NENO NI NURU YA MUNGU

1Habari hii ya yahusu Neno la uzima lililokuwako tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu. Sisi tumepata kulisikia na kuliona kwa macho yetu wenyewe tukaliamini ; tulilitazama na kulishika sisi wenyewe tukapata . Uzima huo ulipotokea sisi tuliuona na sasa tunasema habari zake na kuwaambieni juu ya uzima huo wa milele uliokuwa kwa Baba na uliodhihirishwa kwetu. 3Tulichokiona na kukisikia ndicho tunachowatangazieni ninyi pia ili nanyi mpate kushirikiana nasi katika umoja tulio nao na Baba na Mwanae Yesu Kristo. 4Tunawaandikia ninyi mambo haya kusudi furaha yetu ikamilike. 5Basi, habari tuliyoisikia kwake Yesu na tunayowahubirieni ndiyo hii: Mungu ni mwanga  yaani nuru na hamna giza lolote ndani yake. 6Tukisema kwamba tuna umoja naye,na papo hapo twaishi gizani, tutakuwa tumesema uongo kwa maneno na matendo. 7Lakini tukiishi katika mwanga, kama naye alivyo katika mwanga, basi tutakuwa na umoja sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwanae, inatutakasa dhambi zote. 8Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe na ukweli haumo ndani yetu. 9Lakini tukiziungama dhambi zetu, basi Mungu ni mwaminifu na mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote. 10Tukisema kwamba hatujatenda dhambi, tutakuwa tumemfanya Mungu mwongo, na neno lake halimo ndani yetu.

YESU KRISTO ANAJIBU NINI KUHUSU TALAKA?

1Yesu alitoka hapo akaenda mkoani Yudea na hata ng`ambo ya mto Yordani. Umati wa watu ukamwendea tena, naye akawafundisha tena kama ilivyokuwa desturi yake. 2Basi, Mafarisayo wakamwendea, na kwa kumjaribu wakamwuliza, "Je, ni halali mtu kumpa talaka mkewe?" 3Yesu akawajibu, "Mose aliwapa maagizo gani?" 4Nao wakasema, "Mose aliagiza mume kumpatia mkewe hati ya talaka na kumwacha." 5Yesu akawaambia, "Mose aliwaandikia amri hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. 6Lakini tangu kuumbwa ulimwengu, Mungu aliumba mwanamume na mwanamke. 7Hivyo mwanamume atawaacha baba yake na mama yake, ataungana na mkewe, 8nao wawili watakuwa mwili mmoja. Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja. 9Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asitenganishe." 10Walipoingia tena ndani ya nyumba, wanafunzi wake walimwuliza juu ya jambo hilo. 11Naye akawaambia, "Anayemwacha mkewe na kuoa mwingine, anazini dhidi ya mkewe. 12Na mwanamke anayemwacha mumewe na kuolewa na mwingine anazini." 13Watu walimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawakemea. 14Yesu alipoona hivyo, alikasirika akawaambia, "Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu walio kama watoto hawa. 15Nawaambieni kweli, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hataingia katika Ufalme huo." 16Kisha akawapokea watoto hao, akawawekea mikono, akawabariki. 17Yesu alipoanza tena safari yake, mtu mmoja alimjia mbio, akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, "Mwalimu mwema, nifanyeje ili niupate uzima wa milele?" 18Yesu akamjibu, "Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake. 19Unazijua amri: `Usizini; Usiue; Usiibe; Usitoe ushahidi wa uongo; Usidanganye; Waheshimu baba na mama yako."` 20Naye akamjibu, "Mwalimu, hayo yote nimeyazingatia tangu ujana wangu." 21Yesu akamtazama, akampenda, akamwambia, "Umepungukiwa na kitu kimoja: nenda ukauze vitu ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate." 22Aliposikia hayo, alisikitika, akaenda zake akiwa na huzuni, kwa maana alikuwa na mali nyingi. 23Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, "Jinsi gani itakavyokuwa vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!" 24Wanafunzi walishangazwa na maneno yake. Yesu akawaambia tena, "   25Ni rahisi zaidi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu." 26Wanafunzi wake wakashangaa sana wakaulizana, "Ni nani basi, atakayeweza kuokoka?" 27Yesu akawatazama, akawaambia, "Kwa binadamu haiwezekani, lakini kwa Mungu si hivyo, maana kwa Mungu mambo yote huwezekana." 28Petro akamwambia, "Na sisi je? Tumeacha yote, tukakufuata!" 29Yesu akasema, "Kweli nawaambieni, kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu, au dada, au mama, au baba, au watoto au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Habari Njema, 30atapokea mara mia zaidi wakati huu wa sasa nyumba, ndugu, dada, mama, watoto na mashamba pamoja na mateso; na katika wakati ujao atapokea uzima wa milele. 31Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza."

