SOMO: NGUVU YA NDOTO
Na Nabii Samson Mboya
is not enough to have
visions and dreams while you live as you dreaming
Utangulizi:
Habakuki 2:2-3; Bwana
akanijibu, akasema, Iandike Ndoto hii ukaifanye iwe wazi Sana katika vibao, ili
aisomaye apate kuisoma kama maji.
Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.
Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.
NINI
MAANA YNDOTO ~ ni
mfuatano/mtiririko wa picha, mawazo, na mihemko ya hisia ambazo kikawaida
hutokea katika ufahamu pindi mtu anapokuwa amelala.
Na mara nyingi ukubwa
wa ndoto huanzia sekunde hadi dakika 20-30 kwa ndoto; na ni mara chache sana
mtu kuota Zaidi ya muda huo japo wapo wengine wanaoota ndefu Zaidi
AINA
ZA NDOTO
1.
NDOTO ZITOKAZO KWA MUNGU.Kama
nilivosema hapo awali Mungu pia hutumia njia ya ndoto kuwasiliana nasi pindi
tunapokua tumelala (Ayubu 33:14-16, Yoel 2:28) Hizi ndoto za aina hii mara
nyingi huleta msisimko ndani ya roho na nafsi pia kuashiria jambo jema au baya
na mara nyingi ni ndoto zinazokua na mapambano Zaidi kwani shetani hutaka sana
kukusahaulisha kile ambacho Bwana alikuotesha.
Ayubu 33:14-15
14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu
hajali.
15 Katika ndoto,
katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi
kitandani;
Mungu ndiye chanzo cha
Ndoto ila si kila ndoto inatoka kwake,
Yoel 2:28 28 Hata
itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu wenye mwili; na
wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu
wataona maono;
Usichanganyikiwe hapa
Mungu ndiye chanzo cha ndoto zote tunazoota lakini sio ndoto zote hutoka kwake.
NDOTO
ZITOKAZO KWA SHETANI.Zipo
ndoto zitokazo kwa shetani adui wa nafsi zetu ambazo mara zote huwa na
mifadhaisho na kuogofya sana na mara nyingi ndoto hizi hazisahauliki kwa sababu
shetani huhitaji sana kuharibu hatima yako ndio maana ni vigumu sana kusahau.(1
Samweli 28)
JINSI GANI UTAWEZA KUTUNZA NA KULINDA NDOTO
ZAKO
1. JIFUNZE
KUOMBA ~Jenga
mazingira ya kuomba mara kwa mara pindi unapoota ndoto ya aina yeyote iwe imetoka
kwa Bwana au kwa shetani huna budi kuziombea maana zote huwa haziji bure.Na pia
ni muhimu kabla ya kulala uombe ili Mungu akuwezeshe kujua maana ya tafsiri juu
ya kile ulichokiota;ili kisipotee bure
2.
MSIKILIZE MUNGU~Chukua
muda wako wa kutosha na wa utulivu kwa ajili ya kumsikiliza Mungu juu ya kile
ulichokiota na pindi unapohisi Amani moyoni mwako ni njia mojawapo ya Mungu
kuridhia kile ulichokiona.Ndoto inayokupa Amani na kukupa utulivu inakupa ujue
kabisa ndoto iyo imetoka kwake;maana kumbuka ni Mungu mwenyewe ndiye anaweza
kutupa Amani juu ya yale tunayoyaota.(Mathayo 2)
3. JIFUNZE KUANDIKA NDOTO ZAKO~Kama
nilivotangulia kusema jenga mazingira ya kulala na daftari ili uweze kuandika
kile unachokiota hii itakusaidia kuweza kukumbuka yale uliyoyaota na kuyapa
muda ili yawe Dhahiri baadaye
4. TAFUTA USHAURI TOKA KWA MUNGU~Watu wengi pindi waotapo ndoto huanza kuhangaika
kwenda kwa watu mbalimbali ili kupata tafsiri (Mwanzo 41) Jambo ambalo sio zuri
kwa Bwana maana ndoto husiana na hatima binafsi ya mtu wala sio kwa wengine
penda kumuomba Mungu ili aweze kukupa tafsiri juu ya kile ulichoota.Pia Mungu
huweza kukuongoza pia kwa mtumishi wake kwa ajili ya kukupa tafsiri jua
inategemea sana kwa Amani utakayoiskia pale unapopewa tafsiri.
