Semina ya wiki moja
Baada ya kujifunza vyanzo vya mafanikio na watu kufunguliwa Nira shingoni mwao na Kutuwa mizigo yao sasa hatuwa inayofuata ni ya muhimu pia, unaweza kwenda kuchukuwa hatuwa ulizojifunza ili kujiandaa na kupokea zile Baraka bwana alizokuandalia kupitia kazi za mikono yako,
Iwe ni biashara au ajira, kulima,kufuga na mengineyo uliyojifunza usikae bila shuguli ya kufanya na mikono yako Bwana alimwagiza Adamu kumiliki na kutawala kwakuwa Alisha muwekea vitu vyakutawala na kuvimiliki,naakapewa agizo lakuituza bustani ya Edeni,
Sasa wewe ni nani usiyetaka kujishugulisha na kitu alafu unataka Mungu akufanikishe, ninakushahuri hataukiwa sehemu yenye mahubiri ya neon la Mungu na Muhubiri akaita watu wakuwaombea Baraka, jiulize kwanza hizo Baraka zitapitia wapi,kama utakuwa huna kila kitu, huna njiwa,huna kuku huna bata huna mbuzi huna ng”ombe huna bustani huna shamba, fikiria mara mbili wewe utapokelea mlango upi?
Ninajuwa kwa wewe usiyetaka kujishugulisha na shuguli yeyote huduma hii itakuuthi lakini ni bora upate hasira ukimaliza kusoma huu ujumbe na wewe ukawe na kitu cha kufanya,
Hata kama umemtembelea ndugu yako na unajuwa unaishi naye mwezi mzima hajalishi unasubiri majibu ya shule au ya kazi au unavyo juwa wewe mwenyewe,jitahidi siku isiishe hujafanya jambo lolote pale unapo ishi, ni hatari sana siku nzima kuisha bila kufanya jambo lolote linaloweza kuulipia huo muda,
Uza mda wako upate pesa kama umeshindwa kuutumia wewemwenyewe.
Watu huwa wanapenda kuyatumia maneno ambayo kwao hayafanyi kazi kabisa, mtu anasema muda ni mali haya muulize huo muda anaosema ni mali amezalisha kiasi gani maana kile unacho faidika nacho ndichotunacho kibadilisha na masaa ndipo tuna sema muda ni mali,kwa mfano kuna watu wameajiriwa hao wamekubaliana na mwajiri kwa makubaliano ya kuuziana masaa kwamba mimi nitakuuzia masaa yangu yote ya mwezi mzima unilipe,
Mwingine kibaruwa ana kubaliana na mwajiri wake walipane kwa kutwa kwamba atamuuzia masaa ya kutwa nzima, mwingine kwa nusu siku,mwingie kwa lisaa limoja,inategemea, mwingine anaamuwa kuyanunuwa masaa yake yote kwa kuijajiri shuguli zake mwenyewe anafahamu kabisa ataamuka saa ngapi kwenda kwa shuguli zake na atakamilisha saa ngapi,
Sasa wewe ndugu yangu ambaye umebakia kuwalaumu wazazi na ndugu zako kuwa hawakusaidii,je?wewe umejisaidia vipi au kwa lipi? Maana kuna wale wenzangu wao ni kulaumu tu kwamba ndugu wana uwezo alafu hawamsaidii,wakati huo hataki kujishugulisha na kitu chochote nikwenda kuzurura na marafiki,wasio eleweka na wao,au waliomzidi ujanja wa kimaisha, hatakama ndugu ana mali nyingi hizo si zako nay eye amezingaikia hakukaa kama wewe unavyo kaa,alafu akazipata,
Uondoke sasa ukatafute kitu cha kufanya ukiwa unamuomba
mungu,katika kukaa bila kujishugulisha muovu anaweza kuitumia nafasi hiyo kukupa kazi,ya uwovu ukamuuthi Mungu,ukawa kama daudi daudi alijikuta anaingia kwenye thambi bila hata ya kupana akilini mwake,,,,,,,,,,
Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa UTAJIRI WAKE KRISTO USIOPIMIKA; na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote, ili sasa, kwa njia ya Kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho"(Waefeso 3:8 - 10).
