KWENYE UTAKATIFU KUNA UTUKUFU WA MUNGU

Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; kwa maana hakuna ye yote ila wewe.


Ayubu 34:10

Mungu asidhaniwe kutenda udhalimu; wala Mwenyezi kuf anya uovu.

Isaya 6:3

Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.

Isaya 57:15

Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu.

Zaburi 145:17

BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.

Marko 10:18

Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.

Ufunuo 15:4

Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu.



WATU WA MUNGU NI LAZIMA WAISHI MAISHA MATAKATIFU

Yakobo 2:19, 20

Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka. Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?

1 Yohana 2:4; 3:10

Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.

Njia ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA; bali humpenda mtu afuatiaye wema. —Mithali 15:9

Waebrania 12:14

Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao.

Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote. —1 Petro 1:15

Amosi 5:14

Tafuteni mema, wala si mabaya, mpate kuishi; hivyo BWANA, Mungu wa majeshi, atakuwa pamoja nanyi, kama msemavyo.



MAMBO MUNGU ANAYOYATAKA KWAKO

Mika 6:8

Na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!

Mambo Ya Walawi 19:2

Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wenu, ni mtakatifu.

Luka 10:27

Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.

Marko 10:19

Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usi danganye, Waheshimu baba yako na mama yako.

Warumi 12:2

Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu.

Yoshua 1:8

Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

Marko 11:22

Mwaminini Mungu.



MAMBO MUNGU  ALIYOYATAJA ANAYOCHUKIA

Mithali 6:16-19

Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA; naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; moyo uwazao mawazo mabaya; miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; shahidi wa uongo asemaye uongo; naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.

Isaya 61:8

Maana mimi, BWANA, naipenda hukumu ya haki, nauchukia wivi na uovu.

Ufunuo 21:8

Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Malaki 2:15, 16

Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana. Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA.

Zekaria 8:17

Wala mtu wa kwenu asiwaze mabaya moyoni mwake juu ya jirani yake; wala msipende kiapo cha uongo; maana hayo yote ndiyo niyachukiayo, asema BWANA.



WATU HUPUNGUKIWA NA MATAKWA YA MUNGU,

Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu. —Yohana 5:42

Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. —Yakobo 2:10

Isaya 6:5

Ndipo niliposema, Ole wangu! kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.

Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi. —Yakobo 4:17

Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, hakuna mwenye haki hata mmoja. —Warumi 3:10

Warumi 3:23

Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.

1 Yohana 3:10

Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.

Isaya 53:6

Sisi sote kama kondoo tumepotea; kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe.

Ni nani awezaye kusimama mbele za BWANA, huyu Mungu mtakatifu? —1 Samweli 6:20



KAZI ZETU WENYEWE HAZIWEZI KUMPENDEZA MUNGU KAMA HATUJAMSHIRIKISHA,

Warumi 10:2, 3

Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.

Isaya 64:6

Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi.

Ezekieli 33:13

Nimwambiapo mwenye haki, ya kwamba hakika ataishi; kama akiitumainia haki yake, akatenda uovu, basi katika matendo yake ya haki, hata mojawapo halitakumbukwa; bali katika uovu wake alioutenda, atakufa katika uovu huo.

Warumi 8:8; 3:20

Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria.

2 Wakorintho 3:5

Blog Archive

Followers