozi ni mjumbe au mwakilishi wa nchi moja katika nchi nyingine. Kwa mfano: Balozi wa Tanzania nchini Kenya; kwanza ni raia wa Tanzania anayefahamu vizuri msimamo wa nchi hii katika maswala mbalimbali. Yuko Kenya kwa ajili ya Serikali ya Tanzania na raia wa Tanzania.

Yeye ndiye msemaji mkuu wa Serikali ya Tanzania nchini Kenya. Serikali ya Tanzania inapopeleka ujumbe kwa serikali ya Kenya, inapitia kwa balozi wake aliyeko Kenya.

Balozi huyo ni picha kamili ya Watanzania kwa watu wa Kenya, katika maneno yake na mwenendo wake. Yeye ni mlinzi wa hadhi ya Tanzania nchini Kenya. Na makazi yake ni nchini Kenya.

Balozi ni mjumbe aliyetumwa na mtu mwingine. Balozi wa Tanzania katika umoja wa Mataifa, ametumwa na nchi yetu, awe msemaji na mtetezi wa mawazo ya Tanzania katika maswala mbalimbali ya kimataifa. Balozi hasemi mawazo yake mwenyewe. Balozi anasema tu kile alichotumwa kusema na anafanya kile tu ambacho ametumwa kufanya.

Tunasisitiza hivi, BALOZI HASEMI MAWAZO YAKE MWENYEWE: BALOZI ANASEMA TU KILE ALICHOTUMWA KUSEMA, NA ANAFANYA KILE TU AMBACHO AMETUMWA KUFANYA.Na kitu cha kwanza anachofanya anapofika katika nchi aliyotumwa ni kutoa vitambulisho vilivyo na muhuri na sahihi ya kiongozi wa nchi anayotoka.

Biblia inatuambia kuwa sisi ni mabalozi kwa ajili ya Kristo hapa duniani; sisi ni wajumbe tuliotumwa kwa ajili ya Kristo hapa duniani. Ndiyo maana Paulo alisema kuishi kwake ni Kristo. Wewe ni mjumbe wa Kristo na kwa ajili ya Kristo hapa duniani. Ikiwa wewe ni Mjumbe, basi wewe ni balozi wa Kristo na kwa ajili ya Kristo.

Kumbuka kuwa balozi hasemi mawazo yake mwenyewe. Wewe ni balozi wa Kristo hapa duniani kwa hiyo kutokana na wadhifa huo uliopewa unatakiwa usiseme mawazo yako, wala kufanya mambo yako hapa duniani; bali USEME MAWAZO YA KRISTO NA MANENO YAKE; NA UFANYE YAKE TU ALIYOKUTUMA KUFANYA.

Lakini ni wazi kwamba huwezi kusema mawazo na maneno ya Kristo wakati huyafahamu. Na ikiwa hapa duniani wewe ni balozi basi, inamaanisha hapa duniani si kwako. Na ikiwa hapa duniani si kwako, na wala wewe si mwenyeji wa hapa duniani; basi unatokea wapi na uenyeji (uraia) wako ni wa wapi?

Wewe ni mwenyeji wa wapi? Hili swali ni muhimu sana ambalo ni budi ufahamu jibu lake katika roho yako. Bila kufahamu ulikotoka utaifanye kazi ya ubalozi au ya kuwa mjumbe wa Kristo. Balozi (Mjumbe) yeyote anajua alikotoka; anafahamu uraia wake ni wa wapi. Je wewe unafahamu kuwa wewe ni balozi wa nchi gani ukiwa hapa duniani?

ninakazia swali hili kwa sababu ujumbe utakokuwa unatoa; au mahubiri unayofanya mbele za watu; na matendo yako yanategemea sasa mahali gani umetoka kiroho na kimazingira.

Kuna wengine ni mabalozi wa miili yao wenywe. Wanahubiri kwa sababu ya mwili ili wapate mishahara yao na kuvaa. Wao wanaona kuwa kuhubiri ni kama kazi nyingine ya kuajiriwa.

Lakini la kushangaza ni kwamba wote wanasema ni mabalozi wa Kristo, wajumbe wa neno la Injili. Na hii si kweli. Muda umefika ambapo Roho wa Mungu amekududia kuliweka wazi hili. Mabalozi wa Kristo wawe wazi; mabalozi wa madhehebu wawe wazi, na mabalozi wa miili yao wawe wazi.

