Semina ya wiki moja
Baada ya kujifunza vyanzo vya mafanikio na watu kufunguliwa Nira shingoni mwao na Kutuwa mizigo yao sasa hatuwa inayofuata ni ya muhimu pia, unaweza kwenda kuchukuwa hatuwa ulizojifunza ili kujiandaa na kupokea zile Baraka bwana alizokuandalia kupitia kazi za mikono yako,
Iwe ni biashara au ajira, kulima,kufuga na mengineyo uliyojifunza usikae bila shuguli ya kufanya na mikono yako Bwana alimwagiza Adamu kumiliki na kutawala kwakuwa Alisha muwekea vitu vyakutawala na kuvimiliki,naakapewa agizo lakuituza bustani ya Edeni,
Sasa wewe ni nani usiyetaka kujishugulisha na kitu alafu unataka Mungu akufanikishe, ninakushahuri hataukiwa sehemu yenye mahubiri ya neon la Mungu na Muhubiri akaita watu wakuwaombea Baraka, jiulize kwanza hizo Baraka zitapitia wapi,kama utakuwa huna kila kitu, huna njiwa,huna kuku huna bata huna mbuzi huna ng”ombe huna bustani huna shamba, fikiria mara mbili wewe utapokelea mlango upi?
Ninajuwa kwa wewe usiyetaka kujishugulisha na shuguli yeyote huduma hii itakuuthi lakini ni bora upate hasira ukimaliza kusoma huu ujumbe na wewe ukawe na kitu cha kufanya,
Hata kama umemtembelea ndugu yako na unajuwa unaishi naye mwezi mzima hajalishi unasubiri majibu ya shule au ya kazi au unavyo juwa wewe mwenyewe,jitahidi siku isiishe hujafanya jambo lolote pale unapo ishi, ni hatari sana siku nzima kuisha bila kufanya jambo lolote linaloweza kuulipia huo muda,
Uza mda wako upate pesa kama umeshindwa kuutumia wewemwenyewe.
Watu huwa wanapenda kuyatumia maneno ambayo kwao hayafanyi kazi kabisa, mtu anasema muda ni mali haya muulize huo muda anaosema ni mali amezalisha kiasi gani maana kile unacho faidika nacho ndichotunacho kibadilisha na masaa ndipo tuna sema muda ni mali,kwa mfano kuna watu wameajiriwa hao wamekubaliana na mwajiri kwa makubaliano ya kuuziana masaa kwamba mimi nitakuuzia masaa yangu yote ya mwezi mzima unilipe,
Mwingine kibaruwa ana kubaliana na mwajiri wake walipane kwa kutwa kwamba atamuuzia masaa ya kutwa nzima, mwingine kwa nusu siku,mwingie kwa lisaa limoja,inategemea, mwingine anaamuwa kuyanunuwa masaa yake yote kwa kuijajiri shuguli zake mwenyewe anafahamu kabisa ataamuka saa ngapi kwenda kwa shuguli zake na atakamilisha saa ngapi,
Sasa wewe ndugu yangu ambaye umebakia kuwalaumu wazazi na ndugu zako kuwa hawakusaidii,je?wewe umejisaidia vipi au kwa lipi? Maana kuna wale wenzangu wao ni kulaumu tu kwamba ndugu wana uwezo alafu hawamsaidii,wakati huo hataki kujishugulisha na kitu chochote nikwenda kuzurura na marafiki,wasio eleweka na wao,au waliomzidi ujanja wa kimaisha, hatakama ndugu ana mali nyingi hizo si zako nay eye amezingaikia hakukaa kama wewe unavyo kaa,alafu akazipata,
Uondoke sasa ukatafute kitu cha kufanya ukiwa unamuomba
mungu,katika kukaa bila kujishugulisha muovu anaweza kuitumia nafasi hiyo kukupa kazi,ya uwovu ukamuuthi Mungu,ukawa kama daudi daudi alijikuta anaingia kwenye thambi bila hata ya kupana akilini mwake,,,,,,,,,,
Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa UTAJIRI WAKE KRISTO USIOPIMIKA; na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote, ili sasa, kwa njia ya Kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho"(Waefeso 3:8 - 10).
Na Mungu wangu atawajazeni KILA MNACHOHITAJI KWA KADIRI YA UTAJIRI WAKE KATIKA UTUKUFU,NDANI YA KRISTO YESU" (Wafilipi 4:9)
Kristo ana utajiri usiopimika. Na wote walio ndani yake ni warithi pamoja naye wa utajiri usiopimika. Kutokana na utajiri huo TUNAJAZWA KILA TUNACHOKIHITAJI. Mahitaji haya ni ya kiroho, kiakili na kimwili. Kwa hiyo hakuna sababu ya mkristo kuishi maisha ya kupungukiwa, ikiwa Kristo yuko ndani ya moyo wake pamoja na utajiri wake usiopimika. Kikubwa kama wewe ni mrithi basi ni jukumu lako kuendeleza huo urithi kwakufuata kanuni yake Mungu
Jambo la kujiuliza ni hili; kwa nini utajiri huu wa Kristo usiopimika hauonekani katika maisha ya wakristo wengi? Wakristo waishije katika ushuhuda wa wokovu ndani ya Kristo, wakati wanaishi katika ulimwengu wenye hali ngumu kiuchumi? Watumishi wa Mungu kwa mfano, wachungaji, wainjilisti na kadhalika, waishije katika kumtumikia Mungu vizuri bila kupoteza ushuhuda wao wakati wanaishi katika mazingira yenye maisha magumu kiuchumi na bado wanasimamia amaandiko kuwa wao ni vichwa hawatakuwa mkia,na hata watoto wao wamewafundisha kuishi kama kichwa na siyo mkia wakati watu wakiwatazama kwa macho wanaonekana kama mkia,
wewe kama mkristo ukiyafuata maagizo ya Mungu ipasavyo hutohitajika hata kushuhudia yale Mungu aliyokutendea bali watu watashuhudia maana watakuwa wameshuhudia kwa macho yao,umewahi kujiuliza kuhusiana na maisha wanayoishi,wakristo?
Haya si maswali mepesi kuyajibu, lakini ni muhimu yatafutiwe ufumbuzi. Kabla hatujaanza kuyajibu napenda tusome Waefeso 4:11;
" Naye (Yesu Kristo) alitoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti; na wengine kuwa wachungaji na Waalimu."