AINA
ZA NDOTO
1.
NDOTO ZITOKAZO KWA MUNGU.Kama nilivosema hapo awali Mungu pia hutumia njia ya
ndoto kuwasiliana nasi pindi tunapokua tumelala (Ayubu 33:14-16, Yoel 2:28)
Hizi ndoto za aina hii mara nyingi huleta msisimko ndani ya roho na nafsi pia
kuashiria jambo jema au baya na mara nyingi ni ndoto zinazokua na mapambano
Zaidi kwani shetani hutaka sana kukusahaulisha kile ambacho Bwana alikuotesha.
5.
SUBIRI NA ACHA ITOKEE~Baada ya kufanya
mambo hayo hapo juu unapaswa kusubiri mapenzi ya Mungu yatokee kwa yale
uliyoyaota.Kumbuka ndoto nyingi huwa wazi na kweli ila kuwa mwangalifu Zaidi
katika ndoto zile ambazo zinakaa Zaidi kwenye ufahamu wako na haziondoki kwa
haraka.
ALAMA
CHACHE UNAZOWEZA KUZIONA KATIKA NDOTO
FARASI~Anaashiria mtu; hali ya maisha yake na roho yake pia (Mathayo 7:24-27,
2Timotheo 2:20-21)
Samaki~Watu
Majani makavu~Kuchakaa na kuwa ukiwa
Majani mabichi~Neema na ustawi
Ngazi~Kuongezeka, kukua mafanikio
Mbuzi~Ulafi
Mbwa~uzinzi
Kondoo~Unyenyekevu, upole
Mkono~Bwana atatenda makuu kwa mkono wake
Maji~neema, kurudhika na kuendelea
Daftari na kalamu~Elimu na mafunzo mbele yako
Kuku~papara na kuhangaikia mambo yasiyokuhusu
Mwewe mweusi~Mkuu wa anga wa eneo
Paka~uchawi wa eneo
Nyoka~Njama, shetani, Ibilisi, Njama
Kipara~werevu, uzamani, wingi wa maarifa
Nzige~uharibifu, hasa wa kipawa au huduma
Asali~uponyaji,ulinzi na uzuri
Unapoona ulimi upo nje ya kinywa~roho ya usengenyaji, umbea, kugombanisha
Unapoota unaumwa na kichwa~wachawi na wanga wamekushambulia
Unapoota unatembea lakini hufiki~Jambo unalolofanya sasa linakupotezea muda
fanya jambo jingine achana na hilo.
Unapoota umezaliwa tena~Bwana anakufanya upya hasa katika matendo
yako(kubadilishwa)
Unapoota unaitwa na mtu usiyemjua~Roho ya mauti
Unapoota watu waliokufa wanakuita~Maagano, mauti
Unapoota unafanya mapenzi na ndugu yako wa kuzaliwa~Uhusiano wako na ndugu yako
utaharibika muda sio mrefu,pia utapata aibu
Unapoota unalia na hakuna anayekufariji~Huna uhusiano mzuri na watu
Unapoota ndugu wako wa karibu amekuja kukutembelea na kukuaga~Roho ya mauti ipo
juu yake
Unapoota upo mbele za watu wengi wanakusikiliza~Bwana atakutukuza na
kukujulisha mbele za wengi
Ukiona nyumba/chumba kipya~ Huashiria mawazo chanya; huduma na maisha mapya
katika eneo jingine jipya
Unapoota upo uchi~Aibu; mambo yako yatakuwa hadharani na kuonekana, kuwa
mwangalifu katika siri zako kwa watu
Unapoota unaoa au kuolewa~Bwana ameona upweke na ukiwa wako atakupatia mtu wa
kuwa na wewe maishani
Unapoota unavuka mto lakini umelowana ~Jaribu unalopitia utalishinda ila kwa
taabu nyingi, Lakini utavuka
Unapoota umelala na mtu wa jinsia ambayo sio yako~Kuwa mwangalifu na aina ya
mahusiano uliyonaoyo yatapelekea kumkosea Mungu
Unapoota mti mkubwa uliostawi sana~Mungu atakuinua na kukufanya mkuu
Unapoota upo ziwani unavua samaki~Mungu atakufanya kuwa mvuvi wa watu;
atakutumia kuwaleta watu kwake
Unapoota umeumwa na nyoka~Kuwa mwangalifu sana kwani adui atakushambulia
Unapoota unakimbizwa na watu usiowajua kwa nia ya kukudhuru na ukawazidi
mbio~Uwe mwangalifu kwani shetani atatumia mapepo yake na wachawi kukushambulia
lakini hawatakushinda.
