SOMO: NGUVU YA NDOTO
Na Nabii Samson Mboya
is not enough to have visions and dreams while you live as you dreaming
Utangulizi:
Habakuki 2:2-3; Bwana akanijibu, akasema, Iandike Ndoto hii ukaifanye iwe wazi Sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.
Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.
NINI MAANA YNDOTO ~ ni mfuatano/mtiririko wa picha, mawazo, na mihemko ya hisia ambazo kikawaida hutokea katika ufahamu pindi mtu anapokuwa amelala.
Na mara nyingi ukubwa wa ndoto huanzia sekunde hadi dakika 20-30 kwa ndoto; na ni mara chache sana mtu kuota Zaidi ya muda huo japo wapo wengine wanaoota ndefu Zaidi
AINA ZA NDOTO
 
1.      NDOTO ZITOKAZO KWA MUNGU.Kama nilivosema hapo awali Mungu pia hutumia njia ya ndoto kuwasiliana nasi pindi tunapokua tumelala (Ayubu 33:14-16, Yoel 2:28) Hizi ndoto za aina hii mara nyingi huleta msisimko ndani ya roho na nafsi pia kuashiria jambo jema au baya na mara nyingi ni ndoto zinazokua na mapambano Zaidi kwani shetani hutaka sana kukusahaulisha kile ambacho Bwana alikuotesha.
 Ayubu 33:14-15 14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;
 Mungu ndiye chanzo cha Ndoto ila si kila ndoto inatoka kwake,
Yoel 2:28 28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
 Usichanganyikiwe hapa Mungu ndiye chanzo cha ndoto zote tunazoota lakini sio ndoto zote hutoka kwake.
NDOTO ZITOKAZO KWA SHETANI.Zipo ndoto zitokazo kwa shetani adui wa nafsi zetu ambazo mara zote huwa na mifadhaisho na kuogofya sana na mara nyingi ndoto hizi hazisahauliki kwa sababu shetani huhitaji sana kuharibu hatima yako ndio maana ni vigumu sana kusahau.(1 Samweli 28)
JINSI GANI UTAWEZA KUTUNZA NA KULINDA NDOTO ZAKO
 1.      JIFUNZE KUOMBA ~Jenga mazingira ya kuomba mara kwa mara pindi unapoota ndoto ya aina yeyote iwe imetoka kwa Bwana au kwa shetani huna budi kuziombea maana zote huwa haziji bure.Na pia ni muhimu kabla ya kulala uombe ili Mungu akuwezeshe kujua maana ya tafsiri juu ya kile ulichokiota;ili kisipotee bure
 
2.    MSIKILIZE MUNGU~Chukua muda wako wa kutosha na wa utulivu kwa ajili ya kumsikiliza Mungu juu ya kile ulichokiota na pindi unapohisi Amani moyoni mwako ni njia mojawapo ya Mungu kuridhia kile ulichokiona.Ndoto inayokupa Amani na kukupa utulivu inakupa ujue kabisa ndoto iyo imetoka kwake;maana kumbuka ni Mungu mwenyewe ndiye anaweza kutupa Amani juu ya yale tunayoyaota.(Mathayo 2)
 
 
3.    JIFUNZE KUANDIKA NDOTO ZAKO~Kama nilivotangulia kusema jenga mazingira ya kulala na daftari ili uweze kuandika kile unachokiota hii itakusaidia kuweza kukumbuka yale uliyoyaota na kuyapa muda ili yawe Dhahiri baadaye
 