TUNAELEKEA WAPI?

HUYU NDIYE NABII TITTO ANAYEHAMINI KWAMBA POMBE NI TIBA SAHIHI KWA MAGONJWA YOTE

Leo nilipata mgeni wa ghafla ofisini kwangu aliyejitambulisha kwa jina la Nabii Titto.Nabii Titto yeye anahubiri matumizi ya pombe kwa kutumia Biblia,anasema kuwa mungu ameruhusu watu wanywe pombe kwani ni tiba sahihi kwa magonjwa mbalimbali .Alikuja ofisini kwangu ili nimsaidie kurekodi kanda na cd mbalimbali zitakazomafanya watu mbalimbali duniani kupata neno lake na kunisihi sana na kuniambia nikubali kwani ilo ndio ombi mungu alilomtuma kwangu.Mimi sikumkubalia ombi lake kwani ninavyoamini mimi na imani yanguni vitu viwili tofauti.Je Wadau mnasemaje kuhusu Nabii Titto

Juma Chikoka (Chopa mchopanga) akiwa na Jackline Wolper na Johari wakimsikiliza Nabii Titto kwa umakini mkubwa


Kipeperushi hiki cha Nabii Titto kiliniacha hoi


Nabii Titto yeye anadai kuwa ameoteshwa na mungu kuwa watu wanywe pombe kwani ni tiba sahii tosha kwa magonjwa mbalimbali na si pombe tu mpaka sigara,Sikuamini maneno yake akatumwa mtu alete pombe na Nabii Titto bila hiyana kudhihirisha umma akakata safari beer,Wadau mpooo


Hiki ndicho kipeperushi alichotugawia kinachoeleza jinsi pombe inavyotibu magonjwa yote


Nikisikiliza mahubiri ya Nabii Titto ameniambia yuko njiani kuanzisha kanisa


Nabii Titto akiwa katika mavazi yake ya kikazi


Nabii Titto akinukuu neno kutoka kwenye kitabu cha mungu(BIBLIA)kinachoruhusu matumizi ya pombe huku pombe yake ikiwa pembeni

