SHERIA YA MUNGU KWA WANADAMU NI IPI?
Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya vijito vya maji, uzaao matunda yake kwa majira yake, wala jani lake halinyauki; na kila alitendalo litafanikiwa.
Yesu hutoa maisha yen ye mazao
Yohana 15:4a, 5
Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
MAANDIKO YANA NENA NINI JUU YA YESU KRISTO?
Yohana 5:39, 46
Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. . . . Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu.
Luka 24:27
Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.
NENO LA MUNGU HALIBADILIKI
Zaburi 119:89, 160
Ee BWANA, neno lako lasimama imara mbinguni hata milele. Jumla ya neno lako ni kweli, na kila hukumu ya haki yako ni ya milele.
Isaya 40:8
Majani yakauka, ua lanyauka; bali neno la Mungu wetu litasimama milele.
Mathayo 5:18
Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.
Yohana 10:35
Na maandiko hayawezi kutanguka.
Mtu asijaribu kubadilisha maneno ya Biblia
Kumbukumbu La Torati 12:32
Neno niwaagizalo lo lote liangalieni kulifanya; usiliongeze, wala usilipunguze.
Mithali 30:6
Usiongeze neno katika maneno yake; asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo.
Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima. —Ufunuo 22:19
Mithali 13:13a
Kila alidharauye neno hujiletea uharibifu.
KIFO CHA YESU KILIKAMILISHA MPANGO WA MUNGU
Yohana 10:17, 18
Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena.
Mathayo 26:53, 54
Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika? Yatatimizwaje basi maandiko, ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri?
Matendo 3:18
Lakini mambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza hivyo.
Matendo 2:23
Mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua.
Isaya 53:10
Lakini BWANA aliridhika kumchubua; amemhuzunisha; utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi.
KIFO CHA YESU KUTANGAZWA NA MASHAHIDI
Marko 15:27, 28
Na pamoja naye walisulibisha wanyang’anyi wawili, mmoja mkono wake wa kuume na mmoja mkono wake wa kushoto. Basi andiko likatimizwa linenalo, Alihesabiwa pamoja na waasi.
Mathayo 27:45, 50-51, 54
Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa. . . . Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. . . . nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka. Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo ya liyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.
Yohana 19:32-37
Basi askari wakaenda, wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili, aliyesulibiwa pamoja naye. Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji. ...Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie, hapana mfupa wake utakaovunjwa. Na...watamtazama yeye waliyemchoma.
YESU ALISHINDA KIFO
Matendo 2:24, 32
Ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao. Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake.
Waebrania 2:14, 15
Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.
1 Wakorintho 15:55, 57
Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Ufunuo 1:18
Na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
2 Timotheo 1:10
Na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili.
KUNAFAIDAGANI KUMKIRI KRISTO YESU?
Ufunuo 3:20
Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. Ugumu wa watu wengi ni namna ya kusikia sauti ya Mungu lakini kama ni Mungu watu wanampenda usahuri wangu nyenyekea chini ya mkono wa mungu naye atakusaidia kukutofautishia sauti yake na ya muovu maana sauti ya muovu imepoteza wengi sana japo bado Mungu wete hao hataki wapotee bali anataka wote watakao mwamini wapate kuwa na uzima tele tena wa milele,
Ndugu Mtazamaji/ MSOMAJI; Bila shaka unampenda Mungu Sana tunaamini hivyo Kwa vile ulivyoweza kufika mahali hapa tulipo kupitia Mtandao huu, lipo kusudi la Mungu kutaka kukusaidia jambo Fulani ikiwa uko tayari katika yote jiepushe na mafundisho yasiyokuwa ya ki-Mungu Mathayo 16:6-12) piga simu kwa masaada zaidi huduma hii ni bure 0757328311