Ni jambo gani linatokea Mkristo anapoanguka katika dhambi ya zinaa?
Ni muhimu ufahamu hili, kabla ya kujua utafanyaje ikiwa umeanguka katika dhambi ya zinaa.
Mambo matatu makubwa yanatokea mkristo anapoanguka katika zinaa;
Anaukosa Ufalme wa Mungu:
Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, UASHERATI, Uchafu, Ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo; katika hayo NAWAAMBIA MAPEMA. Kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU. (Wagalatia 5:9-21)
Kumbuka kuwa Mtume Paulo aliandika waraka huu kwa Wagalatia walio wakristo na siyo kwa Wagalatia ambao siyo wakristo. Waraka unaanza hivi; Paulo, Mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu), na ndugu wote walio pamoja nami, kwa MAKANISA YA GALATIA” (1:1,2)
Yesu Kristo alisema. “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi Ni Alfa Na Omega mwanzo Na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Heri wazifuao nguo zao, wawe Na amri kuuendea huo mti WA uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako mbwa, Na wachawi, Na WAZINZI, Na wauaji, Na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.”(Ufunuo 22:12-15)
Soma pia kitabu cha Waefeso 5:5
(b) Anatengwa na Wakristo wenzake.
Mtume Paulo alipokuwa akiwaandikia wakristo wa Korintho alisema hivi:
“Yakini habari imeenea kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika mataifa….. Mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo….. Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi. Sisemi msichangamane kabisa Na wazinzi WA dunia hii, au Na wenye kutamani, au Na wanyanganyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. Lakini mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyanganyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.” (1 Wakorintho 5:1,2-11)
Nchi nzima inaadhibiwa
Lisikieni neno la Bwana, enyi wana WA Israeli, Kwa maana Bwana ana mateto nao wakaao katika nchi, Kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi. Hapana neno ILA kuapa Kwa uongo, Na kuvunja ahadi, Na kuua Na kuiba, Na kuzini; huruka mpaka, na damu hugusana na damu. Kwa ajili hiyo NCHI ITAOMBOLEZA, Na kila mtu akaaye ndani yake ATADHOOFIKA, pamoja Na wanyama WA kondeni Na ndege WA angani, naam, samaki wa baharini pia wataondolewa….. Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa….. Nao watakula, lakini hawatashiba; watafanya zinaa, lakini hawataongezeka, kwa sababu wameacha kumwangalia Bwana. Uzinzi na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu” (Hosea 4:1-3; 6, 10,11)
Kwa sababu ya uzinzi, gharika iliangamiza watu na vitu vilivyokuwa katika nchi, alipona Nuhu na watu wachache na viumbe wachache. Kwa sababu ya zinaa, Sodoma na Gomora iliteketezwa kwa moto, wakapona Lutu na binti zake wawili.
Na kwa sababu ya zinaa siku hizi nchi zimepigwa kwa ugonjwa wa Ukimwi (AIDS). Ni Kama Nabii Hosea alivyotabiri, NCHI ZINAOMBOLEZA, WATU WANADHOOFIKA, WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA YA MUNGU, NA WANAPOTELEWA NA FAHAMU!
Ndiyo maana ni muhimu ufahamu ufanye nini ikiwa umeanguka katika zinaa. Si mapenzi ya Mungu uangamie, usiurithi ufalme wake, wakristo wakutenge na kuiangamiza nchi, bali mapenzi yake ni watu wote waifikie toba ya kweli, waokolewe, waziache njia zao mbaya, na wamgeukie na kumfuata daima!
Kwa hiyo Kama umeanguka katika zinaa, sikiliza ushauri ufuatao:
Usiifiche dhambi:
Najua unaweza kuwaficha wanadamu wasijue umezini, lakini unaweza kwenda wapi utakakojificha Mungu asikuone? Soma Zaburi ya 139:7-13. Na imeandikwa:-
Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. (Mithali 28:13)
Ukifuatilia habari za Mfalme Daudi, utaona ya kuwa kitu alichokifanya baada ya kuanguka katika zinaa na mke wa mtu, ni kujitahidi kutafuta namna ya kuifunika hiyo dhambi, lakini alishindwa. Na mwisho wake aliamua kutafuta mbinu ya kumuua Uria, ambaye mke wake ndiye aliyezini na Mfalme Daudi. Unaweza ukaona ya kuwa ni kweli kwamba uzinzi huondoa ufahamu za mtu. Kwa nini Mfalme Daudi aliamua kuua ili alifiche kosa alilofanya?
Je! Alidhani Mungu naye hajamwona? Mungu aliinua mtu wake, ambaye alikwenda kwa Mfalme Daudi na kumweleza jinsi Mungu alivyochukizwa na kitendo hicho. Daudi alipojua dhambi iko wazi mbele za Mungu alitubu!
“Bwana asema hivi, Angalia, nitakuondoshea uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa wake zako mbele ya macho yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako mbele ya jua hili.