UKIONA MAMBO HAYA YANATOKEA JIANDAE

Ishara hizi maana yake ni nini ukiona mvua chukuwa jembe wahi shambani,

Yesu alitoka Hekaluni, na alipokuwa akienda zake, wanafunzi wake walimwendea, wakamwonyesha majengo ya Hekalu. 2Yesu akawaambia, "Sawa, mnaweza kuyatazama haya yote! Kweli nawaambieni, hakuna hata jiwe moja litakalosalia hapa juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa." 3Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni, wanafunzi walimwendea faraghani, wakamwuliza, "Twambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonyesha kuja kwako na mwisho wa nyakati?" 4Yesu akawajibu, "Jihadharini msije mkadanganywa na mtu. 5Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu wakisema: `Mimi ndiye Kristo,` nao watawapotosha watu wengi. 6Mtasikia juu ya vita na fununu za vita; lakini msifadhaike, maana hayo hayana budi kutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado. 7Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi. 8Yote hayo ni kama mwanzo wa maumivu ya kujifungua mtoto. 9"Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa ajili ya jina langu. 10Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana. 11Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi. 12Kwa sababu ya ongezeko la uhalifu, upendo wa watu wengi utafifia. 13Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, ataokoka. 14Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya Ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote. 15"Basi, mtakapoona `Chukizo Haribifu` lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake), 16hapo, walioko Yudea na wakimbilie milimani. 17Aliye juu ya paa la nyumba yake asishuke kuchukua kitu nyumbani mwake. 18Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake. 19Ole wao kina mama waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo! 20Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe siku za baridi au siku ya Sabato! 21Maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka leo, wala haitapata kutokea tena. 22Kama siku hizo hazingalipunguzwa, hakuna binadamu yeyote ambaye angeokoka; lakini siku hizo zitapunguzwa kwa ajili ya wale walioteuliwa. 23"Basi, mtu akiwaambieni siku hizo: `Kristo yuko hapa` au `Yuko pale,` msimsadiki. 24Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Watafanya ishara kubwa na maajabu ya kuweza kuwapotosha ikiwezekana hata wateule wa Mungu. 25Sikilizeni, nimekwisha kuwaonya kabla ya wakati. 26Basi, wakiwaambieni, `Tazameni, yuko jangwani,` msiende huko; au, `Tazameni, amejificha ndani,` msisadiki; 27maana, kama vile umeme uangazavyo toka mashariki hadi magharibi, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu (Yesu kristo). 28Pale ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai. 29"Mara baada ya dhiki ya siku hizo, jua litatiwa giza, mwezi hautaangaza, nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa. 30Kisha, ishara ya Mwana wa Adamu itaonekana angani, na hapo makabila yote duniani yatalalamika; watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya angani mwenye nguvu na utukufu mwingi. 31Naye atawatuma malaika wake wenye tarumbeta la kuvuma sana, nao watawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, toka mwisho huu wa mbingu hadi mwisho huu. 32"Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. 33Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo haya yote yakitendeka, jueni kwamba yuko karibu sana.Mwana wa Adamu kuja  34Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo yote kutukia. 35Naam, mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu (yesu kristo anasema) hayatapita kamwe. 36"Lakini, juu ya siku au saa hiyo, hakuna mtu ajuaye itakuja lini;

UTAMTAMBUWA VIPI?

Ndugu zangu:, msimsadiki kila mtu asemaye kwamba ana Roho wa Mungu, bali chunguzeni kwa makini kama huyo mtu anaongozwa na Roho wa Mungu au la, Maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguni na wanatumia kitabu kitakatifu kufichia maovu yao. 2Hii ndiyo njia ya kujua kama mtu anaongozwa na Roho wa Mungu au la!: Kila anayekiri kwamba Kristo ni Mungu  na alivaa mwili wa binadamu akaja duniani, mtu huyo anaye Roho wa Mungu. 3Lakini mtu yeyote asiyemkiri Kristo hivyo, hana huyo Roho atokaye kwa Mungu. Mtu huyo ana roho ambaye ni wa Adui wa Kristo; nanyi mlikwisha sikia kwamba anakuja, na sasa tayari amekwisha wasili ulimwenguni! 4Lakini ninyi, watoto, ni wake Mungu na mmekwisha washinda hao manabii wa uongo; maana Roho aliye ndani yenu ana nguvu zaidi kuliko roho aliye ndani ya hao walio wa ulimwengu. 5Wao husema mambo ya ulimwengu, nao ulimwengu huwasikiliza kwani wao ni wa ulimwengu. 6Lakini sisi ni wake Mungu. Mtu anayemjua Mungu hutusikiliza, mtu asiye wa Mungu hatusikilizi. Basi, kwa njia hiyo tunaweza kutambua tofauti kati ya Roho wa ukweli na roho wa uongo. 7Wapenzi wangu, tupendane, maana upendo hutoka kwa Mungu. Kila mtu aliye na upendo ni mtoto wa Mungu, na anamjua Mungu. 8Mtu asiye na upendo hamjui Mungu, maana Mungu ni upendo. 9Na Mungu alionyesha upendo wake kwetu kwa kumtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni, ili tuwe na uzima kwa njia yake. 10Hivi ndivyo upendo ulivyo: si kwamba sisi tulikuwa tumempenda Mungu kwanza, bali kwamba yeye alitupenda hata akamtuma Mwanae awe sadaka ya kutuondolea dhambi zetu. 11Wapenzi wangu, ikiwa Mungu alitupenda hivyo, basi, nasi tunapaswa kupendana. 12Hakuna mtu aliyekwisha mwona Mungu kamwe; lakini kama tukipendana Mungu anaishi katika muungano nasi, na upendo wake unakamilika ndani yetu. 13Tunajua kwamba tunaishi katika umoja na Mungu, naye Mungu anaishi katika umoja nasi, kwani yeye ametupa Roho wake. 14Sisi tumeona na kuwaambia wengine kwamba Baba alimtuma Mwanae awe Mwokozi wa ulimwengu. 15Kila mtu anayekiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu anaishi katika muungano na mtu huyo, naye anaishi katika muungano na Mungu. 16Basi, sisi tunajua na tunaamini upendo alio nao Mungu kwetu sisi. Mungu ni upendo, na kila mtu aishiye katika upendo, anaishi katika muungano na Mungu, na Mungu anaishi katika muungano naye. 17Upendo umekamilika ndani yetu kusudi tuweze kuwa na ujasiri Siku ile ya Hukumu; kwani maisha yetu hapa duniani ni kama yale ya Kristo. 18Palipo na upendo hapana uoga; naam, upendo kamili hufukuza uoga wote. Basi, mtu mwenye uoga hajakamilika bado katika upendo, kwani uoga huhusikana na adhabu. 19Sisi tuna upendo kwa sababu Mungu alitupenda kwanza. 20Mtu akisema kwamba anampenda Mungu, hali anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Maana mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hamwoni. 21Basi, hii ndiyo amri aliyotupa Kristo: Anayempenda Mungu anapaswa pia kumpenda ndugu yake.

