USHINDI JUU YA DHAMBI,

 Kuishinda dhambi hakuna mtu chini ya jua anayeweza kuishinda Dhambi kwa ujanja wake au kwa nguvu zake pasipo kusaidiwa na Mungu,  siku zote anayetuwezesha kuishinda Dhambi ni Mungu peke yake,
Kwa kuwa atakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya; kwa maana Wewe upo pamoja nami.


Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. —Wafilipi 4:13, 19


Namna ya kuishinda Dhambi,

1 Wakorintho 10:13
Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.

Waebrania 4:16
Basi na tukikaribie kiti cha flee-ma kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

2 Timotheo 2:22
Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.

1 Yohana 1:7
Bali tukienenda nuruni, kama yeye ahivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.


Warumi 6:11
Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi, na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.

Yakobo 4:7
Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
Zaburi 119:11
Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi.

Nguvu ya maombi
Zaburi 27:8
Uliposema, Nitafuteni uso Wangu, Moyo wangu umekuambia, BWANA, uso wako nitautafuta.

Zaburi 62:8
Enyi watu, mtumainini sikuzote, ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.

Yeremia 17:14
Uniponye, Ee BWANA, nami nitaponyeka; uniokoe, nami nitaokoka; kwa maana wewe ndiwe uliye sifa zangu.

1 Wathesalonike 5:17, 18
Ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika KristoYesu.

Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. —Yakobo 1:5

Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. —Yohana 15:7

Zaburi 34:4
Nalimtafuta BWANA akanijibu, akaniponya na hofu zangu zote.
Zaburi 66:18; 25:11
Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia. Ee BWANA, kwa ajili ya jina lako, unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi.


Jiweke tayari kwa ujio wa kristo Yesu

1 Wathesalonike 4:16, 17
Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo.



2 Wakorintho 7:1
Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.

1 Yohana 2:28
Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi, atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibike mbele zake katika kuja kwake.

Yakobo 5:8, 9
Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia. Ndugu, msinung’unikiane msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.

Luka 12:40
Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.


Kujazwa na Roho wa Mungu ni jambo la muhimu pia katika maisha ya mwanadamu,

Mithali 1:23
Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; tazama, nitawamwagia roho yangu, na kuwajulisheni maneno yangu.

Matendo 2:38
Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.



Waefeso 5:18-21
Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo; hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.

Wafilipi 2:13

Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.

1 Wakorintho 3:16; 6:2

Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu. na yeye atakaye liharibu Hekalu langu nami nitamuharibu, ukivuta sigara,ukifanya ukahaba,ukinywa pombe,ukilinajisi hekalu la Mungu yaani mwili wako naye Bwana atauharibu, Hebu fahamu hivi alichokiharamisha Mungu mwanadamu Hawezi kukihalalisha au kukitakasa kwa namna yeyote ile,

Na kunzuri zaidi Mungu Hakuwahi kubadilika wala siyo kigeu geu alilolikataza miaka elfu tatu mpaka sasa hajaliruhusu  na aliloliruhusu pia mwanadamu hawezi kulizuwia, kuzuwia kwa mwanadamu ni kujiangamiza, kama ilivyo kuhalalisha asichoalalisha ukaangamia ndivyo na kuzuwia alicho alalisha ishi kama anavyoagiza si kama unavyo taka wewe kuishi,kwasababu hayupo ajuwaye baada ya Dakika tano nini kitamtokea,

hakuna mtu aliyejichaguwa awe alivyo hivi sasa hata kuzaliwa kila mmoja alijikuta yuko kama alivyo awe ni mwanaume,au mwanamke hivyo hayupo anayeweza kutamba kwa mwingine wala kwa chochote alicho nacho, kama ni kutamba Bwana anaruhusu mtu atambe kwaajili ya kumfahamu yeye,,

MBELE ZA MUNGU HAKUNA UBAGUZI

kizibiti chako kitajitambulisha hakutakuwa na ubishi kwa mtu yeyote yule,

Wakorintho 5:10

Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee. kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.


Warumi 2:16
Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, kwa Kristo Yesu.

2 Wathesalonike 1:7, 8
Wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake; katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu.


Luka 19:27

Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu.


SIO WOTE WANAOSHUHUDIA KUMFUATA YESU WALIO WA YESU


Tito 1:16
Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana.

Warumi 8:9

Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.

