Na Mtu wa Mungu Nabii Samson Mboya |
SOMO: KUWA MTUMISHI BORA.
Utangulizi :
Kuna aina nyingi sana za utumishi hapa duniani ila
mimi nitafundisha utumishi wa kimungu tena mtumishi bora maana kuna watumishi
wakidunia na wa kimbingu, na utumishi inategemea unamtumikia nani,yaani wewe ni
mtumishi wa nani,mfano kunamtumishi waserikali,mtumishi wa shetani,mtumishi wa
kampuni mtumishi wa uma naamini umewahi kusikia watu wakitamka hivyo,na kuna
mtumishi wa Mungu- na wao pia wanatofautiana
kuna anayejitambua na asiyejitambua aliyejitambua tunamwita mtumishi
bora baada ya somo hili utajichunguza
wewe mwenyewe kama ni bora, au si bora
Nini maana ya
Mtumishi
Utumishi ni kutumika chini ya mamlaka au agizo
flani au ni kutumwa, sasa katika
utendaji wako mzuri tuna uita bora na hiyo ndiyo inayoitwa (mtumishi bora)
Sifa za Kuwa
mtumishi Bora
- Lazima tuwe na Mahusiano Mazuri na Mungu
- Lazima tuwe na ushirika wakaribu na Mungu
- Lazima tuwe na Uwezo wa kusikia maagizo ya mungu
- Lazima tuwe na uwezo wa kusikia na kutendea kazi Neno la Mungu
- Lazima Uliishi Neno la Mungu
- Lazima Tutambue kusudi la Mungu juu ya Maisha Yetu
- Lazima tujue Mungu anataka tufanye nini(Tujue kusudi la yesu kuja duniani)
Kazi ya
Mtumishi bora,
- Kazi ya mtumishi bora Nikutimiza Mapenzi ya Mungu aliyotuagiza tulifanye hapa duniani
- Kazi ya mtumishi Bora nikutenda kazi pamoja na yesu warumi 8:28
- Kazi ya mtumishi Bora ni mkumdhihirisha Mungu Hapa duniani mfano:
Kuwafunguwa waliofungwa katika magereza ya nguvu za
giza,kuwaponye wagonjwa wote kufufua waliokufa n.k Luka 4:18
- Kazi ya mtumishi Bora Kufungua watu kutoka katika vifungo mbali mbali vya mwil, nafsi na roho.LUKA MTAKATIFU 8:26-29. Wakafika pwani ya nchi ya wageresi, inayoelekea
- Kazi ya Mtumishi bora Kuliandaa kanisa la mwisho liwe tayari kwa ajili ya unyakuo.2 TIMOTHEO 4:1-5 Nakuagiza mbele za mungu, na mbele za kristo yesu,atakayewahukumu walio hai na walokufa;kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake; lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia,kemea,na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima;ila kwa kuzifuata
- Kazi ya Mtumishi bora ni kuwa hodari katika bwana na jasiri,usiyeyumbishwa na chochote kile katika utumishi wako.ili kukamiliza kazi ya Mungu au Maono uliyopewa
- JOSHUA 1:7-9 Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru mussa mtumishi wangu;
- Kazi ya mtumishi Bora ni kumuwakilisha Mungu Katika utakatifu Uwe mtumishi uliye msafi,usiwe na tamaa yoyote,usiwe mwingi wa hasira, usiwe mgomvi, uwe kielelezo safi mbele za watu wa aina zote! 2petro 2:15YAKOBO 4:1-5. Vita vya toka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu,katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu? Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata.Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.Ufanye nini ili uwe mtumishi Bora
- Lazima uwe na mahusiano ya kudumu na Mungu
- Lazima uwetayari kutumika
- Lazima ukae mbali na dhambi
- lazima ukubali kuongozwa na Roho Mtakatifu
- Lazima uwe mtu wakujichunguza kwa Neno Mungu
- Lazima ukubali kuwa Msikivu wa Neno
- Lazima uwe mtendani
- Lazima uwe Mnyenyekevu
- Lazima uwe Mtiifu
- Lazima uwe mkamilifu
- Lazima Ukubali kuwa tayari wakati wowote
- Jifunze Cheni ya Mkono wa Mungu na kudumu katika mafundisho
- Laazima ujiepushe na Maovu ya kila namna,
- Lazima Uchaguwe watu wakushirikiana nao vitu vya kiMungu
- Lazima uwe shujaa wa Imani
- Lazima Uwe tayari kuzibeba chapa za kristo,
- Lazima utembee katika agizo
- Huruhusiwi Kuogopa vipingamizi vya aina yeyote,
- Hutakiwi Kujitharau kwa namna yeyote ile
Usijidharau
kutokana na jinsi ulivyo,na kukata tamaa
kwa sababub yoyote ile, mfano:- Elimu, jinsia,
umri, kabila, taifa. Mungu hana ubaguzi, jinsi ulivyo amekuchagua
uwe mtumishi wake.
Matendo
ya mitume 10:34-35. Petro akafumbua
kinywa chake,akasema,Hakika natambua ya kuwa mungu hana upendeleo; bali katika
kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.2 TIMOTHEO 2:15 -Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli!1
TIMOTHEO 4:16 -Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.
2 TIMOTHEO 2:24-26. Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu; akiwaonya kwa upole wao washindanao naye,ili kama ikiwezekana mungu awape kutubu na kuijua kweli; wapate tena fahamu zao,na kutoka katika mtego wa ibilisi,ambao hao wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake.... LINAENDELEA,,,,