UNATAKA KUOKOKA CHAGUA HAPA!!,,,
SALA YA TOBA:
SEMA SALA HII KAMA UMEMAANISHA UNATAKA KUOKOKA,
Ee Mungu wangu Mtakatifu. Nimesikia neno lako nami nimeamini. Naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizokukosea katika maisha yangu yote. Damu ya Yesu Kristo iliyomwagika kwa ajili yangu, naomba initakase sasa katika roho yangu, nafsi yangu na mwili wangu. Nimefungua moyo wangu sasa; Ee Bwana Yesu Kristo nakuomba uingie ndani yangu, uwe Bwana na Mwokozi wangu kuanzia sasa na siku zote. Ahsante kwa kunisamehe dhambi zangu na Ahsante kwa kuniokoa. Amina”
Ikiwa umeisema sala hii kwa imani, basi sasa wewe umeokoka na dhambi zako zimesamehewa na kusahauliwa na Mungu sawasawa na alivyoandika katika neno lake. Jina la Yesu Kristo ni halali yako kulitumia! Kama mtu hajakombolewa akitumia jina la Yesu ni ubatili,
Ndugu Mtazamaji/ MSOMAJI; Bila shaka unampenda Mungu Sana tunaamini hivyo Kwa vile ulivyoweza kufika mahali hapa tulipo kupitia Mtandao huu, lipo kusudi la Mungu kutaka kukusaidia jambo Fulani ikiwa uko tayari katika yote jiepushe na mafundisho yasiyokuwa ya ki-Mungu Mathayo 16:6-12) piga simu kwa masaada zaidi huduma hii ni bure 0757328311