KWA MTU MMOJA DHAMBI ILIINGIA ULIMWENGUNI,

Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu aliyeumba mbingu na dunia


DHAMBI HUTUFARAKANISHA MUNGU WETU

Warumi 5:12

Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.

Yakobo 1:15

Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.

Ezekieli 18:20

Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa.

Isaya 59:2

Lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.

Mithali 11:19

Haki huelekea uzima; afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe.

2 Mambo Ya Nyakati 24:20

Mungu asema hivi, Kwani ninyi kuzihalifu amri za BWANA, hata msiweze kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha BWANA, yeye naye amewaacha ninyi.

1 Samweli 15:23

Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, yeye naye amekukataa wewe.



GHADHABU YA MUNGU   IKO JUU YA DHAMBI  ZA MWANADAMU

Zaburi 7:11

Mungu ni mwamuzi mwenye haki, naam, Mungu aghadhibikaye kila siku.

Nahumu 1:3

BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe.

Wakolosai 3:6

Kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.

Warumi 1:18

Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.

Warumi 1:29-32

Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.



HUKUMU IKO MBELE NA SAFARI YA MWANADAMU

Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu. —Waebrania 9:27

Ufunuo 20:12, 15

Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

Waebrania 10:31

Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai.

Mathayo 12:36

Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.

Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la sir likiwa jema au likiwa baya. —Mhubiri 12:14

Mathayo 13:49, 50

Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.



HATUWEZI KUMFICHA  MUNGU MAOVU YETU

Mithali 15:3

Macho ya BWANA yako kila mahali; yakimchunguza mbaya na mwema.

Zaburi 139:1-4

Ee BWANA, umenichunguza na kunijua. Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; umelifahamu wazo langu tokea mbali. Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, umeelewa na njia zangu zote. Maana hamna neno ulimini mwangu usilolijua kabisa, BWANA.

1 Samweli 16:7

Kwakuwa BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.

Zaburi 94:9

Aliyelitia sikio mahali pake asisikie? Aliyelifanya jicho asione?

Yeremia 16:17

Maana macho yangu yaziangalia njia zao zote; hawakufichwa uso wangu usiwaone, wala haukusitirika uovu wao macho yangu yasiuone.

Waebrania 4:13

Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.



KUGEUKA NA KUTOKA DHAMBINI KUNAHITAJIKA SANA KWA MWANADAMU,

Ezekieli 18:23

Je! mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi?

Luka 13:3

Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.

Mithali 28:13

Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.

Yoeli 2:12, 13

Lakini hata sasa, asema BWANA, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea; rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema.

Hosea 14:2

Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie BWANA; mkamwambie, Ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema.

Ayubu 33:27, 28

Yeye huimba mbele ya watu, na kusema, mimi nimefanya dhambi, yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni, an uhai wangu utautazama mwanga.



KUTUBU KUNALETA MSAMAHA

Isaya 55:6, 7

Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, mwiteni, maadamu yu karibu; mtu mbaya na aache njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo yake; na amrudie BWANA, naye atamrehemu; na arejee kwa Mungu wetu, naye atamsamehe kabisa.

Zaburi 34:18

BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, na waliopondeka roho huwaokoa.

Blog Archive

Followers