Muda umefika wa kufichuliwa watu wote wanaojiita mabalozi wa Kristo, wameokoka, na ni wakristo?, watumishi wa Kanisa kumbe ni mbwa mwitu wakali wanaowaendea watu wakiwa wamevaa mavazi ya Kondoo (Mathayo 7:15).

Muda umefika ambao watu wote wanokaa karibu na wewe, vitu vyote vinavyokuzunguka, mahali unapopita, watu wote hao wanaokuzunguka wajue, kwamba wanajua KUWA WEWE NI BALOZI WA KRISTO MJUMBE KWA AJILI YA KRISTO!Kweli

UTASEMA MAWAZO NA MANENO YA KRISTO. NA UTAFANYA MATENDO YA KRISTO KWA AJILI YA KRISTO MAHALI POPOTE ULIPO NA UTAKAPOKUWA DUNIANI:

Kuishi kwako hapa duniani ni Kristo na kufa kwako ni faida! Mtume Paulo alipoandika kuwa “Basi tu wajumbe (Mabalozi) kwa ajili ya Kristo,” alikuwa anamhusisha kila mtu ambaye amefanyika kuwa kiumbe kipya ndani ya Kristo. Ikiwa wewe ni kiumbe kipya ndani ya Kristo, basi wewe ni mjumbe(balozi) kwa ajili ya Kristo.

Ikiwa basi wote waliozaliwa mara ya pili, walio viumbe vipya ndani ya Kristo (waliookoka) wanatakiwa kuwa mabalozi wa Kristo; mbona basi ubalozi wao hauonekani ukifanya kazi? Ubalozi hauonekani katika maisha yako, kwa sababu hujafuatilia katika Biblia kujua neno linasemaje juu ya hili.

Ni Duwa yangu na maombi kila atakayepata ujumbe huu akubali kwanzia leo yeye awe Balozi wa serekali ya mbinguni Baada ya kujitabuwa lati tingefahamu uzito wa wadhifa huu wa kuwa mjumbe wa Kristo hapa duniani, hali ya mambo isingekuwa kama ilivyo hivi sasa ya kukata tamaa – iliyojaa katika mioyo ya yetu.na kujiweka mbali na Mungu kiasi hicho

Laiti basi wewe ungejua uzito wa wadhifa huu wa kuwa mjumbe wa Kristo mahali ulipo ikiwa in nyumbani, kazini, safarini, kanisani, sokoni, hali ya mambo isingekuwa kama unavyoiona sasa. Nchi yetu inaharibika kwakuwa watu wameyaacha majukumu yao wakatamani ya wengine wasiyoyaweza je tunakwenda wapi,Hoko?

Ubalozi uzalendo uraia wa mbinguni

Mtu yeyote Yule aliyemwamini kristo kama Bwana na muokozi wa maisha yake yeye ni raia wa mbinguni. Na mzalendo wa Mbinguni kwa mjibu wa maandiko matakatifu,

“Basi tangu sasa ninyi si wageni wala Wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu” (Waefeso 2:19).

Yesu Kristo alipokuwa akituombea alisema:

“Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa WAO SI WA ULIMWENGU, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule muovu. Wao SI WA ULIMWENGU KAMA MIMI NISIVYO WA ULIMWENGU. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo NILIWATUMA HAO ULIMWENGUNI (Yohana 17:4-18)

Weka jambo ili katika moyo wako. Watu wa Kristo si wa ulimwengu huu, bali ni wenyeji wa mbinguni. Watu wa Kristo wako hapa ulimwenguni kwa sababu Kristo amewatuma kufanya kazi muhimu. Kumbuka upo hapa duniani kwa kuwa kuna KAZI ambayo KRISTO amekupa uifanye kabla ya kurudi nyumbani kwetu MBINGINU.kama huitambui leo Roho mtakatifu kupitia Balozi wa Serekali ya Mbinguni ameamua utambuwe sasa, ila kwa msaada zaidi piga simu yangu ya mkono au ya meza Ext;1961/ 0756 809 209, kwa maswali zaidi na msaada,niko tayari usiku na mchana 24 kwa siku 7 za juma hakuna aliyechelewa kuaza kazi ya ubalozi anza sasa kama jana hukufanya

Balozi wa serekali ya mbinguni
(Samson)

Followers