SIMU YA FAIDA

Neema ya Mungu na iwe pamoja nawe, Na ni Duwa yangu na maombi yangu kwa haya machache yakapate kuwa baraka kwako wewe unayesoma wakati huu, ni Jambo la kusadikika kwa wandugu wengi wamekuwa wakipoteza vipato vyao kwa kujisahau tu, ila ukikumbushwa bila nshaka utafanya vizuri hili linakujia kwa manufaa ya wewe mwenyewe hivyo ni ihari yako kuchukuwa hatuwa au kuacha, Umeona kichwa cha habari kina elezea Simu ya Faida ni kweli simu ni chombo kizuri sana japo kizuri pia kinaweza kuwa na kasoro kikitumika kinyume cha matumizi,

Sehemu hii isikushangaze sana kwaajili ya kuelezea habari za simu kama ukizibiti hapa kipato chako kinaweza kuongezeka wafanya Biashara wa mitandao ya simu wanajitahidi sana kuboresha wasasiliano kwakupunguza bei ili kuhakikisha kila mtu amemiliki simu na ametumia sasa kutumia simu siyo vibaya wala huwezi kumpangia mtu atumie vipi pesa zake ila si kila anayefanya jambo anafanya kwauwelewa mkubwa kama wako ndio maana tunachukuwa fursa hii kusaidiana kwa hao wa chache wanaovujisha pesa zao bila matarajio yao,


ninaamini umewahi kuona au kusikia mtu anapigiwa simu au kupiga simu anaanza kuongea karibia mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari anatumia simu tu kuongea na yanasikika anayoongea si biashara useme ametumia pesa kuingiza pesa bali ametowa pesa bila faida na hajutii kupoteza hizo hela, tena anashabikia kwa ushaba kabisa labda kama ni kwenye basi hamuwezi tena kuongea wengine ni yeye tu na maneno yake ya ushamba ila wapo wengine akipokea simu au kupiga simu mara 3 tu ameshatengeneza pesa kama milioni mia nne hivi na bado ametulia sasa wewe unabiga simu ambazo haziingizi hata mia

Sasa kwa mtu wa Mungu jitahidi simu ya itengeneze hela siyo simu ya kuulizia matatizo tu na Harusi piga simu wamekuwekea kiasigani cha pesa bank au wametuma mzigo wa beigani, usione watu wamenyamaza wapinga miruzi peke yao tayari kimeshaeleweka sasa na wewe unaiga si kila kitu ni chakuiga utaumia unamkuta mtu anaangaika na simu masaa mawili anatafuta mtu wakumpigia kisa ana shilingi elfu mbili salio, siku ukiwa huna salio unazima simu au unaanza kuwasumbuwa watu kwa kuwabeep ili wakupigie ukiwa unadaiwa simu haipatikani unawasha kwa machale, ukifikia hivyo yamesha kushinda unaweza ukawahiwa na mgambo siku moja kwa hiyo tabia yako,

Mungu ametupatia akili kila mmoja ajisimamie mwenyewe lazima utumie akili, wengi wanao lalamika sasa hivi kuwa maisha ni mabaya waliyaharibu awali na siyo hivi karibuni hivyo si rahisi kutambuwa kuwa unatengeneza kilio cha baadaye kwa hayo unayoyafanya,badala ya kicheko cha abaadaye,

Lazima mwanadamu aishi kwa utaratibu jifunze hata kwa kuona kwa wengine kilicho watokea, hata kama ni mtu anakuja kukutembelea aje kwako  kwa jambo maalumu  siyo kiholela tu, wenzetu waliwahi kulitambuwa hili ndiyo maana walifanikiwa mapema na haraka, mtu akija kwako mkishamaliza lililomleta mwambie arudi kufanya shuguli zake kwa bidii ni bora akuone katili utakuwa umemsaidia kuliko kumwendekeza ukamsababishia matatizo mbeleni wakati haijulikani kama utakuwepo au hautakuwepo

Lazima tuishi kwa kuukombowa wakati wewe ukizembea zembea kitakacho kuchangamsha ni uzee ambao utakuvamia kama mwifi uzee nao una kuja kwa kasi kubwa mno,wewe usijione kama bado ni kijana ukitaka kufahamu ulipo fikia watafute wale uliosoma nao shule ya msingi ukiwaangalia utajuwa kuwa umeshazeeka,usitake kukamatika waliokamatika walikuwa kama wewe,

Una heri wewe umepata hata wakukumbusha amka sasa jitahidi wewe uwe wa tofauti ili uwe wa tofauti ni lazima ufanye jambo la tofauti na wengine ili upate matokeo tofauti ila ukifanya jambo linalo fanana na wengine usitegemee matokeo tofauti na wengine,

Hata biashara za watu wengi zinaharibika kwa kutotumia maarifa wengine wanafukuzwa kazi kwa kutotumia maarifa wewe unajijuwa ni mfanya biashara ila majibu yako kwa wateja si mazuri kabisa pia unafunguwa  biashara umechelewa unategeme nini usitafute kisingizio lolote katika maisha yako chunguza kabla huja laumu,

Followers