MTAWALA MZURI NI WANAMNA GANI?

Kwanza hebu tufahamu  kidogo mtawala ni mtu wa namna gani  kwa tafsiri niliyoiona nyepesi  Mtawala ni mtu  aliyechaguliwa na watu au kundi la watu kwaajili ya kusimamia maamuzi waliyokubaliana kwa pamoja  kwa manufaa yao wotw na haki zao zote zinazostahili kupatikana au kufanyika, na yeyote atakayefanya kinyume maana yake amekiuka utaratibu yaani kwa maana nyingine amewafanyia mwengine jambo la uovu, wasilokubaliana katika makubaliano yao, 

Kwa mfano mtu akikubali kuoa kwa ndowa ya kikristo ya mke mmoja, wakakubaliana hao wawili sasa ikaja siku mmoja wao akafanya kinyume akaoa au kuolewa kwa siri au kwa wazi basi yeye aliyefanyifa tendo hilo la kuachwa bila rithaa anakuwa amefanyiwa uovu usiyokubalika mbele za Mungu na mbele za wanadamu pia,  tuangalie Maandiko matakatifu yanaelezea nini kuhusu mtawala, 

 wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi: Bali muovu atawalapo watu huuguwa, Mithali 29:2 ukiendelea mbele kidogo inasema Mwenye haki huyaangalia madai ya masikini bali mtu mbaya  Hana ufahamu hata ayajue watu wenye dharau huwasha mji moto: Bali wenye hekima hugeuzia mbali ghadhabu, mwenye hekima akijadiliana na mpumbafu: Akikasirika au Akicheka,pia hapana raha. wamwagao Damu humchukia mtu mkamilifu Bali mwenye Hekima hutuza nafsi yake,mithali 7:10)

Sifa za mtawala kwanza kabisa kabla ya kuchunguza mambo yote anatakiwa ule uhalisi wa uumbaji wa Mungu unatakiwa kuwa ndani yake yaani awe na hofu ya Mungu ndani yake ili aweze kujuwa thamani ya mwanadumu ni nini,

kwa nini muovu shetani anatesa watu anajaribu kuharibu ile thamani ya mandamu aliyopewa na Mungu, hivyo kama mtu hana hofu ya Mungu huyo hanatofauti na mnyama,

myama yeye hafanyi ibada hategemei kwenda mbinguni na hana habari na mbingu,

kama mtawala akiwa na mahusiano na Mungu nirahisi kuyaona hata mambo ya mbeleni maana mungu anaweza hata kutumia maono au ndoto kumjulisha ila kama hana mahusiano na Mungu atakuwa kama mfalume Nebokadraze anaoteshwa ndoto maana ikakosekana tena heri yeye washahuri wake walikuwa wana hofu ya Mungu wakashahuriana watafutwe watumishi wa Mungu wakaenda kutafsiri Ndoto ya mflume,



sasa  kama  mfalme hana mahusiano na  Mungu akipata tatizo sana sana atakimbilia kwa wachawi badala ya Kumgeukia Mungu, tumwangalie mfalme baada ya kutafsiriwa ndoto yake nini kilitokea?

Hata hivyo, hakuamini, kuwa mateka hawa vijana walikuwa ni watu wenye ufahamu mkubwa wa imani ambo walikuwa wako tayari kufa kuliko kumwacha BWANA, Mungu wao.




Danieli 1 na 2



DANIELI NA RAFIKI ZAKE WANAPEWA JARIBIO: Danieli 1:3-21

Kama sehemu yake ya kuwashawishi wafalme vijana ili wawe waabuduo miungu ya Babeli, mfalme Nebukadreza alibadilisha majina yao na akawaita kwa mjina ambayo yanaheshima kwa miungu ya Babeli.

Kisha akaamuru wapewe kila siku chakula na divai kutoka katika meza ya mfalme. Danieli na rfiki zake walitambua kuwa chakula hicho na divai viliwekwa kwanza wakfu kwa miungu ya mfalme, maana hiyo ndiyo iliyokuwa desturi ya nchi ya Babeli.

Wao wakamwambia msimamizi mkuu awapatie mtama (maharagwe na dengu) na maji badala ya chakula cha mfalme. Akimwongopa mfalme, asije kujulikana kuwa hakutii agizo lake hatimaye akakubali kuwaweka katika majaribio kwa muda siku kumi.

Na baada ya siku kumi ilikuwa ni dhahiri kwa watu wote kuwa Danieli na rafiki zake walikuwa na “nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi” kuliko vijana wote ealiokula chakula cha mfalme (mstari 15). Mungu akawajalia kupata kibali na huruma machoni pa huyu mtumishi wa mfalme kwa sababu ya uaminifu wa utii kwa Mungu.

