K2 MAUTI YA KI-ROHO

Fuatilia yale aliyo yasema Yesu ili kupa muongozo zaidi kuhusiana na kile kinacho sadikika kufa ki-roho maana wengi wamezowea kusikia mtu amefariki ile ya mwili kutengana na roho,ila kuna ile ya mtu kutengana na Mungu inakuwaje?unaweza ukawa kimwili uko hai ila kiroho ukawa tayari ni marehemu,

Maneno ya Yesu ni maelezo sahihi kabisa ya washika dini wote ambao hawajawahi kuzaliwa upya kwa njia ya Roho Mtakatifu. Kuzaliwa upya huwasafisha watu ndani, si nje tu.


Mabadiliko Kwa Nafsi Wakati Roho Inapozaliwa Upya?

Roho ya mtu inapozaliwa upya, nafsi yake hapo mwanzoni inabakia kama ilivyokuwa (ingawa kwa akili zake anakuwa amefanya uamuzi wa kumfuata Yesu). Ila, Mungu anatazamia kwamba tufanye kitu na nafsi zetu mara tunapokuwa watoto Wake. Nafsi zetu (au nia) zinapaswa kufanywa upya kwa Neno la Mungu ili tuweze kufikiri kama Mungu anavyofikiri. Kwa kufanywa upya nia zetu, badiliko la kudumu la nje linafanyika maishani mwetu, na kutufanya tuzidi kufanana na Yesu.

Wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu (Warumi 12:2, maneno mepesi kukazia).

Hata Yakobo naye aliandika kuhusu mfuatano huo wa mambo katika maisha ya mwamini, hivi:

Kwa hiyo wekeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa nafsi zenu (Yakobo 1:21,

Ona kwamba Yakobo alikuwa anawaandikia Wakristo – watu ambao roho zao zilikuwa zimekwisha zaliwa upya. Ila, walihitaji nafsi zao kuokolewa, na hayo yangefanyika tu wakati anapopokea “neno lile lililopandwa ndani”. Hii ndiyo sababu waamini wapya wanatakiwa kufundishwa Neno la Mungu.

Usumbufu unaoweza kujitokeza baada ya kuamuwa kuyafuata ya Mungu,

Baada ya kuzaliwa upya kwao, Wakristo wengi hugundua kwamba ni watu wenye asili mbili, na kujikuta wakikabiliana na kile kitu kinachoitwa na Paulo, vita kati ya “Roho na mwili”.

Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili, kwa maana hizi zi mepungana, hata hamwezi kufanya mnayotaka (Wagalatia 5:17).

Mabaki ya ile asili ya kale ya dhambi, yanaitwa “mwili” na Paulo. Hizo asili mbili ndani yetu huleta shauku tofauti, ambazo, kama watu watakubaliana nazo, husababisha matendo tofauti na mitindo tofauti ya maisha. Ona tofauti anayoweka Paulo kati ya “matendo ya mwili” na “tunda la Roho” katika fungu lifuatalo:

Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya: Uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo. Katika hayo nawaambia mapema, kama nilvyokwisha kuwaambia ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Lakini tunda la Roho ni: Upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi. Juu ya mambo kama hayo hakuna sheria (Wagalatia 5:19-23).

Bila shaka inawezekana kwa Wakristo kukubaliana na mwili, vinginevyo Paulo asingewaonya kwamba kuzoea kuufuata mwili kutawafanya wasiweze kuurithi ufalme wa Mungu. Katika barua yake kwa Warumi, Paulo aliandika pia juu ya hizo asili mbili za kila Mkristo, na akaonya tena juu ya matokeo hayo hayo, kama watu watakubaliana na mwili. Anasema hivi:

Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa habari ya dhambi, bali roho yenu iko hai kwa habari ya haki. … Basi ndugu, kama ni hivyo, wote tunawajibika, si kwa mwili kwamba tuishi kwa kufuata mambo ya mwili. Kwa maana, mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili mwataka kufa, bali mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Kwa kuwa wote wanao-ongozwa na Roho wa Mungu ndio wana wa Mungu hao (Warumi 8:10, 12-14, TLR. Maneno mepesi kukazia).

Hilo ni onyo dhahiri kabisa kwa Wakristo kwamba, kuishi (yaani tabia ya kawaida, au mazoea) kulingana na mwili matokeoyake ni kifo. Bila shaka Paulo alikuwa anaonya juu ya kifo cha kiroho maana kila mtu hatimaye hufa kimwili – hata Wakristo wale wanao”yafisha matendo ya mwili”.

Mkristo anaweza kuangukia katika mojawapo ya dhambi ambazo Paulo aliorodhesha hapo kwa kitambo tu. Ila, mwamini anapofanya dhambi, atajisikia hukumu na pengine atatubu. Yeyote anayeungama dhambi yake na kumwomba Mungu amsamehe, atasafishwa (ona 1Yohana 1:9).

Blog Archive

Followers