Unapoota unakula lakini hushibi~Roho ya kutotosheka na kutapanya mali
Unapoota umekatwa kichwa~Mamlaka yako yamehamishwa na kwenda kwa mtu mwingine.
Unapoota unavalishwa joho~Bwana atakufanya kuwa mpatanishi kwa wengine.
Unapoota shamba zuri limejaa mazao~Ni kipindi ambacho Mungu atakurejeshea kwa
wingi mafanikio yako
Unapoota matunda yaliyoiva~Ni wakati wa mafanikio yako tayari
Unapoota mto mkubwa uliojaa mamba~Vikwazo na balaa vimewekwa mbele
Unapoota mlima mkubwa mbele yako~Jaribu mbele yako
Unapoota umekufa~Ni taarifa kwako kwa mambo uliyonayo yamekwisha.
Neno la Mungu linasema
nini juu ya ndoto
Biblia imetaja sana
kwa habari ya ndoto, ukisoma katika kitabu cha Mwanzo pekee, neno “ndoto”
limeandikwa zaidi ya mara 36. Pia, katika kitabu cha Daniel neno ndoto
limeandikwa zaidi ya mara 29. Na ndio maana Mungu alipotaka watu wake wajenge
ama madhabahu au hekelu aliwaonyesha kwanza katika ndoto; kumbe ujenzi wowote
huanzia katika kuona. Vivyo hivyo hata watu wanaomtegemea shetani huingia
ulimwengu wa roho na kujenga kile walichokiona kutoka kwa shetani.
TABIA
YA MUNGU KATIKA NDOTO:
Kutoka 25:8-9; Mungu
akitaka ujenge anaanza kukuonyesha; ndio maana alimwonyesha pia na Musa na
kumtaka ajenge sawa sawa na alichomwonyesha “exactly like the pattern I will
show you” Kutoka 25:37-40; Hii ni tabia ya Mungu kuwaonyesha watu kupitia ndoto
na watu wengi pasipo kujua wamejikuta wakidharau ndoto.
Ukisoma katika kitabu
cha Habakuki 2:2-3; Mungu alimwamuru Habakuki aiandike ile ndoto; kwasababu
asingeweza kufanya kuona kwanza katika ulimwengu wa roho. Na ndio maana neno
ndoto limeandikwa mara nyingi katika kitabu cha Mwanzo kwasababu hicho ndicho
kitabu cha asili (origin). Hiyo inatufundisha kuwa mwanzo wa vitu huanzia
katika ndoto.
Mambo ambayo Mungu
anaweza kuyafanya kupitia ndoto:
i)
Mungu anaweza kufumbua mafumbo kupitia ndoto:-
Mwanzo 40: 2-19; Hapa
tunaona kwa habari ya mwokaji na mwoshaji wa Farao ambao walipata kujua hatari
iliyokuwa imejificha kwa njia ya ndoto. Kwa njia hiyo wote wawili wakajua
maisha yao siku tatu mbele. Kumbe ndoto yaweza kukufunulia mitego au hatari
iliyojificha au kupangwa na watu wabaya.
Farao alikwisha
kupanga kuwa siku ya tatu itakuwa hukumu yao lakini bila kuwambia; lakini
waliweza kufunuliwa katika ndoto. Ni maombi yangu kuwa Mungu na akuonyeshe
hatari zote ulizopangiwa sirini.
