KUNA UMUHIMU GANI WA KUTUBU DHAMBI ZETU KWA MUNGU?

Yeremia 36:3


Wapate kurudi, kila mtu akaiache njia yake mbaya; nami nikawasamehe. . . dhambi yao.

Zaburi 32:5

Nalikujulisha dhambi yangu, wala sikuuficha upotovu wangu. Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA, nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.

1 Yohana 1:9

Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.

Matendo 3:19

Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe.

Kutubu kunamaanisha kugeuka kutoka dhambini pamoja na kuungama mbele za Mungu.



DHABIHU INAYOTAKIKANA KUTUPATANISHA NA MUNGU

(Dhambi ilileta utengano.)

Mambo Ya Walawi 17:11

Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.



Waebrania 9:22

Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo



Kutoka 12:5, 13

Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja. ...Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu.



Mwanzo 22:8, 13

Ibrahimu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu. . . . Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.



YESU NDIYE MWANA KONDOO ALIYETOLEWA NA MUNGU

Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! —Yohana 1:29

Alionewa, lakini alinyenyekea, wala hakufunua kinywa chake; kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, na kama vile kondoo anyamazavyo mbele yao wakatao manyoya yake; naam, hakufunua kinywa chake. —Isaya 53:7

Wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. Kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi. . . . Basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? —Waebrania 9:12,28, 14



1 Petro 1:18, 19

Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.



UKOMBOZI NI KWA MAAFIKANO TU NA MUNGU



Warumi 3:24, 25

Wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake.

Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. —Warumi 5:8,9

Hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu. —Wagalatia 2:16

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. —Waefeso 2:8,9

Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi. —Matendo 10:43



Matendo 4:12

Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.





KUZALIWA KWA YESU KWATANGAZWA



Luka 1:26-38

...Malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. ...Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, ...na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.... kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake.

Watu tu walioingia Ulimwenguni pasipo uzao wa Mume na Mke walikuwa Adamu na Kristo. Adamu alileta dhambi katika Ulimwengu, lakini Yesu alileta ushindi juu ya dhambi.

yesu unamtambuwaje?

Wafilipi 2:6, 8

Ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.



Yohana 10:30, 36

Mimi na Baba tu umoja. Je! yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?

Yesu Kristo, Neno la Milele, amekuwako daima. Kwa muujiza, Mungu alisababisha atungwe mimba katika tumbo la Mariamu. Kimwili anajulikana kama Mwana wa Mtu, na Kiroho anajulikana kama Mwana wa Mungu. Maandiko yanatumia neno "Mwana" kueleza uhusiano ulioko kati ya Mungu na Neno lake—Yesu Kristo.



Waebrania 10:5

Kwa hiyo ajapo . . . Lakini mwili uliniwekea tayari.

Na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu. —Warumi 1:4

Blog Archive

Followers