NAMNA YA KULINDA
HATIMA
Utangulizi
Mwenye
jukumu la kuifuata hatima ya maisha na kuilinda ni mtu mwenyewe wewe ndiyo
muhusika mkuu na kiongozi wa kuiongoza hatima ya maisha yakow ewe mwenyewe,
maana fikra zako unazielekeza wewe mweneyewe hata kama utashahuriwa bado wewe
unajukumu kubwa la kulinda hatima ya maisha yako,kama vile mzazi anavyolinda
mtoto wake ndivyo kila mmoja wetu wanatakiwa kulinda hatima yake,
Hatima
inayotakiwa kulindwa ni nini?
Hatima ni Hali
au uwezo Wa mtu kufikia katika Kusudi
alilokusudia au kusudiwa au ni sababu iliyo ndani ya Mutu, mipango au malengo
yake kama alivyoiona au kupanga moyoni mwake, maisha ni ule uwepo wa uhai wa
kiumbe chochote amacho kipo katika hii Dunia, sasa uhai wako unaambatana na
mahitaji yako ili huu uhai uendelee kuwepo hadi kufikia kusudio la Mungu, kila
kiumbe chenye Uhai kina mahitaji yanayo hitajika, hiyo mipango iwepo ili kufikia ile hatima,
Imeandikwa Mithali 16:1 Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu;
Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana.haya maandaliyo ya moyo ni mipango ya
hatima yako kumbuka katika moyo ndiko Roho mtakatifu anapaswa kukaa na ndiko
karakana ya kuunda kila unachokitaka
kitokee,
Yale
uliyoyaanda yote ndani ya moyo wako na
unategemea kuyakamilisha haijalishi mda
Usitafute
Adui wa hatima ya maisha yako,
Wakati
mwingine tumekuwa tukiwalalamikia watu mbalimbali na wengine walikuwa watu wetu
wa karibu kwamba wametuharibia maisha. Kwa mfano unaweza kusikia mtu
akilalamika kuwa : “…… ameniharibia maisha yangu!”, “……..ameniaribia masomo
yangu!” au “…….. amenifanya niitelekeze familia yangu!” na kadhalika. Lakini ni
vizuri tukafahamu kuwa kila mmoja anawajibu wa kuilinda thamani yake aliyopewa
na Mungu kabla ya wengine kuilinda na kuijali.
Pengine
inawezekana tukaona kuwa kuna sababu za kuwalaumu watu kwamba walihusika
kuyaharibu maisha yetu; lakini je tuliwahi kujiuliza ni hatua gani tulichukua
kuzilinda hatima za maisha yetu?
Umepokea
ushauri wa watu wangapi wanaokushauri vibaya kuhusu malengo hatima yako?unataka
kuolewa,kusoma,kufanyabiashara,kujenga,kuanza Huduma,je hatima ya maisha yako
uliilinda,
Uliwapa watu
wangapi nafasi ya kuchezea hatima yako!?
Umeenda
maeneo mangapi yanayopunguza kasi ya kufikia ndoto zako!?
Umependa
vingapi vinavyoondoa kusudi la hatima ya maisha yako hapa duniani!
Haya ni
baadhi ya maswali tunayoweza kujiuliza kama msaada wa kulinda hatima zetu ili kuanza hatua mpya au kuendelea mbele pamoja na hatima
ya maisha yangu,
Imeandikwa 2 Petro 1:3 “kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote
vipasavyo uzima na utauwa kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema
wake mwenyewe.
Kwakuwa
tulivyo navyo vipo ndani yetu jukumu la kulinda ni la mtu binafsi, na hatima ya
Mtu inaanzia wapi?