Maana wewe ulifanya jambo hili mbele ya Israeli wote na mbele ya jua. Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia Bwana dhambi. Nathani akamwambia Daudi, Bwana naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa. LAKINI, KWA KUWA KWA TENDO HILI UMEWAPA ADUI ZA BWANA NAFASI KUBWA YA KUKUFURU, motto atakayezaliwa kwako hakika yake atakufa.” (2 Samweli 12:11-14)
Ni kweli kwamba unaweza ukafanya uzinzi kwa siri, Mke wako asijue, au mume wako asijue, au wazazi wako na ndugu zako wasijue, au waliookoka wenzako wasijue, Lakini, FAHAMU HAKIKA YA KUWA MUNGU AMEKUONA.
Na mshahara wa dhambi ni mauti, kwa hiyo kama unataka kudumu katika uzima uliopewa na Kristo, usijaribu kuificha dhambi.
Tubu, Tengeneza na Usirudie tena.
Ikiwa umeanguka katika dhambi ya uzinzi, njia iliyo wazi ni wewe kutubu kwa Mungu katika Roho na Kweli, halafu tengeneza (tubu) kwa wale uliowakosea na usirudie tena; na mwisho songa mbele katika wokovu aliokupa Bwana.
Kuna mtu mmoja aliniambia nimsaidie katika kumwombea Kwa kuwa kuna wakati alianguka katika zinaa, na baadaye akatubu. Lakini kila wakati yalikuwa yanamjia mawazo ya kuhukumu ya kuwa alizini na kwa hiyo anajiona hafai tena hata kuomba wala kuendelea na wokovu. Ingawa alitubu bado alishitakiwa Sana moyoni na kosa alilolifanya. Aliona Kama vile Mungu hajamsamehe.
Inawezekana na wewe ukasumbuliwa na hali ya namna hii. Nafahamu ya kuwa wanadamu ni wagumu kusamehe na kusahau, hata kama wanajua umekwisha tubu na kutengeneza.
Lakini nataka nikuambie hivi, usiupime msamaha anaokupa Mungu unapotubu kwa kuangalia na kusikiliza wanadamu wanasemaje juu yako; bali angalia neno lake katika biblia linasemaje. Imeandikwa hivi;
Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi anaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zenu, wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote (1 Yohana 2:1,2)
Ndugu Mtazamaji/ MSOMAJI; Bila shaka unampenda Mungu Sana tunaamini hivyo Kwa vile ulivyoweza kufika mahali hapa tulipo kupitia Mtandao huu, lipo kusudi la Mungu kutaka kukusaidia jambo Fulani ikiwa uko tayari katika yote jiepushe na mafundisho yasiyokuwa ya ki-Mungu Mathayo 16:6-12) piga simu kwa masaada zaidi huduma hii ni bure 0757328311
MWENYE HAKI ATAISHI KWA IMANI:
Ukisha mkri kristo yesu kuwa kama Bwana na Muokozi wa maisha yako, unatakiwa uishi kwa imani
Kuwa na imani ni kuwa na hakika ya mambo tunayotumainia; kusadiki kabisa mambo tusiyoyaona. Maana wazee wa kale walipata kibali cha Mungu kwa sababu ya imani yao.
Kwa imani sisi tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu; vitu vinavyoonekana kutoka vitu visivyoonekana. Kwa imani Abeli alimtolea Mungu dhabihu iliyokuwa bora zaidi kuliko ile ya Kaini. Kwa imani yake alikubaliwa na Mungu kuwa mwadilifu; Mungu mwenyewe alizikubali sadaka zake. Kwa imani yake ingawa amekufa, bado ananena.
Kwa imani Henoki alichukuliwa na Mungu, asipate kufa. Hakuonekana tena kwa sababu Mungu alikuwa amemchukua. Maandiko yasema kwamba kabla ya kuchukuliwa kwake, yeye alikuwa amempendeza Mungu. 6Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu.
Kwa maana kila mtu anayemwendea Mungu ni lazima aamini kwamba Mungu yuko, na kwamba huwatuza wale wanaomtafuta. 7Kwa imani Noa alionywa na Mungu juu ya mambo ya baadaye ambayo hakuweza kuyaona bado. Alimtii Mungu, akajenga ile safina ambamo aliokolewa yeye pamoja na jamaa yake. Kutokana na hayo ulimwengu ulihukumiwa, naye Noa akapokea uadilifu unaotokana na imani. Kwa imani Abrahamu alimtii Mungu alipoitwa aende katika nchi ambayo Mungu angempa iwe yake. Ingawa hakujua alikokuwa anakwenda, Abrahamu alihama. Kwa imani aliishi kama mgeni katika nchi aliyoahidiwa na Mungu. Aliishi huko katika hema kama walivyoishi Isaka na Yakobo, ambao pia walishiriki ahadi ileile.
Maana Abrahamu alikuwa akingojea mji wenye misingi imara, mji ambao Mungu mwenyewe ndiye fundi aliyeubuni na kuujenga. Kwa imani hata Sara aliamini kwamba Mungu hutimiza ahadi zake, Kwa hiyo akajaliwa kuchukua mimba ingawaje alikuwa amepita umri. Kwa hiyo, kutoka katika mtu huyo mmoja, Abrahamu, ambaye alikuwa kama amekufa, walitokea watu wengi wasiohesabika kama vile nyota za mbinguni na mchanga wa pwani. Watu hawa wote walikufa wakiwa na imani.
