muda gani ambao ungetaka kuoa au kuolewa?
Utasikia mwingine anasema, siku Mungu atakapo nipa mume au mke, hii ni hatari sana! Biblia inasema kwenye kile kitabu cha Mhubiri.3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu”.
Kila kitu kilichoko chini ya mbingu kimeratibiwa, kwa lugha nyingine, ni kwamba kila mwanadamu ana kalenda yake, iko kalenda yako ya kuzaliwa, na ipo kalenda ya matukio na mipango mbalimbali. Mungu anaijua. Mungu anatangaza mwisho tangu mwanzo, anajua mwisho wa maisha yako wakati wewe unapozaliwa.
Katika mwanzo wa maisha yako, Mungu anakuwa amekwishajua mwisho wako; utakavyokuwa; na kama amekwishajua mwisho wako, maana yake ameshatembea kwenye maisha yako yote toka mwanzo mpaka alipofika mwisho, na alipokamilisha maisha yako akarudi mwanzo ndipo akakuongoza kuzaliwa.
Mungu anapokuacha uzaliwe duniani, hakika ujue kabisa ya kwamba amekwisha tembea na wewe katika maisha yako, amesharatibu mambo yako na yako hatua kwa hatua; kwa mfano, kitu gani utafanya, wapi utasoma, utasoma nini, utaolewa na nani au utaoa nani na itakuwa, lini, maisha yako yatakuwaje, utamtumikiaje, mpaka mwisho wako. Akiishafika mwisho wa maisha yako anarudi mwanzo, akishafika mwanzo anatangaza mwisho tangu mwanzo; kwa hiyo kuanzia hapo unapozaliwa ujue maisha yako yote yamesharatibiwa!
Ni vizuri ufahamu hii mistari itakusaidia, maana inakujengea msingi mzuri wa maisha hapa. Isaya.46:9-10 inasema, “Kumbukeni mambo ya zamani za kale maana mimi ni Mungu wala hapana mwingine, mimi ni Mungu wala hapana aliye kama mimi. Nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado, nikisema, shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote”.
Kwa lugha nyingine anatuambia ya kwamba, ‘wewe unaona kila kitu ni kipya, unapoishi kila siku ni mpya, kila dakika inayokuja ni mpya, Mungu anasema hiyo safari unayopita, mimi nilikwishaipita tayari, nikafika mwisho wa maisha yako ndipo nikakuruhusu uzaliwe. Ulipokuwa unazaliwa nikatangaza mwisho wako tangu wakati unazaliwa.
Sasa mimi ninataka nikuambie kama Mungu anajua, na shauri lake anasema litasimama katika maisha yako, ili mapenzi yake ayatende katika maisha yako, unahitaji kuwa mwangalifu. Kwa sababu kuna mpango na saa ya Mungu ya kuoa au kuolewa, - ipo!
Mungu anapokuletea mawazo ya kuoa au kuolewa, ni kwa ajili yakuimarisha maisha yako na wito wako na kazi na makusudi, ambayo ameyaweka hapa duniani. Atakuletea mtu atakaye imarisha wito wako, atakuletea mtu atakaye saidiana na wewe, uwe ni mwanamke au uwe ni mwanaume.
Mungu anapo kukutanisha na mtu wa kuoana naye ni kwa ajili ya kuimarisha nguvu zenu ili mtimize kusudi la Mungu wakati mwingine unaweza kuchelewa kuowa au kuolewa kwasababu yakutokuwa na kazi ya Mungu ya kufanya hapa duniani kwasababu ataimarishaje nguvu ambazo hazitatumika? Kwa hiyo wakati mwingine usilalamike kutooa au kuolewa ipo sababu nzuri tu anayoifahamu Mungu na si mwanadamu awae. Kwa hiyo lazima anajua kuna saa huyu mvulana anahitaji mke, au huyu msichana anahitaji mume! Lakini watu wengi sana hawalifuatilii hili. Kunakuja kuwa na watoto
Maana watoto wakiwa wadogo wote, mimi ninakuambia kumtumikia Mungu ni kuna kuwa kugumu sana, usije ukafikiri ni kurahisi. Maana unahitaji kuwa karibu nao; wanahitaji kusoma shule, wanahitaji kufanya vitu mbalimbali, wanahitaji kuwa na baba karibu, wanahitaji kuwa na mama karibu. Saa nyingine mnataka kusafiri nao; unaweza ukasafiri nao lakini usije ukafikiri ni kitu kirahisi sana ila kwa wale ambao hawajaujuwa wito wao wanaweza hata kupuuzia haya yote,
Ndugu Mtazamaji/ MSOMAJI; Bila shaka unampenda Mungu Sana tunaamini hivyo Kwa vile ulivyoweza kufika mahali hapa tulipo kupitia Mtandao huu, lipo kusudi la Mungu kutaka kukusaidia jambo Fulani ikiwa uko tayari katika yote jiepushe na mafundisho yasiyokuwa ya ki-Mungu Mathayo 16:6-12) piga simu kwa masaada zaidi huduma hii ni bure 0757328311