SIMU YA FAIDA

Neema ya Mungu na iwe pamoja nawe, Na ni Duwa yangu na maombi yangu kwa haya machache yakapate kuwa baraka kwako wewe unayesoma wakati huu, ni Jambo la kusadikika kwa wandugu wengi wamekuwa wakipoteza vipato vyao kwa kujisahau tu, ila ukikumbushwa bila nshaka utafanya vizuri hili linakujia kwa manufaa ya wewe mwenyewe hivyo ni ihari yako kuchukuwa hatuwa au kuacha, Umeona kichwa cha habari kina elezea Simu ya Faida ni kweli simu ni chombo kizuri sana japo kizuri pia kinaweza kuwa na kasoro kikitumika kinyume cha matumizi,

Sehemu hii isikushangaze sana kwaajili ya kuelezea habari za simu kama ukizibiti hapa kipato chako kinaweza kuongezeka wafanya Biashara wa mitandao ya simu wanajitahidi sana kuboresha wasasiliano kwakupunguza bei ili kuhakikisha kila mtu amemiliki simu na ametumia sasa kutumia simu siyo vibaya wala huwezi kumpangia mtu atumie vipi pesa zake ila si kila anayefanya jambo anafanya kwauwelewa mkubwa kama wako ndio maana tunachukuwa fursa hii kusaidiana kwa hao wa chache wanaovujisha pesa zao bila matarajio yao,


ninaamini umewahi kuona au kusikia mtu anapigiwa simu au kupiga simu anaanza kuongea karibia mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari anatumia simu tu kuongea na yanasikika anayoongea si biashara useme ametumia pesa kuingiza pesa bali ametowa pesa bila faida na hajutii kupoteza hizo hela, tena anashabikia kwa ushaba kabisa labda kama ni kwenye basi hamuwezi tena kuongea wengine ni yeye tu na maneno yake ya ushamba ila wapo wengine akipokea simu au kupiga simu mara 3 tu ameshatengeneza pesa kama milioni mia nne hivi na bado ametulia sasa wewe unabiga simu ambazo haziingizi hata mia

Sasa kwa mtu wa Mungu jitahidi simu ya itengeneze hela siyo simu ya kuulizia matatizo tu na Harusi piga simu wamekuwekea kiasigani cha pesa bank au wametuma mzigo wa beigani, usione watu wamenyamaza wapinga miruzi peke yao tayari kimeshaeleweka sasa na wewe unaiga si kila kitu ni chakuiga utaumia unamkuta mtu anaangaika na simu masaa mawili anatafuta mtu wakumpigia kisa ana shilingi elfu mbili salio, siku ukiwa huna salio unazima simu au unaanza kuwasumbuwa watu kwa kuwabeep ili wakupigie ukiwa unadaiwa simu haipatikani unawasha kwa machale, ukifikia hivyo yamesha kushinda unaweza ukawahiwa na mgambo siku moja kwa hiyo tabia yako,

