Mke wa kuwoa- Sifa zake

MKE WA KUWOA


Na Balozi samson mboya

Unapoongelea mke fahamu yakuwa huongelei habari ya mwanamke kwakuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya mke na mwanamke,

Tofauti hiyo

1:Mwanamke anaweza kuwa yeyote yule aliye na jinsia ya kike

: Mke ni yule aliyeandaliwa Na Mungu maalumu kwaajili ya mtu fulani kuishi naye maisha yake yote ya hapa Duniani Kitabu cha mithali 31 kuanzia msitari wa 10 hadi 31 kimeelezea sifa mbalimbali za mke mwema, tuangalie kwa uchache sifa hizo kwa kuzichambua katika maeneo tofauti.

1. Imani

Mithali 31:26, 29, 30

Mke mwema anayashika na kuyafanyia kazi maneno ya Mungu na ni mtu ambaye anamtumikia Mungu kwa moyo wake wote na akili yake yote. Anatafuta makusudi ya Mungu katika maisha yake na kuyafuata. Zaburi 119;15

2. Ndoa

Mithali 31:11-12, 23, 28

Mke mwema humuheshimu mume wake na anahakikisha anamtendea mambo mema siku zote za maisha yake. Ni wa kuaminika na msaidizi kwa mume wake. Efeso 5:22-24, 1Petro 3

3. Malezi

Mithali 31: 26, 28

Mke mwema anawafundisha watoto wake njia za Mungu na pia anawatunza kwa upendo. Huwafundisha kwa hekima na kuwaelekeza njia iwapasayo kuiendea. Mithali 22:6

4. Huduma

Mithali 31:12-15, 17, 20

Mke mwema anamhudumia mume wake na familia yake yote kwa ukarimu na upendo. Anahakikisha wanapata chakula kilicho bora na chenye afya. Ni mtu mwenye huruma na ukarimu.

5. Mali

Mithali 31:14, 16, 18

Mke mwema anatafuta kwanza ushauri wa mumewe kabla ya kutumia fedha na pia anafanya manunuzi kwa hekima. Ni muangalifu kununua bidhaa zenye ubora kulingana na mahitaji ya familia yake.Efeso 5:23

6. Nyumba

Mithali 31:15, 20-22, 27

Mke mwema ni mtu anayeifanya nyumba iwe mahali pa kuishi. Anatengeneza mazingira ya kuvutia kwa familia yake na wageni wote na anawahudumia watu wake wote kwa ukarimu. 1pet 4:9, Ebrania 13:2

7. Muda

Mithali 31:13, 19, 27

Hutumia muda wake vizuri na kuhakikisha anakamilisha kazi zake za kila siku. Kamwe hapotezi muda katika kufanya mambo ambayo hayampendezi Mungu na yasiyo na faida.

8. Uzuri / Urembo

Mithali 31:10, 21-22, 24

Ni mrembo na mwenye thamani, ana uzuri wa ndani unatoka kwa Yesu Kristo. Anatumia ubunifu wake na utanashati wake kuleta uzuri katika maisha yake na ya watu wake.

Mungu atusaidie ili maisha yetu yaonyeshe kweli tunamjua na kumwamini yeye.

Kwa mafundisho zaidi endelea kufuatilia

(baloziwamungu) au piga simu no kwa msaada

0756 809 209/0786608801

Followers