4.    TAFUTA USHAURI TOKA KWA MUNGU~Watu wengi pindi waotapo ndoto huanza kuhangaika kwenda kwa watu mbalimbali ili kupata tafsiri (Mwanzo 41) Jambo ambalo sio zuri kwa Bwana maana ndoto husiana na hatima binafsi ya mtu wala sio kwa wengine penda kumuomba Mungu ili aweze kukupa tafsiri juu ya kile ulichoota.Pia Mungu huweza kukuongoza pia kwa mtumishi wake kwa ajili ya kukupa tafsiri jua inategemea sana kwa Amani utakayoiskia pale unapopewa tafsiri.
AINA ZA NDOTO
1.      NDOTO ZITOKAZO KWA MUNGU.Kama nilivosema hapo awali Mungu pia hutumia njia ya ndoto kuwasiliana nasi pindi tunapokua tumelala (Ayubu 33:14-16, Yoel 2:28) Hizi ndoto za aina hii mara nyingi huleta msisimko ndani ya roho na nafsi pia kuashiria jambo jema au baya na mara nyingi ni ndoto zinazokua na mapambano Zaidi kwani shetani hutaka sana kukusahaulisha kile ambacho Bwana alikuotesha.
5.     SUBIRI NA ACHA ITOKEE~Baada ya kufanya mambo hayo hapo juu unapaswa kusubiri mapenzi ya Mungu yatokee kwa yale uliyoyaota.Kumbuka ndoto nyingi huwa wazi na kweli ila kuwa mwangalifu Zaidi katika ndoto zile ambazo zinakaa Zaidi kwenye ufahamu wako na haziondoki kwa haraka.
ALAMA CHACHE UNAZOWEZA KUZIONA KATIKA NDOTO  FARASI~Anaashiria mtu; hali ya maisha yake na roho yake pia (Mathayo 7:24-27, 2Timotheo 2:20-21)
        Samaki~Watu
        Majani makavu~Kuchakaa na kuwa ukiwa
        Majani mabichi~Neema na ustawi
        Ngazi~Kuongezeka, kukua mafanikio
        Mbuzi~Ulafi
        Mbwa~uzinzi
        Kondoo~Unyenyekevu, upole
        Mkono~Bwana atatenda makuu kwa mkono wake
        Maji~neema, kurudhika na kuendelea
        Daftari na kalamu~Elimu na mafunzo mbele yako
        Kuku~papara na kuhangaikia mambo yasiyokuhusu
        Mwewe mweusi~Mkuu wa anga wa eneo
        Paka~uchawi wa eneo
        Nyoka~Njama, shetani, Ibilisi, Njama
        Kipara~werevu, uzamani, wingi wa maarifa
        Nzige~uharibifu, hasa wa kipawa au huduma
        Asali~uponyaji,ulinzi na uzuri
        Unapoona ulimi upo nje ya kinywa~roho ya usengenyaji, umbea, kugombanisha
        Unapoota unaumwa na kichwa~wachawi na wanga wamekushambulia
        Unapoota unatembea lakini hufiki~Jambo unalolofanya sasa linakupotezea muda fanya jambo jingine achana na hilo.
        Unapoota umezaliwa tena~Bwana anakufanya upya hasa katika matendo yako(kubadilishwa)
        Unapoota unaitwa na mtu usiyemjua~Roho ya mauti
        Unapoota watu waliokufa wanakuita~Maagano, mauti
        Unapoota unafanya mapenzi na ndugu yako wa kuzaliwa~Uhusiano wako na ndugu yako utaharibika muda sio mrefu,pia utapata aibu
        Unapoota unalia na hakuna anayekufariji~Huna uhusiano mzuri na watu
        Unapoota ndugu wako wa karibu amekuja kukutembelea na kukuaga~Roho ya mauti ipo juu yake
        Unapoota upo mbele za watu wengi wanakusikiliza~Bwana atakutukuza na kukujulisha mbele za wengi
        Ukiona nyumba/chumba kipya~ Huashiria mawazo chanya; huduma na maisha mapya katika eneo jingine jipya
        Unapoota upo uchi~Aibu; mambo yako yatakuwa hadharani na kuonekana, kuwa mwangalifu katika siri zako kwa watu
        Unapoota unaoa au kuolewa~Bwana ameona upweke na ukiwa wako atakupatia mtu wa kuwa na wewe maishani
        Unapoota unavuka mto lakini umelowana ~Jaribu unalopitia utalishinda ila kwa taabu nyingi, Lakini utavuka
        Unapoota umelala na mtu wa jinsia ambayo sio yako~Kuwa mwangalifu na aina ya mahusiano uliyonaoyo yatapelekea kumkosea Mungu
        Unapoota mti mkubwa uliostawi sana~Mungu atakuinua na kukufanya mkuu
        Unapoota upo ziwani unavua samaki~Mungu atakufanya kuwa mvuvi wa watu; atakutumia kuwaleta watu kwake
        Unapoota umeumwa na nyoka~Kuwa mwangalifu sana kwani adui atakushambulia
        Unapoota unakimbizwa na watu usiowajua kwa nia ya kukudhuru na ukawazidi mbio~Uwe mwangalifu kwani shetani atatumia mapepo yake na wachawi kukushambulia lakini hawatakushinda.
        Unapoota unakula lakini hushibi~Roho ya kutotosheka na kutapanya mali
        Unapoota umekatwa kichwa~Mamlaka yako yamehamishwa na kwenda kwa mtu mwingine.
        Unapoota unavalishwa joho~Bwana atakufanya kuwa mpatanishi kwa wengine.
        Unapoota shamba zuri limejaa mazao~Ni kipindi ambacho Mungu atakurejeshea kwa wingi mafanikio yako
        Unapoota matunda yaliyoiva~Ni wakati wa mafanikio yako tayari
        Unapoota mto mkubwa uliojaa mamba~Vikwazo na balaa vimewekwa mbele
        Unapoota mlima mkubwa mbele yako~Jaribu mbele yako
        Unapoota umekufa~Ni taarifa kwako kwa mambo uliyonayo yamekwisha.
 