Na Mungu wangu atawajazeni KILA MNACHOHITAJI KWA KADIRI YA UTAJIRI WAKE KATIKA UTUKUFU,NDANI YA KRISTO YESU" (Wafilipi 4:9)
Kristo ana utajiri usiopimika. Na wote walio ndani yake ni warithi pamoja naye wa utajiri usiopimika. Kutokana na utajiri huo TUNAJAZWA KILA TUNACHOKIHITAJI. Mahitaji haya ni ya kiroho, kiakili na kimwili. Kwa hiyo hakuna sababu ya mkristo kuishi maisha ya kupungukiwa, ikiwa Kristo yuko ndani ya moyo wake pamoja na utajiri wake usiopimika. Kikubwa kama wewe ni mrithi basi ni jukumu lako kuendeleza huo urithi kwakufuata kanuni yake Mungu
Jambo la kujiuliza ni hili; kwa nini utajiri huu wa Kristo usiopimika hauonekani katika maisha ya wakristo wengi? Wakristo waishije katika ushuhuda wa wokovu ndani ya Kristo, wakati wanaishi katika ulimwengu wenye hali ngumu kiuchumi? Watumishi wa Mungu kwa mfano, wachungaji, wainjilisti na kadhalika, waishije katika kumtumikia Mungu vizuri bila kupoteza ushuhuda wao wakati wanaishi katika mazingira yenye maisha magumu kiuchumi na bado wanasimamia amaandiko kuwa wao ni vichwa hawatakuwa mkia,na hata watoto wao wamewafundisha kuishi kama kichwa na siyo mkia wakati watu wakiwatazama kwa macho wanaonekana kama mkia,
wewe kama mkristo ukiyafuata maagizo ya Mungu ipasavyo hutohitajika hata kushuhudia yale Mungu aliyokutendea bali watu watashuhudia maana watakuwa wameshuhudia kwa macho yao,umewahi kujiuliza kuhusiana na maisha wanayoishi,wakristo?
Haya si maswali mepesi kuyajibu, lakini ni muhimu yatafutiwe ufumbuzi. Kabla hatujaanza kuyajibu napenda tusome Waefeso 4:11;
" Naye (Yesu Kristo) alitoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti; na wengine kuwa wachungaji na Waalimu."
Ni kwa kusudi gani Bwana Yesu Kristo aliamua kuwaweka hawa katika kazi yake kanisani? Waefeso 4:12-16 inatupa maelezo:-
"Kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo, ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. Katika yeye mwili wote ukiunganishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo
siku ya pili
Kutafuta chanzo cha mafanikio yako kabla ya kutaka mafanikio,
Tumejifunza na kuona baathi ya mateso unayopiti au magonjwa hukuyapatia ukubwani wala hukuambukizwa kwa sababu zako bali chanzo chake kimetokea mbali sana kwa wazazi na hata mara nyingine si kwa wazazi hao ulio nao yaani Baba na mama la! Inawezekana kutoka kwa Mababu na ma Bibi, yapo mambo mengi umetamkiwa tangu ukiwa tumboni,au ulipozaliwa tu,
Inawezekana kabisa mengi yakawa ulitamkiwa mazuri lakini je? Na katika hayo yakakufanikisha mipango mzima ya hapa duniani je nay ale maneno mabaya waliyo kutamkia nayenyewe ulishawahi kuambiwa lolote kuhusiana na hilo,
Si rahisi kugunduwa kuwa unalo tatizo la kurithishwa na wazazi, je? Kwa nini baathi ya makabila mtoto akizaliwa kwenda kumuona ni mpaka yule anayetaka kumshika mtoto anatakiwa awe na hela mkononi ya kumzawadia, wengine mtoto akizaliwa anakabithiwa hale ya noti mkononi mwake, kwa nini?wengine wanaonyeshwa majembe ya kulimia,
kila kabila lina imani yake kuhusiana na kuzaliwa kwa mtoto wewe mwenyewe unafahamu kwa kabila lako kuwa mtoto akizaliwa huwa wanamuonyesha kitu gani,na kutamka nini juu ya mtoto, wengine nimpaka wafanyiwe matambiko ya kimila,(kimizimu)