Mungu ametupatia akili kila mmoja ajisimamie mwenyewe lazima utumie akili, wengi wanao lalamika sasa hivi kuwa maisha ni mabaya waliyaharibu awali na siyo hivi karibuni hivyo si rahisi kutambuwa kuwa unatengeneza kilio cha baadaye kwa hayo unayoyafanya,badala ya kicheko cha abaadaye,

Lazima mwanadamu aishi kwa utaratibu jifunze hata kwa kuona kwa wengine kilicho watokea, hata kama ni mtu anakuja kukutembelea aje kwako  kwa jambo maalumu  siyo kiholela tu, wenzetu waliwahi kulitambuwa hili ndiyo maana walifanikiwa mapema na haraka, mtu akija kwako mkishamaliza lililomleta mwambie arudi kufanya shuguli zake kwa bidii ni bora akuone katili utakuwa umemsaidia kuliko kumwendekeza ukamsababishia matatizo mbeleni wakati haijulikani kama utakuwepo au hautakuwepo

Lazima tuishi kwa kuukombowa wakati wewe ukizembea zembea kitakacho kuchangamsha ni uzee ambao utakuvamia kama mwifi uzee nao una kuja kwa kasi kubwa mno,wewe usijione kama bado ni kijana ukitaka kufahamu ulipo fikia watafute wale uliosoma nao shule ya msingi ukiwaangalia utajuwa kuwa umeshazeeka,usitake kukamatika waliokamatika walikuwa kama wewe,

Una heri wewe umepata hata wakukumbusha amka sasa jitahidi wewe uwe wa tofauti ili uwe wa tofauti ni lazima ufanye jambo la tofauti na wengine ili upate matokeo tofauti ila ukifanya jambo linalo fanana na wengine usitegemee matokeo tofauti na wengine,

Hata biashara za watu wengi zinaharibika kwa kutotumia maarifa wengine wanafukuzwa kazi kwa kutotumia maarifa wewe unajijuwa ni mfanya biashara ila majibu yako kwa wateja si mazuri kabisa pia unafunguwa  biashara umechelewa unategeme nini usitafute kisingizio lolote katika maisha yako chunguza kabla huja laumu,

SWALI LA MAISHA

JE USALAMA UPO?
Babu wa miaka 70 alinamuuliza mkewe je mke wangu unajisikia huzuni mimi ninavyo kimbinzana na Mabinti wadogo? mke anamjibu hapana mpenzi wangu  siuzuniki maana hata umbwa hukimbiza magari wakati hawawizi  hata kuendesha, sasa sababu ya mbwa kukimbiza magari ni nini ikiwa hawezi hata kuendesha? JE umeshawahi kuona au kusikia watu wa namna hii kama jibu ndiyo,sababu ni zipi? umewahi kujiuliza na jibu ukapata lipi?

kwa nini mtu ambaye hajakuzaa  wala hajui hata chanzo chako akuuwe kabla ya wakati wako, vifo vingine ni vya kujitakia kama jambo huliwezi kwanini usikubali matokeo, na kwanini usiombe msaada, hata inchi zikiwa zinapigana vita mara nyingine huomba msaada kwa inchi jirani, yupo Rafiki wa karibu sana mwenye uwezo wa kukusaidia ila unampita unakwenda kupata ushahuri kwa mwanadamu, Dunia yote asilimia ya watu wengi wanatembea na shida zao unaweza kufikiria yako ni kubwa kumbe ukakuta ya mwenzako ni kubwa zaidi yako, je mtu kama huyu atakusahuri nini ikiwa na yeye uko kwenye kibano chake.