Neno la Mungu linasema nini juu ya ndoto
Biblia imetaja sana kwa habari ya ndoto, ukisoma katika kitabu cha Mwanzo pekee, neno “ndoto” limeandikwa zaidi ya mara 36. Pia, katika kitabu cha Daniel neno ndoto limeandikwa zaidi ya mara 29. Na ndio maana Mungu alipotaka watu wake wajenge ama madhabahu au hekelu aliwaonyesha kwanza katika ndoto; kumbe ujenzi wowote huanzia katika kuona. Vivyo hivyo hata watu wanaomtegemea shetani huingia ulimwengu wa roho na kujenga kile walichokiona kutoka kwa shetani.
TABIA YA MUNGU KATIKA NDOTO:
Kutoka 25:8-9; Mungu akitaka ujenge anaanza kukuonyesha; ndio maana alimwonyesha pia na Musa na kumtaka ajenge sawa sawa na alichomwonyesha “exactly like the pattern I will show you” Kutoka 25:37-40; Hii ni tabia ya Mungu kuwaonyesha watu kupitia ndoto na watu wengi pasipo kujua wamejikuta wakidharau ndoto.
 
Ukisoma katika kitabu cha Habakuki 2:2-3; Mungu alimwamuru Habakuki aiandike ile ndoto; kwasababu asingeweza kufanya kuona kwanza katika ulimwengu wa roho. Na ndio maana neno ndoto limeandikwa mara nyingi katika kitabu cha Mwanzo kwasababu hicho ndicho kitabu cha asili (origin). Hiyo inatufundisha kuwa mwanzo wa vitu huanzia katika ndoto.
Mambo ambayo Mungu anaweza kuyafanya kupitia ndoto:
i)                    Mungu anaweza kufumbua mafumbo kupitia ndoto:-
Mwanzo 40: 2-19; Hapa tunaona kwa habari ya mwokaji na mwoshaji wa Farao ambao walipata kujua hatari iliyokuwa imejificha kwa njia ya ndoto. Kwa njia hiyo wote wawili wakajua maisha yao siku tatu mbele. Kumbe ndoto yaweza kukufunulia mitego au hatari iliyojificha au kupangwa na watu wabaya.
 
