UJUMBE :KIPAJI KILICHO FUNGWA 

Utangulizi,

Ni wazi katika Katika maisha tunayoyaishi kila mmoja anahitaji kufanikiwa japo si kila mmoja aliyefanikiwa,na wengine wanatafuta mafanikio yasiyokuwa na gharana na wengine mafanikio yasiyokuwa na channzo, wengine hawajui hata wanachotafuta, hata hivyo mafanikio ninayoyaongea hapa siyo ya mtu kuwa ma pesa nyingi,nyumba,au mali, Mhubiri 5:10 10 Apendaye fedha hatashiba fedha, Wala apendaye wingi hatashiba maongeo. Hayo pia ni ubatili.
11 Mali yakiongezeka, hao walao nao waongezeka na mwenyewe hufaidiwa nini, ila kuyatazama kwa macho yake tu?
12 Usingizi wake kibarua ni mtamu, kwamba amekula kidogo, au kwamba amekula kingi; lakini kushiba kwake tajiri hakumwachi kulala usingizi.

Maisha ya mwanadamu ishi yake yote anaishi siku mbili tu, furaha au huzuni, Muhubiri 7:14 Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake. Mungu alimpatia kila mmoja akili yake ili awe fundi wa maisha yake mwenyewe juu ya vile anataka kwa ajii ya faida ya wengine, na kila unachokifanya ukiongeza nafasi moja ya furaha fahamu pia umeongeza moja ya huzuni, hizi siku mbili zinaenda sambamba 

 Lakini pamoja na yote hayo Mungu amegawa vipawa mbali mbali na ni tofauti na karama (karama zinatoka kwa Roho mtakatifu,)

Ila tabia inatoka ndani ya mtu mwenyewe ndani ya yai kupitia kwa wazazi au kuiga, tabia ya mtu.

TABIA YA ROHONI NA TABIA YA MWILINI -ASILI:
Biblia imeainisha tabia za aina mbili, yaani tabia ya Kimungu na tabia ya kiasili au ya mwilini. Katika 1Wakoritho 2:14 “Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.”

1Wakorintho 3:1 kuna tabia za rohoni na tabia za mwilini. Hivyo anachosema Mtume Paulo ni kwamba unapoongea na watu inabidi ujue ama mtu huyo ana tabia za rohoni au za mwilini. Mfano mtu anaweza kuwa mwimbaji mzuri lakini ana tabia ya uongo;

Mithali 18:16 “KIPAIJI-zawadi ya mtu humpatia nafasi, humleta mbele ya watu

wakuu; ” hili neno zawadi kwenye Biblia ya kingereza linaitwa “GIFT” au kwa Kiswahili kipawa. Sasa basi kipawa cha mtu chaweza kumfikisha mbele za watu wakubwa na kujulikana. Mfano mtu anaweza kuwa na kipawa cha uwimbaji lakini anakaa kijijini na umaskini, ila kile kipawa chake kikionekana kinaweza kumleta mtu huyo mjini hii ndio maana ya sehemu ya kwanza ya andiko hilo. Kwasababu hiyo kila mtu aliyepo duniani amepewa kipawa na Mungu ambacho kwa hicho anaweza kufika kwenye hatua ya juu zaidi.

KIPAWA/KIPAJI KINAFUNGWA VIPI,

Sasa basi kama kipaji cha mtu humleta mtu kwenye mafanikio yake, tatizo linakuja pale mtu anapokuwa na kipawa lakini –Amefungwa na taibia mbaya

Tabia yake si nzuri. Hivyo tabia ndio ambayo inakubakiza katika sehemu uliyopo

Mtu anaweza kuwa na macho ya rohoni au upako lakini kama tabia yake ni mbaya hakuna mtu atakayetamani kuwa karibu naye. Ili Mungu akutumie kwa kiwango cha juu ni muhimu kuanza kwa kubadili tabia yako.

Mtu mwingine anaweza kuwa na kipawa kitakachomfanya apate mchumba; lakini kama tabia yake ni mbaya ana uongo, au umbeya au uzinzi inaweza kumfanya kuachwa na mchumba wake sio kwasababu hapendwi bali kwasababu ya tabia. Tabia ya Kimungu ni tabia njema na nzuri lakini tabia ya kibinadamu ni tabia mbaya aliyonayo mtu.