Walikufa kabla ya kupokea mambo ambayo Mungu alikuwa ameahidi, lakini kwa mbali waliyaona, wakashangilia, na kukiri wazi kwamba wao walikuwa wageni na wakimbizi duniani. Watu wanaosema mambo Kama hayo, huonyesha wazi kwamba wanaitafuta nchi yao wenyewe.
Kama wangalikuwa wanaifikiria nchi walikotoka zamani, wangalipata nafasi ya kurudi huko. Lakini sasa wanataka nchi iliyo bora zaidi, yaani nchi ya mbinguni. Ndiyo maana Mungu haoni haya wakimwita yeye Mungu wao, kwa sababu yeye mwenyewe amekwisha watayarishia mji. 17Kwa imani, Abrahamu alimtoa mwanae Isaka sadaka wakati Mungu alipomjaribu.
Huyo Abrahamu ndiye aliyekuwa amepokea ahadi ya Mungu, lakini, hata hivyo, alikubali kumtoa dhabihu mwanae wa pekee, ingawa Mungu alikuwa amemwambia: "Wazawa wako watatokana na Isaka." Abrahamu aliamini kwamba Mungu anaweza kuwafufua wafu: na kwa namna fulani kweli Abrahamu alimpata tena mwanae kutoka wafu. 20Kwa imani Isaka aliwabariki Yakobo na Esau, wapate baraka zitakazokuja baadaye. 21Kwa imani Yakobo alipokuwa karibu kufa, aliwabariki kila mmoja wa wana wa Yosefu, akamwabudu Mungu akiegemea ile fimbo yake.
Kwa imani Yosefu alipokuwa karibu kufa, alinena juu ya kutoka kwa Waisraeli katika nchi ya Misri, na pia akawaachia maagizo kuhusu mifupa yake. 23Kwa imani wazazi wa Mose walimficha huyo mtoto kwa muda wa miezi mitatu baada ya kuzaliwa kwake. Walimwona kuwa ni mtoto mzuri, wala hawakuiogopa amri ya mfalme.
Kwa imani Mose alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mwana wa binti Farao. Aliona ni afadhali kuteseka pamoja na watu wa Mungu kuliko kufurahia raha ya dhambi kwa kitambo kidogo. Alitambua kwamba kuteseka kwa ajili ya Masiha kuna faida kubwa zaidi kuliko utajiri wote wa nchi ya Misri, maana alikuwa anatazamia tuzo la baadaye. Kwa imani Mose alihama kutoka nchi ya Misri bila kuogopa hasira ya mfalme; na wala hakurudi nyuma, kwani alikuwa kama mtu aliyemwona yule Mungu asiyeonekana. Kwa imani aliadhimisha siku ya Pasaka, akaamuru damu inyunyizwe juu ya milango, ili yule Malaika Mwangamizi asiwaue wazaliwa wa kwanza wa Israeli. 29Kwa imani watu wa Israeli walivuka bahari ya Shamu, kana kwamba ilikuwa nchi kavu; lakini Wamisri walipojaribu kufanya hivyo walikufa maji.
Kwa imani kuta za mji wa Yeriko zilianguka watu wa Israeli walipokwisha zunguka kwa muda wa siku saba. Kwa imani Rahabu aliyekuwa malaya hakuangamia pamoja na wale waliomwasi Mungu, kwa sababu aliwakaribisha wale wapelelezi. Basi, niseme nini zaidi? Wakati hauniruhusu kueleza juu ya Gedeoni, Baraki, Samsoni, Yeftha, Daudi, Samweli na manabii.
Kwa imani hawa wote walipigana vita na wafalme, wakashinda. Walitenda mambo adili, wakapokea yale aliyoahidi Mungu. Walifunga vinywa vya simba, 34Walizima mioto mikali, waliepuka kuuawa kwa upanga. Walikuwa dhaifu lakini walipata nguvu. Walikuwa hodari katika vita wakashinda majeshi ya kigeni. Na, wanawake walioamini walirudishiwa wafu wao wakiwa wamefufuliwa.
Baadhi yao walikataa kufunguliwa, wakateswa mpaka kufa ili wapate kufufuliwa na kuingia katika maisha bora zaidi. 36Wengine walidhihakiwa na kupigwa mijeledi, na wengine walifungwa minyororo na kutupwa gerezani. Walipigwa mawe, walipasuliwa vipandevipande, waliuawa kwa upanga. Walizungukazunguka wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi, walikuwa watu maskini, walioteswa na kudhulumiwa. Ulimwengu haukustahili kuwa na watu hao.
Walitangatanga jangwani na mlimani, wakaishi katika mashimo na mapango ya ardhi. Watu hawa wote walionekana kuwa mashujaa kwa sababu ya imani yao. Hata hivyo, hawakupokea yale ambayo Mungu aliwaahidia, maana Mungu alikuwa ameazimia mpango ulio bora zaidi kwa ajili yetu; yaani wao wangeufikia ukamilifu wakiwa pamoja nasi.

Subscribe to:
Posts (Atom)