Ni kwa kusudi gani Bwana Yesu Kristo aliamua kuwaweka hawa katika kazi yake kanisani? Waefeso 4:12-16 inatupa maelezo:-
"Kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo, ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. Katika yeye mwili wote ukiunganishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo
siku ya pili
Kutafuta chanzo cha mafanikio yako kabla ya kutaka mafanikio,
Tumejifunza na kuona baathi ya mateso unayopiti au magonjwa hukuyapatia ukubwani wala hukuambukizwa kwa sababu zako bali chanzo chake kimetokea mbali sana kwa wazazi na hata mara nyingine si kwa wazazi hao ulio nao yaani Baba na mama la! Inawezekana kutoka kwa Mababu na ma Bibi, yapo mambo mengi umetamkiwa tangu ukiwa tumboni,au ulipozaliwa tu,
Inawezekana kabisa mengi yakawa ulitamkiwa mazuri lakini je? Na katika hayo yakakufanikisha mipango mzima ya hapa duniani je nay ale maneno mabaya waliyo kutamkia nayenyewe ulishawahi kuambiwa lolote kuhusiana na hilo,
Si rahisi kugunduwa kuwa unalo tatizo la kurithishwa na wazazi, je? Kwa nini baathi ya makabila mtoto akizaliwa kwenda kumuona ni mpaka yule anayetaka kumshika mtoto anatakiwa awe na hela mkononi ya kumzawadia, wengine mtoto akizaliwa anakabithiwa hale ya noti mkononi mwake, kwa nini?wengine wanaonyeshwa majembe ya kulimia,
kila kabila lina imani yake kuhusiana na kuzaliwa kwa mtoto wewe mwenyewe unafahamu kwa kabila lako kuwa mtoto akizaliwa huwa wanamuonyesha kitu gani,na kutamka nini juu ya mtoto, wengine nimpaka wafanyiwe matambiko ya kimila,(kimizimu)
Ndiyo maana wengine wanakimbilia kanisani kumuweka wakufu kwa mungu,wengine kwa wachawi wanaita kuzindika,je wewe unalijuwa hilo juu yako kwamba nini kilifanyika,hiyo ni siri ya wazazi na wakati mwingine kwa kutofahamu kwa wazazi wako anakupelekea wewe kusumbuliwana magonywa ya kurithi,au kujikuta unaishi na mapepo mwilini bila yaw ewe kufahumu maana wazazi inawezekana walifanya hivyo kwalengo la kutaka kukulinda,je unafikiri yule mchawi aliyekuzindika bado yupo hai,na kama bado anaishi je wateja zake si wewe na wazazi wako,hivyo kama aliweza kukuwekea mapepo ya kukulinda na wachawi wenzake
Basi anaweza kukuloga pia ili mradi wake uweze kuwa endelevu hayupo mtu yeyote hapa Duniani anayependa kufanya kazi kwa hasara hakuna lazima atahakikisha amekutumia mapepo ya kuku sumbuwa ili muwe wateja wa kudumu kwake, wengine kweli hamkwenda hata kwa wachawi bali, mmekuwa mkitembea na magonjwa ya kuamkiwa na wazazi,au na laana ya kutamkiwa tangu tumboni mwa mama yako.kwa sababu ya babishano ya wazazi,
Ujumbe uliyokuwa umetawala katika mabango yaliyokuwa yanawakaribisha watu wote wa mji ili waje kuhuthuria katika semina ile ya siku tatu pele nyantorotoro katika mji wa geita, ulikuwa unasomeka
Tena itakuwa katika siku hiyo Mzigo wake utaondoka begani mwako na Nira yake shingoni, nayo Nira itaharibiwa kwasababu ya kutiwa mafuta, Isaya 10:27 somo hili lili fafanuliwa kwa kina sana na hata wewe ni vema ukafahamu kwamba vifungo vingi kufunguka vina hitajika kwaza mtu aliyefungwa kufundishwa Neno la Mungu kuhusiana na kifungo maana kila mtu ambaye hajakombolewa anacho kifungo chake, anahitaji kufundishwa na kuombewa kaajili ya kuharibiwa hivyo vifungo na maagano na laana,na mikosi ya kila namna,
Kwa mfano Kuna wakati mwingine unajikuta unahasira za kupita kawaida, na hata hujachokozwa na mtu yeyote yule umejikasirisha mwenyewe tu tena umeamka kitandani na unaishi chumbani peke yako, huja wowa wala kuolewa lakini ukiamka asubuhi unahisi hasira kali kabisa zakutaka hata kuuwa mtu, wakati mwingine mpaka unalia.sababu huielewi,
Hizo ni roho za mapepo zimekuvamia bila wewe kufahamu, si mpango wa Mungu wewe kuamka umejinyonga na hasira neno la Mungu halisemi juu ya Adamu kuamka na jaziba au asira katika ile bustani ya Edine, bali huyu bwana aliishi kwa Furaha mpaka thambi ilipoingia pale bustanini na kumvamia kupitia mkewe ndipo vurugu zikaanzia hapo, hivyo tunaona kwamba chanzo cha mwanadamu kuvamiwa na roho chafu nipale anapoaza kumkosea Mungu kwa kutofuata maagizo yake,na kutenda thambi,
Kwa sababu wazazi wako inawezekana kwamba mungu walimjuwa na hata sasa wato wengi swala la Mungu ukilionea wanalikubali na wengine wanakuambia kuwa hakunashida kabisa yeye anamfahamu Mungu toka utotoni mwake,asijuwe ni kwa sababu wazazi walimlelea hivyo,
Kwa kumfundisha maadili ya kwamba Mungu yupo na mahala pakukutana na Mungu wengine wakafundishwa ni kanisani,ila mimi nina kuambia mungu hakai mahala pamoja bali yupo kila mahala, na wala hayuko upande mmoja wewe unaweza kugeukia popote pale na ukiwa vyo vyote, bila ya kuangalia unauwezo au huna bila ya kuangalia nguo uliyovaa au viatu au huna Mungu anachokiangalia ni moyo wa mwanadamu ambao unaweza kumsababisha mwanadamu kutenda thambi,
Kuhubiriwa mahubiri ya kupata Baraka peke yake bila kufundishwa hizo Baraka zinatokea upande upi,au chanzo chake ni nini,hiyo ni hatari sana maana kunahatari watu waka endelea kuogelea katika bwawa la umasikini na ikiwa kila siku ana hubiriwa kubarikiwa, Mungu anazo kanuni zake si mchawi useme ukishamwambia tu kuwa unahitaji utajiri au kupona tatizo lako,basi anafanya hapo kwa papo la! Upo wakati Mungu anaweza akafanya hapo kwa papo na anaweza asifanye,anafanya kila jambo kwa utukufu wake na siyo kwa matakwa ya wanadamu,
Unamkua mtu anakimbilia kwa watumishi kuombewa ili afanikiwe kwanza hana kazi yeyote anayoweza kuifanya na mikono yake ili Mungu azidishe kipato chake,bali yeye anachotaka na mali,na hataukimpa kashuguli kakufanya hataki au hafanyi na akifanya anafanya kwa uvivu,
Isitoshe anahitaji mafanikio ukimuuliza anatakakufanikiwa ili mafanikio ayafanyie nini hana jibu,anataka akanyanyase ndugu zake,na na kutaka kuonekana kwamba nayeye amepata, kingine huyu mtu anayetaka mafanikio ya kifetha,wazazi wake Alisha korofishana nao mda mrefu tu wakati mwingine ana miaka sita au kumi hawana hata mawasiliano kwamba wazazi wapo hai au walisha fariki,yeye anaishi maisha kama ndege,
Lakini si kosa lake yeye hajitambuwi anaona kama kawaida tu, ndiyo maana kunawengine wanataka kuombewa kuowa au kuolewa ila hawako tayari kubeba majukumu,bali wameona tu,harusi zimekuwa nyingi sasa na wao wanataka kuongeza hesabu ya harusi yao,wengine wivu tu,kwasababu rafiki yake ameowa au kuolewa,nitalielezea hilo somo baadaye,
Hata kama utaombewa na mtumishi gani hapa duniani kama na wewe hutofuata kanuni za ki-Mungu kwa lolote unalolitaka ni bure utazeeka mpaka kufa maisha yako hayatabadilika badi wewe utaishi kwa kutiwa moyo na kushahuriwa kila inapo itwa leo,
Fuatilia maandiko hapa ili ubarikiwe nilazima kuwepo na chanzo cha hayo mafanikio, na kama ukiwa na chanzo alafu umefungwa kufanikiwa ni kugumu pia
Utabarikiwa mjini,utabarikiwa mashambani,utabarikiwa uzao wa tumbo lako,na uzao wa nchi yako.na uzao wa wanyama wako wa mifugo yako,maungeo ya ng”ombe wako na wadogo wa kondoo zako,litabarikiwa kapu na chombo cha kukandia unga, kumbu kumbu la tarati 28:3-5)
Chakunishangaza mimi nipale unamkuta mtu kila kukicha ni kwa watumishi anataka kuombewa maombi ya kufanikiwa ki uchumi lakini yeye mwenyewe,anatamka kabisa kwamba ameamuwa kuviacha vyote na kumtumikia Mungu, Kuacha vyote na kumtumkia Mungu ni jambo nzuri sana,ila kumbuka na wewe unatakiwa kuishi kimwili na kiroho kimwili unahitaji chakula cha kupika ule upate nguvu ya kumtumikia yeye aliyekuita, cha kiroho utakipata mathabauni mwa Bwana,
Yupo mwingine anataka kuishi kwaimani kuliko ile Mungu aliyoagiza.ukisoma hilo andiko hapo unaonalimeanza kukubariki mjini,yaani kile unachokifanya pale mjini,atakibariki pale ulipo haijalishi ni mjini au kijijini,ila uwe nakitu cha kufanya, utabarikiwa mashambani mtu hata bustani kidogo hana na wakati mwingine hataki alafu anataka Baraka sasa hizo Baraka unazotaka je?zianguke kama mvua?
Kisha bwana anaendelea kukubariki atabariki uzao wako,hapo kwenye uzao ndipo kwenyewe wengi wameshindwa hatakuelewa wafanye nini,maana wanafanya bidii kweli kweli,na kusoma hilo andiko kwamba kuzaa ni Baraka za bwana, sasa kama unaliamini andiko la kuzaa mbona la kujishugulisha iliufanikiwe kiuchumi uslisomi?
