UFUFUO WETU BAADA YA MAUTI YA MWILI WA DAMU NA NYAMA

kufufuliwa baada  ya mauti ya huu mwili wa damu na nyama

Warumi 8:11

Lakini, ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.

1 Wakorintho 6:14

Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake.

Yohana 11:25, 26

Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele.

1 Wakorintho 15:21-23

Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja.

Yohana 14:19

Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai.

USIDHARAU WOKOVU HUU MKUU — 40

Waebrania 10:28, 29
Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu. Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?

Yohana 12:48

Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.

Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakuf a katika dhambi zenu. —Yohana 8:24

Luka 12:4, 5

Nami nawaambia ninyi rafiki zangu, msiwaogope hao wauuao mwili, kisha baada ya hayo hawana wawezalo kutenda zaidi. Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanum; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo.



Waebrania 2:3

Sisi je! tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii?


YESU KRISTO ATATUHUKUMU — 41

Matendo 17:31

Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.

Yohana 5:22, 23

Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote; ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba.



2 Wakorintho 5:10

Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee. kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.

Warumi 2:16

Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, kwa Kristo Yesu.


2 Wathesalonike 1:7, 8

Wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake; katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu.

Luka 19:27

Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu.

SIO WOTE WANAOSHUHUDIA KUMFUATA YESU WALIO WA YESU — 42

Tito 1:16

Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana.


Warumi 8:9

Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.

Ezekieli 33:31

Nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao.

Mathayo 15:8
Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami.

Mathayo 7:21-23

Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika uf alme wa mbinguni; bali ni yeye af anyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

WAFUASI HALISI WA YESU HUMII — 43

1 Yohana 2:3

Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.

Ezekieli 36:27

Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.
Waebrania 5:9

Naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii.
Warumi 6:18

Na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.
Waefeso 2:10

Followers