Farao alikwisha kupanga kuwa siku ya tatu itakuwa hukumu yao lakini bila kuwambia; lakini waliweza kufunuliwa katika ndoto. Ni maombi yangu kuwa Mungu na akuonyeshe hatari zote ulizopangiwa sirini.
 Katika kitabu cha Danieli pekee, neno “ndoto” limeandikwa zaidi ya mara 29; Danieli alikuwa uhamishoni Babeli; akiwa huko Mungu akamwonyesha kwa habari ya kumrudisha mahali pake. Vivyo hivyo katika maisha yako inawezekana ulikuwa na mafanikio lakini sasa hayapo; au ulikuwa na afya nzuri lakini sasa haipo; katika ndoto Mungu aweza kukurudisha sehemu unayotakiwa kuwapo.
 
Na ndio maana kila siku huwa nasema Tanzania mpya niliyoiona katika ndoto inakuja; Tanzania yenye maendeleo; yenye hospitali nzuri, yenye gesi, Tanzania yenye madini inakuja na sifi leo ama kesho mpaka ndoto itimie.
 
Ni maombi yangu Mungu akurudishie ile hatma njema ya maisha yako ambayo shetani aliichukua katika maisha yako.
 
iii)               Faida mbali mbali za ndoto
Ndoto zaweza kukuonya usichukue maamuzi ambayo sio sahihi, uache tabia mbaya ambayo ina mwisho mbaya. Mathayo  2: 13-16; Baada ya Herode kugundua kuwa amedhihakiwa na mamajusi akaamua kuua watoto ili amwangamize Yesu; lakini Yusufu akapewa onyo na Mungu kuwa ampeleke mtoto Misri. Ni kweli Herode aliangamiza lakini walioangamizwa ni wale ambao baba na mama zao hawakuota ndoto.
 
Hapa tunaona athari moja ya kutoota ndoto, maana madhara yake yaliwahi kugharimu maisha ya watoto wao. Kupitia ndoto Yesu aliokolewa, Mungu huongea pia kupitia ndoto. Ndio maana ni muhimu kumwomba Mungu akupe ndoto ya kuokoa familia au ukoo wako.
iv)   Mungu anaweza kutufariji katika ndoto:-
Katika maisha unaweza kupitia wakati mgumu, umezungukwa na madeni au kukata tamaa lakini Kupitia ndoto Mungu aweza kukuonyesha utakuwa nani baadaye. Kwa njia hii Yusufu alifarijiwa kupitia ndoto; kwa njia hiyo Yusufu alipokea faraja na kuhakikishiwa ushindi.
 