Ndiyo maana wengine wanakimbilia kanisani kumuweka wakufu kwa mungu,wengine kwa wachawi wanaita kuzindika,je wewe unalijuwa hilo juu yako kwamba nini kilifanyika,hiyo ni siri ya wazazi na wakati mwingine kwa kutofahamu kwa wazazi wako anakupelekea wewe kusumbuliwana magonywa ya kurithi,au kujikuta unaishi na mapepo mwilini bila yaw ewe kufahumu maana wazazi inawezekana walifanya hivyo kwalengo la kutaka kukulinda,je unafikiri yule mchawi aliyekuzindika bado yupo hai,na kama bado anaishi je wateja zake si wewe na wazazi wako,hivyo kama aliweza kukuwekea mapepo ya kukulinda na wachawi wenzake
Basi anaweza kukuloga pia ili mradi wake uweze kuwa endelevu hayupo mtu yeyote hapa Duniani anayependa kufanya kazi kwa hasara hakuna lazima atahakikisha amekutumia mapepo ya kuku sumbuwa ili muwe wateja wa kudumu kwake, wengine kweli hamkwenda hata kwa wachawi bali, mmekuwa mkitembea na magonjwa ya kuamkiwa na wazazi,au na laana ya kutamkiwa tangu tumboni mwa mama yako.kwa sababu ya babishano ya wazazi,
Ujumbe uliyokuwa umetawala katika mabango yaliyokuwa yanawakaribisha watu wote wa mji ili waje kuhuthuria katika semina ile ya siku tatu pele nyantorotoro katika mji wa geita, ulikuwa unasomeka
Tena itakuwa katika siku hiyo Mzigo wake utaondoka begani mwako na Nira yake shingoni, nayo Nira itaharibiwa kwasababu ya kutiwa mafuta, Isaya 10:27 somo hili lili fafanuliwa kwa kina sana na hata wewe ni vema ukafahamu kwamba vifungo vingi kufunguka vina hitajika kwaza mtu aliyefungwa kufundishwa Neno la Mungu kuhusiana na kifungo maana kila mtu ambaye hajakombolewa anacho kifungo chake, anahitaji kufundishwa na kuombewa kaajili ya kuharibiwa hivyo vifungo na maagano na laana,na mikosi ya kila namna,
Kwa mfano Kuna wakati mwingine unajikuta unahasira za kupita kawaida, na hata hujachokozwa na mtu yeyote yule umejikasirisha mwenyewe tu tena umeamka kitandani na unaishi chumbani peke yako, huja wowa wala kuolewa lakini ukiamka asubuhi unahisi hasira kali kabisa zakutaka hata kuuwa mtu, wakati mwingine mpaka unalia.sababu huielewi,
Hizo ni roho za mapepo zimekuvamia bila wewe kufahamu, si mpango wa Mungu wewe kuamka umejinyonga na hasira neno la Mungu halisemi juu ya Adamu kuamka na jaziba au asira katika ile bustani ya Edine, bali huyu bwana aliishi kwa Furaha mpaka thambi ilipoingia pale bustanini na kumvamia kupitia mkewe ndipo vurugu zikaanzia hapo, hivyo tunaona kwamba chanzo cha mwanadamu kuvamiwa na roho chafu nipale anapoaza kumkosea Mungu kwa kutofuata maagizo yake,na kutenda thambi,
Kwa sababu wazazi wako inawezekana kwamba mungu walimjuwa na hata sasa wato wengi swala la Mungu ukilionea wanalikubali na wengine wanakuambia kuwa hakunashida kabisa yeye anamfahamu Mungu toka utotoni mwake,asijuwe ni kwa sababu wazazi walimlelea hivyo,
Kwa kumfundisha maadili ya kwamba Mungu yupo na mahala pakukutana na Mungu wengine wakafundishwa ni kanisani,ila mimi nina kuambia mungu hakai mahala pamoja bali yupo kila mahala, na wala hayuko upande mmoja wewe unaweza kugeukia popote pale na ukiwa vyo vyote, bila ya kuangalia unauwezo au huna bila ya kuangalia nguo uliyovaa au viatu au huna Mungu anachokiangalia ni moyo wa mwanadamu ambao unaweza kumsababisha mwanadamu kutenda thambi,