 Na ingawa walikuwa katika nchi za watu asiomjua Mungu, wakiwa mbali na nchi ambayo Mungu aliwapatia baba zao, vijana hawa waliendelea kumwabudu Mungu wao, naye akaendelea kuwabariki, “akiwapatia maarifa na ujuzi katika elimu na hekima: Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote na ndoto” (mstari 17)



NDOTO YA NEBUKADREZA: Danieli 2

Usiku mmoja, mfalme Nebukadreza aliota ndoto ya kubwa sana na ya kushangaza na ya kutisha.Ilimhangaisha sana, hata asiweze kulala usingizi tena.Aliwaita wote wenye hekima ili waweze kumwambia ndoto kwa kuwa alidhamiria kujua maana ya ndoto hiyo inayotisha sana.Ikawa wenye hekima walipokuja walimwambia mfalme,

“Tuonyeshe sisi watumishi wako ile ndoto, nasi tutakuonyesha ile tafsiri yake” (mstari 4). Nebukadreza aliwafahamu watu wake hao wenye hekima kuwa wana akili sana, na hakutaka kusikiliza maelezo yoyote ya kuvutia kugeuza kusudi la nia yake. Alitaka kujua kweli. Alikataa kuwajulisha ndoto yake. Na hii ilionekana kwao kuwa ni jambo lisilowezekana. Ni njia gani gani wangeweza kujua ndoto ya mfalme aliyoota kitandani mwake / Hata hivyo mfalme hakubadilisha nia yake.

Wamwambie ndoto na tafsiri yake ama wafe. Walilalamika, Hapana mtu duniani awezaye kulionyesha neno hili la mfalme; kwa maana hapana mfalme wala bwana, wala liwali, aliyetaka neno kma hili wala hapana mwingine awezye kumwonyesha mfalme neno hilo, ila miungu, wasio na kikao pamoja na wenye mwili” (mstari 10-11)



Mfalme akagadhabika sana, akatoa amri ya kuwaangamiza wenye hekima wote-“wakawatafuta Danieli na wenzake ili wauawe” (mstari 13).



Danieli aliposikia amri ya mfalme ya kuwaua wote,alimwomba mkuu wa walinzi, “mbona amri hii ya mfalme ina ukali namna hii” (mstari 15). Mkuu wa walinzi akamwambia sababu, Danieli mara moja akamwomba muda na atamwezesha mfalme kufahamu yote mawili ndoto na tafsiri ya ndoto hiyo. Kwa hiyo Danieli na rafiki zake watatu wakmwomba Mungu awafunulie ile ndoto ya mfalme. Mungu akasikia maombi yao, akamwonyesha Danieli yote mawili, ndoto namaana ya ndoto. Danieli, akaingia kwa mfalme Nebukadreza kwa kujiamini sana.



Danieli, akasema, “yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho” (mstari 28).



DANIELI ANAIFUNUA NDOTO: Danieli 2:31-35

Katika yake, mfalme aliona sanamu kubwa sana mbele yake. Ilikuwa na uzuri wa ajabu na ilikuwa na mwangaza sana na kuonekana kwake kulikuwa kwa kutisha sana.



KICHWA cha sanamu kilikuwa cha DHAHABU safi



TUMBO na MIKONO ilikuwa ya FEDHA



TUMBO na MAPAJA ilikuwa ya SHABA



MIGUU ilikuwa ya CHUMA



NYAYO zilikuwa ni za CHUMA na UDONGO



Na alipokuwa akitazama aliona jiwe, “lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono” likipiga sanamu kwenye nyayo likaivunja sanamu vipande vipande. Na kwa kuwa nyayo zilipondwapondwa na sanamu yote ili anguka na kupondekapondeka. Sanamu yote ikawa imevunjika vunjika na upepo ukavipeperusha “vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari” (mstari 35). Lile jiwe lililoipiga sanamu hiyo likaongezeka, likaongezeka hata likawa mlima mkubwa sana likaijaza dunia yote.



TAFSIRI YA NDOTO: Danieli 2:37-45

Na hii ndiyo iliyokuwa ndoto ya Nebukadreza na Danieli akaendelea kumjulisha mfalme maana ya ndote yake yote. Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu,” Danieli akamweleza, “wewe u kichwa kile cha dhahabu” (mstari 37, 38). Madini mengine manne yaliyofuata yaliwakilisha falme nne ambazo zingefuata baada ya ufalme wa Babeli.

FEDHA inasimama baada ya UMEDI-UAJEMI



SHABA inasimama baada ya ,UYUNANI



CHUMA inasimama baada ya RUMI



CHUMA na UDONGO



inawakilisha Ulaya iliyogawanyika.Ambapo leo tunaona baadhi ya nchi zina nguvu za kijeshi na zingine ni dhaifu.



