SAMINA YA UREJESHO YA NENEO LA MUNGU

UREJESHO WAKO!
Ikiwa Uzima wa Mungu umo ndani yako, Pumzi yake iko ndani yako! Unaweza kutamka lolote likawa maana siyo wewe unayeishi bali Kristo ndani yako!
Kuna kurejeshwa kwa baadhi yenu mliokua mateka, lakini kwanza tambua uthamani ulionao kwake, tambua kwamba Una uzima wake ndani yako, kama umelalamika sana, umeona kama Mungu hakuoni ebu kumbuka ni wapi umeanguka, kumbuka upendo wako wa kwanza kwa Mungu, nyenyekea UTUBU urudi kwa Mungu.
Mungu anakwenda kurejesha kitu kwako, Ndoa yako inarejeshwa, huduma yako inarejea kwa jina la Yesu Kristo, watoto wako utawaona, kibali kinarudi tena kwa jina la Yesu.

Kila kilichokua kimerudi nyuma katika maisha yako, kinarejea tena kwa jina la Yesu Kristo. Hakuna atakayekugusa MASIHI wa BWANA maana umerejeshwa.
Usirudie kuwa mateka tena. Kaa kwenye line na Mungu. Amen
MAANA YA WOKOVU
“Kwasababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa mtu hukiri hata KUPATA WOKOVU”. (Rum 10:9-10.)

Baada ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako, ni muhimu sana kupata mafundisho ya awali, yatakayokusaidia kujua kwa hakika, maana ya KUOKOKA au WOKOVU; “ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.” (Efe 4:14)
Ndio maana Yesu alisema, tukishawahubiri na kuwasaidia kuokoka, tuwafundishe yote!“Yesu akaja kwao akasema nao, akawaambia, nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,

mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na mkiwafundisha kuyashika yale yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote hadi ukamilifu wa dahari”. (Math 28:18-20).
“Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara katika imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani”. (Kol 2:6-7)
“Wakawa wakidumu katika fundisho la Mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali” (Mdo 2:42)
“Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu, lakini kwa upole na kwa hofu” (1Pet 3:15)
Watu wengi wamechanganya sana maana halisi ya neno “kuokoka”. Unaweza kupewa tafsiri nyingi na watu, juu ya neno “kuokoka”.

Wengine hudhani kuokoka ni dini au dhehebu Fulani la “walokole”. Wengi hudhani wokovu ni maisha Fulani ya kujinyima raha na kujitenga na jamii. Wengi hudhani wokovu ni maisha duni nay a umasikini au kutokuwa na mali za kifahari. Ndani ya fikra za watu, kuna tafsiri nyingi tofauti juu ya “kuokoka” na hizo tafsiri nyingi si sahihi. Lakini hii hapa chini nadhani ndio tafsiri rahisi zaidi kueleweka.

KUOKOKA NI NINI?

Kunusurika, kusalimika, kupona, kukombolewa, kufunguliwa au kutoka katika janga au hatari fulani. Kuzaliwa mara yapili
Mfano:-
Kunusurika; Paulo aliposafiri mashuani pamoja na watu wengine mia mbili na sabini na sita, alisema;“safari hii itakuwa na madhara na hasara nyingi, si ya shehena na merikebu tu, ila na ya maisha yetu pia … baada ya muda mchache, ukavuma upepo wa nguvu wa namna ya tufani … na kwa maana tulikuwa tukipigwa sana na ile tufani, siku ya pili yake, wakaanza kuitupa shehena baharini.

Siku ya tatu wakatupa vyombo vya merikebu kwa mikono yao wenyewe. Jua wala nyota havikuonekana kwa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, basi tukakata tamaa ya kuokoka … na baharia walipotaka kukimbia na kuiacha merikebu … Paulo akawaambia akida na askari, hawa wasipokaa ndani ya merikebu, hamtaweza kuokoka … Shauri la askari lilikuwa kuwauwa wafungwa, mtu asiogelee na kukimbia. Bali akida akitaka kumponya Paulo, akawazuia wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea, wajitupe kwanza baharini, wafike nchi kavu … na hivyo watu wote wakapata kuifikilia nchi kavu salama.

Tulipokwisha kuokoka, ndipo tulipojua ya kuwa kisiwa kile chaitwa Melita”. (Mdo 27: 1-44. 28:1)
H Hivyo tunaona “KUOKOKA” katika mistari hii, imetumika kama “KUNUSURIKA”.
- Kupona; Wayahudi walimdhihaki Yesu , “Jiponye nafsi yako, ushuke msalabani.
( Mk 15:30)
Sisi je, tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukadhibitishwa kwetu na wale waliosikia. (Ebr 2:3)
“KUOKOKA” katika mistari hii imetumika kama “KUPONA


SIKU YA KWAZA SEMINA YA UREJESHO:

NA MCH: SAMSON O MBOYA

KUTOKA 2;7
Mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaondoka akaoa binti mmoja wa Lawi. Yule mwanamke akachukua mimba akazaa mwana, na alipoona ya kuwa ni mtoto mzuri akamficha miezi mitatu.
Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akampatia kisafina cha manyasi akakipaka sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka katika majani kando ya mto.
Umbu lake mtoto akasimama mbali ili ajue yatakayompata.

Basi binti Farao akashuka, aoge mtoni, na vijakazi wake wakatembea kando ya mto; naye akakiona kile kisafina katika majani, akamtuma kijakazi wake kwenda kukileta.

Akakifungua, akamwona mtoto, na tazama, mtoto yule analia. Basi akamhurumia, akasema, Huyu ni mmojawapo wa watoto wa Waebrania.

Basi umbu lake mtoto akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu?
ISHARA YA KWANZA YA MUSA YA FIMBO KUWA NYOKA
Musa akajibu akasema, Lakini, tazama, hawataniamini, wala hawataisikia sauti yangu; maana watasema, Bwana hakukutokea.
Bwana akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, Ni fimbo. Akamwambia, Itupe chini; akaitupa chini, nayo ikawa nyoka; Musa akakimbia mbele yake.

Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako, kamshike mkia; (akaunyosha mkono wake akamshika, naye akageuka kuwa fimbo mkononi mwake;)

Kutoka 4:1-4 uwoga hautakiwi katika kutoa maamuzi
1wakorintho1:26
Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;
bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;
tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;
mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu

WAACHILIE WAKATOE DHABIHU MBELE ZA BWANA:
KUTOKA 1:1

Hata baadaye, Musa na Haruni wakaenda wakamwambia Farao, wakasema, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Wape watu wangu ruhusa waende, ili kunifanyia sikukuu jangwani.
ISAYA 43:26
Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.
Mungu akubariki sana kwakufuatilia somo hili la urejesho

Followers