Kwa nini maombi yako hayajibiwi?

Neema ya Mungu ikusaidie sana Ndugu yangu mpendwa,
ni vema ukafahamu leo kwanini maombe yako hayajibiwi  kila mmoja wetu anatamani akifanya maombi majibu ayapate siku hiyo hiyo au kesho yake, kwanza faaha kuwa Mungu hafikirii kama wewe unavyo fikiri yeye anakuwazia mambo makubwa sana,na mazuri, ila katika hayo unayoyaomba Mungu akijibu au asijibu, Bado ni Mungu na usimtafute mtu wa kumlaumu,

Sasa kuna hatua chache hapa ambazo napenda tushirikiane na wewe,
(1) hakikisha unajitakasa tafakari kwanza kabla hujaaza kuomba ili utambuwe ni wapi umeishi kinyume na mapenzi ya Mungu kisha omba toba ya kumaanisha toka moyoni naye Mungu atakusamehe, Isaya 59:1

1 Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;


2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.

3 Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong'ona ubaya.

4 Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.
 
moja ya vizuizi vya maombi ya muombaji ni Dhambi,
 
(2) Baada ya toba mkaribish  Warumi 8:26  Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.


27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.

Roho mtakatifu akusaidie kuomba,
 
(3) Mathayo 6:12 jambo la tatu jitahidi kusamehe wale wote waliokukosea bila kuchukulia kosa ulilofanyiwa,
 
 
12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.


13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]

14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.

15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
Nenda sasa kafanya maombi nawe utayaona majibu,

Followers