KUWA MTENDAJI WA NENO LA MUNGU
Katika utangulizi fahamu mambo matatu makubwa yafuatayo:
Wewe ni balozi wa Kristo na kwa ajili ya Kristo hapa ulimwenguni. “Basi tu wajumbe (mabalozi) kwa ajili ya Kristo….” (2Wakorintho 5:20)
Ikiwa wewe ni balozi, basi wewe si wa ulimwengu huu kama vile Kristo asivyo wa ulimwengu huu (Yohana 17:16). Uraia wako au wenyeji wako si wa hapa ulimwenguni, bali ni wa nyumbani mwake Mungu. “ Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.” (Waefeso 2:19)
Ikiwa wenyeji wako ni mbinguni katika ufalme wa Mungu, nyumbani mwake Mungu unafanya nini hapa ulimwenguni? Kuna sababu kubwa za wewe kuwa hapa ulimwenguni. Ni kwa sababu umetumwa kama Kristo alivyotumwa. “Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.” (Yohana 17:18)
Tunajua hukutumwa hapa ulimwenguni ili ufanye kazi peke yako. Tuko hapa ulimwenguni tukiwa wafanyakazi pamoja na Mungu. “ Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu…” (1Wakorintho 3:9)
Huwezi ukawa mfanyakazi pamoja na Mungu bila ya kuwa mtendaji wa Neno; kwa kuwa Mungu ni Neno (Yohana 1:1). Kuwa balozi wa Kristo maana yake ni kuwa mwakilishi wa Neno; kwa kuwa Kristo ni Neno (Yohana 1:14). Uwakilishi huu hauonekani kwa sabatu watu wa Mungu walio wengi hawaelewi namna ya kuwa watendaji wa Neno ili Neno lionekane hapa ulimwenguni.
Katika somo hili tunajifunza juu ya namna ya kuwa mtendaji wa Neno, ili ufanye kazi ya ubalozi wa Kristo vizuri. Ni maombi yangu na duwa kwa Mungu ya kuwa uliyoyasoma hapa yakapaete kuzaa matunda katika maisha yako ya kiroho katika kuifanya kazi ya Kristo. yesu aliyouagiza tukaifanye,