Kwanza hapa uzao kutajwa ni wa tatu,inamaanisha unabarikiwa kwaza mjini kile unachokifanya upate fetha za kutosha hata ukijakuzaa unakuwa na uwezo wa kulea,na pili linabarikiwa shamba lako, maana akija mtoto anakuta Baraka za mjini na za mashambani, na mifugo mbali mbali sasa wengine wanaanza uzao kwaza kabila ua Baraka zilizo tangulizwa na Bwana,
Kwanza nikuambie tu ndugu yangu kuanza kuzaa kabila ya kupata Baraka hizi nyingine zilizo tajwa lazima kichwa kitakuuma tu,achana na wale wanaokuambia eti kila mtoto anazaliwa na riziki yake baada ya mda akishakuwa anaanza kuwahi kwenye vyombo vya habari kutaka misaada,mimi
Mimi siipingi misaada.mtu kuomba au kupewa, hata mimi ni mmoja wa mtu ninayependa kusaidia wahitaji,ila nimejionea kwa macho watu wanafanya vitu ambavyo wanahisi wako sawa lakini kumbe wamefungu ufahamu na muovu, hata wanacho fanya, hawakielewi, kusema kila mtoto anakuja kwa riziki yake,
Je kuna mtoto anayezaliwa na na chakula au mavazi? Hayupo hata kuishi kwake anahitaji kula kunywa kusoma na mengineyo,hivyo tafuta kwanza chanzo ndipo uombe Baraka za kuzidishiwa, na Mungu musa akaulizwa una nini mkononi,yesu alipotaka kuwalisha maelfu akawauliza mnanini?
Mungu alipotaka kumuokowa Lutu akamwambia ajenge safina,bwana hakushindwa kumuokowa kwa kutumia njia nyingine,bali alitaka Lutu ajishugulishe ili kuwepo na chanzo,tafuta chanzo cha mafanikio yako acha kutafua njia ya mkato,ni wakati wa umakini sana kwa sasa vinginevyo utajikuta unaliwa kekundu
Ndugu Mtazamaji/ MSOMAJI; Bila shaka unampenda Mungu Sana tunaamini hivyo Kwa vile ulivyoweza kufika mahali hapa tulipo kupitia Mtandao huu, lipo kusudi la Mungu kutaka kukusaidia jambo Fulani ikiwa uko tayari katika yote jiepushe na mafundisho yasiyokuwa ya ki-Mungu Mathayo 16:6-12) piga simu kwa masaada zaidi huduma hii ni bure 0757328311
ROHO MTAKATIFU NA KAZI ZAKE KWETU
SOMO LA 1 semina
ROHO MTAKATIFU,MTOA UTAKATIFU
Katika somo la kwanza katika mfululizo wa masomo haya yanayohusu Roho Mtakatifu,Tulijifunza kwamba Roho Mtakatifu,ni mtakatifu,hivyo anakuwepo na kudumu mahali palipo na utakatifu tu.Tukiwana maisha ya uchafu,yaani dhambi;humfanya Roho Mtakatifu akose makao kwetu,na hivyo hawezi kuwepo kwetu.Kama alikuwepo mwanzo kwetu,huondoka (1Samweli 16:14;
Zaburi 51:4,10-11).Sasa swali linakuja,tunawezaje kuwa watakatifu katika maisha yetu ili Roho Mtakatifu afanye makao
kwetu?Jibu ni kwamba,Roho Mtakatifu ,ndiye huyohuyo anayetoa utakatifu tunaouhitaji.Sasa tunamwangalia Roho
Mtakatifu kama Mtoa Utakatifu,kwa kutafakari kazi yake hiyo katika vipengere vitano:-
1. ROHO MTAKATIFU,ROHO ATUPAYE KUZALIWA MARA YA PILI
2. ROHO MTAKATIFU ROHO AWAFUFUAYE WATU WALIOKUFA KIROHO
3. ROHO MTAKATIFU, ROHO AWATIAYE UZIMA WATU WALIOZIMIA KIROHO
4. ROHO MTAKATIFU ROHO ATUPAYE UTAKASO
5. ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUPAYE TUNDA LA ROHO

Hatupaswi kamwe kudanganyika kwamba utakatifu siyo duniani ni mbinguni,Maandiko yanaeleza waziwazi
kwamba watakatifu walioko duniani ndiyo anaopendezwa nao Mungu(Zaburi 16:3).Hatupaswi pia
kudanganyika kwamba tunaweza kufanya dhambi hapa duniani,halafu tukasalimika baada ya kufa,kutokana
na misa ya wafu n.k(1Wakorintho 6:9-10;Waefeso 5:5-7;Wagalatia 6:7;Waebrania 9:27;IYohana 5:16;Kumbukumbu 10:17) la maana hapa ni kufahamu ni jinsi gani tunavyoweza kuwa na ushindi dhidi ya
dhambi hapa duniani,na kuokoka kutupwa motoni,maana bila shaka tunatakiwa kuokoka tukiwa hapahapa
duniani (Luka 19:8-10);Tito 3:3-4)Tunawezaje kuwa na ushindi dhidi ya dhambi?Ni kwa kuzaliwa mara
ya pili,kwa Roho Mtakatifu(Yohana 3:3-10;Tito 3:3-5)Yesu Kristo,alijaribiwa sawasawa na sisi lakini
hakutenda dhambi(Waebrania 4:14-15)Ni nini siri ya ushindi wake huo?Ni kwa sababu alizaliwa kwa
Roho Mtakatifu,yaani alizaliwa tofauti na kawaida ya kimwili ya mume na mke.Sisi nasi tunapotubu dhambi
zetu kwa kumaanisha kuziacha,tunapata rehema hii kwa imani tu(Mithali 28:13)Tunazaliwa mara ya pili
katika ulimwengu wa roho,na hivyo kuwa na uwezo wa kushinda dhambi kwa muujiza mkubwa.Katika
hali ya kawaida ya jinsi tulivyozaliwa kimwili,kamwe hatuwezi kushinda dhambi.Ni mpaka tufanyike viumbe
vipya kwa Roho Mtakatifu.Mwambie Roho Mtakatifu kwamba unataka kuzaliwa mara ya pili,naye atafanya.

Kurudi nyuma na kuacha wokovu kunaitwa pia kufa kiroho(Ufunuo 3:1;Waefeso 2:1).Kwa kila aliyerudi nyuma
na kuacha wokovu,hii ni saa ya kuamka usingizini na kuanza upya(Warumi 13:11-12).Lakini,je,inawezekana
kuanza upya tena katika hali hii?Ndiyo,kwa msaada wa Roho Mtakatifu.Hii ni kazi yake nyingine.Roho Mtakatifu
ndiye aliyemfufua Yesu,alipokufa(Warumi 8:11).Kwa jinsi hiyo hiyo,Roho Mtakatifu anaweza kutufufua kiroho
na kutupa uhai tena wa kiroho(Waefeso 2:1,4-6).Mwambie Roho Mtakatifu kwamba unataka kufufuliwa kiroho,
naye atafanya.
3. ROHO MTAKATIFU, ROHO AWATIAYE UZIMA WATU
Kabla ya kufa kiroho,hutangulia kuzimia kiroho.Shetani hutupeleka hatua kwa hatua,kama upepo katika tairi
unavyotolewa kidogo kidogo kutokana na pancha ndogo.Tukizimia kiroho,upendo wa kwanza unatoweka.
Ingawa bado hatujafikia hali ya kufanya dhambi za uzinzi,uasherati,ulevi n.k kama mataifa,hata hivyo,mambo
ya rohoni yanakuwa hayana mvuto kwetu kama mwanzo.Kuomba,kushuhudia,kuhudhuria ibada n.k,yanakuwa
mzigo kwetu.Tunaanza kuvutwa zaidi na mambo ya dunia.Katika hali hii tunahitaji nguvu mpya,uzima mpya
(Isaya 40:28-31).Anayefanya kazi hii pia ni Roho Mtakatifu,Roho wa uzima(Warumi 8:2).Pepo wa udhaifu
wanatolewa kwa Roho wa Mungu(Mathayo12:28),na vivyo hivyo udhaifu wetu kiroho unatolewa na
Roho wa Mungu.Je umezimia kiroho,Mwambie Roho Mtakatifu akuzindue,naye atafanya.
4. ROHO MTAKATIFU ROHO ATUPAYE UTAKASO
Baada ya kuokolewa,tunahitaji pia kutakaswa.Bila utakaso,tutajikuta bado hatuna ushindi dhidi ya dhambi
za ndani katika mawazo,na moyoni,ingawa tayari tuna ushindi dhidi ya dhambi za kutenda.Dhambi za ndani
,ni kama hasira,wivu,chuki,masengenyo,kugombania ukubwa,kiburi,majivuno,kutokusamehe,kinyongo,
kupenda udunia n.k.Hivi vinaweza vikaonekana kwa watu waliookoka ambao hawajatakaswa:Mawazo
yasiyo ya ki Mungu (Mathayo 16:21-23),kugombania ukubwa (Luka 22:24-26;Mathayo 20:20-22,25-28;
Marko 9:30-37),hasira (Mathayo 20:24)wivu,fitina,ugomvi (Marko 9:38-39;Luka 9:49-50;
1Wakorintho 3:3-5),faraka na matengano(1Wakorintho1:10-13),umimi(Mathayo 28:6-13),
kutokusamehe(Mathayo 18:21-35),chuki,kushindwa kuvumilia maudhi,kushtakiana wapendwa mahakamani
(Luka 9:51-56;1Wakorintho 6:1-8);Warumi 7:15 n.k .Mambo haya huondolewa kwa utakaso.
