Msaada wa Maombi ya ulinzi,


MAUTI YA ULIMI

Mithali 18:21

Utangulizi:

Kuna watu wengi sana wamepata Madhara makubwa sana wingine wameangamia, kwakujuwa au kwakutojuwa sababu ya ulimi, biashara zilishafilisika sasa wamebakiza madeni, wengine, uchumba zilisha vunjika kwasababu ya ulimi,wengine ndoa zilisha farakana,wengine wako magerezani wamefungwa maisha yao yoye,wengine wapo katika majuto kwasababu ya ulimi,

Imaeandikwa Hosea 4:6Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.

Kukataliwa ni kutohusishwa,au kutohitajika mahali flani ulipaswa kuwa,

MADHARA YA ULIMI

  • Kukataliwa na Mungu
  • Ulimi unaweza kukutenga na jamii daima
  • Ulimi unaweza kukusababishia laana mbaya sana imeandikwa MWANZO 4:8-12 ) kaini na Abeli,
  • Ulimi unaweza kukuhamisha mahali pako na kukupeleka kusiko julikana
  • Kukosa mema uliyoandaliwa na Mungu haswa ya baadaye,
  • Ulimi unasababisa mauti ya kimwili au kiroho 
  • Ulimi unaweza kukusababishia  ukoma imeandikwa ( HESABU 12:1-2 , 9-10 Mariamu na Haruni
  • Ulimi unaweza kukukunyima mafanikio uliytakiwa kuwa nayo
  • Ulimi unaweza kuzuwia hatima ya maisha yako
  • Ulimi unaweza  kumkasirisha Mungu ( HESABU 11:1 ).Manung’uniko
  • Ulimi unaweza kuharibu hatima ya maisha yako
  • Ulimi unaweza kuyaangamiza maisha yako,
  • Ulimi unaweza kukupotezea kukupotezea mafanikio
  • Ulimi unaweza kukufanya msaliti … (MATHAYO 26:69-75 ).Petro kusaliti,Yuda jehanamu kisa ulimi
  • Ulimi unaweza kukucheleweshea au kukuwahishia mafaniko
  • Ulimi unaweza kukutesa au kukupatia aibu ambayo hukutarajia
  • Ulimi unaweza kukuzuwia katika maisha usifanikiwe kabisa,
  • Ulimi unaweza kusababisha matatizo kwa wengine,
  • Ulimi unaweza kukuharibia huduma,kipaji,nyota
  • Ulimi unaweza kusababisha ukapoteza nguvu za Mungu
  • Samson alitoa siri kwa ulimi akajiumiza yeye mwenyewe,,

Tayari hata hivi tunavyojifunza ujumbe huu ulimi umesha waumiza wengi, Sana waliyotutangulia na wajao kama hawatapata neema ya kujifunza kuulinda ulimi wao,

 

 UFANYE NINI KUWA SALAMA NA ULIMI,

  • Kwa kumkiri Yesu kwa ndimi zetu kuwa ni Bwana au Mtawala wa maisha yetu na kuokolewa WAFILIPI 2:11; WARUMI 10:8-10 ). Kufanya toba ya kweli
  • Kuruhusu hofu ya Mungu katika maisha yako kwa kukubali neno likaye
    Ndani yenu, imeandikwa zaburi 119:11 moyoni nimeliweka neno lake nisitende dhambi,
  • Kuwa mtendaji wa neno kwa kuliishi, yaani kwa kuliamini,
  • Kunyeyekea chini ya Mkono wa Mungu,
  • Kudumu  hemani pa bwana katika mafundisho yaani maarifa,

Imeandikwa (ZABURI 15:1-4 ; ZABURI 101:6-7; macho ya Mungu yatakutazama ikiwa utakaa hemani wakati wote,

  • Ili kuuchunga ulimi  unatakiwa kuuchukia ubaya kabisa,
  • Ili kuuchunga ulimi angalia mazingira na marafiki unaokaa nao imeandikwa zaburi 1;1  MITHALI 19;29; ZABURI 1;1 ) 
  • Epuka roho ya kiburi kabisa ukaidi dharau, Amdharauye mwenzake -(HESABU 16:12 )afanya dhambi (MITHALI 14:21).”Wengine Wakiomba pepo hawawezi kutoka, mpaka nije Mimi”. “Bila mimi hakuna
  • Jitahidi  acha masihara ,utani wa desturi au wa mazowea,
  • Acha mabishano au mashindano ya kuongea au Kuasi kauli za Mtumishi

Punguza maneno mengi, imeandikwa (YAKOBO 1:19). uovu (MITHALI 10:19). (MATHAYO 27:11-14 ).

