Sababu za Mtumishi kuvunjika moyo katika huduma

. DALILI  AU ALAMA ZA KUCHOKA KATIKA HUDUMA  YAKO



Kuna aina mbili za dalili za kuchoka –dalili za ndani na dalili za nje


. DALILI ZA NJE NI PAMOJA NA MAMBO YA FUATAYO

· Kuongezeka kwa shughuli lakini uzalishaji/ufanisi unabaki uleule, ambao unaitwa uwendawazimu insanity-kufanya jambo lilelile kwa muda mrefu na kupata matokeo yale yale. Kuwa na shughuli nyingi si Kiroho.Kimsingi unapaswa kutumia nguvu kidogo tu na kuwa na matokeo makubwa-maarifa ni ya muhimu zaidi ya nguvu na bidii nyingi.

 Kuchoka kimwili,kuishiwa nguvu-kuchoka mfululizo ni dalili ya Burn-out,kujiona hupendi kufanya jambo lolote lile.Kupenda kulala tu,kuona kero kuamka hasa alfajiri.

 Kutokuwa tayari kujihatarisha au kuthubutu-kukwepa changamoto katika huduma,kukwepa watu na marafiki,kupoteza imani juu yako mwenyewe na kupoteza uwezo wa kukamilisha mambo.

· Kukwazika kirahisi/kukasirishwa na mambo na watu ,hata Mungu mwenyewe kirahisi- Musa na Yeremia ni mfano mzuri –Hesabu 11:11 Yeremiah 20:7,

 Kukosa usingizi ,kupoteza hamu ya kula,Kuwa na mawazo mengi,kupenda kuwa pekee yako , “kujificha katika upweke”


Kupooza /stroke,shinikizo la moyo,kipanda uso,kichwa kuuma mara kwa mara

 Matatizo ya kuyeyusha chakula,matatizo katika utumbo mkubwa (coronary problem),vidonda ya tumbo/ulcers.


. DALILI ZA NDANI NI PAMOJA NA MAMBO YAFUATAYO:


 Kupoteza ujasiri

 Kupoteza kujiamini na uthamani wako binafsi

· Kuwa na mtazamo hasi

 Kupoteza makusudi- kumwona Mungu ni chanzo cha kushindwa kwako,kujikasirikia mwenyewe kwa kushindwa kufikia malengo

 Kuchoka kihisia,depression,mkandamizo

 Hatia ya kujiona hufanyi vya kutosha,huna matokeo ya kutosha, na kufikiri pengine ukiongeza bidii nyingi ndipo utaona matokeo,kwa wengine hupelekea kufunga sana mfululizo kuomba sana,kukesha sana,wakifikiri kwa kufanya hivyo kutakuwa na matokeo kinyume chake,hupelekea uchovu zaidi na hakuna matokeo.

 Martha complex-kuwa na shughuli nyingi sana na kukosa muda binafsi wa Mungu kukuhudumia


. Kuanza kuwadharau watu ulioitwa kuwapenda na kuwahudumia

. Unaanza kurushu mawazo yako kuchukuliwa na mambo mengine ambayo ungeweza kuyafanya zaidi yakufanya huduma .

. Unajihisi ni kama “mashine ya huduma” hivyo unafanya yale ufanyayo ukiwa na hatia ya kwamba ni Lazima uyafanye badala ya kutenda kwako kutokane na kutembea kwako karibu na Mungu(Mahusiano),kazi ya Bwana Vs Bwana wa Kazi.Juhudi vs Ufanisi.


. Unaanza kufanya maaumzi kulingana na nini ni rahisi kuliko vile unavyojua ndivyo Mungu anakutaka ufanye.


. Unazidi kuwa mkosoaji na kupita kiasi juu ya makanisa,watu,na huduma za watu wengine ambazo unafikiri Mungu anazibariki kuliko huduma yako na wewe


. Hukumbuki lini mara ya mwisho ulifungua Biblia kwaajili kwaajili ya ushirika wako binafsi na Mungu,bali ni kwaajili ya kutafuta Mahubiri na Masomo ya kufundisha Biblia


. Unaanza kuwaona watendakazi wanaotumika pamoja na wewe kama watumishi wako badala yakuwaona kama ni watumishi wa Mungu.

 Unatumia kugawa majukumu kama udhuru ya kuwa mvivu,una kwepa majukumu kwa kuwagawia wengine wafanye.

. Hukumbuki mara ya mwisho ni lini ulikuwa na mazungumzo na mke wako ambayo haya husiani na mambo ya kanisa

Hukumbuki mara ya mwisho ni lini ulitumia muda na watoto wako na mkafurahia pamoja.

. Unaanza kutilia mashaka nguvu za Mungu ndani yako na ndani ya maisha ya watu wengine.



Followers