MBELE ZA MUNGU HAKUNA UBAGUZI

kizibiti chako kitajitambulisha hakutakuwa na ubishi kwa mtu yeyote yule,

Wakorintho 5:10

Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee. kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.


Warumi 2:16
Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, kwa Kristo Yesu.

2 Wathesalonike 1:7, 8
Wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake; katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu.


Luka 19:27

Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu.


SIO WOTE WANAOSHUHUDIA KUMFUATA YESU WALIO WA YESU


Tito 1:16
Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana.

Warumi 8:9

Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.

Ezekieli 33:31
Nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao.

Mathayo 15:8
Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami.


Mathayo 7:21-23

Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika uf alme wa mbinguni; bali ni yeye af anyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.


WAFUASI HALISI WA YESU HUMII

1 Yohana 2:3

Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.

Ezekieli 36:27
Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.


Waebrania 5:9
Naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii.


Warumi 6:18

Na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.

Waefeso 2:10

Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.


Warumi 8:10, 13

Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki. Kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.

2 Timotheo 2:19

Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.


ULIMWENGU UNACHUKIA WAFUASI WA YESU

Yohana 15:18, 19

Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake, lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.

Yohana 16:2, 3

Naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.

1 Yohana 3:1

Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.

Matendo 14:22
Na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.


2 Timotheo 3:12

Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.

Yohana 16:33

Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

AHADI KWA WANAO DHULUMIWA

Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. —1 Petro 5:7

Isaya 41:10

Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

Baba yangu na mama yangu wameniacha, bali BWANA atanikaribisha kwake. —Zaburi 27:10

Waebrania 13:6

Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?

1 Petro 4:14

Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia.
Zaburi 91:11; 23:4 Fuatilia maandiko

Followers