NENO LA MUNGU LINA NENA NINI JUU YA USHOGA?

Je, Neno la Mungu lina nena  nini juu ya ushoga? Je, ni( dhambi?)

 
Biblia inasisitiza kila mara kwamba ushoga ni dhambi (mwanzo 19:1-13; mambo ya walawi 18: 22; warumi 1:26-27; wakorintho wa kwanza 6:9). Warumi 1:26-27 inatufundisha ya kwamba ushoga ni njia mojawapo ya kumkana na kutomtii Mungu. Mtu anapodumu katika dhambi na kutokuamini biblia inatuambia ya kwamba “Mungu huwaachilia” kutenda maovu zaidi ili wapate kujua ubatili wa maisha bila Uwepo wa Mungu. Wakorintho wa kwanza 6:9 inasema kuwa mashoga hawataurithi ufalme wa Mungu.

Mungu haumbi mwanadamu mwenye tamaa ya ushoga. Biblia inatuambia mtu huwa shoga kwa sababu ya dhambi. (warumi 1:24-27), na pia kwa sababu ya uamuzi wake mwenyewe. Mtu anaweza kuzaliwa na msukumo juu ya ushoga

kama vile watu pia huzaliwa na msukumo juu ya fujo na dhambi nyinginezo. Hili halihalalishi dhambi yoyote inayofanywa na wanadamu. Je, mtu akizaliwa na msukumo wa hasira mbaya, ni halali aendeleze hasira zake mbaya? La, hasha. Hata kwa ushoga pia si halali.

Hata hivyo Biblia haiitaji dhambi ya ushoga kuwa ndiyo kubwa zaidi. Kila dhambi ni chukizo kwa Mungu. Ushoga ni mojawapo ya mambo yaliyoorodheshwa katika wakorintho wa kwanza 6:9-10 yatakayozuia mtu asiingie katika ufalme wa Mungu. Kulingana na Biblia msamaha wa Mungu juu ya shoga upo sawa na wa mzinzi, muabudu sanamu, muuaji, mwizi na kadhalika. Mungu tena aahidi uwezo juu ya kushinda dhambi, pamoja na ushoga, kwa wale wote watakao mwaminiYesu kristo kwa wokovu wao (wakorintho wa kwanza 6:11; wakorintho wa pili 5:17).

Sina maana ya kufuatilia maisha ya mtu lah! Bali ni mimi ninatumika tu kufikisha ujumbe kwa jamii yetu na nina amini hata mashoga matatembelea hii Safu bila shaka itanamsaidia mwenye tabia hii ya ushoga kuiacha mara moja

,japo wapo wengine ambao sijazungumzia sana  hapa ila watakuwa wameelezewa ukurasa mwingine wale wanao lawiti, watoto,wadogo,wake zao au wake za watu wengine  kwa yeyote anayefanya tendo hili ni vema kama ulikuwa haufahamu  fahamu sasa kuwa unafanya  chukizo mbele ya uso wa Mungu, acha mara moja na utubu kabisa,

Followers