Kuoshwa miguu
Yohana 13:3-8
Neno la msingi   Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu,
 aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni.
 Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga.
 Hivyo yuaja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi?
Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.
Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.
Utangulizi:
kuoshwa miguu ni moja ya tukio lililoanzishwa na Yesu kristo na akaacha agizo kwa wanafunzi wake kwamba zoezi lakuosha miguu  liendelezwe kufanyika mara zote,kama alivyosema kushiriki meza ya bwana, kwasababu kila tukio linamaana yake kimwili na kiroho,
Viwango viningine tunavyovitaka kila siku katika maisha yetu haviwezekani pasipo  kuunganishwa hivyo kuna huduma tunazipata kupitia sehemu flani ila unapoonganishwa unakuwa tofauti maana unakuwa sehemu ya kile unachokihitaji
Mfano:
Kunawakati unataka kubarikiwa ila unapounganishwa unakuwa wewe ndiye baraka kwa wengeine,unapoonganishwa wewe unakuwa mwanachama,unapoonganishwa unakuwa mshirika,unapoonganishwa unakuwa mwamini,unapoonganishwa unakuwa mfuasi, unapoonganishwa unakuwa kitu kimoja,mashambulizi,na matatizo mengi ya watu katika huduma zao hawajaonganishwa na hizo huduma,
Ni mwimbaji lakini si sehemu ya kile anachokiimba,ni mhubiri ila hajaonganishwa na kile anachokiongea, 
Kwa nini watu waonganishwa  ni kwasababu tunataka matokeo sawa,mtazamo mmoja,jicho moja safari moja nguvu moja agizo moja la kristo,
Watu wengi wanaishi katiki maisha ya kwao hawana ushirika na Mungu Wanamtaja Mungu ila hawajaunganika,Yohana 1:12 kwasababu kuna watu wamehama viwango ila hawajaonganishwa kuhama kituo na kuonganishwa ni mambo mawili tofauti,
Matokeo mazuri ya kile unachokitaka ni maandalizi ya uliyofanya,
*      Kutengeneza
*      Kurejeshwa
*      Kuonganishwa
*      kujengwa
ili uwene mabadiliko na matokeo makubwa katika maisha yako ya kiroho ni lazima ukubali kuonganishwa,
Faida za kuonganishwa
v  Unapoonganishwa Unakuwa umeingizwa ulimwengu mpya wa kiroho,
v  Faida ya kuonganishwa unaishi katika mamlaka za ki Mungu
v  Unaishi duniani ila huwazi kama dunia huyaoni mambo kama Dunia inavyoona hisia zako ni zatofauti kabisa
v  Unapoonganishwa Unakuwa na uhalalimkuwa wa kuhudumiwa kipekee na Mungu wa madhabahu,
v  Unapoonganishwa mmoja kwa moja unapata fursa ya kupatajambo jipya kia inapoitwa leo,
v  Unapoonganishwa ni rahisi kuhama vituo kila inapoitwa leo,
v  Unapoonganishwa na Mungu utatetewa na nguvu ya pale ulikojiunganishia watu
v  Unapata mwili wa Mungu
v  Unawaza kwa ufahamu wa KiMungu
v  Unaishi na moyo wa Mungu
v  Utaishi maisha ya kuzidishwa,
v  Utaishi maisha yako halisi
v  Faida ya kuonganiswa unadumu katika Huduma,
v  Faida ya kuonganishwa Mungu anakuwa upande wako
v  Faida ya kuonganishwa  kazi zote unazozitenda zinafanikiwa Waphili 1:5
Matendo 1:14  wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.

Wagalatia 2: 9.tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;
10 ila neno moja tu walitutakia, tuwakumbuke maskini; nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya.
Ufanye nini kuonganishwa
Utayari wa akili moyo
 
 

 

 

 

 

 

 

 

 

Followers