Katika kitabu cha
Danieli pekee, neno “ndoto” limeandikwa zaidi ya mara 29; Danieli alikuwa
uhamishoni Babeli; akiwa huko Mungu akamwonyesha kwa habari ya kumrudisha
mahali pake. Vivyo hivyo katika maisha yako inawezekana ulikuwa na mafanikio
lakini sasa hayapo; au ulikuwa na afya nzuri lakini sasa haipo; katika ndoto
Mungu aweza kukurudisha sehemu unayotakiwa kuwapo.
Na ndio maana kila
siku huwa nasema Tanzania mpya niliyoiona katika ndoto inakuja; Tanzania yenye
maendeleo; yenye hospitali nzuri, yenye gesi, Tanzania yenye madini inakuja na
sifi leo ama kesho mpaka ndoto itimie.
Ni maombi yangu Mungu
akurudishie ile hatma njema ya maisha yako ambayo shetani aliichukua katika
maisha yako.
iii) Faida
mbali mbali za ndoto
Ndoto zaweza kukuonya
usichukue maamuzi ambayo sio sahihi, uache tabia mbaya ambayo ina mwisho mbaya.
Mathayo 2: 13-16; Baada ya Herode kugundua kuwa amedhihakiwa na mamajusi
akaamua kuua watoto ili amwangamize Yesu; lakini Yusufu akapewa onyo na Mungu
kuwa ampeleke mtoto Misri. Ni kweli Herode aliangamiza lakini walioangamizwa ni
wale ambao baba na mama zao hawakuota ndoto.
Hapa tunaona athari
moja ya kutoota ndoto, maana madhara yake yaliwahi kugharimu maisha ya watoto
wao. Kupitia ndoto Yesu aliokolewa, Mungu huongea pia kupitia ndoto. Ndio maana
ni muhimu kumwomba Mungu akupe ndoto ya kuokoa familia au ukoo wako.
iv) Mungu
anaweza kutufariji katika ndoto:-
Katika maisha unaweza
kupitia wakati mgumu, umezungukwa na madeni au kukata tamaa lakini Kupitia
ndoto Mungu aweza kukuonyesha utakuwa nani baadaye. Kwa njia hii Yusufu
alifarijiwa kupitia ndoto; kwa njia hiyo Yusufu alipokea faraja na
kuhakikishiwa ushindi.
Yusufu alipoota ndoto
zilisababisha achukiwe na ndugu zake, na wakamtupa shimoni na baadaye kumuuza
Misri lakini ndoto yake ilibaki palepale. Haikutosha hapo, bali alisingiziwa
ametaka kumbaka mke wa waziri mkuu wa Misri na akaja kufungwa. Lakini katika
mateso yake Mungu alikuja kumfariji kupitia ndoto na kumrudisha katika nafasi
yake.
Vivyo hivyo katika
maisha yako inawezekana ulisingiziwa na kupoteza nafasi ambayo Mungu alikupa;
leo kila aliyekunyang’anya nafasi naamuru uchukue nafasi yake; nafasi ya ndoa,
nafasi ya umeneja, nafasi ya uongozi ninaiamuru irudi kwako katika jina la Yesu
Kristo. Yule Yule aliyekupiga vita mwaka jana mwaka huu utachukua nafasi
yake katika jina la Yesu.
Kutoka katika ufungwa
gerezeni hadi kuwa mkuu katika nchi ya Misri, yote hii ilianza katika ndoto.
Kumbuka ndoto za Yusufu zilianza alipokuwa na miaka 16 lakini alikuja kuimiliki
akiwa na miaka 40. Tatizo la watu wengi wanakata tamaa mapema; hutakiwi kufa moyo,
hapo katikati wakati unaisubiria ndoto unaweza ukapitia mateso na mabonde
lakini ndoto itakuja na itatimia usipozimia moyo.
v) Mungu
aweza kukuonyesha utakuwa nani baadaye katika ndoto:-
Mungu hutenda kazi
tofauti na sisi tunavyowaza; Yule mtu unayemuona mdhaifu ndiye ambaye Mungu
anamuona shujaa; vivyo hivyo kwa habari ya Yesu, yeye alizaliwa katika hema ya
ng’ombe; Samweli alizaliwa na Hana ambaye alikuwa hazai hapo mwanzo; Musa naye
alitupwa kwenye mto akakulia kwa baba wa kambo; Samson alizaliwa na mama ambaye
alikuwa tasa hapo mwanzo; na ndio maana hata siku moja usidharau mambo madogo
kwasababu ndiyo ambayo Mungu huyatumia.
