Kuishi bila baraka za wazazi ni Hatari sana kuna sababu gani ya wewe kuwatharau wazazi wako, huwezi kukumbuka hata kidogo vile alivyokuwa anakuangaikia kukuongesha kulima vibaruwa ili wewe upate kuishi wakati mwingine alitharaulika kwakuomba misaada kwaajili yako baba akajitahidi kulipia kila kilicho hitajika ili wewe upate kufurahia ukajibiwa maswali yako yote hata yale yasiyoya kimsingi ili wewe ufurahi sasa umemaliza masomo au umepata mali unawatharau wazazi kisa unaiga utamaduni wa wenzetu wao tangu awali wameumbwa hivyi na wamelelewa hivyo upo utaratibu mwingine watu wanaufuta kwakisingizio cha maendeleo kwama hizo mila hatuziitaji lakini uliza kwa nini wazazi wetu walifanikiwa kuishi umri mkubwa moja wapo ya utamaduni wao uliwasaidia sana kwa mfano siku za leo mavazi yanayovaliwa na vijana wetu siyakutembela barabarani labda ni kwaajili ya wana ndowa tu,au kupumzikia ndani wao wanafanya ndiyo mitindo, ukitaka kukosana nao fuatilia au uliza hatakama ni kwa maana nzuri lazima yataanza mengine makubwa matusi,kwamba mzazi amepitwa na wakati,
yeye amezaliwa kabla yako miaka 20 iliyopita na sasa mnaishi wote je? ni nani aliyepitwa na wakati kama siyo wewe tukubali kuonywa ndugu zangu, kuna matendo mengine tunawafanyia wazazi tunawaachia kilio wakati wote mara nyingine mzazi anapigwa na mtoto ati mtoto anamwambia mzazi hana adabu, au angechelewa angemzaa,hiyo ni laana ya wazi kabisa kufanya hivyo wengine hawafanikiwi kimaisha kwasababu hiyo ya kuzarau wazazi,unaweza kutofanikiwa au kuchukiwa na watu na Mungu pia kwa kuwauthi wazazi tuwapende wazazi jamani pia utamaduni wa wenzetu usitubadilishie wetu,
mbona wakija kwetu huwa wanatuiga inamaanisha tuna fanya vizuri kwanzia kuvaa kwetu kula kwetu ila nikujisahau tu sasa ni jukumu lletu sote kukumbushana,wengine anatapanya mali na ovyo wazazi wanataabika huko kijijini wanakufa njaa kwanini usipate mathara ni hatari unaweza kuzuwa matatizo ambayo huwezi juwa yameanzia wapi,je wewe ukibebeshwa mtoto mgongoni na kuni kichwani jembe mkononi utaweza? je umewahi kumubeba mtoto wako mara ngapi ukatembea naye kwa miguu kilomita 5 yu ukasikia uzito wake.
uwapende wazazi kama kuna namna ya kuwasaidia tuwasaidie hizo ni baraka za kwanza kabisa maana wao ndio walio kuleta hapa duniani,,,,,,