SABABU YA MWANADAMU KUTENGANA NA MUNGU:

  Maovu ni chanzo kikubwa  kinacho sababisha maombi ya mtu yasijibiwe na hata kutenganisha  kati ya  mwanadamu na Mungu, isaya 59:2 lakini maovu yenu yamewafarakanisha ninyi na Mnungu wenu na Dhambi zenu zimeuficha uso wake Mungu musiuone,
MunguMtakatifu hana ushirika na dhambi. Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi Mwanadamu hujaribu kumfikia Mungu kwa nija nyingi: dini, matendo mema, sala, n.k., lakini hizi zote hazitoshi. Mwanadamu bado ni mwenye dhambi. na wala hakuna Dini yenye uwezo wakumfutia mwanadamu thambi zake mwenye uwezo wakufuta thambi za mwanadamu ni mmoja tu yesu kristo,

YESU KRISTO NI NJIA YA PEKEE YA KUONDOA DHAMBI. Alikufa kwa ajili yetu ili tujue upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yetu. 1 petro 3:18  Yesu akawaambia mimi ndimi  njia na kweli na uzima Mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi yohana 14:6 hakuna mtume wala nabii wa aina yeyote aliyepita hapa Duniani aliyewahi kutamka haya maneno zaidi ya Yesu mwana wa Mungu aliye hai,kwamba yeye ni njia na kweli na uzima

Ni yeye aliyekubali kuutowa uhai wake kwaajili ya ulimwengu na hayupo mwingine  aliyewahi hata kujaribu kufanya hivyo,ila yeye akafa na kisha akashinda mauti  akafufuka baada ya siku tatu  Yesu peke yake  hivyo Mwanadamu peke yake hawezi kushirikiana na Mungu. kwakuwa  mwanadamu alitenda dhambi  Mungu alimtuma Yesu afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na tena awe daraja kati yetu na Mungu ili atulete kwa Mungu.  inawezekana ukahitaji kurudisha mahusiano yako Na Mungu kama kweli umemahanisha unaweza kuisali kama hujamaanisha haikuhusu, endelea kusoma mengine,yatakayokusaidia kukupa wewe muongozo wa kuishi vile Mungu anavyoagiza,

Followers