Sanamu iliyosimama mbele zake iliwakilisha FALME ZA WANADAMU, maana kila utawala ulioonyeshwa katika sanamu ulikuwa ukitawali na wanadamu ambao hawakumjua kabisa au hawakumtii Mungu wa mbinguni. Wote walikuwa wagumu wa mioyo, wakatili na wapenda vita. Nia yao kubwa katika maisha yao ilikuwa ni kujiwezesha wao wenyewe kuwa na nguvu za kijeshi na utajiri, kwa kuyafanya maisha ya maelfu ya watu wanaotawaliwa kuwa ya umaskini na mateso kutoka kwa wanowatawala.



Leo tunaishi katika siku za mwisho za ufalme wa wanadamu.Uovu wa aina hiyo ulionekana katika ufalme wa zamani wa wanadamu, unaendelea kuonekana katika miongoni mwa viongozi siku hizi. Hawa wote ni watu wasiomcha Mungu wanaofurahia kutumia nguvu dhidi ya watu wengine na sifa na nyadhifa zao.



NGUVU ZA JIWE: Danieli 2:44-45

Jiwe linawakilisha nini? Lilikuwa ni dogo mwanzo, lakini linapiga nyayo za chuma na udongo na kusababisha sanamu yote kuharibika. Nguvu za JIWE zinawakilisha UFALME WA MUNGU.



Bwana Yesu Kristo atarudi kuangamiza falme za wanadamu. Kwanza kabisa atayaangamiza majeshi ya mataifa yote, ambayo yatakuwa yamekuja katika nchi ya Israeli kupigana na Yerusalemu (Zekaria 14:2). Kuanzia hapo ufalme wake utaongezeka mpaka utaijaza dunia yote. Ufalme huo utaanzishwa baada ya kuangamizwa kwa mataifa yote ya duniani.



Tofauti na Ufalme wa wanadamu, Ufalme wa Mungu utakuwa na mfalme mwenye busara na wa haki akitawala kwa kicho cha Mungu (2 Samweli 23:3). Atakuwa mwenye haki mwenye huruma na atawajali sana masikini na wahitaji.



(Zaburi 72 maelezo ya uzuri ajabu wa mfalme atakayetawala ufalme wa Mungu). Ulimwengu utakuwa na amani wakati wanadamu wote watakapomtii Mungu na mwisho dunia yote taijawa na utukufu wa Mungu (Isaya 9:6-7;11:9).



Hili litatokea lini? Danieli aliweza kueleza kuwa mambo haya yote yatapita katika siku ambazo sanamu yote itakuwa imesimama juu ya nyayo zake za chuma na udongo.



“Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme, ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipandevipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele” (Danieli 2:44).



FUNDISHO KWETU NI LIPI?

Ndoto ailiyomsumbua sana Nebukadreza ni ya muhimu sana kwetu kwasababu inazungumzia mambo ya siku zetu, inaelekea chini kabisa ukianzia kwenye kichwa cha dhahabu mpaka wakati wa nguvu za Jiwe zitakapofunuliwa.Na siku yoyote sasa Bwana Yesu Kristo anaweza kutokea. Yeye mwenyewe alitupatia maneno ya kututahadharisha: “Kesheni basi; kwa maana hamujui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu” (Mathayo 24:42). Yesu anatutaka sisi kuendelea kuwa waaminifu kwake, ili kwamba tuweze kumsaidia kuubadilisha ulimwengu uwe mahali pa kuishi penye utukufu na furaha.



Umewahi kujiuliza maswali haya haswa nyakati Hizi tulizo nazo? kama umewahi kupasoma hapa na kama hujawahi je? Umejifuza nini?





1. Nebukadreza alitaka awafundishe nini Danieli na rafiki zake waliokuwa utumwani?

2. Ni kwa nini Nebukadreza alibadilisha majina ya Daniele na rafiki zake?

3. Ni kwa nini walikataa chakula cha mfalme?

4. Waliomba wapewe nini badala yachakula cha mfalme?

5. Ni jinsi gani Mungu aliwabariki Danieli na rafiki zake?

6. Ni kwa nini Nebukadreza alikataa kuwapatia wenye hekima ndoto yake?

7. Wenye hekima walimwambia nini mfalme baada ya kukataa kuwapatia ndoto yake?

8. Danieli alijuaje ndoto aliyoota mfalme? Lingani sha na maisha haya tunayoyaishi hivi sasa

9. Ilitokea nini kwa sanamu baada yajiwe kuipiga kwenye nyayo za chuma na udongo?

10. Je jiwe linawakilisha nini?

11. Ni nani atakayeziangamiza falme za wanadamu?

12. Ufalme wa wanadamu utawekwa wapi? Mungu atusaidi sana,

Followers