HUYU NDIYE NABII TITTO ANAYEHAMINI KWAMBA POMBE NI TIBA SAHIHI KWA MAGONJWA YOTE
Leo nilipata mgeni wa ghafla ofisini kwangu aliyejitambulisha kwa jina la Nabii Titto.Nabii Titto yeye anahubiri matumizi ya pombe kwa kutumia Biblia,anasema kuwa mungu ameruhusu watu wanywe pombe kwani ni tiba sahihi kwa magonjwa mbalimbali .Alikuja ofisini kwangu ili nimsaidie kurekodi kanda na cd mbalimbali zitakazomafanya watu mbalimbali duniani kupata neno lake na kunisihi sana na kuniambia nikubali kwani ilo ndio ombi mungu alilomtuma kwangu.Mimi sikumkubalia ombi lake kwani ninavyoamini mimi na imani yanguni vitu viwili tofauti.Je Wadau mnasemaje kuhusu Nabii Titto
Juma Chikoka (Chopa mchopanga) akiwa na Jackline Wolper na Johari wakimsikiliza Nabii Titto kwa umakini mkubwa
Kipeperushi hiki cha Nabii Titto kiliniacha hoi
Nabii Titto yeye anadai kuwa ameoteshwa na mungu kuwa watu wanywe pombe kwani ni tiba sahii tosha kwa magonjwa mbalimbali na si pombe tu mpaka sigara,Sikuamini maneno yake akatumwa mtu alete pombe na Nabii Titto bila hiyana kudhihirisha umma akakata safari beer,Wadau mpooo
Hiki ndicho kipeperushi alichotugawia kinachoeleza jinsi pombe inavyotibu magonjwa yote
Nikisikiliza mahubiri ya Nabii Titto ameniambia yuko njiani kuanzisha kanisa
Nabii Titto akiwa katika mavazi yake ya kikazi
Nabii Titto akinukuu neno kutoka kwenye kitabu cha mungu(BIBLIA)kinachoruhusu matumizi ya pombe huku pombe yake ikiwa pembeni