MAANDALIZI YA KUOWA AU KUOLEWA

Ndowa inakuunganisha na kukuingizakatika familia nyingine mya.

Unafahamu watu wengi sana wakioa au kuolewa wanafikiria tu mahusiano ya wao wenyewe tu; na hii ni hatari sana. Kwa sababu unapooa unaingia kwenye undugu na familia nyingine kabisa tofauti, na sio mahusiano ya kwenu tu wawili. Ninyi ni kigezo tu cha kuunganisha hizo familia mbili, lakini mkiishaoana hizo familia zenu mbili ni ndugu kuanzia wakati huo.
Ndio maana unapofika unataka kuoa au kuolewa, sio suala la kumtazama kijana tu, au kumtazama msichana yeye mwenyewe tu; kwa mfano alivyosoma, lakini ni lazima pia utazame na hali ya familia yake ili ujue unajiingiza kwenye familia ya namna gani. Unapofika kwenye masuala ya namna hiyo kuna vitu vingi sana vya kuangalia.
Unaweza ukaingia kwenye familia ambayo ni wavivu, mimi ninakuambia jasho litakutoka ukioa msichana wa namna hiyo; au ukipata kijana toka kwenye familia ya namna hiyo. Itakuwa kazi sana kumshawishi mwenzako juu ya kujishughulisha na maisha. Maana inategemea; kwa kuwa unaweza kuoa msichana hata kusonga ugali hajui. , kwa mfano kwetu tuna wasichana watatu, tumezaliwa watoto 6 wa kiume 3, wasichana 3
Lakini mama yetu alikuwa na bidii ya kutufundisha wote kufanya kila kitu kwa bidii sana, alitufundisha kupika, alitufundisha kulima, kufanya biashara ndogo ndogo Kwa hiyo nilijifunza kwanza kutoka kwa wazazi wangu hayo yote.
Sasa wengine hawapati nafasi ya namna hiyo kwa sababu ya wazazi kuachana au kutokuwa na uhusiano mzuri na familia zao, na ni mbaya zaidi haswa kwa wasichana. Mungu amenipa nafasi ya kuwa na mtoto mmoja wa kike na itakuwa ni aibu kwetu kama wazazi, ikafika wakati wanaingia katika ndoa zao na hawajui kupika ni aibu kwetu sisi wazazi japo wengi wazazi hawalikubali hilo jambo lolote baya au la aibu litakalo onekana kwa binti anayeolewa ni aibu kwa wazazi; wengine baada ya kutegea kumlea mtoto katika maadili,mtoto akipata mme wa kumwoa anawapa wa mama eti wamfundishe kwenda kuishi na mwanaume, kinachonishangaza wao walimu wanaofundisha, karibia ya wote hawana ndowa,sasa watafundisha kitu gani,
Kama umechelewa kumfundisha mtoto wako ni heri ukampeleka kwa watumishi wa Mungu,ambao una uhakikanao kwa matendo yao,maana wingine wanajiita tu ni watumishi wa Mtungu ila haijulikani hata ailiyewatuma kwasababu ya matendo yao, kwa hiyo lazima uwafundishe watoto wako wajue kupika hata wakiume maana ipi siku wataendakuanza maisha yao kuishi bila wazazi, . Maana kwa kujua hilo anaonyesha anatoka familia ya namna gani, na imemlea kwa namna gani! Sikatai wewe kumuweka mtumishi wa kazi za ndani nakini na wewe pia kama mzazi simama nafasi yako ya mzazi,
Unaweza ukafikiri unamlea mtoto wako vizuri kwakuto mshugulisha ila utakuwa unamuumza bila yaw ewe kufahamu, maana siku hizi kuna shida ya kuwa na wafanya kazi majumbani mwetu. Ukishakuwa na mfanyakazi nyumbani basi watoto wengine hawafanyi kitu chochote, wakati mwingine wanakula chakula na wanaacha sahani hapo hapo mezani hawafuti meza hawatandiki kitanda.
Kuna watoto wengine inakuwa mpaka yuko sekondari hawezi kufua nguo zake. Kwa kuwa nyumbani kama hakuna wa kumfulia basi kuna mashine za kufulia. Huko unakokwenda kuolewa inawezekana hata mashine ya kufulia hawajawahi kuiona wala kuisikia! Unafika pale na unauliza mashine iko wapi, wanakuambia yakufanyia nini au ipi, - ya kusagia mahind ipo pale mtaa wa pili Maana ndio wanayoijua kuwa ndio mashine!
Hujui hata namna ya kushika kioo cha taa ya chemli wala namna ya kuiosha kule ndani lile vumbi likaondoka. Inawezekana mwingine umezaliwa kwenye nyumba yenye umeme, lakini utakapokuwa katika ndoa unaenda kwenye nyumba ambayo haina hata umeme, unafika kule na unashangaa kweli maana hujui hata namna kuwasha taa ya chemli! Kwa hiyo tunawaambia vijana suala la kujifunza hivi vitu sio suala la kuchagua, hata kama kuna mtu pale nyumbani wa kuwasaidia, ni lazima wajue kufanya kazi! Zamani mimi niliwasikia wazazi wangu wakisema kijana alikuwa hapati mchumba bilaya kuonyesha nizamu na bidii ya kufanya kazi acha wale wanaotoroka kijijini wanakuja mjini maisha yakiwaonea kidogo tu basi wanajirahisisha na kujipeleka wenyewe kwenye ndowa,ndowa siyoyakujipeleka ni maisha yako hivyo ukikosea unakosea kuishi unaweza ukafa muda wako bado kabisa,
Nilienda kwenye mkoa mmoja wakasema, sisi ukitaka kuoa kwenye nyumba ya mtu, ukitaka kujua huyo msichana amelelewa vizuri au vibaya wakasema usimtazame alivyovaa. Badala yake wanafika kwenye uwanja wa nyumba ya wazazi wake, na wanaangalia ile barabara inayokwenda nyumbani kwao, na wakiikuta chafu, basi wanajua huyu msichana ni mchafu, hawahangaiki tena kuja kuzungumza, wanajua hapa kama tunaamua kuoa tujue tunacho oa, huyu msichana ni mchafu!
Ukienda kuoa kwenye familia nyingine utakuta wanasumbuliwa na ugonjwa wa kurithi, na usipojua kitu cha kufanya unaweza ukapata shida sana. Lakini ninachotaka kukuambia ni kwamba, uamuzi wa kuoa au kuolewa unakuingiza kwenye familia nyingine kabisa, na inaunganisha hiyo familia yao na familia yako; kwa hiyo hayo sio maamuzi madogo. Kumbuka unapooa au kuolewa unawaingiza watu katika famila ambazo kama usipokuwa mwangalifu inaweza ikaleta shida sana, lakini pia inaweza ikaleta baraka!.

Ukienda kuoa kwenye familia nyingine utakuta wanasumbuliwa na ugonjwa wa kurithi, na usipojua kitu cha kufanya unaweza ukapata shida sana. Lakini ninachotaka kukuambia ni kwamba, uamuzi wa kuoa au kuolewa unakuingiza kwenye familia nyingine kabisa, na inaunganisha hiyo familia yao na familia yako; kwa hiyo hayo sio maamuzi madogo. Kumbuka unapooa au kuolewa unawaingiza watu katika famila ambazo kama usipokuwa mwangalifu inaweza ikaleta shida sana, lakini pia inaweza ikaleta baraka!.

Followers