TOFAUTI YA MIUNGU NA MUNGU MUUMBA MBINGU NA DUNIA,

Kama Abraham alivyokuwa "rafiki Wa Mungu" kwa uvumilivu na utiifu kwa Mungu, wewe pia unaweza kumjua Mungu na kupata rehema zake, amani, na baraka. Kumjua Mungu kwa uvumilivu wa kweli katika kumwamini ni ujuzi muhimu zaidi katika maisha. Ni ajabu namna gani kwamba Mungu hujidhihirisha Mwenyewe kwa wote wanao Mtafuta kwa mioyo yao yote!




Ikiwa utageuka kuiacha njia yako na kweli kujitolea kwa Mungu, Roho Wake ataishi ndani yako. Hakuna kitakacho kutenganisha na upendo Wake unapo tumainia ahadi Zake na Kumfuata kwa utiifu. Yeye atakuwa Mungu wako, nawe utakuwa hazina Yake Mwenyewe. Utagundua kwamba alikununua kwa gharama kuu, na anataka kuwa na ushirika nawe—sasa na hata milele.



Uliza Mungu akupe ufahamu unapojifunza kurasa hizi za vifungu kutoka Neno la Mungu. Mungu aliongoza watu wamchao kuandika maneno haya na kwa kimiujiza ameyahifadhi katika vizazi vyote kutoka kwa majaribio yote ya Shetani ya kuyakomesha.

______________________________________________________________

Maandiko yanayo husika katika kijitabu hiki yametolewa kutoka Biblia: Sheria (Torah), Zaburi (Zabur), maandiko ya manabii, na Injili (Injil).



KUNA MUNGU WA KWELI MMOJA TU

Kumbukumbu La Torati 6:4, 5

BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja. Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.



Isaya 45:18

Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.

1 Wafalme 8:60

Watu wote wa ulimwengu Wajue ya kuwa BWANA ndiye Mungu; hakuna mwingine.

Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. —Isaya 42:8

Isaya 43:10, 11

Ninyi ni mashahidi wangu, asema BWANA,. . . mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine. Mimi, naam, mimi, ni BWANA, zaidi yangu mimi hapana mwokozi.

Isaya 45:22

Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine.



MUNGU NI WA REHEMA NA NEEMA

Zaburi 103:8, 11

BWANA amejaa huruma na neema, haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili. Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, kadiri ileile rehema zake ni kuu kwa Wamchao.

Zaburi 103:17, 18

Bali fadhili za BWANA zina Wamchao tangu milele hata milele,...maana, wale walishikao agano lake, na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye.

Mika 7:18

Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu,...kwa maana yeye hufurahia rehema.

Maombolezo 3:22

Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, kwa kuwa rehema zake hazikomi.

Maombolezo 3:32

Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.

Zaburi 18:25

Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili.

1 Mambo Ya Nyakati 16:34

Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele.



MUNGU ANAKUPENDA  KULIKO UNAVYOWEZA KUWAZA WEWE

Yeremia 31:3

BWANA alinitokea zamani, akisema, Naam, nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.

Yeremia 29:11

Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani, wala Si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Malaki 1:2

Nimewapenda ninyi, asema BWANA.

Zaburi 103:13

Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao.

Isaya 38:17

Tazama; nalikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; Lakini kwa kunipenda [ee Mungu] umeniokoa na shimo la uharibifu; kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.

1 Yohana 4:16, 19

Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza.

Sefania 3:17

BWANA, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; atakushangilia kwa furaha kuu, atatulia katika upendo wake. Atakufurahia kwa kuimba.



JAMBO KUBWA MUHIMU MAISHA NI MTU  KUMJUA MUNGU NA ANATAKA UFANYE NINI,

Danieli 11:32

Lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu.

Yeremia 9:24

Bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni BWANA, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema BWANA.

Kumbukumbu La Torati 30:19, 20

Nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, kumpenda BWANA, Mungu wako, kuitii sauti yake na kushikamana naye: kwani hiyo ndiyo uzima wako.

Zaburi 119:2

Heri wazitiio shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wote.

Zaburi 42:1

Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.

Kutoka 33:14

Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.



KUJITEGEMEA PASIPO MUNGU NI KUJIANGAMIZA WEWE MWENYEWE

2 Mambo Ya Nyakati 15:2

BWANA yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja naye; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimwacha atawaacha ninyi.

Yeremia 17:9

Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?

Mithali 16:25

Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; lakini mwisho wake ni njia za mauti.

2 Petro 2:4, 9

Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu. Basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu.

1 Samweli 12:15

Bali msipoisikia sauti ya BWANA, mkiiasi amri ya BWANA, ndipo mkono wa BWANA utakuwa juu yenu.

Yohana 15:6

Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatu. pa motoni yakateketea.



UKIMJUA MUNGU NI LAZIMA UTAMTAFUTA NA KUFANYA MAPENZI YAKE.

Yeremia 29:13

Nanyi mtanitafuta, na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.

Mithali 2:4, 5

Ukiutafuta kama fedha, . . . ndipo utakapo . . . pata kumjua Mungu.



Mathayo 7:7

Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.

Waebrania 11:6

Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

Mithali 8:17

Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.

Maombolezo 3:25

BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, kwa hiyo nafsi imtafutayo.

Matendo 17:26, 27

Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja. ...Ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.



MUNGU ANATUTAKA TWENDE KWAKE

2 Mambo Ya Nyakati 30:9

Kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye mwenye neema, na mwenye rehema, wala hatawageuzia mbali uso wake, mkimrudia.

Zaburi 86:5

Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili, kwa watu wote wakuitao.

Yakobo 4:8

Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi.

Zaburi 145:18

BWANA yu karibu na wote Wamwitao, wote wamwitao kwa uaminifu.

Isaya 1:18

Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

Mathayo 11:28, 29

Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu.

Yohana 6:37

Wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.



MUNGU NI MTAKATIFU, NA ANATAKA TUWE WATAKATIFU KAMA YEYE ALIVYO MTAKATIFU

Kutoka 15:11

. . . Ni nani aliye kama wewe, Ee BWANA, . . . mtukufu katika utakatifu.

1 Samweli 2:2 Maandiko yana tuakikishia wazi wazi,

Blog Archive

Followers