Yusufu alipoota ndoto zilisababisha achukiwe na ndugu zake, na wakamtupa shimoni na baadaye kumuuza Misri lakini ndoto yake ilibaki palepale. Haikutosha hapo, bali alisingiziwa ametaka kumbaka mke wa waziri mkuu wa Misri na akaja kufungwa. Lakini katika mateso yake Mungu alikuja kumfariji kupitia ndoto na kumrudisha katika nafasi yake.
Vivyo hivyo katika maisha yako inawezekana ulisingiziwa na kupoteza nafasi ambayo Mungu alikupa; leo kila aliyekunyang’anya nafasi naamuru uchukue nafasi yake; nafasi ya ndoa, nafasi ya umeneja, nafasi ya uongozi ninaiamuru irudi kwako katika jina la Yesu Kristo.  Yule Yule aliyekupiga vita mwaka jana mwaka huu utachukua nafasi yake katika jina la Yesu.
Kutoka katika ufungwa gerezeni hadi kuwa mkuu katika nchi ya Misri, yote hii ilianza katika ndoto. Kumbuka ndoto za Yusufu zilianza alipokuwa na miaka 16 lakini alikuja kuimiliki akiwa na miaka 40. Tatizo la watu wengi wanakata tamaa mapema; hutakiwi kufa moyo, hapo katikati wakati unaisubiria ndoto unaweza ukapitia mateso na mabonde lakini ndoto itakuja na itatimia usipozimia moyo.
v)   Mungu aweza kukuonyesha utakuwa nani baadaye katika ndoto:-
Mungu hutenda kazi tofauti na sisi tunavyowaza; Yule mtu unayemuona mdhaifu ndiye ambaye Mungu anamuona shujaa; vivyo hivyo kwa habari ya Yesu, yeye alizaliwa katika hema ya ng’ombe; Samweli alizaliwa na Hana ambaye alikuwa hazai hapo mwanzo; Musa naye alitupwa kwenye mto akakulia kwa baba wa kambo; Samson alizaliwa na mama ambaye alikuwa tasa hapo mwanzo; na ndio maana hata siku moja usidharau mambo madogo kwasababu ndiyo ambayo Mungu huyatumia.
vi)   Mungu anaweza kutuonyesha ushindi juu ya adui zetu katika ndoto:-
Kila mtu ana adui wa maisha wake; awe rais, waziri, mchungaji, au askofu lazima utakuwa na adui wa maisha yako. Yaani kwa kila hatua unayopiga unatengeneza marafiki na adui wengi kwasababu hiyo kila mtu ana adui zake. Lakini Mungu anaweza kukuonyesha ushindi wako katika ndoto. Ukisoma katika kitabu cha Waamuzi utaona kwa habari za Gideoni ambaye alitakiwa kupigana na Wamidiani; lakini kabla ya kwenda vitani Mungu akatumia ndoto kumwonyesha ushindi unaokuja mbele.
Ni maombi yangu Mungu akuonyeshe ushindi juu ya adui zako katika jina la Yesu Kristo. Kumbe kupitia ndoto unaweza kuonyeshwa adui ambaye hapendi mafanikio yako yaani Mungu akupe ushindi dhidi ya hila zake mbaya katika Jina la Yesu.
Shuhuda wa ndoto:
Siku moja nikiwa nimelala katika usingizi mzito nikaota mke wangu anafagia mayai mengi ya nyoka chumbani kwetu nikashtuka nikaanza kuomba nilipo washa taa sikuamini na macho yangu gafla jeshi kubwa la siafu lilianza kuingia ndani ya chumba chakulala nilimwamusha mwenzangu tukashirikiana kufanya maombi, pia tukatumi sumu ya sprei baadaye waliondoka zao, hawakumdhuru mtu,
vii) Mungu anaweza kukuonyesha jinsi ya kumtendea mtu katika ndoto:-
Kupitia ndoto Mungu anaweza kukuonya juu ya uamuzi mbaya unaotaka kuuchukua juu ya mtu Fulani katika ndoto; hii tunaiona kwa habari ya Yesu ambapo mkewe pilato alionywa katika ndoto juu ya hatua alizotaka kuchukua Pilato juu ya hukumu ya Yesu. Kumbe Mungu aweza kumuonya mtu juu ya uamuzi mbaya ambao waweza kumgharimu mtu huyo kupitia ndoto.
Mungu anaweza kukuonya juu ya uamuzi unaotaka kuchukua juu ya mtu wakati wa hasira, wakati wa uoga au wakati mgumu. Mungu huonya kupitia ndoto na ndio maana ni muhimu kutokufanya maamuzi yoyote wakati wa hasira; hofu; wakati mgumu kwasababu unaweza kujikuta unafanya maamuzi ambayo sio sahihi. Watu wengi wamevunja mahusiano mazuri na watu kwasababu ya maamuzi mabaya lakini kupitia ndoto Mungu aweza kukuonya na kukuonyesha njia ya kufanya.
NINI CHA KUFANYA UNAPOOTA NDOTO:
      Baada ya kuota ndoto ambayo si nzuri unatakiwa usimame kinyume katika maombi. Sambaratisha ndoto zote na wasimamizi wake wote katika ulimwengu wa roho.
   Na ikitokea umeota ndoto nzuri unatakiwa uiteke na kuimiliki ndoto hiyo; kushindwa kuchukua hatua kutakufanya usiimiliki hiyo ndoto. Ukiota umefanikiwa katika biashara Fulani, unatakiwa uanze kwa kuomba halafu chukua hatua ya kuimiliki ndoto hiyo.
  Ukiota ndoto halafu huilewi ni nzuri au mbaya unatakiwa uamuru katika maombi kuwa kama ndoto hii ni mbaya ninaisambaratisha katika jina la Yesu na kama ndoto hii ni nzuri imiliki katika jina la Yesu. 
 

Followers