Ezekieli 33:31
Nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao.

Mathayo 15:8
Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami.


Mathayo 7:21-23

Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika uf alme wa mbinguni; bali ni yeye af anyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.


WAFUASI HALISI WA YESU HUMII

1 Yohana 2:3

Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.

Ezekieli 36:27
Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.


Waebrania 5:9
Naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii.


Warumi 6:18

Na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.

Waefeso 2:10

Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.


Warumi 8:10, 13

Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki. Kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.

2 Timotheo 2:19

Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.


ULIMWENGU UNACHUKIA WAFUASI WA YESU

Yohana 15:18, 19

Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake, lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.

Yohana 16:2, 3

Naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.

1 Yohana 3:1

Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.

Matendo 14:22
Na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.


2 Timotheo 3:12

Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.

Yohana 16:33

Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

AHADI KWA WANAO DHULUMIWA

Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. —1 Petro 5:7

Isaya 41:10

Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

Baba yangu na mama yangu wameniacha, bali BWANA atanikaribisha kwake. —Zaburi 27:10

Waebrania 13:6

Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?

1 Petro 4:14

Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia.
Zaburi 91:11; 23:4 Fuatilia maandiko

UFUFUO WETU BAADA YA MAUTI YA MWILI WA DAMU NA NYAMA

kufufuliwa baada  ya mauti ya huu mwili wa damu na nyama

Warumi 8:11

Lakini, ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.

1 Wakorintho 6:14

Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake.

Yohana 11:25, 26

Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele.

1 Wakorintho 15:21-23

Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja.

Yohana 14:19

Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai.

USIDHARAU WOKOVU HUU MKUU — 40

Waebrania 10:28, 29
Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu. Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?

Yohana 12:48

Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.

Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakuf a katika dhambi zenu. —Yohana 8:24

Luka 12:4, 5

Nami nawaambia ninyi rafiki zangu, msiwaogope hao wauuao mwili, kisha baada ya hayo hawana wawezalo kutenda zaidi. Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanum; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo.



Waebrania 2:3

Sisi je! tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii?


YESU KRISTO ATATUHUKUMU — 41

Matendo 17:31

Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.

Yohana 5:22, 23

Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote; ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba.



2 Wakorintho 5:10

Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee. kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.

Warumi 2:16

Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, kwa Kristo Yesu.


2 Wathesalonike 1:7, 8

Wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake; katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu.

Luka 19:27

Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu.

SIO WOTE WANAOSHUHUDIA KUMFUATA YESU WALIO WA YESU — 42

Tito 1:16

Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana.


Warumi 8:9

Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.

Ezekieli 33:31

Nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao.

Mathayo 15:8
Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami.

Mathayo 7:21-23

Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika uf alme wa mbinguni; bali ni yeye af anyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

WAFUASI HALISI WA YESU HUMII — 43

1 Yohana 2:3

Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.

Ezekieli 36:27

Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.
Waebrania 5:9

Naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii.
Warumi 6:18

Na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.
Waefeso 2:10

SI KILA MTU ANAYEFUNGWA GEREZANI ANAHATIA,

Si kila anayetuhumiwa kosa ni kweli amelifanya"

Siku za leo watu wanapitia mateso makali sana tena wasiyo stahili kupitia kwamakosa ya kusingiziwa tu kabla ya kuendelea kufafanuwa sana tuangalie maandiki yanatuhakikishia nini kuhusiana na hili ninalotaka tushirikiane na wewe leo, Bilblia inatueleza juu ya mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Yusufu wengi mnazifahamu habari zake hapa nitazitolea mfano kidogo ili kukuwezesha wewe kuelewe zaidi

Baada ya kitambo Mke wa potifa akamtamani Yusufu akamwambia njoo ukutane nami kimwili lakini yusufu akakataa akamwambia yule mwanamke mimi nikiwa katika uongozi Bwana wangu hausiki na kitu chochote katika nyumba hii kila kitu alicho nacho amenikabithi  Hapa nyumbani hakuna aliye mkuu kuliko mimi bwana wangu hakunizuilia kitu chochote isipokuwa wewe kwakuwa wewe ni mke wake nitawezaje basi kufanya uovu huu na kutenda Dhambi zidi ya Mungu? ingawa yule mwanamke aliendelea kumshawishi  siku baada ya siku yusufu alikataa kukutana naye kimwili  wala kukaa karibu naye

