BARAKA ZA KWELI

BARAKA ZA MUNGU KWA MWANADAMU NI ZIPI?


Baraka za kweli ni kule kuishi hapa ulimwenguni ukifurahia aina Zote za mafanikio Mungu aliyokupatia,Na pia kuwa na matumaini ya maisha ya abaadaye kule mbinguni katika maisha ,katika hizo Baraka za kweli,ukiwa unajitahidi kuishi maisha matakatifu ya kumpendeza Mungu,,,

tena ukiwa unatafakari kwamba Je Mungu akikuita hivi sasa ujipime kwamba utakuwa na ujasiri wa kufikiria maisha ya mbinguni?

kwa hayo maisha unayoishi?kuishi maisha yasiyo mpendeza Mungu ni kama Dereva anayeendesha Gari ambayo haijalipiwa Bima,ikitokea uharibiu wa gaghafla inakuwa inamgarimu,na sisi ni hivyo hivyo kuishi maisha yasiyoongozwa na Mungu,ni kama kuishi maisha yasiyo na Bima huna uhakika nayo maana mwanadamu Hapa Duniani anaishi kwa sekunde tu



Kwa uhakika mulize Dakitari huwa mapigo ya moyo ya mwanadamu Huwa anayapima kwa kutumia nini, utamuona anatumia (Saa) utapata uhakika wa haya niliyoyaandika hapa,huna sababu ya kumyanyasa mwanadamu mwezako aliyeumbwa kama wewe,na kupita kama wewe,kisicho pita ni Neno la Mungu tu,maana limeandikwa kabla mababu na mabibi kuzaliwa lakini mpaka leo,bado nijipya na ni muongozo wa vizazi vyote vitakavyo pita katika hii Dunia,haijalishi kwa yule anaye kataa au asiye kataa,



Maana anayeamini na asiyeamini wote hawa watasimama mbele za Mungu kutowa hesabu ya yale waliyoyafanya wakiwa hapa Duniani,na kipimo hakita pendelea,kuwa ulikuwa masikini au ulikuwa Taji,wala ulikuwa msomi au hukusoma,wapo wengine wataukumiwa hata kwa yale waliyoyasikia kutoka kwa watumishi wa Mungu mbaili mbail,hivyo usiichezee nafasi uliyoipata ya kuishi hapa ulimwenguni,ta futa kusudi la wewe kuwepo hapa ulimwenguni ni nini?



ndiyo maana ukimuuliza yeyote anayeishi hapa duniani kuhusu habari ya Dakika tano zijazo hawezi kukujibu,Bali Mungu akipendezwa na mumoja kati yako Basi unaweza ukajulisha kinachoweza kutokea Mbele ya Maisha yako

uhakika wa kwenda kuishi kule tuliko andaliwa Mbinguni.

Followers