Hakuna wokovu katika mwingine:
“kuokoka maana yake halisi kwanza ninapenda ufahamu siyo Dini wala thehebu fulani,bali kuokoka ni kuokolewa kutoka katika hatari,sasa mtu anapookolewa kutoka katika hatari ya kwenda jehanamu kwaajili ya maovu akipata neema ya uokovu huo akatubu thambi zake zote na kuziacha basi huyo anaweza kusema ameokoka,ndiyo maana wengi unaowasikia kuwa wameokoka,kwanza wanakuwa na furaha sana,kwa kunusurika na jehanamu,
pia fahamu hili hapa duniani kuokoka kupo acha wale walioshindwa kuelewa,na anayeweza kuokowa ni mmoja tu, hayupo mwingine,awe ni kiongozi wako wa thehebu au mtume,nabii hayopo mwenye uwezo wakuokowa,wala jina lenye nguvu na mamlaka zaidi ya moja tu
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo ya Mitume 4:12).
“Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao” (Mathayo 1:21).
“Bali wote waliompokea (Yesu Kristo) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake, waliozaliwa si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu” (Yohana 1:12 – 13)
“Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani, maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa, kila atakayeliitia jina la Bwana (Yesu Kristo) ataokoka” (Warumi 10:12 – 13). Hivyo kwa siku za leo tungesema hakunatofauti ya mchaga na msukuma au nakabila lolote huu ni mfano tu,wote wanahitajika kuokolewa na mmoja tu Yesu kristo mwana wa Mungu,
Ndugu Mtazamaji/ MSOMAJI; Bila shaka unampenda Mungu Sana tunaamini hivyo Kwa vile ulivyoweza kufika mahali hapa tulipo kupitia Mtandao huu, lipo kusudi la Mungu kutaka kukusaidia jambo Fulani ikiwa uko tayari katika yote jiepushe na mafundisho yasiyokuwa ya ki-Mungu Mathayo 16:6-12) piga simu kwa masaada zaidi huduma hii ni bure 0757328311