Siku moja yusufu akaingia ndani  ya nyumba kufanya kazi zake hapakuwa na mfanyakazi yoyote ndani ya nyumba mke wa potifa akashika Vazi alilokuwa amevaa yusufu akamwambia njoo tukutane kimwili, lakini yusufu akaacha vazi lake mkononi na kukimbia nje ya nyumba  akawaita watumishi wake wanyumbani akawaambia  "Tazameni huyu mwibrania ameletwa haoa kututhihaki!! aliingia hapa ndani ili akutane nami kimwili, lakini nikapiga kelele  aliposikia kelele za kuomba msaada  akaacha vazi lake kando yangu  akakimbilia inje

Yule mwanamke akaliweka vazi karibu naye mpaka potifa alipo rudi  yumbani ndipo akamwelezea kisa hiki  akisema yule mtumwa wa kiibrania uliyemleta  alinijia ili kunithihaki!  aliingia hapa ndani ili akutane nami kimwili lakini nikapiga kelele aliposikia kelele za kuomba msaada akaacha vazi lake kando yangu akakimbia inje ya nyumba,

Wakati potifa aliposikia kisa hiki mkewe alicho mueleza Hivi ndivyo mtumwa wako alivyo tenda "Hasira ya potifa ikawaka  Potifa akamchukuwa Yusufu na kumweka  Gerezani  Mwanzo 39:7, kwa hivyo tunamuona huyu kijana wawatu pamoja na kujitahidi kukimbia bado kesi inamwangukia ya kusingiziwa wewe mwenyewe ni shahidi wa maisha yako ni mara ngapi umesingiziwa na jambo na watu wote akaliamini kuwa ni lakeli ninajuwa lili kuumiza sana,

Unapo ona misukosuko mbele yako ujuwe katika ulimwengu wa ki-Roho kunasehemu Mungu anataka kukufikisha kwa sababu maalumu kwaajili ya utukufu wake leo hii kama ningemueleza mtu bila ushahidi kama nilioutumia hapa engeweza asiamini lakini ndugu yangu ninakutia moyo wewe songa mbele usibabaike na ushahidi unaoonyeshwa usio wa kweli, kama ushahidi uliobakiza mikononi ni wakweli jitahidi kutubu na kukiri kosa na uanze maisha mapya,bali kama moyo wako unauhakika hujatenda jambo unalotuhumiwa nalo wewe tulia Mungu atafanya jambo kwaajili yako,

wengine wameachia nafasi kwa ibilisi anawatesa kila siku maana wamemuachia ushahidi ndio anaokwenda nao kwa Mungu wetu kushitaki ana mwambia Munngu Tazama huyu mtumishi wako anakuita kila jumapili tena anataka umubariki lakini juzi tu alikuwa kwa wachawi anamtengeneza jirani yake ,mkewe,mmewe,mtoto wa jirani yake,au kutafuta Dawa ya biashara na ushahidi huu hapa anaonyeshea yale madawa uliyoyakumbatia au kuyavaa kiunoni,shingoni au kuweka chini ya godoro lako la kitanda, sasa Mungu akiangalia kizibitisho akakikuta kipo na ni cha kweli huwezi kupokea uponyaji wala baraka maana yeye ni Mungu mwenye wivu apaswae kuabudiwa ni yeye tu wala hashirikiani na mtu wala kitu katika utukufu wake,

Chunguza haya niliyoelezea hapa kama ndani yake unashuhudiwa wewe kuufuta ushahidi uliomwachia ibilisi akapata nafasi ya kukushitaki nayo kwa Baba yako wa mbinguni, kama kuna umuhimu nenda kautupe ule uchawi na madawa uliyopewa na yule mchawi, kama ni ushahidi wa mtu kamtangazie kuwa sasa basi uhusiano na mke asiye mke wako,au mme asiye wako baki na wakwako,mwambie Mungu akutoshelezee huyo huyo tu, kama ni umbea acha mara moja, wizi acha mara moja lolote unalolijuwa kuwa halitamtukuza Mungu liache na usilifanye tena maana utakuwa ndio ushahidi wa wako utakaotumika na Muovu kukushitaki wewe,