Shetani akitaka kuharibu kipawa cha mtu anaanzia kwenye tabia yake; kwa maana hiyo tabia ya kibanadamu au ya mwilini ndio hiyohiyo Biblia inaiita tabia ya kishetani. Imeandikwa katika Yakobo 3:15 “Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani.” Unaona kumbe tabia mbaya ya kinadamu ndio hiyo inaitwa tabia ya kishetani.

Mhubiri 10:1 “Mainzi mafu huvundisha marhamu ya mwuza marashi; Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima.” Hili ni neno la hekima la Mfalme Suleimani kusema mainzi wanaweza kuharibu marhamu nzuri; ikimaanisha unaweza kupata mpenyo katika maisha lakini tabia mbaya inaweza kukupeleka mbali kabisa na upenyo wako.

Ndio maana waweza kumkuta mtu ni mwombaji au anatenda miujiza lakini tabia yake ikawa mbaya kwasababu ya asili. Jambo hili ndlo linalosabisha watu wengine kusema “kama ulokole ndio huu sitaki kuokoka” kumbe mtu huyo aliwahi kumuona mtu ambaye ameokoka na ananena au anaombea watu lakini ni mwongo au mzinzi.

Vifungo vya tabia haviangalii cheo cha mtu,

Katika Biblia, Samson alikuwa mnadhiri wa Mungu na alikuwa amepakwa mafuta tangu tumboni mwa mamaye. Japokuwa alikuwa mpakwa mafuta lakini alikuwa na tabia mbaya ya kutaka wasichana wa kifilisti ambao Mungu alikataza tangu mwanzo.

Hii ni sawa na mtu kung’ang’ania kufungwa nira na mtu asiyeamini. Kwa njia hii Samson akakutana na Delila ambaye lengo lake halikuwa upendo bali ni kumharibia kipawa chake kwa kuijua siri yake. Vivyohivyo shetani amewaangamiza watu wa Mungu wengi kwa kuwafanya waoe au kuolewa na watu wasiomjua Kristo na matokeo yake kile kipawa cha Kimungu kilichokuwa ndani yao kinashindwa kuonekana tena.

UFANYE NINI KUTOA KIPAJI CHAKO KIFUNGONI

1. Kuiamini kweli ya Mungu ambalo ni Neno la Mungu

Yohana 8:32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
 Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?
 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
 Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote.
 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli

2. Kubali kuzaliwa mara ya pili

Yohana 3:5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.  Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.yohana 1:12

3. Kukubali kuhamishwa kutoka katika mamlaka iliyokufunga,

Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;
 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi
;

Wakolosai 1:13

4. Kubali kugeuka Kwa kubadili tabia:
Warumi 12:2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; Bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Tabia mbaya ya mtu huondoka kwa kuamua mwenyewe, hata kama mchungaji akuombee mara zote kama tabia yako ni mbaya kwa asili inakulazimu kuamua kuibadili mwenyewe.

Ni kweli tabia yako inaweza kuwa Imekufunga hapo ulipo, imekuhamisha pazuri ukajikuta pabaya,hata kibali kwa watu au imeshakupotezea upenyo katika maisha lakini ukiamua kuanza upya na BWANA na kuacha zile tabia mbaya Mungu wetu anatoa nafasi ya pili imeandikwa, “usifarahi ee adui yangu niangukapo mimi nitasimama tena” simama tena sasa kwakuruhusu tabia ya Mungu kiishi ndani yako mika 7:8 Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo, nitasimama tena; nikaapo gizani, Bwana atakuwa nuru kwangu.

Leo naongea na watu ambao walikuwa waombaji leo hawaombi tena, walimuhofu Mungu lakini leo hawana hofu, walikuwa watakatifu lakini leo ni waovu wakubwa Mungu anayo nafasi ya pili kwaajili yako. Amua kutubu na kuacha dhambi na tabia hiyo mbaya; Mungu atakuwezesha tena kama alivyomwezesha Samson kuwaangamiza wafilisti wote. Hivyo uamuzi wa kwanza ni kuamua mwenyewe kuacha tabia hiyo.

 Hitimisho

 Zaburi 119:129 Shuhuda zako ni za ajabu, Ndiyo maana roho yangu imezishika.
130 Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga.
131 Nalifunua kinywa changu nikatweta, Maana naliyatamani maagizo yako.
132 Unigeukie, unirehemu mimi, Kama iwahusuvyo walipendao jina lako.
133 Uzielekeze hatua zangu kwa neno lako, Uovu usije ukanimiliki.
134 Unikomboe na dhuluma ya mwanadamu, Nipate kuyashika mausia yako.
135 Umwangazie mtumishi wako uso wako, Na kunifundisha amri zako.

Followers