Ndiyo maana Yesu aliwaombea Utakaso wanafunzi wake waliokuwa tayari wameokoka(Yohana 17:14-19)
Roho Mtakatifu ndiye atupaye Utakaso(1Wakorintho 6:11;1Petro1:2)Je,hujatakaswa,mwambie
Roho Mtakatifu akutakase,yeye ni mwaminifu,atafanya(1Thesalonike 5:23-24)

Katika Wagalatia 5:22-23,tunajifunza juu ya tunda la Roho.Katika lugha ya asili,yote katika mistari hii
yanamaanisha kwamba Tunda la Roho ni moja tu,Upendo.Hata hivyo,upendo huo unadhihirishwa kwetu
katika tabia na matendo kama furaha,amani,uvumilivu,utu wema,fadhili,imani,upole,na kiasi.Ni pale tu
tunapokuwa na maisha yaliyojaa upendo,ndipo tunapokuwa tunatimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yetu.
Pasipo upendo,tunakuwa shaba iliayo na upatu uvumao,tunakuwa si kitu.Lolote jingine tunalolifanya linakuwa
halina faida(1Wakorintho 13:3).Hatuwi wanafunzi wa Yesu (Yohana 15:8)Sasa basi ,ni muhimu kufahamu
kwamba upendo ni tunda la Roho,tunalolipokea kutoka kwa Roho Mtakatifu.Tukilipokea tunda hili,na kukua
kila siku katika upendo (1Wathesalonike 3:12),Kama matunda yanavyokua,ndipo tunapokuwa wanafunzi wa Yesu kwelikweli.Tukiwa na tunda la Roho la upendo,tunakuwa na Furaha ya wokovu ambayo haiwezi kuondoka kwetu
kwa sababu ya majaribu yoyote au kukosekana kwa lolote la kimwili(Yakobo1:2).Tutakuwa na amani ipitayo fahamu
zote(Wafilipi 4:7)inayotuwezesha kuwa na amani na watu ambao tusingeweza kuwa na amani nao.Tutakuwa na
lengo la kutafuta amani na watu wote wakati wote(Waebrania 12:14)Tutakuwa na uvumilivu wa kipekee katika mateso,makwazo kutoka kwa watu n.k Tutakuwa na utu wema kwa watu wengine hata wale ambao hawajaokoka
(Marko 10:17).Tutakuwa na fadhili yaani hali ya kutaka wakati wote watu wanaotuzunguka wawe na furaha.
Tutakuwa watu tuliojaa imani,tusiotetereka kirahisi.Tutakuwana upole yaani unyenyekevu (Mathayo 11:29;
Wafilipi2:5-8)Na pili tutakuwa na kiasi (self-control)yaani uwezo wa kukataa kufanya lile ambalo Yesu hataki,
kwa gharama yoyote.Je,unataka kuwa na tunda la Roho katika maisha yako?Mwambie Roho Mtakatifu,naye atafanya.
SOMO LA 3:ROHO MTAKATIFU,ROHO ATUSAIDIAYE KUOMBA
Kila Mkristo,au mtu aliyeokoka,hana budi kuwa na lengo la kufikia kimo na cheo cha utimilifu wa Kristo katika tabia na Utumishi wa
Mungu(Waefeso 4:11-15)Kufikia kiwango cha Yesu Kristo katika tabia ni jambo linalowezekana,Kama siyo,tusingetakiwa
kuwa wakamilifu na watakatifu kama Baba wa mbinguni alivyo Mtakatifu(Mathayo 5:48;1`Petro 1:15-16)Neno la Mungu pia,
linatufundisha uwezekano wa kuwa na viwango vya utumishi vya yesu alipokuwa duniani,na hata kuzidi(Yohana 14:12).Hata
hivyo haya yote hayawezekani kama sisi siyo waombaji kama Yesu alikuwa mwombaji namba moja.Alifanya maombi alfajiri na mapema
(Marko 1:35).Alijitenga na shughuli mchana na kufanya maombi (Luka 5:15-16)Aliomba jioni (Mathayo 14:23)Wakati mwingine
alifanya maombi usiku kucha(Luka 6:12)Je,sisi tunaweza kuwa waombaji kiasi hiki?Kwa nguvu na jitihada zetu hatuwezi.
Tunaweza tu,tukisaidiwa na Roho Mtakatifu.Ndiyo maana tunajifunza somo hili muhimu leo katika mfululizo wa masomo haya
ya Roho Mtakatifu ,na kichwa cha somo la sasa ni ” ROHO MTAKATIFU,ATUSAIDIAYE KUOMBA”,
NA TUTAJIFUNZA SOMO HILI KATIKA VIPENGERE VINNE:-
6. UMUHIMU WA MAOMBI KATIKA MAISHA YA KIROHO
7. KUSHUKA KWA MUNGU BAADA YA MAOMBI YA KUUGUA NA KULIA
8. MAFUNDISHO TUNAYOYAPATA KUTOKANA NA MAOMBI YA YESU
9. ROHO MTAKATIFU,MSAIDIZI ATUSAIDIAYE KUOMBA
2. UMUHIMU WA MAOMBI KATIKA MAISHA YA KIROHO
Shetani ndiye adui yetu mkuu.Kazi yake ni kuiba chochote kizuri cha kiroho tulicho nacho,na tena kuchinja au kuua na kuharibu yote
mema kwetu kiroho na kimwili.Tukiwa peke yetu,kamwe hatuwezi kupambana na shetani na kumshinda.Hatuna budi kuwa na
Mungu katika maisha yetu ili tumshinde ibilisi.Daudi alimshinda Goliathi kwa Jina la Bwana.Hakumshinda kwa nguvu zake.Kwa maana nyingine hatuwezi kuzaa matunda yoyote mema ya kiroho kama hatuko ndani ya Yesu.Usalama wetu na ushindi wetu wa kiroho,unategemeana
sana na sisis kukaa ndani yake Yesu,yaani sisi kuwa na uhusiano au ushirika na Kristo.Pasipo yeye,sisi hatuwezi kufanya neno lolote
.(Yohana 15:4-5).Kukaa ndani ya Yesu,kunafananishwa na tawi lililounganishwa na shina.Kuunganishwa huko ndiyo uhai wa tawi.
Tawi likijitenga na shina,linanyauka na kufa.Sasa basi,tunaunganisha na Mungu na Mungu tunapokuwa tunawasiliana naye katika maombi.Tukiwa hatuna maisha ya maombi,kimsingi ni kwamba tunakuwa ni tawi lililojenga na shina,na hivyo tunanyauka na hatimaye
kufa kiroho.Hatuwezi kuwa na kitu tusipoomba(Yakobo 4:2)
Tutaingia majaribuni tusipoomba (Mathayo 26:41).Tutapepetwa kama ngano na ibilisi na mazuri yote ya kiroho yataondoshwa,na
imani yetu itatoweka(Luka 22:31-32).Shetani atatumeza na kuturudisha katika ufalme wake(1Petro 5:8).Hatuwezi kuwaleta watu
kwa Yesu,tusipokuwa waombaji,maana Shetani hatawaachia(Zaburi 2:8).Hatuwezi kuona watu wakifunguliwa katika vifungo vya
shetani vya kimwili(Luka 13:16) na vile vinavyotokana na mambo ya rohoni (Matendo 12:5-17).Kwa ufupi tutachukuliwa na
mafuriko ya Shetani(Zaburi 32:6).
3. KUSHUKA KWA MUNGU BAADA YA MAOMBI YA KUUGUA NA KULIA
Maandiko yanatufahamisha kwamba makao ya Mungu mbinguni,ni Mahali palipoinuka,na Mlimani kwenye kiti cha enzi
cha Mungu (Isaya 57:15;Kutoka 24:12-13;Ufunuo 7:9-10).Ingawa Mungu wetu yuko mlimani,maandiko yanasema
tukimwomba,yeye husikia huko mbinguni na kutujibu maombi yetu kwa kuyatenda tunayoyataka (1Wafalme 8:32;Zaburi 76:8;102:19).Hata hivyo,hatuna budi kufahamu pia kwamba katika mazingira Fulani Mungu hushuka kutoka mlimani na kuja
duniani katika hali isiyo ya kawaida.Mungu anaposhuka kwa jinsi hii,hutenda mambo ya kutisha,na ya kushangaza,yasiyo ya
kawaida na hivyo kuwavuta wengi mno kwake(Waamuzi 4:12-16,5:13;Isaya 31:4;Hesabu 11:23-25,31-32).Uamsho hutokea
Mungu anaposhuka,na watu wagumu wa mioyo huvutwa kwa Yesu,walio vuguvugu huwa moto,mambo mengine makubwa ya
kuitikisa jamii kama mamia ya wenye ukimwi kupona kwa mpigo,hutokea,Mungu akishuka.
