Mimi na mke wangu, Queen pamoja na mtoto wangu Sophia, tukishirikiana na wenzetu wa timu ya maombi tunaohudumu nao katika kuitenda kazi ya Mungu – tunapenda kukutia moyo na kukutakia baraka za Bwana na ushindi tele katika maisha haya mpya ya wokovu uliyoanza.
Jipe moyo mkuu kwa kuwa, Mungu amekusudia mambo mazuri juu yako. Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, uweze kumjibu kila mtu akuulizaye juu ya uhusiano wako na Mungu katika Kristo Yesu.
Na sisi hatutaacha kutoa shukrani zetu kwa Mungu kwa kukuokoa, tukikukumbuka katika sala ya kuwa Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, akupe wewe, roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; macho ya moyo wako yatiwe nuru ujue tumaini la mwito wa wokovu wake juu yako jinsi ulivyo; na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yako jinsi ulivyo; kwa kadri ya utendaji wa nguvu za uweza wake; aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa Roho.
Basi, Mungu huyu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa Kondoo kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu kristo, akufanye wewe kuwa mkamilifu katika kila tendo jema, upate kuyafanya mapenzi yake; naye Mungu akifanya ndani yako lipendezalo mbele zake; kwa Yesu Kristo; Utukufu una yeye milele na milele Amina.
Ikiwa utapenda kutushirikisha mahitaji yako ya maombi ili tushirikiane nawe katika maombi basi niandikie kupitia anuwani hii
Samson .o.mboya
Adrass: p.o.box 532 Geita gold mine
Cell phone no 0756809209/0784713604
Email: Samson.mboya@geitagold.com/samsonoxpel@gmail.com
Web site: www.samsonoxpel@blogspot.com
Muumba mbingu na Dunia akubariki sana,
Ndugu Mtazamaji/ MSOMAJI; Bila shaka unampenda Mungu Sana tunaamini hivyo Kwa vile ulivyoweza kufika mahali hapa tulipo kupitia Mtandao huu, lipo kusudi la Mungu kutaka kukusaidia jambo Fulani ikiwa uko tayari katika yote jiepushe na mafundisho yasiyokuwa ya ki-Mungu Mathayo 16:6-12) piga simu kwa masaada zaidi huduma hii ni bure 0757328311