Kuhubiriwa mahubiri ya kupata Baraka peke yake bila kufundishwa hizo Baraka zinatokea upande upi,au chanzo chake ni nini,hiyo ni hatari sana maana kunahatari watu waka endelea kuogelea katika bwawa la umasikini na ikiwa kila siku ana hubiriwa kubarikiwa, Mungu anazo kanuni zake si mchawi useme ukishamwambia tu kuwa unahitaji utajiri au kupona tatizo lako,basi anafanya hapo kwa papo la! Upo wakati Mungu anaweza akafanya hapo kwa papo na anaweza asifanye,anafanya kila jambo kwa utukufu wake na siyo kwa matakwa ya wanadamu,
Unamkua mtu anakimbilia kwa watumishi kuombewa ili afanikiwe kwanza hana kazi yeyote anayoweza kuifanya na mikono yake ili Mungu azidishe kipato chake,bali yeye anachotaka na mali,na hataukimpa kashuguli kakufanya hataki au hafanyi na akifanya anafanya kwa uvivu,
Isitoshe anahitaji mafanikio ukimuuliza anatakakufanikiwa ili mafanikio ayafanyie nini hana jibu,anataka akanyanyase ndugu zake,na na kutaka kuonekana kwamba nayeye amepata, kingine huyu mtu anayetaka mafanikio ya kifetha,wazazi wake Alisha korofishana nao mda mrefu tu wakati mwingine ana miaka sita au kumi hawana hata mawasiliano kwamba wazazi wapo hai au walisha fariki,yeye anaishi maisha kama ndege,
Lakini si kosa lake yeye hajitambuwi anaona kama kawaida tu, ndiyo maana kunawengine wanataka kuombewa kuowa au kuolewa ila hawako tayari kubeba majukumu,bali wameona tu,harusi zimekuwa nyingi sasa na wao wanataka kuongeza hesabu ya harusi yao,wengine wivu tu,kwasababu rafiki yake ameowa au kuolewa,nitalielezea hilo somo baadaye,
Hata kama utaombewa na mtumishi gani hapa duniani kama na wewe hutofuata kanuni za ki-Mungu kwa lolote unalolitaka ni bure utazeeka mpaka kufa maisha yako hayatabadilika badi wewe utaishi kwa kutiwa moyo na kushahuriwa kila inapo itwa leo,
Fuatilia maandiko hapa ili ubarikiwe nilazima kuwepo na chanzo cha hayo mafanikio, na kama ukiwa na chanzo alafu umefungwa kufanikiwa ni kugumu pia
Utabarikiwa mjini,utabarikiwa mashambani,utabarikiwa uzao wa tumbo lako,na uzao wa nchi yako.na uzao wa wanyama wako wa mifugo yako,maungeo ya ng”ombe wako na wadogo wa kondoo zako,litabarikiwa kapu na chombo cha kukandia unga, kumbu kumbu la tarati 28:3-5)
Chakunishangaza mimi nipale unamkuta mtu kila kukicha ni kwa watumishi anataka kuombewa maombi ya kufanikiwa ki uchumi lakini yeye mwenyewe,anatamka kabisa kwamba ameamuwa kuviacha vyote na kumtumikia Mungu, Kuacha vyote na kumtumkia Mungu ni jambo nzuri sana,ila kumbuka na wewe unatakiwa kuishi kimwili na kiroho kimwili unahitaji chakula cha kupika ule upate nguvu ya kumtumikia yeye aliyekuita, cha kiroho utakipata mathabauni mwa Bwana,
Yupo mwingine anataka kuishi kwaimani kuliko ile Mungu aliyoagiza.ukisoma hilo andiko hapo unaonalimeanza kukubariki mjini,yaani kile unachokifanya pale mjini,atakibariki pale ulipo haijalishi ni mjini au kijijini,ila uwe nakitu cha kufanya, utabarikiwa mashambani mtu hata bustani kidogo hana na wakati mwingine hataki alafu anataka Baraka sasa hizo Baraka unazotaka je?zianguke kama mvua?