Hata hivyo kushuka kwa Mungu hutokea baada ya maombi ya kuugua na kulia kwa uchungu mkubwa(Kutoka 2:23-24;3:7-8;
Matendo 7:32-34).Wakati wote Yesu Kristo alimfanya Mungu kushuka katika huduma yake kwa kuwa aliomba kwa kulia sana
na machozi(Waebrania 5:7),na wengine walimuombolezea kwa kilio na uchungu mkubwa(Luka 23:27)Kulia kwa kuugua katika
maombi hushusha majibu ya maombi namna ya kipekee(2Nyakati 34:27;Zaburi 34:17;39:12;51:1-2,17;72:12;12;88:1-2;Isaya 58:9;Yeremia 31:9;Luka 18:7).Sasa basi ni rahisi kuomba maombi kwa kulia na kuugua?jibu ni la,bila msaada wa Roho Mtakatifu,itakuwa kama tunaigiza tu.
4. MAFUNDISHO TUNAYOYAPATA KUTOKANA NA MAOMBI YA YESU
Tunajifunza mambo mengi zaidi kuhusiana na maombi kwa kuyaangalia maisha ya maombi ya Yesu,na
mafundisho yake kuhusu maombi:-
§ Yesu Kristo alikuwa na wakati wa kuomba pamoja na wanafunzi wake(Luka 9:18),Lakini pia alikuwa na muda mrefu wa
maombi ya peke yake (Luka 5:16;Marko 6:45-46).Ni muhimu kujiunga na kikosi cha maombi cha Kanisa na kushiriki
maombi
________________________________________
ya pamoja na wengine,lakini ni lazima kila mmoja kuwa na muda wa kuomba mwenyewe.
§ Yesu hakukubali kuchukuliwa na huduma za kushauri watu,kuwaombea watu n.k na kuziruhusu zimkoseshe kuomba.
Alijua bila maombi,huduma hizo zitakuwa hazina nguvu.Aliziacha huduma,akafanya maombi(Luka 5:15-16).Kabla ya
kuzungumza na watu,alizungumza na Mungu KWANZA.Alifanya maombi ya alfajiri na mapema sana na baadaye
alipokutana na watu ilikuwa rahisi mno kwake kuponya ukoma na kutoa pepo.(Marko 1:35-42).
§ Kabla ya Yesu kutembea juu ya maji,na kukomesha upepo,alikuwa na kipindi kirefu cha maombi(Marko 6:46-51).Vipindi virefu vya maombi vinaweza kutupa uwezo wa kuona yasiyowezekana yakiwezekana!
§ Utukufu wa Yesu ulitokana na maombi!(Luka 9:28-29)Hatuna utukufu wa Mungu kwa kuwa siyo waombaji!Mwombaji,
utukufu wake humwogopesha shetani
§ Alipokuwa na huzuni aliomba hakunung’unika tu na kulalamika,na ghafla alipata ujasiri wa kukabili lolote lile
(Mathayo 26:36-39;47-49).Hatuna ujasiri na tumejaa woga kwa kuwa hatuombi
§ Maombi yake yalikuwa ni vita hasa.Alipokuwa akiomba,alitoka jasho(hari)kama matone ya damu(Luka 22:44)
.Maombi ni mapambano dhidi ya shetani anayezuia majibu yetu(Danieli 10:12-13).Ni lazima iwe ni vita.Mwili ni lazima
tuushughulishe kama wapiganaji hasa,tukiwa katika roho Maombi yenye matokeo makubwa,ni yale ya kutoka jasho!Ni
lazima tumkabili shetani katika vita ya maombi kabla hata hajatushambulia.Katika vita ya siku sita kati ya waisraeli na wamisri,
miaka kadha iliyopita;Waisraeli walishinda Wamisri ingawa walikuwa na ndege nyingi zaidi za kivita kuliko wao,kwa kuwa
walizipiga KABLA hazijaondoka katika vituo vyao.Tusingoje matatizo ndio tuombe!
§ Imani yetu na ya ndugu zetu,inaweza kutokutindika,ikiwa tu tutakuwa waombaji;kinyume cha hapo ni rahisi kumezwa na
shetani(Luka 22:31-32;1Petro 5:8-9)
§ Maombi ndiyo yanafanya tuutunze utakatifu wetu,na kuwa mbali na dunia.Bila maombi ni rahisi kuvutwa na masumbufu
ya dunia(Luka 21:34-36)
§ Yesu aliliombea Kanisa(Yohana 17:14-15).Ni muhimu kuliombea kanisa na siyo kujiombea wenyewe tu wakati wote.
Je tunaweza kuyatendea kazi yote haya kwa nguvu zetu?jibu ni la.Kwa nguvu zetu hatuwezi,bila msaada wa Roho Mtakatifu.
5. ROHO MTAKATIFU MSAIDIZI ATUSAIDIAYE KUOMBA
Shetani anafahamu sana umuhimu wa maombi,na hivyo atatuzuia sana kufanya maombi kuliko yote mengine,
ili tubaki kama matawi ambayo hayajaunganishwa na shina.Anajua pasipo Mungu,sisi hatuwezi neon lolote.
Kwa kujifunza tu juu ya maombi,bado hatuwezi kuwa na maisha ya maombi.Tunaweza kuomba sisi hatuwezi
neon lolote.Kwa kujifunza tu juu ya maombi,bado hatuwezi kuwa na maisha ya maombi.Tunaweza kuomba
siku mbili,tatu,halafu basi.Pamoja na wanafunzi wa Yesu kuhimizwa kuomba na Yesu mwenyewe,bado
walishindwa kuwa waombaji(Matahyo 26:37-43).Ndipo hatimaye akawaambia atakuja Msaidizi ambaye
kazi yake mojawapo,ni kutusaidia kuomba(Yohana 16:7;Warumi 8:26-28).Yeye Roho,kwa kuwa
hutuombea kwa kuugua,na tena ni Roho ya neema na kuomba,huweza kutupa msaada wa kutuwezesha
kuomba kwa kuugua na kulia(Zekaria 12:10)Baada ya Roho Mtakatifu kuja na kuwasaidia wanafunzi wa
Yesu,maisha yao ya maombi yalibadilika(Matendo 10:9).Siri ni hii,usitumie nguvu zako kuomba.Kabla ya
kuingia katika maombi,mwombe Msaidizi akusaidie kuomba.
SOMO 4:
UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
Ili tuweze kuwa mashahidi wa Mungu,tunahitajika kubatizwa kwa Roho Mtakatifu baada ya kuokoka na kutakaswa.Ili tumtendee Mungu
kazi kikamilifu,ni lazima tupokee nguvu ya Roho Mtakatifu (Matendo 1:8;Luka 24:49).Kwa sababu hili,somo hili,ni la muhimu sana
kwa mtu yeyote anayetaka kuwa mtendakazi mzuri wa Mungu.Tutaligawa somo hili katika vipengere vinne:-
10. MAANA YA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
11. UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU,UWEZA WA KUTUWEZESHA KUWA MASHAHIDI WA MUNGU
12. ALAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU NA JINSI ZINAVYOTUPAUFAHAMU KUHUSU
UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
13. JINSI YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU
14. ISHARA YA KWANZA YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU NA NIDHAMU INAYOAMBATANA
15. UMUHIMU WA KUUCHOCHEA MOTO WA ROHO MTAKATIFU
6. MAANA YA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
Baada ya mtu kuokolewa,inambidi kubatizwa kwa maji kwa jina la baba,Mwana na Roho Mtakatifu(Mathayo 28:19).Hata hivyo,huo siyo ubatizo wa mwisho.Baada ya mtu kutakaswa,anahitajika kubatizwa kwa Roho Mtakatifu(Mathayo 3:11)Ubatizo wa maji,unamfanya mtu azamishwe ndani ya maji na kuzungukwa na maji pande zote.Vivyo hivyo,Ubatizo wa Roho Mtakatifu unamfanya mtu aliyeokoka,kuzamishwa ndani ya Roho Mtakatifu na kuzungukwa na Roho Mtakatifu pande zake zote.Roho Mtakatifu,anakuwa msaidizi wake(Yohana 15:26).Ubatizo wa maji,tunabatizwa na wanadamu waliopewa Agizo la Mungu lakini Ubatizo wa Roho Mtakatifu,tunabatizwa na Yesu mwenyewe(Mathayo 3:11).
6. UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU,UWEZA WA KUTUWEZESHA KUWA MASHAHIDI WA MUNGU
Neno “mashahidi”katika (Matendo 1:8),linatokana na neno la lugha ya Kiyunani “Martus” ambalo linatafsiriwa katika Kiingereza,” Martyr” ambalo maana yake ni “Mtu anayekuwa tayari kuteswa sana au hata kuuawa kwa sababu ya imani yake,pamoja na hayo,
hawezi kuiacha imani yake”.Bila ubatizo wa Roho Mtakatifu,hatuwezi kuwa mashahidi kama walivyokuwa Stefano na Antipa
(Matendo 22:20;Ufunuo 2:13).Kabla ya kubatizwa kwa Roho Mtakatifu,Petro alisema asingemkana Yesu hata ikibidi kuuawa,
lakini kinyume chake alimkana mara tatu,na yeye pamoja na wanafunzi wenzake walipoyaona mateso yanakuja,walimwacha na
kumkimbia Yesu (Mathayo 26:31-35,56) Lakini baada ya ubatizo walikuwa na ujasiri mkubwa. Matendo 4:13
7. ALAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU NA JINSI ZINAVYOTUPA UFAHAMU KUHUSU UBATIZO WA ROHO
MTAKATIFU
§ Maji (Yohana 7:37-39)Hakuna maisha bila ya maji.Mwanadamu ni asilimia 60%maji.Kuharisha na kutapika sana
humfanya mtu kupoteza maji mengi na huweza kusababisha mtu kupoteza uhai.Vilevile sisi tunaosema tumeokoka,
hatuwezi kabisakuwa na maisha ya kiroho yaliyo hai yenye nguvu,bila Ubatizo wa Roho Mtakatifu.Ni lazima tunyweshwe
Roho(1Wakorintho 12:13)Jambo jingine,maji ni muhimu katika usafi wa miili yetu hutuondolea kunuka n.k Roho Mtakatifu hutumulikia dhambi au uchafu wowote.
§ Moto (Mathayo 3:11).Kuwepo kwa moto ni alama ya uwepo wa Mungu (Kutoka 3:1-5;Matendo 2:2-3).Moto vilevile,unangarisha madini kama dhahabu na fedha(Malaki 3:2-3).Ubatizo wa Roho Mtakatifu hufanya uwepo wa
Mungu uwe dhahiri kwa mtu na pia humngÂ’arisha mtu na kuwa mtumishi wa Mungu anayengÂ’aa .Siyo hayo tu,moto
huleta mwanga.Ubatizo wa Roho Mtakatifu hutupa mwanga mkubwa wa maandiko yaani Biblia na kutupa mwanga wa
uzuri wa mbinguni na ubaya wa Jehenam.Ukiwa na mwanga huo hakutakuwa na gharama kubwa yoyote ya kukufanya
ushindwe kufanya mapenzi ya Mungu.Moto pia huleta nguvu ya kuendesha,magari,treni,Ndege n.k vifaa vyote hivyo
huendeshwa kutokana na moto unaotokea baada ya cheche za umeme kuunguza mafuta.Kazi ya Mungu inaendeshwa
kwa nguvu ya moto,ubatizo wa Roho Mtakatifu na kwa moto.Mtu aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu,moto unawake
ndani yake na hawezi kuacha kushuhudia au kuhubiri na kufundisha(Yeremia 20:9;Isaya 62:1;Matendo4:20).Mtu
aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu,maneno yake huwa moto unaoteketeza kila ugumu wa mioyo ya watu kwa kuwa
Roho Mtakatifu hushuhudia pamoja naye na hivyo matokeo yake ya utumishi wake huwa makubwa.Ni nguvu kwa ajili
ya Utumishi (Yeremia 5:14;Yohana 15:26-27;16:6-8;Mika 3:8).
§ Upepo (Yohana 3:8)Upepo wakati wote unatembea,na uko mahali pote.Roho Mtakatifu hakufanya kazi wakati wa mitume tu,hata sasa anatembea na yuko kwetu tayari,ni wajibu wetu kumpokea tu.Upepo huvuma upendako.Ni vigumu kuubadilisha
mkondo wa upepo tunavyotaka sisi,jahazi hufuata mkondo wa upepo.Ni muhimu kutakaswa kwanza kabla ya Ubatizo huu.Utakaso humfanya mtu kuwa mtii mno katika yote na Roho Mtakatifu ni mshirika wa wale wamtiio(Matendo 5:32)Upepo pia hutuletea hewa safi inayotuburudisha wakati wa joto,moshi n.k Mazingira yoyote magumu tukiyakabili katika utumishi wa Mungu,Roho Mtakatifu huwa hewa safi kwetu inayorekebisha mazingira.
§ Mafuta (Luka 4:16-21)Roho Mtakatifu hututia mafuta au kutuweka katika utumishi wa Mungu (1Samweli 16:13;Kutoka 30:30;1Wafalme 19:16;Yohana 2:27)Rais kabla hajaapishwahuitwa Rais mteule na hana mamlaka sana wakati huo kisheria.Kuapishwa kwa leo ndiyo kutiwa mafuta kwa zamani.Bila ubatizo huu,mamlaka yetu huwa hafifu.Mafuta
yanalainisha na kuzuia msuguano.Ubatizo wa Roho Mtakatifu hutupa hekima ya kuvuta roho za watu(Mithali 11:30)
mafuta huufanya mwili uwe laini.Ubatizo wa Roho Mtakatifu hulainisha ukavu wa maombi yetu (Warumi 8:26)
§ Mvua (Zaburi 72:6;Hosea 6:3)Nchi haiwezi kutoa matunda bila mvua.Mtu aliyeokoka hawezi kuwa na matunda mengi bila mvua yaani ubatizo wa Roho Mtakatifu(Yohana 15:16)
§ Mvinyo(Waefeso 5:18;Matendo 2:12-13) mvinyo kwa walevi unasahaulisha shida.Ubatizo wa Roho Mtakatifu,
humwezesha mtu kudharau majaribu na kuondoa wasiwasi na kubabaishwa na mambo madogomadogo tu.Mvinyo kwa walevi,pia
unawapa ujasiri wa kufanya lolote lile,aibu,woga vinatoweka.Ubatizo wa Roho Mtakatifu humfanya mtu kuwa jasiri
kama simba na mtu aliye kuwa mwoga kama Petro,kuwa jasiri(Mithali 28:1;Mathayo 26:31-35,56;Matendo 4:13).
§ Hua (njiwa)- (Yohana 1:32) Ubatizo wa Roho Mtakatifu haufanyiki kwa mtu wa ulimwengu huu yaani ambaye
hajaokoka.Njiwa hakutua kwenye ulimwengu,alirudi safinani kwa waliookoka(Mwanzo 8:8-9)Roho Mtakatifu ni
mweupe,kama hua.Ni Mtakatifu,huja kwa watakatifu waliotakaswa.
§ Muhuri (Waefeso 1:13)Muhuri ni alama ya mamlaka.Bila muhuri barua hupungua mamlaka yake.Ubatizo wa Roho
Mtakatifu humfanya mtu kuwa na mamlaka ya Yesu kwake na shetani husema “ Yesu namjua na Paulo namfahamu
(Matendo 19:15)Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni mamlaka au uwezo kutoka juu wa kuzifanya kazi za Yesu.
§ Arabuni (2Wakorintho 1:21-22)Neno arabuni maana yake- Uhakikisho au uthibitisho wa Uimara.Ubatizo wa Roho Mtakatifu,hutufanya kuwa na uthibitisho wa uimara wa Neno la Mungu,hutuongezea imani ya kufanya maajabu.Shetani
hawezi kumpeperusha huku na kule mtu aliyebatizwa kwa Roho Mtakatifu.
8. JINSI YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU
q Kuokoka au kuzaliwa mara ya pili.Mafuta haya hayatiwi kwa mtu mgeni ambaye jina lake haliko katika kitabu cha Uzima mbinguni (Kutoka 30:31-33)
q Kutakaswa(Yohana 17:17;1Wathesalonike 5:23)Wanafunzi 120 orofani,walitakaswa kabla ya Ubatizo wa
Roho Mtakatifu.
q Kuwa na Imani kama Roho Mtakatifu yuko kwetu tayari na kwamba ni ahadi ya Mungu kwetu(Matendo 2:38-39);Luka 11:10-13)
q Kuwa na kiu ya kumtumikia Mungu(Isaya 44:3)
q Kuomba kwa kufumbua sana kinywa na kutokuruhusu kutumia akili,wala kuwaza kwambatutasema lugha ya
mapepo.(Luka 11:10-13;Zaburi 81:10).
9. ISHARA YA KWANZA YA KUBATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU NA NIDHAMU INAYOAMBATANA
Mtu akibatizwa kwa Roho Mtakatifu,kutakuwa na mambo ya kusikia kwake na ya kuyaona kwake(Mathayo 3:16-17).
