UPONYAJI NI HAKI YA NANI?



Uponyaji Wa Mungu


Ingawa jambo la uponyaji wa Mungu lina utata kiasi fulani kwa baathi ya watu, si kitu kilichofichika katika Maandiko. Ukweli ni kwamba, kiasi cha moja ya kumi yakila kitu kilichoandikwa katika zile Injili nne kinahusu huduma ya uponyaji ya Yesu. Zipo ahadi za uponyaji wa Mungu katika Agano la Kale, Injili na katika nyaraka za Agano Jipya. Wale walio wagonjwa wanaweza kupokea faraja kubwa sana katika wingi wa maandiko yenye kujenga imani.



Nimeona katika safari zangu zote katika kuifanya kazi ya Mungu kwamba, kwa ujumla, uponyaji wa Mungu ni kitu cha kawaida katika makanisa yaliyojaa waamini waliojitolea kikamilifu (wanafunzi wa kweli). Mahali ambapo kanisa limepoa na ni la kimaendeleo, uponyaji unatokea kwa nadra sana. Hayo yote yasitushangaze kwa sababu Yesu alisema kwamba ishara moja itakayofuatana na waaminio ni kwamba wataweka mikono juu ya wagonjwa nao watapona  afya (ona Marko 16:18). Tungepima makanisa kwa ishara ambazo Yesu alisema zitafuatana na waamini, tungefikia mahali pa kuamua kwamba makanisa mengi hayana waamini. kwaanzia wahudumu na wanaopokea,



[Yesu] Akawaambia, Enendeni ulimwengu mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya (Marko 16:15-18).



Mtumishi afanyaye watu kuwa wanafunzi, akiwa anaiga huduma kamilifu ya Kristo, hakika atatumia vipawa vyake kuendeleza huduma ya uponyaji wa Mungu katika eneo lake la ushawishi. Anajua kwamba uponyaji wa Mungu hukuza ufalme wa Mungu kwa njia mbili. Kwanza – miujiza ya uponyaji ni matangazo mazuri sana kwa Injili, kama mtoto yeyote anayesoma Injili au kitabu cha Matendo atakavyoelewa (ingawa watumishi wengi wenye madigirii makubwa wanaonekana hawaelewi). Pili – wanafunzi wenye afya njema hawazuiwi kufanya huduma kwa magonjwa binafsi.



Pia, mtumishi anayefanya wengine kuwa wanafunzi anahitaji kuwa makini kwa wale katika mwili wa Kristo wanaohitaji uponyaji, ila wana shida ya kupokea. Mara nyingi wanahitaji mafundisho ya taratibu na kutiwa moyo kwa upole, hasa kama wamefikia mahali pa kupingana na ujumbe wowote wa uponyaji. Mtumishi anayefanya wengine kuwa wanafunzi anakabiliwa na uchaguzi: anaweza kuepuka kufundisha kuhusu uponyaji wa Mungu moja kwa moja. Akifanya hivyo, hakuna atakayekwazika wala hakuna atakayeponywa. Au, anaweza, kwa upendo sana, kufundisha somo hilo na kudiriki kuwakwaza wengine huku akiwsaidia wengine kupokea uponyaji. Mimi binafsi nimeamua kufanya la pili, nikiamini kwamba ni kufuata mfano wa Yesu.

Followers