MAHUBIRI YA MAFANIKIO BILA TOBA YANACHOCHEA TAMAA MBAYA,

. Wachungaji wana njaa ya kujifunza jinsi ya kuongeza wahudhuriaji katika makanisa yao na Si kuwafundisha watu jinsi ya kuishi Maisha matakatifu, na mara nyingi ni wepesi kupokea ushauri wa wachungaji wa kigeni kutoka inchi kama marekani Kimarekani naijeria na ninginezo nyingi, wenye makanisa makubwa, wanaodhaniwa kuwa wamefanikiwa kwa sababu ya ukubwa wa majengo yao na wingi wa watu wanaoabudu kwenye ibada zao siku za Jumapili.


Ila, wale wenye utambuzi kidogo hutambua kwamba ukubwa wa wahudhuriaji na jengo si alama ya ubora wa huduma ya kufanya watu kuwa wanafunzi. Makanisa mengine ya Marekani yamekua kwa sababu ya mafundisho yenye kuvutia, ambayo ni upotoshaji wa kweli za KiBiblia.

 Kinacho sikika kila siku ni kwamba wachungaji wengi wa Kimarekani wanaamini na kuhubiri kwamba mtu akiisha okoka tu, hawezi kupoteza wokovu wake hata akiamini nini au akiishi vipi hilo ni kukwepa ukweli wa Mungu imeandikwa aliyesimama Aangalie asije akaanguka ukianguka moja kwa moja wewe unakuwa umefarakana na mungu yaani umepoteza ufalme wa Mungu.

Pia, wachungaji wengi wa Kimarekani huhubiri Injili iliyotiwa maji kuhusu neema isiyo na gharama, sihitaji kuwazungu sana iwe kama ninawasema lah! Bali wito wangu kwako msikilize Roho mtakatifu zaidi kuliko Mwanadamu wanakuwa wakiwaongoza watu kudhani kwamba wanaweza kuingia mbinguni pasipo utakatifu.

Kuna wengi pia wanaohubiri Injili ya mafanikio, wakichochea roho ya tamaa katika watu ambao dini ni njia ya kujipatia hazina zaidi za kujiwekea hapa duniani. Hao ni wachungaji ambao mbinu zao za ukuaji wa kanisa hazifai kuigwa.Yapo mazuri na mema mengi kama kusaidia yatima wajane masikini wasiyojiweza na mengineyo siyo yakuwa watamukia kupata vitu ambavyo ujaongozwa na Mungu kuwaambia unaweza kukaharibu kundi la Mungu badala ya kulijenga,

Unapo mtamukia mtu atapata gari leo au wiki hii au mwezi huu au mwaka huu na yeye akapokea na unajuwa hana hata kazi wala kibaruwa wala shamba lakulima,wala hajafuga hata njiwa  mimi kwa nafasi yangu ya ushahuri kama Mungu hajakushuhudia usichochee tamaa kwa watu inawezekana alisha ishinda thambi lakini kwa ushawishi wako wa kuwafundisha wataokota hela na kujenga majumba na kununuwa magari mazuri mazuri ikiwa hata basikile hana inaweza ikasababisha watu wakafanya thambi ya tamaa na hata kujikuta wanaingia katika mashindano wao kwa wao na kufikia katika wizi au kama ni mwanamke anajikuta ameharibu ndoa kwakutaka asiyokuwa na uwezo nayo kisa ameambiwa avae kama wengine au aishi kama wengine watu wafundishwa namna ya kuishi maisha matakatifu

Ili mungu aseme nawao wenyewe kuhusu baraka zao hizo na hata kama zikipitia kwako basi awe na yeye anaziona katika ulimwengu wa ki-Roho siyo mtu bado ni mchanga hajafundishwa kuikana Dunia na maovu yake gafla anakumbana na matangazo ya utajiri utajiri bila Mungu si kitu usalama wa kwaza kwa mwanadamu ni kuishi na Mungu
ukisoma kwa upana sana Baathi ya vitabu juu ya mada ya ukuaji wa kanisa, nami nashindwa kutoa uamuzi juu ya vitabu hivyo kabisa .

Vingi vina mbinu na ushauri ambao kwa kiwango fulani ni wa KiBiblia, na hivyo vinafaa kusomwa. Lakini karibu vyote vina misingi kwenye taratibu za makanisa jengo – taratibu zenye umri wa miaka elfu na mia saba hivi – badala ya utaratibu wa KiBiblia. Basi, lengo lake si kuujenga mwili wa Kristo kwa kuwaongeza wanafunzi na wenye kufanya watu kuwa wanafunzi, bali ni kujenga makanisa jengo ya kipekee, ambayo kila mara yatahitaji majengo makubwa zaidi, watumishi wenye taaluma za hali ya juu pamoja na mipango aina hiyo, na mtiririko wa uongozi kama wa shirika au kampuni, badala ya familia ya wana wa Mungu.


Kuna mbinu za kisasa za ukuaji wa kanisa ambazo zinatosha ushauri kwamba, kwa ajili tu ya kupata washirika wengi, ibada ziwe za kuvutia kwa ajili ya watu wasiotaka kumfuata Yesu. Zinashauri kwamba kuwe na mahubiri mafupi, yasiyokuwa na maneno makali yaani ya kukemea Dhambi ya kuudhi, na ibada tulivu, na mambo mengi ya kijamii, na fedha zisitajwe kwaajili ya matoleo, na kadhalika.

Hii haisababishi kuzaa wanafunzi wanaojikana na kutii amri zote za Kristo. Husababisha watu wanaojiita Wakristo, wasioweza kutofautishwa na wana wa dunia, na ambao wanaelekea jehanamu kupitia barabara ile pana. Hiyo si mbinu ya Mungu ya kuwaleta watu Kwake bali ni ya Shetani ya kuliteka kanisa. Huo si “ukuaji wa kanisa” bali ni “ukuaji wa dunia ya yule muovu nah ii imewaumiza watumishi wengi sana, na wengine kufikia sehemu ya kupoteza uelekeo wa kazi ya Mungu, na Hata jina la Bwana likaazwa kutukanwa ovyo

Hukumu ya namna hii utaibebea wapi ndugu yangu?

Followers