Ishara ya kwanza ni kusikia kutoka kwake kabla ya kuona mengine.Atasema au ananena kwa lugha mpya asiyoifahamu
ambayo siyo ya dunia hii(Matendo 2:4;10:44-46;19:6).Ni muhimu mno kwa mtu aliyeokoka kuomba kwa kunena kwa
lugha hii(1Wakorintho 14:2,4-5,15).Hata hivyo hatupaswi kunena kwa lugha mbele ya mataifa wasioelewa kitu.Watadhani
sisi ni wendawazimu(1Wakorintho14:18-25)Kunena kwa lugha mbele ya mataifa wasiojua kitu nikuwapa mbwa kilicho
kitakatifu na kutupa lulu zetu mbele ya nguruwe matokeo yake watatudhihaki kwa kuwa hawajui maana (Mathayo 7:6).
10. UMUHIMU WA KUUCHOCHEA MOTO WA ROHO MTAKATIFU
Moto bila kuchochewa huzimika(Mithali 26:20).Hatuna budi kuwa waombaji na kuomba kwa Roho,yaani kunena kwa lugha katika maombi mara kwa mara katika maombi yetu binafsi(1Wakorintho 14:14-15;Yuda 1:20)Vile vile hatuna budi kudumu katika usafi kwa Neno(Zaburi 51:4,11;119:11;Yohana 15:3).Hatuna budi pia kujihusisha katika kushuhudia na kuwaleta watu kwa Yesu (Mika 3:8).
Nyimbo:
Kutakaswa:
1. I will say “YES” Lord x2, “YES” Lord x2 ,I will say YES Lord
Nitasema “NDIO” X2 , “NDIO” Bwana x2,Nitasema “NDIO”
Ubatizo wa Roho Mtakatifu:
2. Moto moto moto moto umewaka x 2, siku ile ya Pentekoste moto umewaka x2.
Moto moto moto moto umewaka x 2, siku ya leo ACL moto umewaka x2
Moto moto moto moto umewaka x 2, siku ya leo Rohoni mwangu moto umewaka x2
Tafuta utakatifu kwani pasipo huo Utakatifu hakuna mtu atakayemwona Mungu.

SAMINA YA UREJESHO YA NENEO LA MUNGU
UREJESHO WAKO!
Ikiwa Uzima wa Mungu umo ndani yako, Pumzi yake iko ndani yako! Unaweza kutamka lolote likawa maana siyo wewe unayeishi bali Kristo ndani yako!
Kuna kurejeshwa kwa baadhi yenu mliokua mateka, lakini kwanza tambua uthamani ulionao kwake, tambua kwamba Una uzima wake ndani yako, kama umelalamika sana, umeona kama Mungu hakuoni ebu kumbuka ni wapi umeanguka, kumbuka upendo wako wa kwanza kwa Mungu, nyenyekea UTUBU urudi kwa Mungu.
Mungu anakwenda kurejesha kitu kwako, Ndoa yako inarejeshwa, huduma yako inarejea kwa jina la Yesu Kristo, watoto wako utawaona, kibali kinarudi tena kwa jina la Yesu.
Kila kilichokua kimerudi nyuma katika maisha yako, kinarejea tena kwa jina la Yesu Kristo. Hakuna atakayekugusa MASIHI wa BWANA maana umerejeshwa.
Usirudie kuwa mateka tena. Kaa kwenye line na Mungu. Amen
MAANA YA WOKOVU
“Kwasababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa mtu hukiri hata KUPATA WOKOVU”. (Rum 10:9-10.)
Baada ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako, ni muhimu sana kupata mafundisho ya awali, yatakayokusaidia kujua kwa hakika, maana ya KUOKOKA au WOKOVU; “ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.” (Efe 4:14)
Ndio maana Yesu alisema, tukishawahubiri na kuwasaidia kuokoka, tuwafundishe yote!“Yesu akaja kwao akasema nao, akawaambia, nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,
mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na mkiwafundisha kuyashika yale yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote hadi ukamilifu wa dahari”. (Math 28:18-20).
“Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara katika imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani”. (Kol 2:6-7)
“Wakawa wakidumu katika fundisho la Mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali” (Mdo 2:42)
“Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu, lakini kwa upole na kwa hofu” (1Pet 3:15)
Watu wengi wamechanganya sana maana halisi ya neno “kuokoka”. Unaweza kupewa tafsiri nyingi na watu, juu ya neno “kuokoka”.
Wengine hudhani kuokoka ni dini au dhehebu Fulani la “walokole”. Wengi hudhani wokovu ni maisha Fulani ya kujinyima raha na kujitenga na jamii. Wengi hudhani wokovu ni maisha duni nay a umasikini au kutokuwa na mali za kifahari. Ndani ya fikra za watu, kuna tafsiri nyingi tofauti juu ya “kuokoka” na hizo tafsiri nyingi si sahihi. Lakini hii hapa chini nadhani ndio tafsiri rahisi zaidi kueleweka.
KUOKOKA NI NINI?
Kunusurika, kusalimika, kupona, kukombolewa, kufunguliwa au kutoka katika janga au hatari fulani. Kuzaliwa mara yapili
Mfano:-
Kunusurika; Paulo aliposafiri mashuani pamoja na watu wengine mia mbili na sabini na sita, alisema;“safari hii itakuwa na madhara na hasara nyingi, si ya shehena na merikebu tu, ila na ya maisha yetu pia … baada ya muda mchache, ukavuma upepo wa nguvu wa namna ya tufani … na kwa maana tulikuwa tukipigwa sana na ile tufani, siku ya pili yake, wakaanza kuitupa shehena baharini.
Siku ya tatu wakatupa vyombo vya merikebu kwa mikono yao wenyewe. Jua wala nyota havikuonekana kwa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, basi tukakata tamaa ya kuokoka … na baharia walipotaka kukimbia na kuiacha merikebu … Paulo akawaambia akida na askari, hawa wasipokaa ndani ya merikebu, hamtaweza kuokoka … Shauri la askari lilikuwa kuwauwa wafungwa, mtu asiogelee na kukimbia. Bali akida akitaka kumponya Paulo, akawazuia wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea, wajitupe kwanza baharini, wafike nchi kavu … na hivyo watu wote wakapata kuifikilia nchi kavu salama.
Tulipokwisha kuokoka, ndipo tulipojua ya kuwa kisiwa kile chaitwa Melita”. (Mdo 27: 1-44. 28:1)
H Hivyo tunaona “KUOKOKA” katika mistari hii, imetumika kama “KUNUSURIKA”.
- Kupona; Wayahudi walimdhihaki Yesu , “Jiponye nafsi yako, ushuke msalabani.
( Mk 15:30)
Sisi je, tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukadhibitishwa kwetu na wale waliosikia. (Ebr 2:3)
“KUOKOKA” katika mistari hii imetumika kama “KUPONA
SIKU YA KWAZA SEMINA YA UREJESHO:
NA MCH: SAMSON O MBOYA
KUTOKA 2;7
Mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaondoka akaoa binti mmoja wa Lawi. Yule mwanamke akachukua mimba akazaa mwana, na alipoona ya kuwa ni mtoto mzuri akamficha miezi mitatu.
Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akampatia kisafina cha manyasi akakipaka sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka katika majani kando ya mto.
Umbu lake mtoto akasimama mbali ili ajue yatakayompata.
Basi binti Farao akashuka, aoge mtoni, na vijakazi wake wakatembea kando ya mto; naye akakiona kile kisafina katika majani, akamtuma kijakazi wake kwenda kukileta.
Akakifungua, akamwona mtoto, na tazama, mtoto yule analia. Basi akamhurumia, akasema, Huyu ni mmojawapo wa watoto wa Waebrania.
Basi umbu lake mtoto akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu?
ISHARA YA KWANZA YA MUSA YA FIMBO KUWA NYOKA
Musa akajibu akasema, Lakini, tazama, hawataniamini, wala hawataisikia sauti yangu; maana watasema, Bwana hakukutokea.
Bwana akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, Ni fimbo. Akamwambia, Itupe chini; akaitupa chini, nayo ikawa nyoka; Musa akakimbia mbele yake.
Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako, kamshike mkia; (akaunyosha mkono wake akamshika, naye akageuka kuwa fimbo mkononi mwake;)
Kutoka 4:1-4 uwoga hautakiwi katika kutoa maamuzi
1wakorintho1:26
Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;
bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;
tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;
mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu
WAACHILIE WAKATOE DHABIHU MBELE ZA BWANA:
KUTOKA 1:1
Hata baadaye, Musa na Haruni wakaenda wakamwambia Farao, wakasema, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Wape watu wangu ruhusa waende, ili kunifanyia sikukuu jangwani.
ISAYA 43:26
Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.
