Hii wakati mwingine inaweza kutusababishia hata sisi kupoteza kibali cha kuhudumu mbele za Mungu wetu wa Mbinguni,
Watu wengi wamekuwa wakiniuliza maswali mengi tofauti tofauti kila mara ninapokuwa na mazungumuzo na wao ya kirafiki haswa kuhusiana na kazi ya Mungu aliyotuagiza kuifanya tuwapo hapa Duniani, napia inawezekana na wewe ukawa miongoni mwa wale wenyemaswali mbali mbali ya ki-Mungu usiogope kutuandikia uwe huru, Ndugu yangu Roho Mtakatifu yupo kwaajili ya kujibu maswali yanayowasumbuwa wanadamu,
Hapa kuna baathi ya maswali yaliyojibiwa mengine endelea kusoma safu nyingine hizo zinazo onekana hapo utayapata,
KANISA NI NINI? LENGO LA KANISA, UTAWALA WA KANISA, MWISHO: MUNGU ANATAKA NINI KWA VIONGOZI WA KANISA,
Hayo ndiyo utakayojifunza katika safu hii na haswa kwa wale ambao wameshazitambuwa huduma zao ni zipi, kwakifupi kabisa kanisa siyo jingo la mawe au matofali bali ni wewe maana Mungu anaabudiwa ndani yako, wakati unakuja watakao niabudu halisi wataniabudu mimi (Mungu) katika Roho na kweli
Ndugu yangu Roho haikai ndani ya jingo inakaa ndani ya mwanadamu ndiyo maana ninamaanisha kanisa ni Mtu yule aliyeamuwa kukatashahuri na kumkaribisha Mungu Ndani yake akakataa uovu wote, haya majengo tunayo yaita makanisa siyo kosa bali ifahamike zaidi kwamba tunayaita makanisa kwasababu sisi tunakusanikia humo, hivyo ndio maana halisi kwa wale wanye masali kama hayo,kwahiyo kahabari ya majengo haijalishi ni jingo la namna gani kubwa au dogo,ila tunapokusanyika pamoja tukaaza kujifunza Neno la Mungu Tayari hilo ni kanisa,
Lengo la kanisa nikuyatimiza mapenzi ya Mungu anayoyataka yatendeke kupitia kanisa kwa utukufu wake,
Uawala, Ndani ya kanisa hakuna utawala bali kuna uongozi kwamaana tunaongozwa na roho wa Mungu,utawala upo Duniani kwa mambo ya kidunia kama kutawala inchi na mengineyo,
Wewe ni mchungaji wa kanisa lako Mungu alilokukabithi na utaulizwa siku ya mwisho kwamba ulijisimamia vipi, akasema ninyi ni mahekalu ya Roho mtakatifi ya kuabudia atakayeliharibu hekalu langu nami (Mungu) nitamuharibu, iwe unajisimamia mwenyewe au kundi la Bwana kuwa makini na ni Duwa yangu na maombi ukase mwendo mpaka ujio wa kristo utakapokuja,
umeshatambuwa kinachuzungumziwa hapa
Sasa wewe
Kumbe wewe ni mchungaji na ungependa kanisa lako likue. Hiyo ni shauku ya kawaida kabisa kwa wachungaji wingi. Lakini – kwa nini unataka kanisa likue? Sababu ya kweli ndani ya moyo wako ni nini?unaweza usimwambie mwanadamu ila Mungu hafichwi na jambo lolote lile,
Je, unataka kanisa likue ili ujisikie umefanikiwa? Je, unataka uheshimiwe na kuwa na ushawishi mkubwa serekalini? Je, unataka kuwa na mamlaka juu ya watu? Je, unatazamia kutajirika? Hizo zote ni sababu mbaya za kutaka kanisa lako likue.
Ukitaka kanisa lako likue ili Mungu atukuzwe kadiri watu wengi wanavyobadilishwa maishani kwa Roho Mtakatifu, basi hiyo ni sababu nzuri ya kutamani kukua kwa kanisa.
Inawezekana kujidanganya – kufikiri kwamba makusudi yetu ni safi na huku ni ya kimwili kabisa, tena ya kibinafsi.
Tunawezaje kujua ukweli wa makusudi yetu? Tunawezaje kujua kama kweli tunataka kujenga ufalme wa Mungu au kujenga ufalme wetu binafsi tu?
Njia moja ni kwa kufuatilia jinsi tunavyoitikia mafanikio ya wachungaji wengine. Kama tunafikiri makusudi yetu ni safi, kama tunafikiri kwamba kweli tunataka ufalme wa Mungu na kanisa Lake likue, lakini tukigundua wivu mioyoni mwetu tunaposikia juu ya kukua kwa makanisa mengine, hiyo inadhihirisha kwamba makusudi yetu si safi. Huonyesha kwamba kweli hatujali sana kukua kwa kanisa, bali tunajali kuhusu kukua kwa kanisa letu (kusanyiko). Mbona iwe hivyo? Kwa sababu makusudi yetu yana kiasi fulani cha ubinafsi ni tofauti kabisa na mpango mzima wa Mungu.
Pia tunaweza kukagua makusudi yetu kwa kupima itikio letu la ndani tunaposikia kwamba kanisa jipya limeanzishwa katika eneo letu. Tukijisikia kutishika au kutofurahia, hiyo ni ishara kwamba tunajali zaidi kuhusu ufalme wetu kuliko ufalme wa Mungu.
Hata wachungaji wa makanisa makubwa au yanayokua wanaweza kukagua makusudi yao hivyo hivyo. Wanaweza kujiuliza maswali kama haya: “Je, ningekubali kuanzisha makanisa mapya kwa kuwatuma na kuwaachilia kabisa viongozi muhimu na watu wa kanisani kwangu, na kwa njia hiyo kupunguza idadi ya washirika wangu?” Mchungaji anayepinga sana wazo hilo bila shaka anajenga kanisa lake kwa ajili ya utukufu wake.
(Kwa upande wa pili, mchungaji mwenye kanisa kubwa anaweza kuanzisha makanisa mapya kwa ajili ya utukufu wake pia, ili aweze kujigamba kuhusu idadi ya makanisa yaliyozaliwa na kanisa lake.) Swali lingine la kujiuliza ni hili: “Je, nina mahusiano na wachungaji wa makanisa Mengine hata yale madogo au machanga? au nimejitenga nao, nikijiona kwamba niko juu kuliko wao?
Je, nitakuwa tayari kuwa mchungaji wa watu kumi na mbili hadi ishirini katika kanisa la nyumbani, au hiyo itaniathiri katika ubinafsi wangu?” ni mambo machache sana wewe kama mtu wa Mungu unayoweza kujiuliza wewe mwenyewe maana inawezekana ukiulizwa ukarusha ngumi au ukaanza kulaani hii nafasi ni yako na inawezekana uko peke yako hata saa hii chunguza uliza roho mtakatifu kama bado hujamuacha,usije ukawaubiri wengine na wewe ukabaki ni Mbaya sana, inaendelea
Ndugu Mtazamaji/ MSOMAJI; Bila shaka unampenda Mungu Sana tunaamini hivyo Kwa vile ulivyoweza kufika mahali hapa tulipo kupitia Mtandao huu, lipo kusudi la Mungu kutaka kukusaidia jambo Fulani ikiwa uko tayari katika yote jiepushe na mafundisho yasiyokuwa ya ki-Mungu Mathayo 16:6-12) piga simu kwa masaada zaidi huduma hii ni bure 0757328311