kama vifo vingine siyo vya kujitakia unamkuta mtoto yuko bado masomoni tena kidato cha pili ana mchumba huyo mchumba ni wakazigani wakati huo kama siyo mtu kuwabize na kuing"owa roho yake, maana huyu binti akuachika akiwa kidato cha pili hawezi hatakujisimamia mwenyewe atakimbilia kujiuwa, wazazi tupunguze umbali wa sisi na watoto wetu kuwa mbali na mtoto siyo kumtuza kwa maadili mema kama unavyofikiria wewe inawezekana mtoto wako kashaumizwa na mwanaume maana watoto ni wageni hapa duniani sisi tumewatangulia tuwasaidie kwa ukaribu,

magonya makubwa  na mengi hivi leo ospitalini ukiuliza ni magonjwa ya moyo,ukiuliza kwa nini utaambiwa mawazo hayo mawazo kwa nini yakuvuruge na mtu ambaye hujazaliwa naye wala humjui vizuri kwasababu ya ahadi za hapa na pale tayari wewe unakubali umwachia moyo wako wate, usiyachokoze mambo ambayo hayajafikia mda wake yata kutanguliza kaburini alifu yenyewe yataendelea kusona mbele, si kila unacho kiona unaweza kukipata au kinaweza kuwa chako lah! na si kila unachosikia kuhusu wewe au mtu mwingine ni kweli,na si kila unachokipenda lazima ukipate akili kichwani mwako,

 je umbwa anakimbiza Gari analipenda?au anataka kukwenda wapi,au analipata kama analihitaji? unaweza ukakipenda kitu kumbe ni sumu kwako je mbwa akikosea akaingia kwa tairi anaweza kupoteza maisha yake lakini yeye mwenyewe ndiye chanzo cha kifo chake usikubali kujiua mwenyewe kabla ya umri wako kwa kukimbiza usichojuwa unakimbizia nini,

70 yr old man asks his wife "Do you feel sad
 when you see me running after young girls?"
Wife replied, “No, not at all; even dogs chase
 cars yet they can't drive''. 


SABABU YA MWANADAMU KUTENGANA NA MUNGU:

  Maovu ni chanzo kikubwa  kinacho sababisha maombi ya mtu yasijibiwe na hata kutenganisha  kati ya  mwanadamu na Mungu, isaya 59:2 lakini maovu yenu yamewafarakanisha ninyi na Mnungu wenu na Dhambi zenu zimeuficha uso wake Mungu musiuone,
MunguMtakatifu hana ushirika na dhambi. Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi Mwanadamu hujaribu kumfikia Mungu kwa nija nyingi: dini, matendo mema, sala, n.k., lakini hizi zote hazitoshi. Mwanadamu bado ni mwenye dhambi. na wala hakuna Dini yenye uwezo wakumfutia mwanadamu thambi zake mwenye uwezo wakufuta thambi za mwanadamu ni mmoja tu yesu kristo,

YESU KRISTO NI NJIA YA PEKEE YA KUONDOA DHAMBI. Alikufa kwa ajili yetu ili tujue upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yetu. 1 petro 3:18  Yesu akawaambia mimi ndimi  njia na kweli na uzima Mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi yohana 14:6 hakuna mtume wala nabii wa aina yeyote aliyepita hapa Duniani aliyewahi kutamka haya maneno zaidi ya Yesu mwana wa Mungu aliye hai,kwamba yeye ni njia na kweli na uzima

Ni yeye aliyekubali kuutowa uhai wake kwaajili ya ulimwengu na hayupo mwingine  aliyewahi hata kujaribu kufanya hivyo,ila yeye akafa na kisha akashinda mauti  akafufuka baada ya siku tatu  Yesu peke yake  hivyo Mwanadamu peke yake hawezi kushirikiana na Mungu. kwakuwa  mwanadamu alitenda dhambi  Mungu alimtuma Yesu afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na tena awe daraja kati yetu na Mungu ili atulete kwa Mungu.  inawezekana ukahitaji kurudisha mahusiano yako Na Mungu kama kweli umemahanisha unaweza kuisali kama hujamaanisha haikuhusu, endelea kusoma mengine,yatakayokusaidia kukupa wewe muongozo wa kuishi vile Mungu anavyoagiza,

Followers