Mungu akubariki sana kwakufuatilia somo hili la urejesho

MASOMO MAALUMU KWA MWANAFUNZI
MUONGOZO WA MASOMO
1. Biblia Imetoka kwa Mungu
2 Petro 1:20-21 Roho wa Mungu aliwaongoza manabii
Wagalatia 1:11-12 Mitume walifunuliwa Injili na Yesu
Yohana 14:26; 16: 13,14 Roho Mtakatifu aliwaongoza mitume
1 W athesalomike 2: 13 Mitume walihubiri neno lililotoka kwa Mungu
2 Timotheo 3: 16-17 Neno la Mungu (Biblia) linatosha kutukamilisha
2. Tusiliongeze wala tusipunguze neno la Mungu
Kumbukumbu 4:2 Tusilibadili Neno la Mungu; Mithali 30:5, 6
Wagalatia 1: 6-8; Abadilishaye Injili atalaniwa; 2 Petro 2:1-3
Ufunuo 22:18-19; Aongezaye neno la Mungu atapata mapigo
Wakolosai 2: 8; Tusifuate mapokeo ya watu badala ya neno la Mungu
Mathayo 15:3, 8,9,14; Wafuatao mapokeo huhalifu amri ya Mungu
1 Wakorintho 4: 6; Tusipite yaliyoandikwa wala tusifuate wanadamu
Yuda 1:3; Tuishindanie Injili ile iliyohubiriwa na Mitume .
3. Je! Wakristo wafuate Agano la kale au wafuate Agano Jipya?
“ Agano” ni mapatano kati ya watu. Mungu alifanya Agano la kale na Waisraeli.
Aliahidi angewabariki maadamu wangelishika masharti ya Agano lake.
Kumbukumbu 6:17-16; 11: 8, 9; Mungu alisema Waisraeli wangeimiliki nchi
ya kanani maadamu wangezishika zile sheria za Agano la kale.
Kutika 34:27,28; Amri kumi ndiyo Agano la Kale. Kum. 4: 12,13;
Yeremia 31:31-34; Waisaraeli walivunja Agano; Mungu aliliondoa na kuleta
Agano Jipya lililo tofauti na zile Amri kumi. Mathayo 5:21-22, 27-28;
Waebrania 8: 6-13; Agano la Kale lilikuwa na upungufu
Waebrania 10:4-9; Agano la Kale limeondolewa
Hosea 2:11; Mungu alisema ataikomesha Sabato
Wakolosai 2:16,17; Sheria ya Sabato iliondolewa pamoja na Amri kumi
Matendo 20:7; Wakristo wanasali siku ya kwanza ya juma, siyo Sabato
1 Wakirintho 16:1,2;
Mathayo 28:18; Yesu anayo mamiaka yote.
Waebrania 9:15; YESU AMELETA Agano Jipya
Mathayo 5;21-22,27,28,31-32,38,43-45; Sheria ya Yesu ni kamilifu
Yohana 13:34-35; 15:12-17; Tumepewa sheria mpya
Warumi 13:8-10; Mwenye upendo hana haja na Amri kumi
Warumi 7: 6,7 Hatupo chini ya Torati (Amri kumi ); Wagalatia 3:23-26;
Wagalatia 5:4; Hatuwezi kufuata Torati na Injili pia Warumi 7:1-6;
Warumi 10: 2; Marko 2:21, 22;
4. Agano la Kale lilitimilizwa na kuondolewa Yesu alipokufa
Wagalatia 4:4; Yesu alizaliwa chini ya Torati na, kwa hiyo, akaishika
Mathayo 5:17,18; Yesu alikuja kutimiliza Torati , siyo kuivunja
Luka 24:44 – 46; Torati ilitimilizwa na kuondolewa Yesu alipokufa
Warumi 7: 6; Tumefunguliwa katika Torati ( Agano la Kale ) . Ebr. 10:1-9;
Waebrania 9:15-17 ;Agano Jipya lilianzwa Yesu alipokufa msalabani;
Matahayo 28:18-20; sasa Yesu anayo mamlaka yote; Marko 9:2-9;
Wakolosai 2:13-25; Sheria za Musa ziligongamewa msalabani
Waefeso 2:11-16 Yesu aliondoa Torati iliyokuwa na uadui kwetu alipokufa
Wagalatia 5:4; Hatuwezi kushika Torati pamoja na sheria za Yesu ;
Warumi 7:1-4’ Warumi 10: 4; Marko 2: 21,22;
( Kubuka kuwa Torati , Amri kumi na Agano la Kale yote ni mamoja)
5. Mamlaka katika kanisa
Mathayo 23:8-10; Wanadamu hawana mamlaka kanisani .
Mathayo 28:18; Yesu anayo mamlaka yote mbinguni na dumiani .
Waefeso 2:20 Petro si msingi wa kanisa; 1 Wakorintho 3:11.
Wakolosai 1:13-18; Yesu ni kichwa ( kiongozi) cha kanisa
Waebrania 1: 1, 2 Musa na manabii hawatuongozi. Bali Yesu tu.
Yohana 12: 48 Tutahuhumiwa kwa neno alilolisema Yesu.
Yohana 1: 8-11 Tsishirikiane na wasiofuata mafundisho ya Yesu
Luka 21:33 Maneno ya Yesu hayapiti kamwe. Tusijaribu kuyabadili
6. Nifanye nini ili niokoke?
Waebrani 11: 6; Lazima kuamini; Yohana 3:16-18;
Warumi 10:17; Lazima kusikia Injili kwanza kusudi uamini
Yakobo 2:24, 26; Imai peke yake haiwezi kumwokoa mtu
Matendo 17:30,31; Lazima kutubu ( kujuta na kuacha dhambi)
Mathayo 10:32-33; Lazima kumkiri Yesu kuwa ni mwana wa Mungu
Marko 16:15-16; Lazima kubatizwa ( Yohana 3:3-7;
Matendo 2:37-38; (127) Matendo 22:16; 1 Petro 3:20,21;
(Soma pia nambari hapo nchini )
7. Ubatizo mmoja wa Yesu .
Ubatizoa ni neno la Kiyunani ( Batti (w ) na maana yake ni “Kutoswa”majini
Yohana 3: 23; Ubatizo unahitaji maji mengi
Matendo 8: 35 –36; Katika ubatizo watu hutelemka na kupanda majini
Mathayo 3:16; Baada ya kubatizwa Yesu alipanda kutoka mjin
Wakolosai 2:12; Ubatizo ni kuzikwa katika maji
Warumi 6:3-5; Ubatizo ( kutoswa ) ni mfano wa kuzikwa kwake Yesu
Yohana 3:1-7; Ubatizo ni mfano wa kuzaliwa kwake mtoto
Mathayo 7: 21; Imani bila kumtii Mungu haifai Luka 6:46;
Yakobo 2: 24,26; Imani peke yake haifai; Imani pasipo Matendo imekufa
1 Petro 3: 20,21; Lazima kubatizwa ili kuokolewa; Matendo 2:38;
Waefeso 4:5 ;Kuna ubatizo mmoja tu. Ubatizo huo ni kutoswa majini
8. Je! Watoto wadogo wabatizwe?
Kuwabatiza watoto si amri ya Mungu
Marko 10:13- 16; Yesu hakubatiza watoto bali aliwabariki tu
Matendo 2: 38; Kusudi la ubatizo ni kuondoa dhambi
Ezekieli 18: 1-4, 19, 20; Watoto hawarithi dhambi
Mathayo 18:2,3,10 ; Watoto hawana dhambi Marko 10:16;
Kumbukumbu 24:16; Mwana asiuawe kwa danmbi ya Baba
Yohana 9:1-3; Ugonjwa na mauti siyo ishara ya kurithi dhambi ; hata
ukimbatiza mtoto hatimaye atafariki
Matendo 8: 36-37; Ni lazima kuamini kabla mtu hajabatizwa
Marko 16:16 ; Watoto wadogo wasibatizwe maana hawawezi kuamini
Ezekieli 18: 20; Haki yake mzazi haiwezi kumokoa mtoto wake
9. Wakristo wawe na umoja
Yohana 10:16; Yesu alituweka tuwe kundi moja tu
Yohana 17:20-12; Yesu alituombea tuwe na umoja
1 Wakorinto1 :10-13; Kujitenga katika madhehebu ni dhambi
Waefesko 4: 3 –5; Kuna mwili mmoja , Imani moja, ubatizo mmoja
Wafilipi 1:27; 2:1-3; Wkristo wote wawe na umoja
10. Ibaada ya Kikristo
Warumi 12:1 ; Tujitoe mili yetu kuwa dhabihu iliyo hai
Waebrania 13:15-16; Tutende mema na kushirikiana
Matendo 2: 41-42 Wakristo walidumu katika fundisho la mitume
ukitaka ufafanuzi zaidi wasiliana na muhusika wa safu hii unayoisoma Mchungaji samson o mboya 0756-809209/0786608801 karibu sana

Subscribe to:
Posts (Atom)