Hatima ya
mtu inaanzia katika mawazo ya Mungu inakamilishikia tumbomi mwa mama imeandikwa yeremia 1:4
WATAMBUWE
MAADUI WA HATIMA YAKO
Nini maana ya adui ni nguvu ya
upizani au uasi unaokutana nao juu ya
hatimaya maisha yako,
- Kukatisha tamaa juu ya jambo ulilofanya,au unalojaribu,au wazo zuri unalopanga kulifanya
- 2. Kumwonea wivu mtu kwa sababu ya mafanikio yake ya kimwili au kiroho – imeandikwa MWANZO 37:9-11;
- Marafiki wasiyokutakia mema watu wasiyotaka kuona unasonga mbele Jiepushe nao,
- Kukusudia mabaya juu ya wengine MWANZO 50:20; NEHEMIA 6:2; EZEKIELI 38:10-
- Marafiki wasiyokuwa na mtazamo mkubwa na wakuona mbali
- Marafiki wanaotaka kunufaika kupitia wewe
- Kuhisi umefika safari yako ikiwa bado
- Kuhisi wewe unaweza kufanya chochote bila wengine,kujiona wewe wa muhimu kuliko wengine
- Kuona wewe ni Zaidi ya watu wote yaani kuwa nakiburi cha mali,uzima,heshima
- Dharau kwa wenzako ikiwa ili ufanikiwe unahitaji watu katika maisha ,kuuza au kununua unahitaji watu,
- Tabia ya asili yaani tabia inayotokana na desturi ya ukoo au kablia
- familia
- Mazingira ya kifamilia ya kwenu,ikiwa mlikuwa masikini inaweza yanaweza kuwa adui kwako ukafikiri hayo ndiyo maisha halili unayotakiwa kuishi maana ndiyo uliyoyakuta,
- Kutokubali mabadiliko katika yanayoweza kukufanikisha jambo Fulani,
- Kutamani madaraka Zaidi kama Namani na modikae
- Kukosa umakini na mafanikio ya hatua ya kwanza
- Kutokutambuwa udhamani wa maisha nan a talanta uliyopewa
- Kuwa na marafiki wenyemitazamo ya yakushindwa,
- Kukosa uvumilivu wakati wa kujaribiwa
- a yaani wakati wa magumu,
- hali ngumu ya uchumi inasababisha kukata tamaa na kulalamika,
- mafanikio ya kiuchumi kuwa juu
- au kupata madaraka makubwa bila matarajio ya hiyo nafasi,
- Jinsia inaweza kuwa adui wa hatima yako kujiona kwakuwa wewe uko hivyo ulivyo,mke,mme,
- Kutodhubutu hatuwa ya mafundisho unayofundishwa,
- Kutumia ulimi wako vibaya
- Kukosa maarifa juu ya hatima ya maisha yako,
- Kupoteza shahuku ya kuendelea mbele juu ya kufanikisha hatima yako,
- Kukosa mlengo yaani kukosa maono ni adui wa wewe kufika katika hatima au kutunza hatima yako,
- Kushindwa kutoa shukrani juu ya kile Mungu alichokutendea,shukuru wazazi,
- Kukosa mvuto juu ya kile unalolitaka na juu ya watu waliyokuzunguka,
- Kujiamini hadi kumzidi roho mtakatifu,
Dalili
za mtu hatima yake imevamiwa
- Hatima iliyoharibika mtu kuishi maisha ya kuiga wengine
- Hana maamuzi na maisha yake
- Ni mtu anayeishi kwa ubishi wa kila jambo
- Hatima iliyotekwa anaishi kwakulinganisha maisha yake na wengine
- Hatima iliyoharibika ni anaishi kwakubahatisha,(kwa kuhisi)
- Nimtu wa kujitenga na wengine au kutaka kuhurumiwa sana
- Mtu hatima yake iliyoharibika ni mlalamikaji san ahata umtendei jema hana shukrani maana haoni udhamani
- Mtu hatima imeharibika ni mtu wakuvunjika moyo haraka sana
- Mtu hatima imeharibika anahisi kukataliwa na wengine,
- Mtu hatima imeharibika akianzisha jambo hawezi kukamilisha,
Ufanye
nini kulinda hatima ya maisha yako
Jifunze kumtumaini Mungu kwa akili zako zote na kwa moyowako
wote mithali 3:5
Jifunze kuwa mnyeyekevu siku zote za maisha yako kanuni ya
kupanda ni kushika,
Jitahidi kukubalika mbele za Mungu na mbele za wanadamu 1timotheo
7:15
Mshukuru Mungu kwakila kiwango anachokufikisha maana kuna
ambao hawajafika kiwango hiko
Tafuta macho ya rohoni na masikio ya rohoni kuweza kutembea
ndani ya maono ya Mungu, marko 8:18
Jitahidi kutumia muda wako vizuri sana na furusa iliyombele
yako pia,
Jikubali na jisimamie wewe mwenyewe kwa kuamini kwamba
unaweza kufanya Zaidi ya hapo ulipo jikubali hivyo ulivyo haijalishi
umepungukiwa nini kubali sauiti mwili,elimu uliyo nayo,
Jitahidi kuwa na subira ya ahadi za Mungu alizokuhaidi
kupitia vyinywa vya manabii mambo ya
nyakati 20:20
Kukubali kushinda majaribu unayotakiwa kupita,
Usikubali kukatatamaa mapema kwakutoamini Imani yako usiwe
mtu wa kusita sita, waibrania 10;38
Chochea moto wa madhabahu unayoiamini,
Hitimisho:
Maombi ya
toba kwakutojuwa hili…………..