KUVUNJA USHIRIKA NA MUNGU

Dhambi inamuharibia mwanadamu ushirika na Mungu,

Mkristo anapotenda dhambi haimaansihi kwamba amevunja uhusiano wake na Mungu. Maana yake ni kwamba amevunja ushirika wake na Mungu. Yeye bado ni mtoto wa Mungu, lakini sasa ni mtoto asiyeti. Ikiwa mwamini hataungama dhambi yake na kutubu, anajiweka kwenye nafasi ya kuadhibiwa na Bwana.


Vita Baada ya kukata shahuri

Kama umejikuta unatamani kufanya mambo unayojua ni makosa, basi umeanza kukabiliana na “tamaa ya mwili”. Bila shaka umegundua pia kwamba unapojaribiwa na mwili kufanya kisicho sawa, kuna kitu ndani yako kinachopinga majaribu hayo. Hicho ni “tamaa ya Roho”. Na kama unajua jinsi kujisikia hatia kunavyokupata ukikubaliana na majaribu, basi unaifahamu sauti ya roho yako, tunayoiita “dhamiri” yetu.

Mungu alijua vizuri sana kwamba tamaa zetu za mwili zingetujaribu tufanye makosa. Lakini, hiyo si sababu inayoturuhusu kukubaliana na tamaa za mwili. Bado Mungu anatutazamia tutende kwa utii na utakatifu, na tushinde asili ya mwili.

Lakini nasema hivi: Enendeni katika Roho, nanyi hamtazitimiza tamaa za mwili (Wagalatia 5:16, .

Hakuna mbinu ya kiuchawi ya kushinda mwili. Paulo alisema tu kwamba “tuenende katika Roho” nasi “hatutatimiza tamaa za mwili” (Wagalatia 5:16). Hakuna Mkristo mwenye uwezo zaidi ya mwenzake katika jambo hili. Kutembea katika Roho ni uamuzi ambao kila mmoja wetu lazima aufanye, na kujitolea kwetu kwa Bwana kunaweza kupimwa kwa kiwango cha kutojitolea kwetu kwa tamaa za mwili.

Paulo akaandika hivi tena:

Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya, na tamaa zake (Wagalatia 5:24).

Ona anachosema Paulo: Wale walio wa Kristo wameusulubisha mwili (anatumia lugha ya wakati uliopita). Hayo yalitokea wakati tulipotubu na kumwamini Bwana Yesu Kristo. Hapo, tulisulubisha ile asili ya dhambi, tukaamua kumtii Mungu na kupingana na dhambi. Sasa, si swala la kusulubisha mwili tena, bali kudumisha kule kusulubiwa.

Si rahisi kuendelea kuusulubisha mwili, lakini ni kitu kinachowezekana. Kama tutatenda kulingana na kuongozwa kwa utu wa ndani badala ya kukubaliana na misukumo ya mwili, tutaonyesha maisha ya Kristo na kuenenda katika utakatifu mbele Zake.

Asili Ya Roho Kurejeshwa tena Upya,

Kuna neno moja lenye kueleza vizuri zaidi asili ya roho zetu zilizoumbwa tena. Neno hilo ni Kristo. Kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ana asili ile ile ya Yesu, sisi ndani yetu tuna asili ya Yesu. Paulo aliandika hivi: “Si mimi ninayeishi tena, bali Kristo anaishi ndani yangu” (Wagalatia 2:20,

Kwa sababu tuna uwezo Wake na asili Yake ndani yetu, tunao uwezo wa ajabu sana wa kuishi kama Kristo. Hatuhitaji upendo zaidi, au uvumilivu, au kiasi – ndani yetu tunaye Mtu mwenye upendo sana, mwenye uvumilivu sana, mwenye kiasi sana – anakaa ndani yetu! Tunachohitaji kufanya ni kumruhusu Yeye kuishi kwa kututumia sisi.

Ila, wote tuna adui mmoja mkubwa ambaye anapambana na asili ya Yesu, akiizuia isijidhihirishe kupitia kwetu, naye ni mwili wetu. Ndiyo maana Paulo alisema lazima kuusulubisha mwili wetu. Ni wajibu wetu kufanya kitu juu ya mwili wetu, na ni kupoteza wakati kumwomba Mungu afanye chochote kuhusu mwili. Hata Paulo alikuwa na matatizo na asili yake ya kimwili, lakini aliwajibika na kuushinda. Anasema hivi:

Ninautesa mwili wangu na kuufanya mtumwa, ili, baada ya kuwahubiri wengine, mimi mwenyewe nisije nikakataliwa (1Wakor. 9:27,

Hata wewe itabidi kuufanya mwili wako kuwa mtumwa wa roho yako, kama unataka kuenenda kwa utakatifu mbele za Bwana. Na, inawezekana! kabisa ila ukitaka mwili ufanye mapenzi yake nayo ni hatari kwa mkristo unaweza kumpeleka pabaya

Blog Archive

Followers