vi)
Mungu anaweza kutuonyesha ushindi juu ya adui zetu katika ndoto:-
Kila mtu ana adui wa
maisha wake; awe rais, waziri, mchungaji, au askofu lazima utakuwa na adui wa
maisha yako. Yaani kwa kila hatua unayopiga unatengeneza marafiki na adui wengi
kwasababu hiyo kila mtu ana adui zake. Lakini Mungu anaweza kukuonyesha ushindi
wako katika ndoto. Ukisoma katika kitabu cha Waamuzi utaona kwa habari za
Gideoni ambaye alitakiwa kupigana na Wamidiani; lakini kabla ya kwenda vitani
Mungu akatumia ndoto kumwonyesha ushindi unaokuja mbele.
Ni maombi yangu Mungu
akuonyeshe ushindi juu ya adui zako katika jina la Yesu Kristo. Kumbe kupitia
ndoto unaweza kuonyeshwa adui ambaye hapendi mafanikio yako yaani Mungu akupe
ushindi dhidi ya hila zake mbaya katika Jina la Yesu.
Shuhuda
wa ndoto:
Siku moja nikiwa
nimelala katika usingizi mzito nikaota mke wangu anafagia mayai mengi ya nyoka
chumbani kwetu nikashtuka nikaanza kuomba nilipo washa taa sikuamini na macho
yangu gafla jeshi kubwa la siafu lilianza kuingia ndani ya chumba chakulala
nilimwamusha mwenzangu tukashirikiana kufanya maombi, pia tukatumi sumu ya
sprei baadaye waliondoka zao, hawakumdhuru mtu,
vii) Mungu
anaweza kukuonyesha jinsi ya kumtendea mtu katika ndoto:-
Kupitia ndoto Mungu
anaweza kukuonya juu ya uamuzi mbaya unaotaka kuuchukua juu ya mtu Fulani
katika ndoto; hii tunaiona kwa habari ya Yesu ambapo mkewe pilato alionywa
katika ndoto juu ya hatua alizotaka kuchukua Pilato juu ya hukumu ya Yesu.
Kumbe Mungu aweza kumuonya mtu juu ya uamuzi mbaya ambao waweza kumgharimu mtu
huyo kupitia ndoto.
Mungu anaweza kukuonya
juu ya uamuzi unaotaka kuchukua juu ya mtu wakati wa hasira, wakati wa uoga au
wakati mgumu. Mungu huonya kupitia ndoto na ndio maana ni muhimu kutokufanya
maamuzi yoyote wakati wa hasira; hofu; wakati mgumu kwasababu unaweza kujikuta
unafanya maamuzi ambayo sio sahihi. Watu wengi wamevunja mahusiano mazuri na
watu kwasababu ya maamuzi mabaya lakini kupitia ndoto Mungu aweza kukuonya na
kukuonyesha njia ya kufanya.
NINI
CHA KUFANYA UNAPOOTA NDOTO:
Baada ya kuota ndoto ambayo si nzuri unatakiwa usimame kinyume katika maombi.
Sambaratisha ndoto zote na wasimamizi wake wote katika ulimwengu wa roho.
Na
ikitokea umeota ndoto nzuri unatakiwa uiteke na kuimiliki ndoto hiyo; kushindwa
kuchukua hatua kutakufanya usiimiliki hiyo ndoto. Ukiota umefanikiwa katika
biashara Fulani, unatakiwa uanze kwa kuomba halafu chukua hatua ya kuimiliki
ndoto hiyo.
Ukiota ndoto
halafu huilewi ni nzuri au mbaya unatakiwa uamuru katika maombi kuwa kama ndoto
hii ni mbaya ninaisambaratisha katika jina la Yesu na kama ndoto hii ni nzuri
imiliki katika jina la Yesu.