SEMINA YA SIKU TATU ZA MABADILIKO
SIKU YA 03
Baada ya kujifunza vyanzo vya mafanikio na watu kufunguliwa Nira shingoni mwao na Kutuwa mizigo yao sasa hatuwa inayofuata ni ya muhimu pia, unaweza kwenda kuchukuwa hatuwa ulizojifunza ili kujiandaa na kupokea zile Baraka bwana alizokuandalia kupitia kazi za mikono yako,
Iwe ni biashara au ajira, kulima,kufuga na mengineyo uliyojifunza usikae bila shuguli ya kufanya na mikono yako Bwana alimwagiza Adamu kumiliki na kutawala kwakuwa Alisha muwekea vitu vyakutawala na kuvimiliki,naakapewa agizo lakuituza bustani ya Edeni,
Sasa wewe ni nani usiyetaka kujishugulisha na kitu alafu unataka Mungu akufanikishe, ninakushahuri hataukiwa sehemu yenye mahubiri ya neon la Mungu na Muhubiri akaita watu wakuwaombea Baraka, jiulize kwanza hizo Baraka zitapitia wapi,kama utakuwa huna kila kitu, huna njiwa,huna kuku huna bata huna mbuzi huna ng”ombe huna bustani huna shamba, fikiria mara mbili wewe utapokelea mlango upi?
Ninajuwa kwa wewe usiyetaka kujishugulisha na shuguli yeyote huduma hii itakuuthi lakini ni bora upate hasira ukimaliza kusoma huu ujumbe na wewe ukawe na kitu cha kufanya,
Hata kama umemtembelea ndugu yako na unajuwa unaishi naye mwezi mzima hajalishi unasubiri majibu ya shule au ya kazi au unavyo juwa wewe mwenyewe,jitahidi siku isiishe hujafanya jambo lolote pale unapo ishi, ni hatari sana siku nzima kuisha bila kufanya jambo lolote linaloweza kuulipia huo muda,
Uza mda wako upate pesa kama umeshindwa kuutumia wewemwenyewe.
Watu huwa wanapenda kuyatumia maneno ambayo kwao hayafanyi kazi kabisa, mtu anasema muda ni mali haya muulize huo muda anaosema ni mali amezalisha kiasi gani maana kile unacho faidika nacho ndichotunacho kibadilisha na masaa ndipo tuna sema muda ni mali,kwa mfano kuna watu wameajiriwa hao wamekubaliana na mwajiri kwa makubaliano ya kuuziana masaa kwamba mimi nitakuuzia masaa yangu yote ya mwezi mzima unilipe,
Mwingine kibaruwa ana kubaliana na mwajiri wake walipane kwa kutwa kwamba atamuuzia masaa ya kutwa nzima, mwingine kwa nusu siku,mwingie kwa lisaa limoja,inategemea, mwingine anaamuwa kuyanunuwa masaa yake yote kwa kuijajiri shuguli zake mwenyewe anafahamu kabisa ataamuka saa ngapi kwenda kwa shuguli zake na atakamilisha saa ngapi,
Sasa wewe ndugu yangu ambaye umebakia kuwalaumu wazazi na ndugu zako kuwa hawakusaidii,je?wewe umejisaidia vipi au kwa lipi? Maana kuna wale wenzangu wao ni kulaumu tu kwamba ndugu wana uwezo alafu hawamsaidii,wakati huo hataki kujishugulisha na kitu chochote nikwenda kuzurura na marafiki,wasio eleweka na wao,au waliomzidi ujanja wa kimaisha, hatakama ndugu ana mali nyingi hizo si zako nay eye amezingaikia hakukaa kama wewe unavyo kaa,alafu akazipata,
Uondoke sasa ukatafute kitu cha kufanya ukiwa unamuomba mungu,katika kukaa bila kujishugulisha muovu anaweza kuitumia nafasi hiyo kukupa kazi,ya uwovu ukamuuthi Mungu,ukawa kama daudi daudi alijikuta anaingia kwenye thambi bila hata ya kupana akilini mwake,,,,,,,,,,
Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa UTAJIRI WAKE KRISTO USIOPIMIKA; na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote, ili sasa, kwa njia ya Kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho"(Waefeso 3:8 - 10).
Na Mungu wangu atawajazeni KILA MNACHOHITAJI KWA KADIRI YA UTAJIRI WAKE KATIKA UTUKUFU,NDANI YA KRISTO YESU" (Wafilipi 4:9)
Kristo ana utajiri usiopimika. Na wote walio ndani yake ni warithi pamoja naye wa utajiri usiopimika. Kutokana na utajiri huo TUNAJAZWA KILA TUNACHOKIHITAJI. Mahitaji haya ni ya kiroho, kiakili na kimwili. Kwa hiyo hakuna sababu ya mkristo kuishi maisha ya kupungukiwa, ikiwa Kristo yuko ndani ya moyo wake pamoja na utajiri wake usiopimika. Kikubwa kama wewe ni mrithi basi ni jukumu lako kuendeleza huo urithi kwakufuata kanuni yake Mungu
Jambo la kujiuliza ni hili; kwa nini utajiri huu wa Kristo usiopimika hauonekani katika maisha ya wakristo wengi? Wakristo waishije katika ushuhuda wa wokovu ndani ya Kristo, wakati wanaishi katika ulimwengu wenye hali ngumu kiuchumi? Watumishi wa Mungu kwa mfano, wachungaji, wainjilisti na kadhalika, waishije katika kumtumikia Mungu vizuri bila kupoteza ushuhuda wao wakati wanaishi katika mazingira yenye maisha magumu kiuchumi na bado wanasimamia amaandiko kuwa wao ni vichwa hawatakuwa mkia,na hata watoto wao wamewafundisha kuishi kama kichwa na siyo mkia wakati watu wakiwatazama kwa macho wanaonekana kama mkia,
wewe kama mkristo ukiyafuata maagizo ya Mungu ipasavyo hutohitajika hata kushuhudia yale Mungu aliyokutendea bali watu watashuhudia maana watakuwa wameshuhudia kwa macho yao,umewahi kujiuliza kuhusiana na maisha wanayoishi,wakristo?
Haya si maswali mepesi kuyajibu, lakini ni muhimu yatafutiwe ufumbuzi. Kabla hatujaanza kuyajibu napenda tusome Waefeso 4:11;
" Naye (Yesu Kristo) alitoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti; na wengine kuwa wachungaji na Waalimu."
Ni kwa kusudi gani Bwana Yesu Kristo aliamua kuwaweka hawa katika kazi yake kanisani? Waefeso 4:12-16 inatupa maelezo:-
"Kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo, ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. Katika yeye mwili wote ukiunganishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo
Ndugu Mtazamaji/ MSOMAJI; Bila shaka unampenda Mungu Sana tunaamini hivyo Kwa vile ulivyoweza kufika mahali hapa tulipo kupitia Mtandao huu, lipo kusudi la Mungu kutaka kukusaidia jambo Fulani ikiwa uko tayari katika yote jiepushe na mafundisho yasiyokuwa ya ki-Mungu Mathayo 16:6-12) piga simu kwa masaada zaidi huduma hii ni bure 0757328311