Soma neno la Mungu na ufuate maelekezo yote usitafute kile unachokitaka tu,ukikihitaji unachokitaka pekee utakipata na utakwepana na baraka za Mungu, kitu chochote kinachofaywa bila Mungu kuhusishwa kitawezekana kwa mda mfupi baada ya hapo lolote linaweza kutokea, kwani hujawahi kuona au kusikia mtu anajenga nyumba nzuri sana akimaliza tu kabla hajaingia anafariki dunia, au mtu anaoa hivi karibuni tu lakini chakushangaza inakuwa kama amewaolea watu anakuwa ni mke wa watu na si mke wa mtu, na inawezekana ameenda kuolea mbali ya mji au mkoa au inchi ila akishamfikisha tu tayari anakuwa ni wawatu wengine wakatimwingine anapokonywa kabisha, anakuwa wa wangine unaweza kuyaona haya kumbu kumbu la torati 28:30 

Ushahuri wangu mtangulize Mungu katika maisha yako yote si kwa kutamka kwa kinywa tu bali kwa kumaanisha inaendelea,,,

UZIMA WA MILELE NDIO HUU,

SHERIA YA MUNGU KWA WANADAMU NI IPI?

Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya vijito vya maji, uzaao matunda yake kwa majira yake, wala jani lake halinyauki; na kila alitendalo litafanikiwa.

Yesu hutoa maisha yen ye mazao

Yohana 15:4a, 5

Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.

MAANDIKO YANA NENA NINI JUU YA YESU KRISTO?

Yohana 5:39, 46

Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. . . . Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu.

Luka 24:27

Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.

NENO LA MUNGU HALIBADILIKI

Zaburi 119:89, 160

Ee BWANA, neno lako lasimama imara mbinguni hata milele. Jumla ya neno lako ni kweli, na kila hukumu ya haki yako ni ya milele.

Isaya 40:8

Majani yakauka, ua lanyauka; bali neno la Mungu wetu litasimama milele.

Mathayo 5:18

Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.

Yohana 10:35

Na maandiko hayawezi kutanguka.

Mtu asijaribu kubadilisha maneno ya Biblia
Kumbukumbu La Torati 12:32

Neno niwaagizalo lo lote liangalieni kulifanya; usiliongeze, wala usilipunguze.
Mithali 30:6
Usiongeze neno katika maneno yake; asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo.
Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima. —Ufunuo 22:19
Mithali 13:13a
Kila alidharauye neno hujiletea uharibifu.

KIFO CHA YESU KILIKAMILISHA MPANGO WA MUNGU

Yohana 10:17, 18

Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena.

Mathayo 26:53, 54

Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika? Yatatimizwaje basi maandiko, ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri?

Matendo 3:18
Lakini mambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza hivyo.

Matendo 2:23
Mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua.
Isaya 53:10

Lakini BWANA aliridhika kumchubua; amemhuzunisha; utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi.
KIFO CHA YESU KUTANGAZWA NA MASHAHIDI

Marko 15:27, 28

Na pamoja naye walisulibisha wanyang’anyi wawili, mmoja mkono wake wa kuume na mmoja mkono wake wa kushoto. Basi andiko likatimizwa linenalo, Alihesabiwa pamoja na waasi.

Mathayo 27:45, 50-51, 54
Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa. . . . Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. . . . nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka. Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo ya liyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.

Yohana 19:32-37
Basi askari wakaenda, wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili, aliyesulibiwa pamoja naye. Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji. ...Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie, hapana mfupa wake utakaovunjwa. Na...watamtazama yeye waliyemchoma.

YESU ALISHINDA KIFO
Matendo 2:24, 32
Ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao. Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake.

Waebrania 2:14, 15
Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.

1 Wakorintho 15:55, 57
Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Ufunuo 1:18
Na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.

2 Timotheo 1:10
Na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili.

KUNAFAIDAGANI KUMKIRI KRISTO YESU?
Ufunuo 3:20
Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. Ugumu wa watu wengi ni namna ya kusikia sauti ya Mungu lakini kama ni Mungu watu wanampenda usahuri wangu nyenyekea chini ya mkono wa mungu naye atakusaidia kukutofautishia sauti yake na ya muovu maana sauti ya muovu imepoteza wengi sana japo bado Mungu wete hao hataki wapotee bali anataka wote watakao mwamini wapate kuwa na uzima tele tena wa milele,

Followers