  •  Mtu mwenye maneno mengi wakati wote, yanaweza leta mauti……………
  • Epuka kukasirika ovyo ulimi unaweza kukusababishia mauti, MHUBIRI 7:9;
  • Pima maneno unayotaka kuongea na mwenzako kabla hujaongea (ZABURI 39:1, 9 ).
  • Dumu ndani ya Neno la Mungu kwakuliishi maisha yako yote, YOHANA 15:3; (ZABURI 119:11)………..
  •  Dumu katika maombi maisha yote ( MATHAYO 26:41

HITIMISHO:

 Omba toba ya kweli anza upya maisha yako,

(WAEFESO 2:8-10; MITHALI 28:13).  Tukifanya hivi, kwa ghafla tunakuwa viumbe vipya na ndani mwetu kunakuwa na asili mpya inayotuwezesha kushinda dhambi bila jitihada zozote!  Kuokoka ni muujiza wa ajabu.

 (ZABURI 119:11).  MUNGU AKUBARIKI!!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

 

 

MBINU ZA KUMSHINDA ADUI YAKO

1 Samuel 17: 40, Mhubiri 7:8

Utangulizi

Adui anapopambana na mtu huwa anapambana naye leo kwa lengo la kuzuwia kesho mwisho wako mafanikio yako ni mwisho wa lileulilolianzisha linapofika mwisho uzuri wa jambo ni mwisho hivyo usitishwe na mapigo uliyorushiwa na adui ushindi ni mwisho  Herimwisho kuliko mwanzo


1 Samuel 17: 40 Akaichukua fimbo yake mkononi, akajichagulia mawe laini matano katika kijito cha maji, akayatia katika mfuko wa kichungaji aliokuwa nao, maana ni mkoba wake, na kombeo lake alikuwa nalo mkononi mwake, akamkaribia yule Mfilisti.
 

Huyo Mfilisti naye akamsogelea Daudi na kumkaribia; na mtu yule aliyemchukulia ngao yake akamtangulia.
Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuriAnd

 

1 Samuel 17:26. Daudi akaongea na watu waliosimama karibu, akisema, Je! Atafanyiwaje yeye atakayemwua Mfilisti huyo, na kuwaondolea Israeli aibu hii? Maana Mfilisti huyu asiyetahiriwa ni nani hata awatukane majeshi ya Mungu aliye hai?
 Nao watu wakamjibu vivyo hivyo, wakisema, Ndivyo atakavyofanyiwa mtu yule atakayemwua.
 Naye Eliabu, mkubwa wake, alisikia hapo alipoongea na watu; na hasira yake Eliabu ikawaka juu ya Daudi, akasema, Mbona wewe umeshuka hapa? Na kondoo wale wachache umemwachia nani kule nyikani? Mimi nakujua kiburi chako, na ubaya wa moyo wako; maana umeshuka ili upate kuvitazama vita.


 Naye Daudi akamjibu, Je! Mimi nimekosa nini sasa? Je! Si neno kubwa hilo?
Naye akamgeukia ili kumwelekea mtu mwingine, akasema naye jinsi ile ile; na watu wakamjibu tena jinsi ile ile kama ya kwanza.




Imeandikwa Matendo :2826 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;  ili wamtafute Mungu,

ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.


1 Samuel 18:6-7
Siku utapotamka Neno la ushindi  ndiyoutakuwa umeleta ukombozi na sherehe kwa familia yako na kizazi, Daud alipolitoa jiwe ndani ya mfuko,mkoba,bag lake furaha ilitawala,tunakungoja utoe jiwe lako mfukoni tuanze kushangilia jiwe lako linaweza kuwa tamko lako la kumpa yesu maisha,

.

Kama roho mtakatifu aliyondani yako unamwamini ukitamka hutokuwa na hofu hatakama likichelewa utalisubiri wakati wake, maana litatimia tu

Imeandikwa Yeremia 1:12 Mungu aliliangalia neno la Daudi,imeandikwa  Mithali 23:7 aonavyo mtu nafsini ndivyo alivyo  Daudi alimwamini Mungu akaamua kumtegemea kwa moyo wake wote  imeandikwa  Hesabu 13:30

 

Siku ya kutoa jiwe ndani ya mfuko wako ndiyo siku utawaletea ndugu na jamaa kicheko na furaha itatawala, usiogope kila tatizo linajiwe lake toa kwa mfuko piga uchukuwe ushindi,

 

Imeandikwa Mhubiri 7:8 Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake, Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi.  Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.
Usiseme, Kwani siku za kale kupita siku hizi? Maana si kwa hekima uulizavyo neno hilo.

 

 Hekima ni njema, mfano wa urithi; Naam, nayo ni bora kwao walionao jua.  Kwa maana hekima ni ulinzi, kama vile fedha ilivyo ulinzi; na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo. Tafakari vema kazi yake Mungu; kwa sababu ni nani awezaye kukinyosha kitu kile alichokipotosha yeye?

 

Idadi ya waliookoka ni mwisho siyo mwanzo

,hata safari,uchumba,biashara,mafundisho,elimu kulima matazamio ni mwisho,

Mungu anataka kuona kila unaloanza unalimalizia je, biashara mahesabu ni mwisho wa mauzo,

Imeandikwa Mathayo 10:22 '' Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.''

 

 

 

Warumi 8:35-39 31 Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
 Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?
33 Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.


 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.


 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa Kama kondoo wa kuchinjwa.


Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,
wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.

 

 Haggai 1:2-30 Kama hatutamteemea Mungu

Followers