Kisha bwana anaendelea kukubariki atabariki uzao wako,hapo kwenye uzao ndipo kwenyewe wengi wameshindwa hatakuelewa wafanye nini,maana wanafanya bidii kweli kweli,na kusoma hilo andiko kwamba kuzaa ni Baraka za bwana, sasa kama unaliamini andiko la kuzaa mbona la kujishugulisha iliufanikiwe kiuchumi uslisomi?
Kwanza hapa uzao kutajwa ni wa tatu,inamaanisha unabarikiwa kwaza mjini kile unachokifanya upate fetha za kutosha hata ukijakuzaa unakuwa na uwezo wa kulea,na pili linabarikiwa shamba lako, maana akija mtoto anakuta Baraka za mjini na za mashambani, na mifugo mbali mbali sasa wengine wanaanza uzao kwaza kabila ua Baraka zilizo tangulizwa na Bwana,
Kwanza nikuambie tu ndugu yangu kuanza kuzaa kabila ya kupata Baraka hizi nyingine zilizo tajwa lazima kichwa kitakuuma tu,achana na wale wanaokuambia eti kila mtoto anazaliwa na riziki yake baada ya mda akishakuwa anaanza kuwahi kwenye vyombo vya habari kutaka misaada,mimi
Mimi siipingi misaada.mtu kuomba au kupewa, hata mimi ni mmoja wa mtu ninayependa kusaidia wahitaji,ila nimejionea kwa macho watu wanafanya vitu ambavyo wanahisi wako sawa lakini kumbe wamefungu ufahamu na muovu, hata wanacho fanya, hawakielewi, kusema kila mtoto anakuja kwa riziki yake,
Je kuna mtoto anayezaliwa na na chakula au mavazi? Hayupo hata kuishi kwake anahitaji kula kunywa kusoma na mengineyo,hivyo tafuta kwanza chanzo ndipo uombe Baraka za kuzidishiwa, na Mungu musa akaulizwa una nini mkononi,yesu alipotaka kuwalisha maelfu akawauliza mnanini?
Mungu alipotaka kumuokowa Lutu akamwambia ajenge safina,bwana hakushindwa kumuokowa kwa kutumia njia nyingine,bali alitaka Lutu ajishugulishe ili kuwepo na chanzo,tafuta chanzo cha mafanikio yako acha kutafua njia ya mkato,ni wakati wa umakini sana kwa sasa vinginevyo utajikuta unaliwa kekundu
Ndugu Mtazamaji/ MSOMAJI; Bila shaka unampenda Mungu Sana tunaamini hivyo Kwa vile ulivyoweza kufika mahali hapa tulipo kupitia Mtandao huu, lipo kusudi la Mungu kutaka kukusaidia jambo Fulani ikiwa uko tayari katika yote jiepushe na mafundisho yasiyokuwa ya ki-Mungu Mathayo 16:6-12) piga simu kwa masaada zaidi huduma hii ni bure 0757328311