Si kila anayetuhumiwa kosa ni kweli amelifanya"
Siku za leo watu wanapitia mateso makali sana tena wasiyo stahili kupitia kwamakosa ya kusingiziwa tu kabla ya kuendelea kufafanuwa sana tuangalie maandiki yanatuhakikishia nini kuhusiana na hili ninalotaka tushirikiane na wewe leo, Bilblia inatueleza juu ya mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Yusufu wengi mnazifahamu habari zake hapa nitazitolea mfano kidogo ili kukuwezesha wewe kuelewe zaidi
Baada ya kitambo Mke wa potifa akamtamani Yusufu akamwambia njoo ukutane nami kimwili lakini yusufu akakataa akamwambia yule mwanamke mimi nikiwa katika uongozi Bwana wangu hausiki na kitu chochote katika nyumba hii kila kitu alicho nacho amenikabithi Hapa nyumbani hakuna aliye mkuu kuliko mimi bwana wangu hakunizuilia kitu chochote isipokuwa wewe kwakuwa wewe ni mke wake nitawezaje basi kufanya uovu huu na kutenda Dhambi zidi ya Mungu? ingawa yule mwanamke aliendelea kumshawishi siku baada ya siku yusufu alikataa kukutana naye kimwili wala kukaa karibu naye
Siku moja yusufu akaingia ndani ya nyumba kufanya kazi zake hapakuwa na mfanyakazi yoyote ndani ya nyumba mke wa potifa akashika Vazi alilokuwa amevaa yusufu akamwambia njoo tukutane kimwili, lakini yusufu akaacha vazi lake mkononi na kukimbia nje ya nyumba akawaita watumishi wake wanyumbani akawaambia "Tazameni huyu mwibrania ameletwa haoa kututhihaki!! aliingia hapa ndani ili akutane nami kimwili, lakini nikapiga kelele aliposikia kelele za kuomba msaada akaacha vazi lake kando yangu akakimbilia inje
Yule mwanamke akaliweka vazi karibu naye mpaka potifa alipo rudi yumbani ndipo akamwelezea kisa hiki akisema yule mtumwa wa kiibrania uliyemleta alinijia ili kunithihaki! aliingia hapa ndani ili akutane nami kimwili lakini nikapiga kelele aliposikia kelele za kuomba msaada akaacha vazi lake kando yangu akakimbia inje ya nyumba,
Wakati potifa aliposikia kisa hiki mkewe alicho mueleza Hivi ndivyo mtumwa wako alivyo tenda "Hasira ya potifa ikawaka Potifa akamchukuwa Yusufu na kumweka Gerezani Mwanzo 39:7, kwa hivyo tunamuona huyu kijana wawatu pamoja na kujitahidi kukimbia bado kesi inamwangukia ya kusingiziwa wewe mwenyewe ni shahidi wa maisha yako ni mara ngapi umesingiziwa na jambo na watu wote akaliamini kuwa ni lakeli ninajuwa lili kuumiza sana,
Unapo ona misukosuko mbele yako ujuwe katika ulimwengu wa ki-Roho kunasehemu Mungu anataka kukufikisha kwa sababu maalumu kwaajili ya utukufu wake leo hii kama ningemueleza mtu bila ushahidi kama nilioutumia hapa engeweza asiamini lakini ndugu yangu ninakutia moyo wewe songa mbele usibabaike na ushahidi unaoonyeshwa usio wa kweli, kama ushahidi uliobakiza mikononi ni wakweli jitahidi kutubu na kukiri kosa na uanze maisha mapya,bali kama moyo wako unauhakika hujatenda jambo unalotuhumiwa nalo wewe tulia Mungu atafanya jambo kwaajili yako,
wengine wameachia nafasi kwa ibilisi anawatesa kila siku maana wamemuachia ushahidi ndio anaokwenda nao kwa Mungu wetu kushitaki ana mwambia Munngu Tazama huyu mtumishi wako anakuita kila jumapili tena anataka umubariki lakini juzi tu alikuwa kwa wachawi anamtengeneza jirani yake ,mkewe,mmewe,mtoto wa jirani yake,au kutafuta Dawa ya biashara na ushahidi huu hapa anaonyeshea yale madawa uliyoyakumbatia au kuyavaa kiunoni,shingoni au kuweka chini ya godoro lako la kitanda, sasa Mungu akiangalia kizibitisho akakikuta kipo na ni cha kweli huwezi kupokea uponyaji wala baraka maana yeye ni Mungu mwenye wivu apaswae kuabudiwa ni yeye tu wala hashirikiani na mtu wala kitu katika utukufu wake,
Chunguza haya niliyoelezea hapa kama ndani yake unashuhudiwa wewe kuufuta ushahidi uliomwachia ibilisi akapata nafasi ya kukushitaki nayo kwa Baba yako wa mbinguni, kama kuna umuhimu nenda kautupe ule uchawi na madawa uliyopewa na yule mchawi, kama ni ushahidi wa mtu kamtangazie kuwa sasa basi uhusiano na mke asiye mke wako,au mme asiye wako baki na wakwako,mwambie Mungu akutoshelezee huyo huyo tu, kama ni umbea acha mara moja, wizi acha mara moja lolote unalolijuwa kuwa halitamtukuza Mungu liache na usilifanye tena maana utakuwa ndio ushahidi wa wako utakaotumika na Muovu kukushitaki wewe,
Soma neno la Mungu na ufuate maelekezo yote usitafute kile unachokitaka tu,ukikihitaji unachokitaka pekee utakipata na utakwepana na baraka za Mungu, kitu chochote kinachofaywa bila Mungu kuhusishwa kitawezekana kwa mda mfupi baada ya hapo lolote linaweza kutokea, kwani hujawahi kuona au kusikia mtu anajenga nyumba nzuri sana akimaliza tu kabla hajaingia anafariki dunia, au mtu anaoa hivi karibuni tu lakini chakushangaza inakuwa kama amewaolea watu anakuwa ni mke wa watu na si mke wa mtu, na inawezekana ameenda kuolea mbali ya mji au mkoa au inchi ila akishamfikisha tu tayari anakuwa ni wawatu wengine wakatimwingine anapokonywa kabisha, anakuwa wa wangine unaweza kuyaona haya kumbu kumbu la torati 28:30
Ushahuri wangu mtangulize Mungu katika maisha yako yote si kwa kutamka kwa kinywa tu bali kwa kumaanisha inaendelea,,,
Ndugu Mtazamaji/ MSOMAJI; Bila shaka unampenda Mungu Sana tunaamini hivyo Kwa vile ulivyoweza kufika mahali hapa tulipo kupitia Mtandao huu, lipo kusudi la Mungu kutaka kukusaidia jambo Fulani ikiwa uko tayari katika yote jiepushe na mafundisho yasiyokuwa ya ki-Mungu Mathayo 16:6-12) piga simu kwa masaada zaidi huduma hii ni bure 0757328311