
Kukosa tumaini na muelekeo wa maisha yako ni hatari sana, maana unaweza kuchukuwa maamuzi ambayo hata wewe mwenyewe hukutarajia kuyafanya,unaweza kukimbia hata pasipo kukimbizwa maana huna tumaini huna ujasiri, Na kaitaka maisha ukichaguwa au kuruhusu kuishi maisha ya kukata tamaa huwezi kupata suluwisho la mahitaji yako tena maana kilakitu unakiona kama umekishindwa,
hali ya kukata tamaa inaweza kuathiri mambo mengi sana maisha yako,kutoendeleza maendeleo yako,inaweza kuathiri ndowa yako, afya yako,biashara yako au kazi yako,n.k matokeo yake hali inaweza kuwa mbaya na kusababisha matatizo mengine kuibuka bila wewe kutarajia, na wengine kama hawakushahuriwa vizuri hufikia hata hatuwa ya kujiua, kuwa na tabia sugu na hata mara nyingine unaweza kujikataa wewe mwenyewe, Habari njiema ni hizi juu ya wewe unayepitia katika hali hii, hali yako ya awali ukizingatia haya inaweza kukurudia tena, na ukawa na Tumaini,amani na upendo kama wa awali
Neno la Mungu liwazi kwa yeye aliyetayari kuliishi vile linavyoagiza Zaburi 51:8 unifanyie kusikia furaha na shangwe,mifupa iliyopondeka ifurahi wakati wote wa maisha yako unapopitia hali ngumu kisha Mungu akakushindia hiyo hali kinachofuata siku zote ni furaha, upo mfano wa Mama mjaa mzito akikaribia kujifunguwa anauhisi uchungu mkubwa sana kwa mjibu wa wazazi,ila akifanikiwa kujifunguwa salama huwa anakuja hisi furaha ya mda mrefu,
upo mfano mwingine mmoja kwa timu za mpira zikiwa zinapambana kisha moja ikafungwa iliyofungwa huwa na huzuni,ila ikijarudisha ushindi mikononi mwao tena huwa hushangilia kuliko wale wa awali, heri mwisho wa jambo kuliko mwanzo,wa jambo jambo usiloliweza wewe kulifanya yeye Mungu analiweza, kuna mambo mengine huwezi kujisaidia wewe wala mwanadamu yeyote ndugu yangu unaye teseka kwa namna yeyote ile iwe katika ajira au katika uongozi,ndowa uchumba, huo kwako ni mzigo mkubwa sana unaona ila kwake yeye ana sema
Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha, awezaye kupumzisha ni yesu kristo pekee, wengine wote ni mashabiki tu ukishindwa wanachekelea ukishinda wana shangaa hao wapo tu, na wala usitafute njia zako wewe mwenyewe wala usimpangie au kumlazimisha Mungu atumie njia unayoitaka wewe,
yupo Bwana mmoja katika biblia anafahamika sana kama Ibrahimu baba wa imani lakini kama mwanadamu,
baada ya kuona umri wake umekwenda yeye na mkewe wakashahuriana kutumia njia zao wenyewe kupata mtoto kupitia kwa mfanyakazi wao, wakaacha kusubiria mtoto wa ahadi ashukuriwe Mungu wetu asiyedanganya kama wanadamu wanavyo danganya akawapa mtoto uzeeni ambavyo kwaakili ya mwanadamu wa kawaida asingeweza kuamini kilichofanyika acha Mungu akupe suluwisho acha kutafuta suluwisho wewe mwenyewe, inaendelea,,,,