JE UMEWAHI KUSIKIA AU KUSEMA?

                   Matendo peke yake hayatoshi kukupa ufalme wa Mungu Japo wengi wetu na hata wengine wamekuwa wakiimba namna matendo yanavyo hitajika. hata mimi sipingi juu ya hilo,ila matendo ni kwaajili ya wanadamu,

yeye Mungu anauangalia moyo wako kwamba umemaanisha kiasi gani,kama ni matendo kuna wazoefu wa kuigiza utakatifu,ingekuwa ni kirahisi hivyo,kila mmoja angeweza kuigiza matendo mema,ili arithi ufalme wa Mungu maana tunapo zungumuzia ufalme wa Mungu tunaongelea maisha ya Baadaye ya ahadi kwetu

 Kuna watu wengi sana ambao ni waaminifu sana katika kusali na kumtolea Mungu sadaka, lakini hawakubaliani na jambo kuokoka. Wanaona kuwa wao tayari wameokoka kwa sababu tu wanasali, wanatoa sadaka na kujitahidi kuishi katika matendo mema. Hebu soma   maneno ya mistari hii uone yanavyopingana na msimamo huu;

“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; WALA SI KWA MATENDO, mtu awaye yote asije akajisifu” (Waefeso 2:8,9)

          Tunaokoka kwa njia ya imani itendayo kazi katika Yesu Kristo, “Wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu”. Matendo yana faida zaidi kwa mtu baada ya kuokoka. Na pia imani bila matendo, imani hiyo imekufa nafsini mwake. Biblia inasema hivi:
           “Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! ile imani yaweza kumwokoa?…. Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. Lakini mtu atasema, wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha IMANI YANGU KWA NJIA YA MATENDO YANGU …….. Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa” kwa mkristo anayemkiri kristo kama Bwana na muokozi wa maisha yake ni vema maisha ya kuigiza tukayaacha na kumaanisha,ni rahisi kwa watu wengi kushuhudia kuwa ameokoka akifikiri anamdanganya mwanadamu,ila yupo mwenye uwezo wa kuichunguza Roho,yako na kwa nafsi au kwa akili ya ki-uwanadamu usijidanganye kuishinda thambi,huna uwezo hata kidogo wa kuishinda thambi yaaina yeyote ile ni rahisi kuwadanganya wanadamu kwakuwa hawaishi na wewe ila hiyo nayo ni hatari maana Mungu anaweza kuyafunuwa maovu yako,ukaaibika hapa Duniani mpaka kule mbinguni, je ungependa kupatana na Mungu wako hivi sasa karibu katika wana wa waflume wa Mungu,,,,,

Tamka maneno haya kwa kinywa chako maana kwa moyo mtu huamini  akahesabiwa haki na kwa kinywa mtu hukiri akapata uwokovu" sema Mungu wa nimetambuwa kuwa mimi nilikutenda thambi wewe,hata mara nyingine pasipo kusudia mara nyingi ni mekutenda thambi katika mawazo,na hata katika matendo,Ninakuomba unisamehe na unisafishe kwa kabisa maovu yote niliyokuwa nimeyatenda,ninakiri kutokuyarudia tena,

Ninaamini ya kuwa yesu kristo ni wanawako wa pekee uliyemtuma duniani kuja kutukombowa kwa njia ya msalaba,akasulubiwa pale msalabani,akafa ,akazikwa na siku ya tatu akafufuka toka kwa wafu,na sasa yuko kuume kwa Mungu Baba,nina kuomba bwana uyathibiti maisha yangu tangu sasa,uniongoze jnia ya kwenda Mbinguni, katika jina la Yesu,Amina,

sasa ninaamini mpaka unaitamka sala hii umemaanisha toka moyoni mwako,tayari chukuwa hatuwa  nyingine moja ya imani kama ulivyo soma hapo juu kuwa uwokovu tunaupata kwa imani,umeshafanyika mtoto wa Mungu,Hongera sana karibu katika ufalume wa wana wa mungu wanapigambiyo kwaajili ya mbingu,inawezekana ukawa na maswali kuhusiana na uwokovu tafuta kanisa lolote lile linalofundisha na kuukiri uwokovu nenda pale kutana na mtumishi wa Mungu mweleze kuwa umeokoka baada ya kukutana na sala ya toba kwenye webusaiti ya Mtumishi wa Mungu ukaamuwa kumpa Yesu maisha yako atakusaidia sana,kiroho na hata mara nyingine ki -mahitaji ya kawaida,

ukiona vema Basi karibu unaweza kunipigia simu yangu ya mko,au ukaniandikia baruwa pepe kwa kupitia maelezo haya,,,,

samsonoxpel@gmail.com
samson.mboya@geitagold.com
web site  http://www.samsonoxpel@blogspot.com/
p.obox 532 Geita gold mine
Cell phone no 0756 809 209
"            "       0784 71 36 04

karibu sana ndugu yangu katika Bwana yesu Mungu akubariki  sana kwa maamuzi yaliyo mema katika maisha yako,katika hayo mawasiliano kasoro jumapi kwaanzia asubuhi mpaka jioni sipatikani lakini siku za kawaida ninapatikana,karibu sana,

Followers